SERIKALI YAFAFANUA KUCHELEWA KWA AJIRA ZA WALIMU NCHINI
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu walimu waliomaliza masomo yao na kutopangiwa vituo vya kazi kuwa muda wa kufanya hivyo bado.
Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge
jana mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo
Mulugo alisema kuwa Serikali haijawasahau wala kushindwa kuwaajiri
walimu waliomaliza masomo yao.
"Ni kweli wengi hawajapangiwa vituo
vya kazi, lakini ndugu zangu Watanzania hebu muwe mnakumbuka kuwa ni
muda gani huwa tunawapangia ajira walimu, mbona muda bado,"alihoji
Mulugo.
Alisema kuwa muda wa kuwapangia walimu
huwa ni kati ya Februari Mosi hadi Machi 30 mara baada ya wizara kupata
vibali kutoka Utumishi.
Kuhusu walimu kupangwa na wengine
kuachwa, alisema inatokana na bajeti ambayo wanakuwa wamepewa kutoka
utumishi ambayo lazima inakuwa na ukomo wa idadi ya watu wanaotakiwa.(P.T)
Hata hivyo alisema kuwa walimu ambao
walimaliza na wana sifa za kufundisha wanapaswa kuwa na subira kwani
kumbukumbu zao zipo na kwa vyovyote lazima Wizara itawaangalia.
Kuhusu taarifa iliyotolewa kuwa wako wanafunzi wa darasa la saba, ambao hawajui kusoma Kingereza kwa kiwango cha darasa la pili, alikataa kuzungumza kwa mada ni kuwa hana taarifa na utafiti huo.
"Siwezi kuzungumzia jambo ambalo utafiti wake umefanywa na watu wengine kwa malengo yao wenyewe, naomba wazungumze wao," alisema.
Mjini Morogoro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu, bado kuna changamoto nyingi ikiwamo ya upungufu
wa vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia kama vitabu vya kiada.
Dk Kawambwa aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini na kuwa changamoto zilizopo zinahitajika kutatuliwa ili kiwango cha elimu kiendelee kukuwa na kuongeza uelewa kwa wanafunzi. Alitaja changamoto nyingine kuwa ni ufaulu mdogo katika masomo ya sayansi, hisabati na lugha unaosababishwa na upungufu wa walimu, madarasa ya awali na msingi.
Chanzo:Mwananchi

No comments:
Post a Comment