TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, August 29, 2012

MKUTANO WA KUNDI LA G77 NA CHINA  UNAENDELEA NCHINI CHINA











EVELYN MKOKOI
BANGKOK, THAILAND 
29/8/2012
MKUTANO WA KUNDI LA G77 NA CHINA UNAENDELEA

Mkutano wa mabadiloko ya tabia nchi unaendelea mjini Bangkok, ambapo leo
kundi la G77 na China limekutana kwa mara ya pili na kujadili mambo mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kuangalia namna mpango wa kupunguza gasi joto duniani
utakavyoweza kufanya kazi.

Katika mkutano wa leo, kundi hilo limejadili pia namna ambavyo nchi
zinazoendelea zinapaswa kuainisha taarifa zinazohitajika katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabaia nchi, ikiwa ni pamoja na mipango na masuala ya fedha,
teknolojia na taaluma.

Aidha, washiriki wamejadili kuhusu juhudi za pamoja za kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi kwa ujumla na kuwa na hali ya kuweza kufikia malengo
ya pamoja ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabaia nchi.

Aidha, katika mkutano wa leo umesisitizwa umuhimu wa kila nchi kuwa ‘serious’
katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi
ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua sahihi ili kuweza kufikia malengo ya kuhimili
na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Washiriki pia walitilia mkazo suala la technolojia linavyoweza kuchangia katika
athari za mabadiliko ya tabia nchi, na walipata nafasi ya kujadili kwa kifupi
kuhusu mkutano wa dunia (COP18) wa mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika
mjini Doha mwezi wa Disemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment