TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, December 30, 2013

CAMEROON KWENDA ULAYA KUWASHAWISHI WACHEZAJI KURUDI KUITUMIKIA NCHI YAO 

cameroon-sport-news1 ce483
Ujumbe wa kutoka nchini Cameroon wanatarajiwa kwenye nchi Ulaya kuwashawishi wachezajiwa wa nchi hiyo wanachezea katika nchi za ulaya kujiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo "Indomitable Lions". (HM)

Mpango huo wa kusaka vipaji vipya umekuja wakati Cameroon ikiwa inajiandaa kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka kesho nchini Brazil.
Chama cha soka cha Cameroon - Fecafoot kimesema mpango wao kwa sasa ni kushawishi wachezaji wanne wanaocheza soka ya kulipwa nchini Ufaransa.
Wachezaji hao Axel Ngando anachezea klabu ya Auxerre ya ligi daraja la pili nchini Ufaransa, Samuel Umtiti anachezea Lyon na Jean- Christophe Behebeck anachezea Valenciennes.
Mchezaji mwinginie anayewindwa ili kuuongeza nguvu kwenye timu ya taifa ya Cameroon ni Paul Geoges Ntep de Madiba ambaye pia naye anayechezea Auxerre ya Ufaransa.
Tunataka kuwashawishi hao wachezaji wachezee timu ya taifa ya Cameroon, na hasa kwenye fainali za Kombe la Dunia na pia wachezee Cameroon kwa hapo baadae Shirikisho la soka la Cameroon limesema kwenye taarifa yake. Chanzo: shaffihdauda

BASI JIPYA LA AZAM FC "KAMA ULAYA" 

azam 55b9d
Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki. (HM)

azam2 3d108azam3 7362d
Binzubeiry

JESHI LA CONGO DR LAREJESHA HALI YA UTULIVU KINSHASA

Jeshi la demokrasia ya Congo limesema kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi lisilofahamika la kigaidi.
Waziri wa habari nchini humo Lambert Mende kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.
Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya Taifa.
Amesema kuwa kulikuwa na mtukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.
Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara .
Mashambulizi haya yametokea wakati rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchini humo.
Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhali kwa raia wake kutofanya safari za ndani ya mji wa Kinsasa hadi hali itakapodhibitiwa Zaidi.(P.T)

TEMBO WAZIDI KUUAWA TANZANIA 

 runapa7 a3577

Mauaji ya tembo yameongezeka nchini Tanzania tangia serikali ya nchi hiyo kusitisha Opereshieni tokomeza kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu. (HM)

Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu amesema kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi mwa kumi mwaka huu
Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu
Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu
Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali
Hata hivyo matokeo ya uchunguzi wa kamati maalumu kuhusiana na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ndiyo uliosababisha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri ,Shamsi Vuai Nahodha wa jeshi la ulinzi, Emmanuel Nchimbi wa mambo ya ndani,waziri wa Utalii na maliasili Khamis Kagasheki na waziri wa Maendeleo ya Mifugo David Mathayo.
Nchi za kutoka bara la Asia ndizo zinazodaiwa kujihusisha Zaidi na biashara ya pembe za ndovu hali inayoongeza kasi ya ujangili na mauaji ya tembo nchini Tanzania. Chanzo: bbcswahili

Rais Kikwete amteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam(P.T)

WABUNGE 15 MATATANI

thomas1 e4385
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao. (HM)

Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.
Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.
Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.
"Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa
kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini," alisema Dk Kashililah na kuongeza.
Akizungumzia safari ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe nchini Uingereza, Dk Kashililah alisema Bunge halina uwezo wa kumzuia mbunge yeyote kufanya shughuli zake safarini baada ya kumaliza jukumu lililompeleka.
Dk Kashililah alisema Mbowe alikamilisha ziara yake ya Bunge na kwamba baada ya hapo aliendelea na shughuli za chama chake nchini humo.
"Suala hili lilikuwa limebeba hisia za kisiasa, baada ya kusikika tu bungeni basi vyombo vya habari vikaanza kuwahukumu wabunge ni mafisadi bila hata kutafuta ufafanuzi kutoka wetu. Sisi taarifa hizo tulikuwa nazo kabla ya hata ya kuibuka bungeni, lakini lilivyotafsiriwa sikupenda," alisema Dk Kashililah.
Dk Kashililahb alisema, "Bunge lilikuwa limeratibu jumla ya safari mbalimbali zilizokuwa zimependekezwa na Kamati 16, lakini hazikufanikiwa kwenda zote kwa pamoja.
Alisema ziara zote za kamati huandaliwa kwa mujibu wa kanuni ya 117 ambayo inazipatia mamlaka Kamati hizo kuandaa ziara inazooana zina manufaa kwa ajili ya kuboresha utendaji wake. Chanzo: mwananchi

