TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, October 8, 2015

Mapenzi yake kwa Man United yafanya atumie zaidi ya saa 450 kutengeneza kitu hiki (+Pichaz)

 

Ushabiki wa soka kwa raia wa Uingereza unazidi kuchukua nafasi katika headlines za soka kila kukicha, August 30 2015 tuliona shabiki wa klabu ya West Ham United John High kuchora tattoo ya matokeo ya ushindi wa mechi dhidi ya Liverpool kwani kwa mujibu wa shabiki huyo anaweka kumbukumbu hiyo mwilini mwake kutokana na kuwa ni zaidi ya miaka 50 West Ham haijawahi kuifunga Liverpool.
PAY-Manchester-United-fan (2)
August 7 shabiki mwingine wa klabu ya Manchester United Chris Scott anatajwa kutumia zaidi ya saa 450 katika kipindi cha miezi mitatu kutengeza mfano wa uwanja wa Old Trafford kama sehemu ya mapenzi yake kwa Man UnitedChris Scott ametengeneza mfano wa uwanja wa Man United kama ulivyo hadi rangi.
PAY-Manchester-United-fan (1)
Klabu ya Man United imekuwa ikiutumia uwanja wa Old Trafford kama uwanja wake wa nyumbani toka mwaka 1910, hata hivyo uwanja wa Old Trafford ndio uwanja wa pili kwa ukubwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa Wembley ambao mara nyingi hutumiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo.
PAY-Manchester-United-fan (3)

Top 10 ya wasichana warembo katika mchezo wa tennis 2015 (+Pichaz)

Mchezo wa tennis ni moja kati ya michezo inayokuwa kwa kasi duniani kote, October 7 nakuletea Top 10 ya warembo wanaocheza mchezo wa tennis, list hii haitokani na umahiri wao wa kucheza tennis pekee bali hata fashion, muonekano wao. Katika kipindi cha miaka mitano hadi saba Maria Sharapova, Ana Ivanovic , Maria Kirilenko na Anna Kournikova wamekuwa wakiingia katika headlines ya magazine tofauti tofauti.
1- Eugenie Bouchard ni mchezaji tennis kutokea Canada, mrembo huyu ana umri wa miaka 21 lakini anatajwa kama mmoja kati ya wanamichezo wa kike wanaolipwa fedha nyingi.
LONDON, ENGLAND - JUNE 19: Tennis Player Eugenie Bouchard attends the WTA Pre-Wimbledon Party as guests enjoy Ciroc Vodka presented by Dubai Duty Free at Kensington Roof Gardens on June 19, 2014 in London, England. (Photo by Eamonn M. McCormack/Getty Images for WTA)
Eugenie Bouchard
2- Sorana Cîrstea ni mrembo kutokea Romania ana umri wa miaka 25, mara nyingi huwa haonekani akishika nafasi za juu katika mchezo wa tennis ila anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji tennis warembo kutoka bara la Ulaya.
sorana1-1398004630
Sorana Cîrstea
3- Sania Mirza ana umri wa miaka 28, ukitaja moja kati ya warembo kutoka India basi Sania Mirza huwezi kuacha kumuweka katika list hiyo. Uzuri na urembo wake ni wakuvutia.
Sania-Mirza
Sania Mirza
4- Maria Sharapova ni mrembo wa kirusi na anashika namba 2 katika viwango vya mchezo wa tennis ana umri wa miaka 28, anatajwa kuwa kati ya wanamichezo wanaolipwa nyingi.
Maria-Sharapova-Wallpapers-8-500x281
Maria Sharapova
5-  Caroline Wozniacki ana umri wa miaka 25 raia wa Denmark, ni moaja kati ya wachezaji tennis maarufu sana na amewahi kuiwakilisha nchi yake katika mashindano mbalimbali ikiwemo US Open na Australian Open.
caroline-wozniacki-006 (1)
Caroline Wozniacki
6- Ana Ivanovic ni mrembo kutokea Serbia yupo katika hii list ya wachezaji tennis warembo, ana umri wa miaka 27. Amewahi kutokea mara kadhaa katika magazine za michezo ila mwaka 2013 alikuwa katika list ya wasichana 100 warembo.
ana-ivanovic-the-tennis-superstar-who-never-was-is-on-fire-at-the-australian-open
Ana Ivanovic
7- Agnieszka Radwańska aliwahi kushika namba 2 mwaka 2012 katika viwango vya mchezo wa tennis, ameshiriki na kufika katika hatua ya nusu fainali katika michuano tofauti tofauti. ana umri wa miaka 26 anatokea Poland.
radwanska
Agnieszka Radwańska
8- Victoria Azarenka ni mrembo mwenye umri wa miaka 26 anatokea Belarus nae yupo katika hii list ya wachezaji tennis warembo, amewahi kushinda taji la Australian Open lakini alikuwa namba moja katika viwango vya wachezaji tennis kwa mwaka 2012.
725648-victoria-azarenka
Victoria Azarenka
9- Simona Halep kutokea Romania ana umri wa miaka 23 ni moja kati ya wachezaji tennis mahiri, mwaka 2014 alikuwa namba 10 ya katika viwango vya ubora wa wachezaji tennis.
312106-simona-halep-trophy
Simona Halep
10- Garbiñe Muguruza ni moja kati ya wachezaji tennis wanaochipukia Hispania, amefanikiwa kuingia katika top 10 ya viwango vya wachezaji tennis wa kike, umri wake ni miaka 21
garbine-muguruza-jugara-con-espana-1413543986280
Garbiñe Muguruza

