TEMBO WAZIDI KUUAWA TANZANIA
Mauaji ya tembo yameongezeka nchini
Tanzania tangia serikali ya nchi hiyo kusitisha Opereshieni tokomeza
kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za
binadamu. (HM)
Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu amesema kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi mwa kumi mwaka huu
Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu
Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu
Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali
Hata hivyo matokeo ya uchunguzi wa kamati maalumu kuhusiana na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ndiyo uliosababisha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri ,Shamsi Vuai Nahodha wa jeshi la ulinzi, Emmanuel Nchimbi wa mambo ya ndani,waziri wa Utalii na maliasili Khamis Kagasheki na waziri wa Maendeleo ya Mifugo David Mathayo.
Nchi za kutoka bara la Asia ndizo zinazodaiwa kujihusisha Zaidi na biashara ya pembe za ndovu hali inayoongeza kasi ya ujangili na mauaji ya tembo nchini Tanzania. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment