WANANCHI WATAKIWA KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO
Habari na Salma Mrisho, Geita
Wananchi
wametakiwa kujua kwamba maendeleo hayawezi kuja bila wao kujitambua kuwa wana
nafasi katika kushiriki na kutoa maoni katika kuibua miradi mbalimbali ya
kijamii itakayowaletea maendeleo.
Hayo
aliyasema Afisa mipango wilaya ya Geita mkoani Geita Bw Andrew Chikwanda
alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu uhusikaji wa wananchi
katika uibuaji wa miradi.
Alisema
kuwa wananchi,wadau na serikali ni watu wanaotegemeana katika shughuli
mbalimbali hasa za kuibua miradi na kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa
aisimamie kikamilifu ili matunda ya hiyo miradi ionekane.
“zamani
serikali ilikuwa inatoa fedha na kuanzisha miradi lakini ilionekana ile miradi
matokeo yake yalikuwa madogo na wakati mwingine ilikuwa haionekani
thamani ya miradi lakini kwa sasa wananchi wana nafasi ya kuibua miradi
yao na wafanye hivyo”alisema Bw Chikwanda
Pia
aliwataka wananchi kama walikuwa hawajui wana hiyo nafasi watambue na wakae
katika vijiji vyao na waibue miradi ambapo inatakiwa ipitishwe na mkutano wa
kijiji na mabaraza ya maendeleo ya kata na baada ya hapo wana kaa na madiwani
na wataalamu kuijadili ipi ipewe kipaumbele kulingana na fedha iliyopo kwa
mwaka husika.
Bw
Chikwanda aliongeza kuwa miradi ya wananchi imekuwa na maendeleo kwa kuwa wao
ndio waanzilishi na wanasimamia ipasavyo kuhakikisha inafanikiwa kuliko
angefanya mtu mmoja ambapo ingeweza kuchukua muda kukamilika.
“unajua
wananchi wajue kuwa wao ndio wahusika na wasisibiri ile ruzuku inayotolewa na
serikali kupelekwa ngazi ya kijiji ndio ifanye kila kitu maendeleo yatachelewa
sana waibue tu miradi sisi ni watekelezaji wa kufanikisha hilo”alisisitiza Bw
Chikwanda
Aliongeza
kuwa kuwa mara nyingi wanatembelea miradi iliyobuniwa na wananchi na kuangalia
viwango vya ujenzi kama vinakidhi na wanatoa nyaraka kuwa kila hatua ya ujenzi
ihakikishe nkuwa mhandisi ametoa cheti ili kuruhusu hatua nyingine
iendelee.
Aidha
aliwataka wakuu wa idara na ofisi ya ujenzi kutembelea miradi inayoanzishwa na
kuoana thamani yake na hata kutoa ushauri kuliko kuacha miradi inaendelea na
ikikamilika kuonekana kuna kasoro kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawaangusha
wananchi kwa nguvu kazi zao walizotumia.MWISHO
No comments:
Post a Comment