Wanafunzi wakiwa wamekaa tayari kwa kupokea zawadi zao |
Afisa elimu mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwa kukabidhi zawadi hizo kwa wanafunzi walioshinda |
Mwanafunzi huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza apambo alipatiwa zawadi wa Lap top |
Wanafunzi watano bora ambao walishinda wakipiga picha pamoja na wadhamini wao |
SHIRIKA lilisilo la kiserikali toka Nchini Japan JICA ALUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (JATA) limetumia kiasi cha Dola 800 za
Kimarekani kutoa zawadi kwa wanafunzi wa
shule za sekondali nchini walioweza kuandika
na kuisoma insha iliyoandaliwa
na shirika hilo.
Insha hiyo iliyoandaliwa na JATA ilikuwa inahusu “What are the role of public
secondary school in changing of social economic environment in Tanzania” ambapo
jumla ya wanafunzi zaidi ya 100 walishiriki
kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Katibu wa Shirika hilo nchini DK. Zacharia Mganilwa alisema JATA kwa
kushirikiana na JICA wamekuwa
wakiendesha miradi mbali mbali ya maendeleo ya elimu na kwa mwaka huu
wanafunzi wa shule nyingi walikuwa na mwamko wa kushiriki zoezi hilo tofauti na
mwaka jana ambapo shule sita tu zilizoshiriki.
DK. Mganila alisema lengo la shirikia hilo kuandaa insha hiyo ni kupima
uelewa wa wanafunzi kwa kuwajengea misingi ya kujiamini na kujituma katika masomo yao .
Aidha Afisa elimu wa Mkao wa Dar es Salaam, Bw. Kiduma
Mageni , kwa sasa JICA imekuwa ikitoa msaada mkubwa wa kufadhili miradi mbali
mbali nchini ikiwemo ya ujenzi na upande wa elimu kwa kuwasaidia kuwapeleka
baadhi ya walimu nchini Japan na kuwapatia mafunzo.
“Baadhi ya walimu huwa wanakwenda nchini Japani kwa kupata
mafunzo zaidi ili wanaporudi nchini watoe mafunzo bora kwa watoto kwa kiwango
kinachotakiwa, Aidha pia wajani nao wamekuwa wakijitolea katika kufundisha
masomo ya hisabati na Sayansi kwenye shule za sekondari hapa nchini” alisema
Bw. Mageni.
Alisema mashindano hayo pia yameleta changamoto kubwa kwa
wanafunzi na kuonekana na uelewa mzuri
na kuwajenga uwezo wa kujiamini hasa kwa watoto wa kike ambao ndio
wanakuwa kinara wa kuongoza na kujizolea zawadi kibao,
Alisema Mwaka jana katika shindano hilo mshindi wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi wa kike Faiza
Khanis Ussi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sunni Madressa toka Zanzibar kwa
kupata alama 81 ambapo alizawadiwa Laptop moja aina HP na
Certificate .
Hali kadhalika mwaka huu pia mshindi wa kwanza ni mwanafunzi
wa kike kutoka mkoa wa Kilimanjaro shule
ya secondary ya Oshara ni Zusaz
Mmari wa kidato cha nne,alipata alama 90
ambapo amepatiwa Laptop moja aina ya HP
,Certificate na Dictionary mbili.
Wshindi wengine waliobahatika kupata zawadi zingine mbali
mbali ni Samwel Steven ambaye alikuwa
mshindi wa pili toka shule ya Kilindi iliyopo Sanya Juu, Mariaum Ramadhani toka
shule ya Lumumba toka Zanzibar, Furaha
Mika toka shule ya Malangali Mbeya, ambapo jumla ya wanafunzi kumi walioshinda
walipatiwa zawadi zao.
No comments:
Post a Comment