Sunday, December 29, 2013

UN KUTUMA NDEGE ZA UPELELEZI SUDAN K 

sudan 744f7

Umoja wa Mataifa nchini Sudan umesema kuwa utatumia ndege za upelelezi kujaribu kuhakikisha idadi ya vijana walioripotiwa kuandamana kwenda kwenye mji wa Bor.
Serikali ya Sudan Kusini ilisema siku ya jumamosi kuwa kulikuwa na maelfu ya vijana ambao ni wafuasi wa kiongozi wa waasi Riek Machar.
Vijana hao waliobeba silaha za jadi na fimbo inaelezwa hawana mafunzo yoyote ya kijeshi, Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.
Lakini msemaji wa waasi amesema kulikuwa na askari wa kawaida ambao walikuwa wakirejea serikalini. Msimamizi wa mazungumzo kutoka Afrika amewapa Bwana Machar na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir hadi Decemba 31 wawe wameanza mazungumzo.
Karibu watu 1000 wamekufa katika mapigano yaliyochukua mwezi mmoja sasa, huku wengine 121,600 wanahofiwa kuyakimbia makazi yao.
Tayari maelfu ya raia wanatafuta hifadhi ya ukimbizi katika kambi za Umoja wa Mataifa huku wanajeshi zaidi wa kuongeza nguvu wa Umoja wa Mataifa wakiwa wamewasili nchini humo kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia. Chanzo: bbcswahili

TFF YASEMA: RAGE BADO MWENYEKITI HALALI SIMBA 

rage 83d5a
Ismail Aden Rage ndiye Mwenyekiti halali wa Simba ambapo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtaka kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa taratibu za klabu ya Simba. (HM)

Kamati imebaini upungufu kadhaa wa kisheria kwenye uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya Simba uliofanywa Novemba 18, 2013 kwa kumsimamisha Mwenyekiti wao. Upungufu huo ni pamoja na ukiukwaji wa Ibara ya 33 ya Katiba ya Simba juu uitishaji wa mkutano, ajenda ya kumsimamisha Mwenyekiti kuwasilishwa kwenye kikao kwa utaratibu wa mengineyo.
Changamoto nyingi zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti huyo zingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Simba.
Hivyo, agizo za Rais wa TFF, Jamal Malinzi kumtaka Mwenyekiti wa Simba aitishe mkutano lipo palepale. Pia Mwenyekiti ametakiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kuzingatia Katiba ya klabu hiyo.
Katika mkutano huo wa kujaza nafasi, ndiyo utakaojadili mgogoro kati ya Mwenyekiti na Kamati yake ya Utendaji. Nafasi hiyo kwa sasa inakaimiwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Joseph Itang'are baada ya Geofrey Nyange aliyekuwa akiishikilia kujiuzulu.
TFF inakumbusha wanachama wake wote (vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu) kuzingatia Katiba zao. Kamati pia imegundua ukikwaji wa maadili katika suala hili, hivyo, litapelekwa katika kamati husika.
Kwa vile maslahi ya TFF ni kuona mpira wa miguu unachezwa kwa utulivu, itazikutanisha pande husika wakati wowote kuanzia sasa.
Kuhusu mchezaji Emmanuel Okwi ambaye aliuzwa nchini Tunisia, TFF inafahamu kuwa klabu ya Simba bado haijalipwa na itasaidia kufuatilia FIFA fedha za mauzo ya mchezaji huyo. Chanzo: shaffihdauda

