TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, February 19, 2014

TUZO ZA KILI ZAZINDULIWA RASMI

kili_bf22f.jpg
Dar es Salaam. Tuzo za Muziki, maarufu 'Kilimanjaro Music Award' zimezinduliwa rasmi jana na zitafikia kilele chake Mei 3 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zinaratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na TBL kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro.
Mratibu wa Tuzo hizo kwa upande wa Basata, Kurwijira Ng'oko alisema mwaka huu wameboresha zaidi tuzo hizo, ambapo hivi sasa wanataka muziki uwe ni ajira rasmi kwa hiyo msanii ambaye atapendekezwa katika vipengele vya tuzo hizo kama hajasajiliwa Basata hataruhusiwa kushiriki.
Ng'oko alisema pia tuzo ya mtayarishaji chipukizi wa mwaka haitakuwapo kwa vile watayarishaji ni wale wale kila mwaka na hivyo kufanya tuzo kujirudia.
Naye meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa tuzo hizo, George Kavishe alisema kuwa Watanzania ndio watakaoteua msanii atakayeingia kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha tuzo hizo kwa kutoa mapendekezo yao kwa njia ya simu au mitandao ya kijamii. chanzo, mwananchi

No comments:

Post a Comment