Wednesday, October 7, 2015

Haya ndio maneno ya Rihanna kuhusu Chris Brown sasa hivi…

Siku chache zilizopita Rihanna alifanya interview na gazeti la Vanity Fair, la Marekani na kuzungumza vitu vingi ikiwemo mahusiano yake ya zamani na R&B superstaa Chris Brown.
riri4
Rihanna kwenye cover la Vanity Fair Magazine mwezi huu.
Baada ya kujibu maswali mengine yote, maswali juu ya yeye na aliewahi kuwa mpenzi wake Chris Brown yalifuata… kwenye kuzungumza Rihanna alisema kuwa licha ya yote yaliokuwa yanatokea kati yake na Chris Brown staa huyo bado alikuwa anajaribu kulinda hisia alizokuwa nazo juu yake lakini sasa hivi hana uhusiano wa aina wowote ule na Chris Brown ila bado anamjali sana staa huyo…
riri3
Rihanna: (VF Photo Shoot)
>>> “Nilikuwa najaribu sana kumlinda Chris, yeye pamoja na hisia zangu juu yake… mara nyingi nilikuwa nahisi watu hawamuelewi, hata baada ya ile issue kutokea na watu kuongea… lakini unajua inakuwa ngumu ya wewe kuona picha halisi ya mtu na jinsi mambo yalivyo kama bado umekumbatia baadhi ya vitu fulani, haswa ukiwa bado unahitaji the best kutoka kwa mtu husika, na ukiwakumbusha makosa yao, au ukiyakumbuka yale matukio yaliokuumiza maishani, au hata ukijaribu kuonyesha kuwa upo tayari kuvumilia kitu au mtu, wataishia kukufikiria vibaya na kukushusha hadhi...<<< Rihanna.
riri2
Rihanna: (VF Photo Shoot).
>>> “… na ukijaribu kuvumilia, labda kwasababu unajaribu kujiridhisha kuwa pengine hiki ndicho [unachokistahili na kukihitaji] sasa hapo ndipo unapoanza kugundua kuwa ‘mmmh’ nilikuwa mjinga kuamini kitu hiki kinanifaa. Sometimes maamuzi sahihi na salama ni kuachana na hicho kitu… simchukii, namjali sana na nitaendelea kumjali mpaka siku nitakayokufa… ila tu mimi na Chris sio marafiki na sio kwamba mimi na yeye ni maadui pia. Imetokea tu hatuna uhusiano wowote sasahivi.” <<< Rihanna.

Mastaa wa tennis duniani nao wanamiliki hii mijengo ya kifahari…Pichaz

Mchezo Tennis ni miongoni mwa michezo inayopendwa sana hasa kwa nchi zilizoendelea ukiachana na mpira wa miguu..
Kuna mastaa wengi wamefanikia kwa kiasi kikubwa kupitia mchezo huo ambapo mbali ya utajiri mkubwa walionao kupitia mishahara na makampuni wanayotangaza, pia wamewekeza zaidi katika majumba ya kifahari kama walivyo wachezaji wa soka na wengine.
Hii ni mijengo ya baadhi ya mastaa wa mchezo wa Tennis

hous2
Hii ni nyumba ya Roger Federer ipo Switzerland

hoous3
Mjengo wa Andre Agassi upo katika mji wa Tiburon, Carlifonia

Exterior of Cromlix House near Dunblane
Andy Murrary anaishi hapa

hserena
Nyumba ya Serena na Venus Williams ipo West Palm Beach, Florida

house nadal
Hii ndio nyumba anayomiliki Rafael Nadal

house maria
Mjengo wa Maria Sharapova ipo Carlifonia

hous9
Mjengo anaomiliki Anna Kournikova ipo Miami

noma
Mjengo wa Novak Djokovic ipo Ujerumani

pt
Nyumba ya Pete Sampras

Wednesday, September 30, 2015

Hizi ni safari ndefu zaidi za Ndege Duniani, unakaa mpaka saa 17 angani mtu wangu.. (+Pichaz)

Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16 ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo inafanywa na Ndege za Emirates… umbali toka Dubai mpaka Panama ni Kilometa 13, 820.
emirates (1)2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka Dallas Marekani mpaka Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg– Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
60966325
4. Los Angeles mpaka Dubai– Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili, basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu !!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50 mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai– Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili, safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na Dakika 10… Ndege za Emirates zinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong– Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlines zimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
American_Airlines_Boeing_777-200ER_N775AN_PVG_2013-5-21
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.

Selfie nyingine iliyosababisha kifo cha mwanafunzi huyu.

Bado matukio ya watu kupoteza maisha kutokana na upigaji wa picha za Selfie yameendelea kuripotiwa kila siku.
Hii nyingine ni mwendelezo wa matukio hayo ambapo huko Russia kuna mwanafunzi mmoja kawachukua marafiki zake na kutaka wamsindikize kwenda kupiga selfie ya kipekee kwenye moja ya majengo marefu nchini humo.
Walipofika mwanafunzi huyo akapanda juu ya jengo hilo lenye gorofa tisa na akaanza kupiga picha ili atimize lengo lake la kupiga selfie ya kipekee.
selfie
Sekunde chache baadaye aliteleza na kudondoka chini ambapo alikimbizwa hospitali akiwa na majeraha makubwa na baada ya masaa mawili kupita alifariki dunia.
selfie3

Chris Brown anajutia makosa yake baada ya kuzuiwa kuingia Australia? Kayaandika haya.

Kesi ya Chris Brown kumpiga mpenzi wake wa zamani itabakia kuwa moja ya makosa ambayo Chris Brown anajutia sana kuyafanya… story ambayo iligusa Vichwa vya Habari kwenye Entertainment ikiwa na jina la staa Chris Brown siku chache zilizopita ilikuwa ishu ya Chris kuzuiwa kuingia Australia December 2015 kwa ajili ya kupiga show.
Maombi ya Viza yalikataliwa huku wanaharakati wakionekana kuchochea zaidi Chris azuiwe, hiyo yote ilitokana na hatia aliyokutwa nayo Chris baada ya kumpiga Rihanna miaka zaidi ya mitano iliyopita ..!!
231020130803484502293
Chris kaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba yeye sio yule mtu mkorofi tena, kingine amesema anakubali makosa yake na anaamini makosa yake ingekuwa ni kitu ambacho wengine wangejifunza kupitia kwake…
Chris II Chris
Chris III

Hii ndio adhabu aliyoipata Juma Nyoso baada ya kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji John Bocco

