Kocha wa Liverpool kamkejeli Jose Mourinho? hili ni jina analotaka kuitwa, zipo pia pichaz za utambulisho wake
         
Jioni ya October 7 klabu ya Liverpool ya Uingereza ilitangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Jurgen Klopp na
 kujiunga na klabu hiyo, taarifa zilizotoka  Ijumaa ya October 8 ni kuwa
 atatambulishwa mbele ya waandishi wa habari pamoja na kufanya mahojiano
 na waandishi wa habari.
Jurgen Klopp aliwahi kuwa kocha wa Borussia Dortmund ya Ujerumani kabla ya mwishoni mwa msimu uliyomalizika kuacha kazi na kukaa bila timu kwa kipindi fulani. Jurgen Klopp
 ametambulishwa Ijumaa ya October 9 hii ikiwa ni siku moja imepita toka 
asaini mkataba wa miaka 3 wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja 
zaidi, kocha huyo amesaini mkataba wenye thamani ya pound milioni 21.
Jurgen Klopp ambaye alianza kazi ya ukocha katika klabu ya Mainz 05 mwaka 2001 – 2008 ambapo alihamia katika klabu ya Borussia Dortmund.
 Moja kati ya kauli zinazovutia wengi alizozungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari ni kuwa yeye ni kocha wa kawaida kauli ambayo 
ilihusishwa kama kijembe kwa Jose Mourinho ambaye anajiita ‘the special one’.
” Ni 
heshima kubwa kuwa kocha katika moja kati ya klabu kubwa duniani, hii ni
 fursa kwangu ya kujaribu na kuisaidia klabu, haukuwa muda sahii kwa 
mimi kujiunga lakini naweza sema ni wakati mzuri kwangu. Sitajiita jina 
lolote sabau mimi ni  mtu wa kawaida na mama yangu anatazama huu mkutano
 kupitia Tv akiwa nyumbani, ila kama utapenda kuniita jina itakuwa 
vizuri ukiniita ‘the normal one’ ” >>> Jurgen Klopp





No comments:
Post a Comment