KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014, CHANGAMOTO, FURSA KWA BIDHAA
Na Shaffih Dauda
Mwaka
2014 umetawaliwa na tukio kubwa zaidi la kimichezo nalo ni kombe la
dunia. Ni wakati wa makampuni yenye misuli mikubwa na hata washirika na
wadhamini kujipanga kwa ajili ya kwenda sawa na kipyenga
kitakachopulizwa rasmi jijini Sao Paulo nchini Brazil. Chapa kama
Adidas, Coca-Cola, Visa, Continental na McDonald zimewekeza paundi
bilioni 5.5, kwa ajili tu ya kushiriki kupata haki ya kufanya biashara
kwenye michuano hiyo, inayoandaliwa kila baada ya miaka minne na
shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.
Ni wakati
wa kujiuliza sasa ni zipi changamoto na fursa zitakazozikumba chapa
hizi nchini Brazil? Kombe la dunia ni nafasi kwa bidhaa mpya pia
washirika wa kibiashara kupata nafasi ya kuwasiliana na asilimia 50 ya
watu wote duniani, kwani mashabiki zaidi ya bilioni 4 watawasha
televisheni zao kuangalia michuano hiyo, pia ulimwengu wa digitali
pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni nafasi kwa bidhaa kupata
umaarufu ingawa kutakuwa na ushindani kwenye kupata nafasi. Nani
atawika? Hilo ni swali muhimu sana kwetu.
Brazil
ni nchi ambayo itatawaliwa na rangi za kila aina kutoka kila kona ya
dunia, pamoja na ushabiki uliotukuka wa mchezo wa soka nchini humo, na
ni muda pia wa bidhaa kufikia malengo ya kibiashara kwa kuwa huo ni muda
wa thamani.
Adidas
kwenye ubora wametumia njia zote kukabiliana na wapinzani wao NIKE,
ambayo ni bidhaa maarufu katika bara la Amerika kusini. Mnamo mwezi
Disemba Adidas walizindua mpira maalum utakaotumika kwenye kombe la
dunia uliopewa jina la BRAZUCA, ambapo kampuni hiyo kubwa kwa kuzalisha
vifaa vya michezo yenye makazi yake nchini Ujerumani, ilifanya utafiti
kwa kuwahoji wakazi zaidi ya milioni moja nchini Brazil, ili kufahamu
namna walivyoupokea huo mpira, lakini pia kampuni hiyo ya Adidas iligawa
mpira mmoja mmoja kwa kila mtoto aliyezaliwa ile siku ya uzinduzi.
mmmhh mambo hayo! Wananchi wa Brazil ni moja ya wateja lakini kwa upande
mwingine watatumika kama njia ya kutangaza bidhaa, na makampuni mengi
yanategemea kufaidika na michuano hiyo kwa kuitumia kama ngazi kwa kuwa
karibu na wananchi kupitia mitandao ya kijamii pia na biashara za
kutembeza mitaani. Mitandao ya kijamii ni njia nzuri na bora kwa
mashabiki kufuatilia michezo kwa kubadilishana uzoefu kupitia Twitter,
Facebook and YouTube. Coca-Cola kama wadhamini wa michuano ya kombe la
dunia, wameshaanza kutumia nafasi ya kufanyika kipindi cha kiangazi kwa
kutumia ziara ya kombe la dunia wakijihusisha na mashabiki moja kwa moja
kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram jambo ambalo linamvuto kwa
mashabiki wa soka.
Pamoja
na kufanya mitandao ya kijamii ni vyema kwa mameneja bidhaa kutumia
fursa kama ilivyokuwa kwa (Super Bowl 2013 ) na Adidas (2012 kwenye
michuano ya Olympic ) kufanikisha kuwatumia walaji kama mabalozi kupitia
idadi zao kwenye mitandao ya kijamii.. Walaji watakuwa na uwezo wa
kuangalia video kwa mahitaji ya Brazil, na kutokana na mazingira kumetoa
fursa kwa technolojia kuweza kumsaidia mlaji kupata fursa ya kushuhudia
matukio . Wadhamini wengine wa Kombe la dunia la FIFA 2014 ni kampuni
ya VISA, wameikuza technolojia yao ya digitali kwa walaji kupitia bidhaa
yao ‘Go World’ inayofanana na ile ya kampeni ya michuano ya Olympic
2012.
VISA ni
maarufu kwenye mtandao wa YouTube, kwa maudhui maalum ya video
zinazoonyesha maisha halisi ya watu, pia mashindano ya mbio kuendana na
matakwa ya walaji. Sasa katika hili itasaidia sana kujenga imani ya watu
juu ya VISA. Moja ya changamoto kwa bidhaa ni wananchi kukosa imani na
bidhaa husika kutokana na umaarufu wao, kwenye kujikita katika tasnia ya
michezo. Changamoto ya kombe la dunia la Fifa 2014 kwa washirika wa
kibiashara, ni kutafuta nafasi ya kujikita kwenye nyoyo za watu ili
kupata nafasi ya kuzungumza kutakakopelekea kupata uhuru wa kujitawala
kibiashara kwa muda mrefu, na bidhaa kupata fursa mpaka siku ya fainali
No comments:
Post a Comment