MKUTANO WA TABIA YA NCHI WAZIDI KUENDELEA DOHA
Evelyn Mkokoi
Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Doha
30/11/2012
Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kupunguza hewa ukaa na uharibifu wa misitu (MKUHUMI) ulenge kunufaisha wananchi na nchi katika maeneo husika.
Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kupunguza hewa ukaa na uharibifu wa misitu (MKUHUMI) ulenge kunufaisha wananchi na nchi katika maeneo husika.
Tanzania imesema kuwa, mfumo wa utoaji fedha kwa ajili ya kupunguza utoaji wa gesijoto na
uharibifu katika sekta ya misitu hususan kwa nchi zinazoendelea unatakiwa uwe wenye manufaa
kwa nchi na wananchi katika maeneo husika.
Hayo yameelezwa leo na Bwana Freddy K. Manyika, Afisa Misitu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais,
katika majadiliano kuhusu Mfumo wa Ufuatialia na Utaratibu wa utoaji wa fedha, yanayoendelea
katika mkutano wa 18 wa nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchia unaofanyika mjini Doha, Qatar.
Akiwasilisha msimamo huo wa Tanzania, bw. Manyika ameleeza kuwa,Kuwepo kwa mfumo bora na
wa ufuatialiaji na utoaji wa fedha utatoa motisha kwa uhifadhi na usimamizi endelevu katika sekta
ya misitu kwa nchi maskini..
Akizungumza kwa niaba ya nchi zinazoendela (Least developed Countries -LDCs) Bw. Manyika
alisema kuwa maisha ya wananchi katika nchi zinazoendelea husuan nchi maskini yanategemea
sekta ya misitu kwa ajili ya kupata nishati, chakula, madawa, ujenzi wa makaazi na miundombinu,
malisho ya mifugo, shughuli za kitamaduni, utalii, na huduma mbalimbali za kijamii kwa kiwango
kikubwa, hivyo kwa kuzingatia umuhimu huo, mfumo wa ufuatilaiji na utaratibu wa malipo
unaoandaliwa kwa ajili ya kusaidia sekta ya misitu hauna budi kutoa malipo yenye manufaa na
motisha kwa wananchi wanaotunza misitu badala ya kutaka kutoa mwanya kwa makampuni ya
kibiashara yenye mitaji mikubwa kunufaika na rasilimali hiyo.
“Tanzania na nchi zinazoendelea hazikubaliani na mfumo unaolenga kuwafanya wananchi
wanaozungukwa na kutunza misitu hiyo kwa miaka mingi kugeuzwa vibarua na wapakazi katika
makampuni yenye lengo la kujinufaisha kwa kutumia rasilimali na nguvu za wananchi maskini,
Alisisitiza.”
Aidha Bw. Manyika aliongeza kuwa, kufikiwa kwa makubaliano kuhusu mfumo na utaratibu wa
utoaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za MKUHUMI katika mkutano wa Doha utasaidia kurejesha
motisha kwa wananchi kuhifadhi misitu katika maeneo yao na hivyo kuendeleza shughuli za utunzaji
mazingira na kuchochea maendeleo na uhifadhi endelevu kupitia sekta ya misitu.
Katika majadiliano yanayoendelea hapa mjini Doha, nchi wanachama wanatakiwa kuandaa mfumo
wa ufuatiliaji na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa shughuli za upunguzaji wa gesijoto na utunzaji
wa misitu ili kupunguza uharibifu. Mkutano wa 18 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa
Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unafanyika Doha, Qatar, kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 7
No comments:
Post a Comment