MAPINDUZI: KOCHA WA ITALIA PRANDELLI MGENI RASMI SIMBA VS AFC LEOPARDS 

Cesare-Prandelli--0081 57f77
MAANDALIZI ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu. (HM)

Msemaji wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc, AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati ya maandalizi imeshakamilisha taratibu za kuzipokea.
SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
Karim amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Pambano la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.
"Ninavyozungumza na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar". Alisema Karim.
Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.
"Uwanja wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia. Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao". Alisema Karim.
Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya milangoni kufanikisha mipango.
"Michuano hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo, tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao kwa wingi ndio mafanikio yetu". Aliomba Karim.
Aidha ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea michuano hiyo.
Michuano iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City ambazo hazikushiriki.
Mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.
Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30. Chanzo: Baraka Mpenja

MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI AIBUKA NA PIKIPIKI 

box 58673
Bondia Mohamed Matumla kushoto akipambana na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda. (HM)

box2 70ce0
Chanzo: shaffihdauda

Saturday, December 28, 2013

MAKAMBA AJIPIGIA DEBE LA URAIS KIAINA 

Katika kile kinachoonekana kama kujipigia debe katika kinyang'anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewaambia viongozi wa dini Kanda ya Ziwa kwamba vijana wanapofika kuomba ridhaa yao, muwaangalie, msiwabeze.
Huku akikataa kuweka bayana nia yake ya kuwania urais kwa maelezo kwamba muda wa kufanya hivyo haujawadia, Makamba aliwaambia viongozi hao wa dini kwamba wagombea hao wanapopita wawasomee sifa za uongozi katika Biblia na kusema kumekuwapo mjadala wa sifa za uongozi kuhusu kijana na kusema amekuwa akitoa mwito kwa vijana wasiokuwa na makandokando kushiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Akizungumza juzi usiku mjini hapa katika chakula cha pamoja na maaskofu na wachungaji kutoka Umoja wa Makanisa ya Kikristo wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema: "Huu ni wakati wa kila mmoja kutafakari hatima ya nchi yetu. Ndugu zangu... nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu sote ni Watanzania na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu."(P.T)
Alisema vijana wengi wamekuwa waoga kwa madai kwamba hawana fedha, uzoefu lakini akasema maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo.
"Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimi mdogo mimi siwezi, lakini Mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) .... Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa," alisema na kuongeza:
"Bwana alimwambia usiseme, mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe."
Alisema Tanzania inapita katika kipindi kigumu, hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuongoza maombi yatakayoiwezesha kupata kiongozi mwenye sifa ya kuivusha katika kipindi hicho.
Makamba amesema nchi inakabiliwa na nyufa kama vile rushwa, udini, ukabila, Uzanzibari na Uzanzibara, huku akirejea hotuba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya Machi 1995, ambayo aliyataja mambo hayo kuwa nyufa zinazoweza kuliangamiza taifa.
Alisema Tanzania inahitaji uponyaji na ikibidi kuanza upya kwa maana ya aina ya uongozi unaohitajika hivi sasa na kwamba ili kutimiza lengo hilo, viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutafakari na kuielekeza nchi njia sahihi ya kufuata.
"Shughuli za siasa zimeingiliwa na matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingiliwa na matapeli. Sasa tunapotafuta uponywaji wa nchi yetu ninyi mna nafasi kubwa kwani uponyaji tunaouzungumzia ni wa maovu ya kiroho, uongo, ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mna nafasi kubwa sana," alisema.
Alisema viongozi wa kisiasa pia wanayo nafasi yao katika kuponya taifa lakini lazima wanapofanya kazi hiyo wawe wasafi.
Alisema askofu au mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
"Tunapoomba uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa Mungu ambao ni walewale wanaokuja kanisani ndiyo wanaokuja katika siasa, kuongoza watu wa Mungu siyo kitu kidogo...... hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa viwe vikubwa sana," alisema
Rasilimali za nchi
Alisema Tanzania hivi sasa inakabiliwa na changamoto zinazoweza kuitwa kuwa ni za kidunia na za kibinadamu zinazojumuisha masuala kama vile upatikanaji wa huduma za afya, maji na elimu.
"Tunagawanyika ingawa migawanyiko hiyo si ya kidini, rangi na kikabila... iko ya namna gani, watu wachache wananufaika na keki (rasilimali) ya taifa kuliko wengine," alisema Makamba na kuongeza:
"Sasa Serikali, hili kwetu ni muhimu sana.... hakuna kitu muhimu kama kuendelea kujenga umoja wa taifa letu, migawanyiko hii ndiyo changamoto. Elimu anayoipata mtoto wangu ndiyo anaipata mtoto wa Rwamgasa, Kwimba na Nyarugusu?"
Alisema usawa katika elimu pamoja na huduma nyingine kama afya na nyingine muhimu, ndiyo msingi wa ujenzi wa taifa lenye amani na umoja kwani kila mmoja atajihisi kunufaika na rasilimali za nchi.
Naibu Waziri huyo alisema changamoto nyingine zinazoikabili nchi ni vitendo vya rushwa, ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, ubakaji, utapeli na kuporomoka kwa maadili.
Alisema taifa halipaswi kusubiri adhabu kutoka kwa Mungu kama inavyosomeka katika vitabu vitakatifu ambako kuna ushahidi kuhusu gharika wakati wa Nuhu, pia moto wakati wa Sodoma na Gomora, huku akiwapa changamoto viongozi wa dini kukabiliana uovu unaoshika kasi.
"Sasa taifa letu lina miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika na mwakani tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Zanzibar. Miaka 50 ni mingi kwa binadamu, lakini ukweli ni kwamba kazi ya kulijenga taifa letu ndiyo inaanza."
Shinikizo la maaskofu
Baada ya hotuba yake, baadhi ya maaskofu na wachungaji walisikika wakimshinikiza Makamba atangaze nia ya kugombea urais lakini alisema atafanya hivyo wakati mwafaka ukiwadia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa hayo ya Kikristo, Askofu Charles Sekelwa alisema: "Viongozi wa dini tukubaliane kuwa walezi na tusimkatae mtu kwa dini yake wala kabila lake. Wakijitokeza vijana huko mbele tuwaunge mkono, hayo maneno ni ya mtu mwenye hekima".
Askofu Jacob Lutabija alisema amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake wa Musoma akisema kwa watu wenye hekima zao wametambua nini wanapaswa kufanya
Chanzo:Mwananchi

