Whatsapp yanunuliwa na Facebook, nini tutegemee
Kama ulikuwa haufahamu, habari kuu
katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya leo ni Facebook kuinunua
Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19. Nunuzi
hilo ni la programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa
whatsapp watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja, mission za
whatsapp zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi wa whatsapp.
Kwa wasio fahamu, whatsapp ni moja ya programu ya simu za mkononi
inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye intaneti badala ya
ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia whatsapp, inamaana utaepuka gharama za
sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma
picha, sauti uliyojirekodi nk.
Hadi sasa, whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka
nchi nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni
moja kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa whatsapp ni programu pendwa na
yenye kutumika.
Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa watu binafsi na hata makampuni,
Ingawa makampuni mengi ikiwemo
Facebook yamekuwa yakitegemea huduma za matangazo kama njia ya kuingeza
kipato, whatsapp ni programu ambayo, huwezi kuonana na matanagazo na
wamejizatiti kuwa ni wataendelea hivyohivyo bila ya matangazo. Na pia
whatsapp ni bure kwa kwa mwaka wa kwanza na huchaji $1 kwa mwaka kama
gharama ya kujiunga kwa miaka inayofuata. Hivyo kabla ya Facbook
kuinunua whatsapp ni dhahiri walishajipanga kwenye hili, kwani, hili
ndilo linaloifanya whatsapp iwe tofauti.
Akielezea sababu ya kuinunua
whatsapp, mwanzilishi wa Facebook alisema, wameinunua whatsapp kwa
sababu whatsapp ina thamani. Na wao wakiwa kama wafanya biashara lengo
lao kubwa ni kuongeza thamani ya biashara yao illi waendelee kuwa
salama. Hivyo, wanaamini nunuzi la whatsapp litakuwa na tija na manufaa
kwa wote, wanunuzi na walionunuliwa. Hivyo ubora na misingi ya huduma ya
whatsapp utaendelea kuwa juu kama ilivyo sasa.
Lakini, dili hili la kuinunua whatsapp halikuja ghafla, bali limekuja
kwa kuangalia muelekeo na mabadiliko ya watumiaji wa mtandao. Taarifa
zinaonesha kuwa, asilimia zaidi ya 52% ya watumiaji wa mtandao kwa sasa
ni wale wanaotumia simu. Na pia matumizi ya email kama njia ya
mawasiliano yamezidi kupunguasiku hadi siku. Na siku zinavyozidi kwenda
mbele inamaanisha idadi hii itakua.
Pia, kwenye uwanja wa ujasiriamali, unatakiwa kuishi kwa kuyachunga
mazingra na siyo kuomba dua mambo yasibadilike, hivyo ununuzi huu
umekuja ili kuhakikisha Facebook inakuwa na udhibiti wa mazingira ya
watumia intaneti na mtandao.Kitendo cha Facebook kuinunua whatsapp,
kinaiwezesha kujikita zaidi kwenye kundi kubwa la watumiaji wa intaneti
ambao wengi ni vijana.
Kwakuwa watumiaji wengi wa whatsapp ni wa kwenye simu, na kwakuwa yao
ni moja ya programu zenye mamilioni ya watumiaji, hivyo kuimiliki
whatsapp inamaanisha kumiliki hisa kubwa kwenye soko la watumiaji hao.
Na hii itaiweka Facebook katika hali ya kudhitibi soko. la intaneti na
mitandao jamii. Facebook pia watapata njia wa kuwafikia watumiaji hawa
moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa instagram, hivyo hii ni moja nunuzi
lenye faida kwao.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza, je kitendo za Facebook kuinunua
whatsapp kina faida yoyote kwa kampuni? na nini sisi watumiaji wa
whatsapp tutegemee? Kutokna na sababu nilizozitaja juu (thamani), hivyo
ni yumkini kabisa, Facebook wanaweza kufanya kati ya vifuatavyo.
1. Kuiunganisha whatsapp moja kwa moja na Facebook.
Ikumbukwe kuwa, whatsapp itaendelea kuwa whatsapp, hivyo usifikiri
kwamba kesho hakutakuwa na whatsapp bali watumiaji wote watapelekwa
Facebook, la , ila whatsapp itakuwa na ushirikiano wa kiutendaji na
Facebook na kuzifanya ziwe imara zaidi. Ila, ili whatsapp iunganishwe na
facebook, ni dhahiri kuwa whatsapp lazima ifanyiwe maboresho na
kuongezewa baadhi ya matumizi ambayo yataiwezesha kuiunganisha moja kwa
moja na Facebook, isiishie kwenye mawasiliano tu. Kunatakiwa kuongezwe /
boreshwa zaidi zile huduma ya kijamii.
Kwa
mfano, tutegemee kuwa na uwezo wa kutuma visasisho(updates) ambavyo
vitaonekana kwenye Facebook yako. Hii itaipe ya maisha yako hapohapo
kwenye whatsapp. Hii itaipeleka whatsapp kufanana sana na moja ya
mtandao unaofanya kazi zake kama whatsapp unaoitwa Wechat.Huu ni mtandao
uliofanikiwa sana kwa China.
2. Kutafuta / alika marafiki wa facebook kwa kutumia namba za simu na siyo email pekee
Facebook ilipoanza, ilikuwa inategmea sana email kama njia ya kutafuta
marafiki, ila kadri siku zinavyozidi kwenda, matumizi ya email kama njia
ya mawasiliano ya kawaida yamekuwa yakipungua, hivyo kutegemea email
kunaiweka facebook kwenye kikomo cha kutanuka. Kwakuwa whatsapp inatumia
namba za simu, na kwakuwa facebook imeinunua whatsapp, basi tutegemee
kuwa kutakuwa na uwezo kwa watumiaji wa Facebook kuwaalika watu wajiunge
na facebook kwa njia ya ujumbe wa simu, na hii itaunganishwa vyema kwa
kutumia whatsapp.
3. Kuongezwa huduma zaidi ambazo ni za kulipia.
Kwakuwa lengo la kuwekeza ni kuongeza kipato.Iwe moja kwa moja au la, ni
dhahiri kuwa facebook watakuja na njia zitakazowawezesha kuongeza
kipato kwa kutumia whatsapp, hivyo kutakuwa na huduma zaidi ambazo si za
lazima, ila kama utazihitaji, basi utatakiwa kulipia kiasi fulani. Hii
ni moja ya njia zinazotumika kipindi unaandaa bando la huduma.
Hivyo,kwa watumiaji wa Facebook na Whatsapp, tutegee mambo mengi zaidi.