TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, November 20, 2014

MEMBE AFUNGUA MKUTANO KUHUSU SAYANSI YA JAMII


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi wa   Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano  huo ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani  chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka  Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.

Mhe. Membe akikaribishwa na Prof. Florence Luoga ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii  ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo.(Martha Magessa)
JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii.
<

Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi huku wajumbe wakimsikiliza.
 
Sehemu ya wajumbe wakifurahia jambo wakati Mhe. Membe (hayupo pichani) akitoa hatuba ya ufunguzi.
Mhe. Membe akisindikizwa kwenda kupiga picha ya pamoja na Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwepo kwenye mkutano huo
Mhe. Membe (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano kuhusu masuala
Waziri Membe akifurahia jambo na mmoja wa Wajumbe wanaoshiriki mkutano huo.
Mhe. Membe akihojiwa na Wanahabari kuhusu mkutano huo. Picha na Reuben Mchome

Ukawa wafichua njama za kuizima IPTL bungeni 

James Mbatia.
Wakati kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikianza kupitia ripoti ya IPTL kuhusu uchunguzi wa ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow, wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umedai kwamba kuna mikakati imeandaliwa kuzima ripoti hiyo kusomwa na kujadiliwa bungeni.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema jana kwamba moja ya mikakati hiyo ni madai ya kuwapo barua ya Mahakama kuzuia mjadala huo akisema mkakati huo unatokana na ukubwa wa kashfa na jinsi inavyowahusisha viongozi waandamizi serikalini.
Mbatia aliyeambatana na kundi kubwa la wabunge kutoka Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, alisema: "Iko mikakati na mbinu za kila aina kulihujumu Bunge lisisimamie fedha za walipakodi, ndiyo maana kuna danadana na tuna taarifa za kuwapo barua kutoka mahakamani kuzuia jambo hilo lisijadiliwe bungeni kwa madai eti kuna kesi.(P.T)
"Mahakama haiwezi kuingilia shughuli za Bunge, inatia wasiwasi kwa kuwa Ofisi ya Bunge nayo imekuwa na danadana kila siku kwa kubadilisha badilisha ratiba wakati sisi tunataka hawa waliohusika kwenye kashfa hii wachukuliwe hatua."
Pia, alisema kuna taarifa kwamba Serikali inadai haina fedha, ikitaka kufupisha Bunge na suala hilo lisijadiliwe sasa hivi.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Mnyaa alisema: "Serikali inategesha tegesha tu mambo bungeni na ndiyo maana leo (jana) wameahirisha Bunge hadi kesho (leo) bila sababu za msingi, wanafinya muda wa sisi kujadili sakata hili," alisema Mnyaa.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu alisema escrow ni kama ilivyokuwa kashfa ya Richmond ambayo iliwang'oa wahusika wakuu bungeni, hivyo haiwezekani isijadiliwe bungeni kwa madai kwamba Mahakama imezuia...
"Hakuna utaratibu kama huo wa Mahakama kuelekeza Bunge kitu gani kifanyike na gani kisifanyike pia hata Katiba hairuhusu hilo."
Lissu alishangazwa na Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha Bunge jana hadi leo kwa madai kuwa yeye (Lissu) alikuwa hajakamilisha taarifa ya upinzani kwenye muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2014 akidai kuwa huo ni upotezaji wa muda.
"Nilimwomba Naibu Spika kuwa aahirishe muswada huo hadi kesho kwa kuwa ulikuwa umepangwa tarehe 25 lakini ghafla ukabadilishwa na mimi sikuwapo kwa muda wote huo. Sikuomba aahirishe Bunge nilimwomba aahirishe muswada tu," alisema Lissu.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema naye amesikia kuwapo barua ya Mahakama kuzuia mjadala huo na kusema kama ni kweli, halitakuwa sahihi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Operesheni Delete CCM mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema si Waziri Mkuu wala Jaji Mkuu anayeweza kuuzima mjadala wa escrow bungeni.
Alisema kashfa hiyo ambayo chama chake kina nyaraka zake na ripoti za uchunguzi wa escrow na Takukuru, lilianzia bungeni na lazima lijadiliwe na kumalizikia bungeni.
Ndugai ajibu hoja
Akizungumzia madai hayo, Ndugai alisema hajui kama kuna barua kutoka mahakamani kuzuia mjadala wa escrow bungeni na suala hilo litawasilishwa na PAC bungeni Novemba 27 kama ilivyopangwa.
"Waiamini kamati, kwanza hawa wa upinzani ni yao (kamati) haiongozwi na CCM, mimi naamini kamati itafanya kazi nzuri. Sidhani kama kanuni zinaruhusu kugawa ripoti hiyo kwa kuwa ni siri, kanuni hairuhusu."
Rejea
Ripoti ya Tegeta Escrow inatokana na uchunguzi maalumu wa Sh306 milioni zilizochotwa katika akaunti ya escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Fedha hizo zilitokana na gharama za uwekezaji zilizokuwa zinalipwa na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina ya wabia hao.
Tanesco ililalamika kuwa ilikuwa inailipa zaidi IPTL kinyume na gharama halisi za uwekezaji, hivyo kuamuliwa na Mahakama kuwa fedha hizo ziwekwe katika escrow hadi upatikane ufumbuzi wa mgogoro huo lakini zikachukuliwa kabla kesi kuamuliwa.
Chanzo:Mwananchi

