TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, August 15, 2012


SENSA HAITAWAACHA WAFUGAJI WA GEITA
  
Habari na Salma Mrisho , Geita

Mkufunzi wa sensa ngazi ya Mkoa wa Geita Cosmas Kapinga amewahakikishia madiwani kuwa hakuna mtu yeyote atakayekosa kuhesabiwa katika zoezi la sensa hata akiwa porini.
Kauli yake hiyo ilikuja baada ya Diwani wa Kata ya Iyogero wilaya ya Bukombe katika semina ya madiwani kuhusu sensa ya watu na makazi kutaka kujua jinsi gani wafugaji watahesabiwa kwa kuwa wao wanahama maeneo kila siku.
Diwani huyo alidai kuwa hayupo kiongozi anayejua kuwa mfugaji yuko  wapi na hata kama uliwaona eneo lako ukiwafatilia siku nyingine wwanakuwa wameshahama kwa namana hiyo zoezi hili litakosa idadi ya wafugaji.
Akijibu swali hilo Bw  Kapinga alisema kuwa kwa upande wa wafugaji kutakuwa na karani wa sensa ambaye ataandamana na kiongozi wa sehemu husika kwenye maeneo yake na siku tatu kabla ya sensa karani atakua kehsayajua maeneo kwakua wanayatembelea kabla ya zoezi lenyewe.
“ndugu madiwani hilo lisiwatie shaka kabisa tuna ramani ya kila eneo na karani anayajua maeneo yake ya kazi kwani suala la wafugaji lisiwatie mashaka kabisa “alisema Kapinga
Pia aliwataka madiwani  muda uliobaki wawaelimishe wananchi juu ya umuhimu wa sensa hasa wafugaji wanaohamahama kila kukicha na wajue kuwa agosti 26 ndio zoezi lenyewe na ni muhimu kupata takwimu za wafugaji.
MWISHO

No comments:

Post a Comment