MTU MMOJA AUAWA KATIKA MAPIGANO CAIRO

Mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya wanafunzi wanaokiunga mkono Chama cha Muslim Brotherhood na wakazi jijini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.
Maafisa mjini humo wamesema kuwa mwanafunzi mmoja alipoteza maisha baada ya pande hizo mbili kushambuliana kwa risasi katika mji wa Nasr.
Tukio hilo limetokea siku moja baada ya Serikali ya Misri kukitaja chama cha Muslim Brotherhood kuwa kundi la kigaidi.
Katika tukio jingine, watu watano wamejeruhiwa kwa bomu lililokuwa karibu na basi moja mjini Nasr, bomu hilo lilitegwa na kulipuka wakati basi hilo lilipokuwa likipita karibu na eneo lilipotegwa bomu.
Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo.(P.T)
Siku ya alhamisi, takriban wafuasi 16 wa chama cha Muslim Brotherhood walikamatwa wakishutumiwa kujihusisha na kundi hilo linalodaiwa kuwa la kigaidi.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Mtoto wa Naibu Kiongozi wa Chama hicho.
Shirika la Habari la Misri, Mena limesema Watu hao walikamatwa na kushutumiwa kuchochea machafuko na mapigano dhidi ya Jeshi na Polisi.
Siku ya jumanne, Watu 16 waliuawa na zaidi ya 100 walijeruhiwa katika shambulio la bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika jengo la usalama mjini Mansoura, Maafisa wameeleza.
Serikali imesema kuwa Muslim Brotherhood inahusika na shambulio hilo, madai ambayo yamepingwa vikali na Chama hicho.
Kundi lenye uhusiano na Al Qaeda, Ansar Beit al-Maqdis (washindi wa Yerusalemu) walikiri kuhusika na shambulio hilo.

