WHO YAONYA KUHUSU WIMBI LA SARATANI
Uraibu wa pombe na sigara husababisha saratani
Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa saratani kote duniani.
Shirika hilo limesema nusu ya ugonnjwa
wa Saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili
kufanyika ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi, ulevi na
uvutaji sigara.
Watu milioni kumi na nne wanajulishwa
kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa
kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha miongo
miwili ijayo.
Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa Saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu.
Taasisi hiyo imesema serikali zinahitajika kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu matumizi ya pombe na sukari kama vile kuongeza bei na marufuku ya matangazo ya kibiashara ya bidhaa hizo.
CHANZO:BBC

No comments:
Post a Comment