WANANCHI WA GEITA NA MATATIZO YA USAFIRI 
Habari na Salma Mrisho ,Geita . 
Wananchi
wametakiwa kuwa na subira katika mchakato unaoendelea wa kuhakikisha suala la
usafiri linaboreshwa kuanzia mijini hadi vijijini. 
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Wilaya Manzie Mangochie  wakati wakizungumza na wadau
mbalimbali mwishoni mwa wiki  juu ya kuboresha suala la usafiri wa abiria
mkoani hapa. 
Alisema
kuwa wananchi walikuwa wanapata tabu juu ya usafiri hasa baada ya kupiga
marufuku magari madogo aina ya michomoko iliyokuwa inabeba abiria wengi na ni
kinyume cha sheria na kuongeza kuwa kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa kwani
wafanyabiashara wa  magari aina ya hiace wameyaleta kutoka mwanza  na
yanatoa huduma ya usafiri. 
“wananchi
jamani muwe mnatupa taarifa sio mpaka ajali zitokee na kama kuna michomoko
sehemu inafanya kazi mtujulishe sheria ichukue mkondo wake”alisema Manzie
Alisema
kuwa kwa sasa wanajipanga ili waweze kuweka vituo kila eneo na ili Geita
iendane na hadhi ya Mkoa kuliko ilivyo sasa usafiri wa baiskeli umekuwa mwingi
na pikipiki na wataalamu wamepitia baadhi ya maeneo ambapo umbali wa mji kwa km
10 kuna ruti zishapangwa na kwa vigezo vya Sumatra nauli itakuwa shilingi 500. 
Aidha
aliwataka wananchi watoe taarifa juu ya madereva wanaovunja sheria barabarani
ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika mkoani hapa. 
Kwa
upande wamkuu wa wa Kikosi Cha Barabarani Kamanda John Mfinanga aliwahakikishia
wananchi kuwa watafatilia kwa karibu kero zote za usafiri na kuhakikisha magari
hayajazi abiria wengi na sheria zinazingatiwa.
No comments:
Post a Comment