Wanajeshi wa Somalia wauawa kwa Bomu

Takriban wanajeshi watano na afisa wa jeshi wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu,nchini Somalia mashuhuda wameeleza.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo.
Sababu ya mlipuko huo haijafahamika,majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.
Wanamgambo wa kiislamu, al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo
Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al -Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.(P.T)

Friday, December 27, 2013

Jinsi mastaa walivyosherekea sikukuu ya Christmas na familia zao

combs

Kila mtu huwa anapenda kusherekea Christmas na familia yake ndiyo maana watu wengi husafiri kurudi kwao kwa ajili ya kipindi hiki cha sikukuu.
Hata mastaa na wameacha kazi zao zote na kuzikumbuka familia zao, Rihanna alisafiri hadi kwao Barbados kuungana na familia yake kwa ajili ya kipindi hiki.
Hizi hapa ni baadhi ya picha ya jinsi mastaa mbalimbali walivyosherekea Christmas na familia zao.
christmas-2013-1

P. Diddy na wanae
christmas-2013-2
Mariah Carey, Nick Canon na watoto wao
christmas-2013-3
Rihanna na babu yake
christmas-2013-4
christmas-2013-5
Justin Bieber
christmas-2013-6

Miley Cyrus
christmas-2013-7
Future na mpenzi wakeCiara
christmas-2013-8

Wiz Khalifa na mwanae
christmas-2013-9
Keri Hilson na Sergie Ibaka
christmas-2013-11
christmas-2013-12
Drake
christmas-2013-13
Tyga na Black Chyna
christmas-2013-14
Swizz Beats, Alicia Keys na mtoto wao
christmas-2013-15
Jennifer Hudson na familia yake
christmas-2013-17
Trey Songs
christmas-2013-19
christmas-2013-20
Ciara na mama yake
christmas-2013-21
Ja Rule

WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TAMASHA LA KRISMAS WASUUZA MIOYO YA MASHABIKI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO 

1a
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO) 2
Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni. 3
Boniface Mwaiteje naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
4
Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akakonga nyoyo za mashabiki wake.(P.T)
5
Mwanamama mwingine Upendo Kirahiro akiwaimbisha mashabiki wake. 6
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza mungu wake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri.
7
Vijana wa kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza.
8
Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba na mmoja wa mashabiki wake katika tamasha hilo. 9
Mwimbaji wa kmataifa wa Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani katika tamasha hilo. 10
Hapa akiimba na mashabiki wake 11
Upendo Nkone akicheza na mastaeji shoo wake.

Tuesday, December 24, 2013

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/- 

4_6_8e632.jpg
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.(P.T)
MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).
Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

HII NDIO TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS 

Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.(P.T)
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix "Minziro".
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

