FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI
Action
Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo
ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa
ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa
weledi na utaalamu zaidi.
Mafunzo
yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita,
kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za
asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya
mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo
hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu
na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao
kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org(P.T)
Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho
No comments:
Post a Comment