TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, February 2, 2014

Catherine Panza; mama anayetarajiwa kuleta amani CAR 

 panza_bf7a7.jpg

Kadiri siku zinavyokwenda dhana ya mwanamke kutokuwa na umuhimu kwenye jamii nyingi za Kiafrika inapotea kutokana na kundi hilo kuanza kuaminika na kupewa madaraka makubwa maeneo husika.
Awali, ilikuwa vigumu kwa wanamke kuwa na madaraka ya kutawala nchi, hasa katika Bara la Afrika, lakini sasa hali ya kujiamini, upendo na nguvu za ushawishi walizonazo ndani yao zimeanza kulibeba kundi hili la jamii.
Miongoni mwa wanawake hao waliofanikiwa kuchomoza barani Afrika ni Catherine Samba Panza, aliyechukua jukumu zito la kuiongoza nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambayo katika siku za karibuni imekuwa ikisifika kwa migogoro na machafuko yanayosababisha raia wengi kupoteza maisha kila kukicha.
Licha ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke katika CAR, Samba pia anaweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kuingia madarakani, wakati nchi ikiwa kwenye machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Inawezekana jambo hili likashtua watu wengi hata kujiuliza namna mwanamke huyu alivyopata ujasiri na kujitosa kuongoza katika nchi iliyokithiri umwagaji wa damu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lakini, ukweli utabaki kuwa ni imani,upendo na busara wanazokuwa nazo wanawake wengi, ndizo zilizowafanya viongozi wa makundi ya wapiganaji kukubali kumweka madarakani Catherine, wakiamini kwamba uongozi wake utaleta amani nchini humo.
Kudhihirisha hilo, katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa kiongozi CAR, rais huyo aliyaita makundi ya wapiganaji kama watoto wake na kutaka kuweka silaha chini ili kurudisha hali ya amani Jamhuri ya Afrika ya Kati.
"Niwaombe wanangu wekeni silaha nchini na kutanguliza uzalendo, sihitaji tena kusikia habari za mauaji ya watu wasio na hatia,"alisema Rais Catherine.
Kauli hiyo ya Catherine(59), Meya wa zamani wa mji wa Bangui, inaonyesha wazi namna wanawake wanavyokuwa wanyenyekevu katika kuhakikisha amani inatawala kwenye jamii yake.
Tofauti na siasa, Catherine ambaye ni mama wa watoto watatum, ana taaluma ya sheria inayoaminika kuwa silaha kubwa katika uongozi wake na ndiyo moja ya sababu iliyofanya makundi ya wapiganaji kumkubali bila kipingamizi.
Raia wa nchi hiyo pia wametokea kumkubali na kumwamini Catherine,kutokana na kuchoshwa na utawala uliotangulia, unaoonekana kushindwa kutafuta suluhu ya migogoro iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa mwaka 2003,mama huyu alikuwa mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki biashara mbalimbali nchini humo ikiwemo kampuni ya bima. chanzo MWANANCHI

No comments:

Post a Comment