Jioni ya September 27 ilikuwa ni siku ambayo wadau wengi wa soka walikuwa wakijadili kuhusiana na tukio la kidhalilishaji, lilitokea katika mechi ya Azam FC dhidi ya Mbeya City, mechi ambayo ilipigwa katika uwanja wa nyumbani wa Azam FC Azam Complex Mbande Chamazi.
Tukio lililotokea katika mechi hiyo ambalo kila mpenda soka Tanzania hakulipenda ni beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City Juma Nyoso kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, baada ya tukio kufanyika kila mtu aliongea lake ila Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alithibitisha kupitia account yake rasmi ya twitter kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya Juma Nyoso.
DSC_0104
Juma Nyoso wa Mbeya City akimdhibiti John Bocco katika mechi ambayo ilimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1
Taarifa mpya kutoka katika kamati ya uendeshaji wa Ligi, zinaeleza kukaa chini na kupitia kosa la Juma Nyoso na kuamua kumpa adhabu ya kumfungia kucheza soka katika kipindi cha miaka miwili pamoja na faini ya milioni 2. Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo kutokana na Juma Nyoso kuwa mkosefu sugu wa kitendo hicho cha kidhalilishaji katika mchezo wa soka.
DSC_0107
Hii sio mara ya kwanza kwa Juma Nyoso kufanya tukio kama hilo, kwani alishawahi kufungiwa mechi nane kwa tukio kama hilo, baada ya kumfanyia mshambuliaji wa zamani wa Simba Elias Maguli, hayo ndio matukio ambayo Nyoso amewahi kukamatwa na kuadhibiwa nayo ila September 28 beki wa zamani wa Yanga Amir Maftah amekiri kuwahi kufanyiwa kitendo hicho na Juma Nyoso na yeye kupatwa na hasira na kumpiga kichwa katika mechi dhidi ya Simba, tukio ambalo lilisababisha Amir Maftah kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kama wewe ni mtumiaji wa Twitter basi mpango huu ukufikie!

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mtandao wa Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kutweet kwa Tweet moja… kwa sasa Twitter inamruhusu mtumiaji kutumia uwingi wa maneno 140 tu kutweet message moja lakini kwa wale ambao wanapenda kuchat kwa marefu, Twitter iliamua kongeza idadi ya maneno kufikia 10,000 kwa private messages… je tutegemee mabadiliko yoyote hivi karibuni?
TWEET2
Nimekutana na habari muda huu ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu… inasemekana kuwa Twitter ipo kwenye mpango wa kuongeza idadi ya maneno ambayo mtu anaweza kuandika kwa Tweet moja na kwa mujibu wa mtandao wa http://www.complex.com Twitter ina mpango wakuleta huduma itakayowaruhusu watumiaji wake kutweet ama kuandika Tweets/post zenye maneno zaidi ya 140!
TWWET6
Baadhi ya mitandao kama Re/Code  wa Marekani wanaamini kuwa maamuzi haya yamesukumwa na mabadiliko ya idadi ya maneno ya kutumia kwenye private messages za Twitter>>> “watu wamepokea vizuri ongezeko la maneno ya Twitter kwenye message za private, hii inaonyesha jinsi gani ambavyo bado kampuni ina nafasi ya kukua zaidi ya hapa…” <<< mmoja ya wafanyakazi wa Twitter aliuambia mtandao wa Re/Code.
Je Twitter itaweza kukuza biashara yake katika ushindani wa Teknolojia na mitandao ya kijamii safari hii? Kama ilikuwa haijakufikia basi ichukue hiyo mtu wangu na pengine tutegemee kufaidika very soon na mpango huu!

Monday, September 28, 2015

Mwaka mmoja tangu kupotea wanafunzi Mexico, msimamo wa wazazi ni huu..Serikali je?

Tarehe kama ya leo Mexico iliingia kwenye headlines baada ya kuwepo na taarifa ya kupotea kwa wanafunzi 43 katika mji wa Iguala Kusini mwa nchi hiyo.
Demonstrators take part in a march to mark the first anniversary of the disappearance of the 43 students from Mexico's Ayotzinapa College Raul Isidro Burgos, in Mexico City, September 26, 2015. REUTERS/Ginnette Riquelme
Pamoja na kuwepo utata wa kupotea kwa wanafunzi hao huku ndugu wa wanafunzi hao wakigoma kupokea taarifa ya Serikali iliyotolewa baada ya uchunguzi uliodai wanafunzi hao walitekwa na kuuawa na kundi la kigaidi.
MEXICO2
Maelfu ya ndugu na jamaa wa wanafunzi hao wakiandamaa nchini humo
Ripoti hiyo haijakataliwa tu na ndugu wa wanafunzi hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi la wataalamu wa uchunguzi hivi karibuni ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.
Ndugu wa wanafunzi hao wamesisitiza kuwa hawataacha kuandamana hadi pale watakapojua ukweli juu ya ndugu zao hao.
MEXICO3
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.