Taarifa kuhusu bei mpya za umeme zitakazoanza kutumika tarehe 1 Januari 2014

tanesco
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.
Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.
Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.(P.T)
Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).
USHIRIKISHWAJI WA WADAU
Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.
UCHAMBUZI NA UAMUZI
Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.
Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).
EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.
Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:
Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.
Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.
Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.
Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.
Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.
Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.
Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.
Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.
EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.
Pamoja na maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, pia iliagiza TANESCO kutekeleza yafuatayo:
kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu ("least cost merit order") na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka katika kila mwezi ikionyesha uzalishaji halisi na mpango wa uzalishaji kama ilivyoidhinishwa na EWURA;
kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyoidhinishwa kwenye Mpango wa Umeme wa Taifa (Power System Master Plan). Miradi yote mipya lazima ipatikane kwa njia ya ushindani kwa kufuata Sheria ya Umeme, "Public Private Partnership Act", Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni husika;
kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme (supply and reliability) katika misongo ya 11kV, 33 kV, 66 kV, 132 kV, na 220 kV kwa kila mkoa kwa ajili ya uhakiki. Takwimu husika zinatakiwa kuonyesha jumla ya masaa mteja aliyokosa umeme kwa kila njia ya umeme ("feeder"), kukosekana kwa umeme kulikopangwa (planned outages), na ambao haukupangwa (unplanned outages), idadi ya matukio ya kukosa umeme katika kila "feeder", idadi ya wateja wanaohudumiwa na kila "feeder", idadi ya wateja walioathirika na katizo la umeme katika kila "feeder" na kiasi cha umeme kilichokosekana kutokana na katizo hilo (total unserved energy in kWh);
kuwasilisha kwa Mamlaka, katika kipindi cha miezi mitatu baada kuanza kwa Agizo hilo la Mamlaka, mpango wa utekelezaji wa "Demand Side Management Programme" ili uidhinishwe;
kupunguza kiwango cha upotevu wa umeme (technical and non-technical losses) katika mtandao wa usambazaji kutoka asilimia 19 ya mwaka 2012 hadi asilimia 15.1 ifikapo mwisho wa mwaka 2015;
kubuni mikakati ya kupambana wizi wa umeme utokanao na uunganishaji umeme usio halali, na kuondoa ucheleweshaji usio wa lazima katika kutunganisha wateja wapya;
kuhamisha wateja walio katika kundi la D1 kwenda T1 endapo matumizi yao ya mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo;
kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi, 2014, Mpango wa kuwawekea wateja wake mita za LUKU na AMR ili kupunguza wateja wanaotumia mita za zamani (conventional meters);
kuwasilisha kwa Mamlaka, kila baada ya miezi mitatu, taarifa/ripoti ya ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja wake ili kuongeza mapato ya Shirika;
kutoa elimu kwa wateja wake kuhusu haki na wajibu wa wateja kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kushughulikia kero za wateja kama inavyoelekezwa katika Mkataba husika na Kanuni za Umeme;
kuwasilisha kwa Mamlaka, maombi ya marekebisho ya bei yatokanayo na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na ubadilikaji wa thamani ya fedha; Ukokotoaji wa marekebisho hayo utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Kupanga Bei za Umeme za mwaka 2013 (Electricity (Tariff Setting) Rules, 2013);
kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu hali ya kifedha na kiundeshaji. Taarifa hizi zitatumiwa na Mamlaka katika kutathmini utendaji wa TANESCO ikilinganishwa na mashirika mengine ya umeme katika nchi jirani ili kuboresha utendaji wake. Tathmini hii pia itatumiwa na Mamlaka katika kubaini uhalali wa maombi ya baadae ya kurekebisha bei;
kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi 2014, mpango wa utekelezaji wa kila sharti katika Agizo la EWURA.
Bei mpya za umeme zitaanza kutumika tarehe 1 Januari 2014. Ni matarajio ya EWURA kwamba TANESCO watatumia fursa hii kutoa huduma bora zaidi za umeme na kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wateja kila yanapojitokeza ili kurejesha imani kwa Shirika la Umeme la TANESCO.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
Source: http://www.wavuti.com

Saturday, December 21, 2013

MCHUNGAJI GODSON SJ, PAMOJA NA WACHUNGAJI WENZAKE, AKIENDESHA IBADA YA UBATIZO WA MAJI MENGI KWA WASHIRIKA WA KANISA LA HABARI NJEMA LILILOPO MAJOHE KWA WARIOBA













MMOJA WA ALIYEKUWA AKIBATIZWA ALISHUKIWA NA ROHO MTAKATIFU BAADA YA KUBATIZWA


































ZOEZI LA UBATIZO LIKIENDELEA









MCHUNGAJI ALIYEKUWA AKIWABATIZA WAUMINI AKIFANYA MAOMBI YA KUMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUMALIZA ZOEZI HILO

WAMAMA WAKIWA NA FURAHA BAADA YA KUMALIZA ZOEZI LA UBATIZO


MWANAMKE HUYU ALIYEKUWA MWISLAMU, ALIKUWA AKIFUATILIA TUKIO HILI LA UBATIZO ALIGUSWA NA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU PALEPALE ALIPOKAA, AKAAMUA KUMPA YESU MAISHA HAPOHAPO NA KUOMBA ABATIZWE KATIKA UBATIZO HUOHUO. PICHA YA UBATIZO HAIPO KATIKA KURASA HII.









PICHA YA PAMOJA YA WAUMINI AMBAO WAMEBATIZWA WAKIWA NA WACHUNGAJI

AMBAO WAMESHIRIKI TUKIO HILO