MACHAR: SIHUSIKI NA JARIBIO LA MAPINDUZI
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Sudan
Kusini Riek Machar aliyekimbilia mafichoni amekataa madai kuwa amehusika
katika jaribio la mapinduzi.
Ameiambia BBC kuwa wa kulaumiwa kwa
machafuko yaliyotokea katika mji mkuu wa Juba ni rais Salva Kiir ambaye
anadai kuhusika kwake.
Machar
ambae alifarakana na Rais Salva Kiir mnamo mwezi wa Julai alimshtumu kwa
"kuchochea mapigano ya kikabilai" ili kuficha udhaifu wake..
Rais Kiir amesema kikundi cha
wanajeshi wanaomuunga mkono Bwana Machar kilijaribu kutwaa madaraka kwa
nguvu usiku wa Jumaapili lakini walishindwa.
Alisema mapigano hayo yalianza pale
watu waliovalia mavazi ya kijeshi walipofyatua risasi katika mkuano wa
chama kinachotawala cha (SPLM).
Lakini Bw Machar aliiambia BBC: "Hakukuwepo jaribio lolote la mapinduzi."
Lakini Bw Machar aliiambia BBC: "Hakukuwepo jaribio lolote la mapinduzi."
Rais wa baraza la usalama la umoja wa
mataifa Gerard Arud amesema kuwa mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini
ambao umechukua mrengo wa kikabila unaweza kugeuka na kuwa vita vya
wenyewe kwa wenyewe.
Bwana Arud ameiambia BBC kwamba umoja
wa mataifa umepata habari kwamba mamia ya watu tayari wamepoteza maisha
yao tangia jaribio la mapinduzi lifanyike siku ya jumapili,ijapokuwa
amesisitiza kuwa sio raia wanaolengwa.
Ameiambia BBC kwamba takriban raia
elfu 20 wamepewa hifadhi katika makao ya umoja wa mataifa katika mji wa
Juba na kwamba wanakumbwa na uhaba wa chakula na madawa.(P.T)
No comments:
Post a Comment