TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, February 19, 2014

BARCELONA 2-0 MANCHESTER CITY, ROBO FAINALI YA LIGI MABINGWA ULAYA

Messi akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa penalti usiku huu Uwanja wa Etihad
BARCELONA imejiwekea mazingira mazuri ya kupenya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Manchester City, Uwanja wa Etihad usiku huu katika mchezo wa kwanza, hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Lionel Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 54 kwa penalti ya utata, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Martin Demichelis, lakini refa akatenga tuta, kabla ya beki Dani Alves kufunga la pili dakika ya 90. 

Hilo linakuwa bao la kwanza kabisa Messi anafunga dhidi ya vigogo wa Ligi Kuu ya England tangu ameanza kukutana navyo akiwa na Barca mwaka 2006 na kumaliza ukame wa kucheza saa 12 nchini humo bila kufunga.
Katika mchezo mwingine wa leo 16 Bora Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa BayArena mjini Leverkusen, wenyeji Bayer 04 Leverkusen walichapwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain FC ya Ufaransa.
Mabao ya PSG yalifungwa Matuidi dakika ya tatu, pasi ya Verratti, Ibrahimovic dakika ya na 42 pasi ya Matuidi na Cabaye dakika ya 88 pasi ya Lucas.

Ndani ya eneo la hatari? Martin Demichelis akimkwatua Lionel Messi kusababisha penalti, lakini ilikuwa faulo ya ndani ya boksi? Na chini Messi akipiga penalti hiyo.


Ibrahimovic akishangilia baada ya kuifungia PSG

No comments:

Post a Comment