WAZIRI MKUU ARUHUSU ULEVI ASUBUHI
London, England. Waziri Mkuu, David
Cameron amebatilisha uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuamuru
uongozi wake ufikirie upya wazo la kuruhusu baa kufunguliwa mapema kwa
biashara ya pombe wakati wa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Italia,
Juni 14 mwaka huu.
Uamuzi wa Cameroon ni baada ya
wamiliki wa baa kunyimwa kibali cha kubadili muda wa kufungua biashara
zao katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Watu walio karibu na ofisi ya Cameroon
wameeleza kuwa kiongozi huyo ameamuru pande zote zinazohusika wakiwamo
wamiliki wa baa, polisi na mamlaka za miji wakae pamoja ili kuhakikisha
baa zinafunguliwa wakati wa mchezo huo dhidi ya Italia.
Awali, Wizara ya Mambo ya Ndani
ilipinga maombi ya Chama cha Wauza Bia na Wenye Baa waliotaka muda wa
kufungua biashara zao utazamwe upya wakati wa mchezo huo kwa masilahi ya
nchi. chanzo, MWANANCHI
Hata hivyo, katika majibu yake kupitia mtandao wa kijamii, Twitter, Cameron alisema: "Nimeamuru agizo hilo liangaliwe upya wakati wa mechi zote za England wakati wa fainali za Kombe la Dunia, tunahitaji mawasiliano ya pande zote zinazohusika."
Wamiliki wa Baa waliomba muda wa kufungua biashara ubadilishwe kutoka Saa 5: 00 hadi 7:00, Juni 14 wakati wa mchezo huo na kuendelea ili mashabiki kufuatilia mchezo huo. Waziri wa Mambo ya Ndani, Norman Baker alipinga pendekezo hilo na kuacha jukumu hilo kwa mmiliki mmoja mmoja kwenye mamlaka za miji ili kutoa leseni kwa gharama ya Pauni 21 kwa kila mmoja.

No comments:
Post a Comment