MLEMAVU AFAIDI MKONO WA KIELECTONIKI
Mfumo wa mkono wa kieletroniki
Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis
Aabo amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia
kama ule wa binadamu.
Italia
Katika tukio linalopigiwa upatu
kuimarisha hali ya walemavu katika siku za usoni, madaktari huko Italia
wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki na neva za mabaki ya mkono wa
Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya fataki na hivyo kumwezesha
kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa kielektroniki .
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
'' tumeshangazwa sana na urahisi wa
mgonjwa wetu kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki
kuekelea majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti .
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Dennis hakuficha furaha yake alisema mkono huo umebadilisha kabisa hali yake.
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''
No comments:
Post a Comment