Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Sazi Salula akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo.
Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa muda wa miaka miwili mfululizo kwa mwaka huu 2012 na 2013 , ambapo Mawaziri wa nchi za Afrika wanatarajia kuwasili hapo kuanzia Septemba 10 hadi 14 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mazingira katika nchi za Afrika ambaye ndiye mratibu wa mkutano huo Bw. Mounkaila Goumandakoye , alisema utawashirikisha Mawaziri wa nchi za Afrika kwa kuzungumzia utunzaji wa mazingira na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoikumba nchi za Afrika .
Mkutano huo unashirikisha zaidi ya watu 3000 ambao wote watakuja kuzungumzia swala hilo, ambapo mwenyekiti wa mkutano huo atakuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Rais Mhe, Dkt . Tezezya Huvisa.
No comments:
Post a Comment