Fainali za Caf 2015: Timu 15 zafuzu 

Africa Cup of Nations trophy
Matumaini ya eneo la Afrika Mashariki kuwa na timu angalau moja katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea mwaka 2015, yameyeyuka baada ya mwakilishi pekee wa eneo hilo timu ya Uganda kucharazwa na Guinea mabao 2-0 katika mchezo wa kundi E uliofanyika mjini Casablanca, Morocco, Jumatano.
Uganda iliyokuwa na pointi 7 kama Guinea ilitakiwa kushinda mchezo huo. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 11. Katika kundi hilo Ghana imeicharaza Togo 3-1. Timu za Uganda na Togo zimeaga michuano hiyo.
Mabingwa wa zamani wa michuano hiyo kwa mwaka 1968 na 1974, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(Zaire), imefanikiwa kutinga katika michuano ya mataifa ya Afrika mwakani kwa kuwa na wingi wa pointi kati ya timu zote zilizoshika nafasi ya tatu katika makundi yote nane. DR Congo imeibuka na pointi 9.
Mabingwa watetezi Nigeria imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kutoka sare na Afrika Kusini kwa kufungana mabao 2-2. Nigeria imebaki na pointi 8.
Timu zilizofuzu kutoka kila kundi ni kama ifuatavyo:
Kundi A: Afrika Kusini yenye pointi 12 na Congo pointi 10. Nigeria na Sudan zimetupwa nje.
Kundi B: Algeria na Mali zimesonga mbele kwa alama 15 na 9 kama zinavyofuatana, huku Angola na Lesotho zikifungasha virago.
Kundi C: Gabon na Burkina Faso zimetinga hatua ya fainali kwa kujikusanyia alama 12 na 11 kama zinavyofuatana.
Kundi D: Cameroon, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zina pointi 14, 10 na 9 kama zilivyoongozana. Sierra Leone imetupwa nje.
Kundi E: Ghana na Guinea kwa alama 11 na 10. Uganda na Togo zimeyaaga mashindano hayo.
Kundi F: Cape Verde na Zambia zenye pointi 12 na 11 zikiziacha timu za Msumbiji na Niger.
Kundi G: Senegal na Tunisia zina pointi 13 na 14. Misri na Botswana zimeshindwa kufuzu, pale zilipoambulia pointi 6 na 1 kama zinavyofuatana.
Fainali hizi za Kombe la Mataifa ya Afrika zinafanyika nchini Equatorial Guinea ambayo nayo imepewa nafasi kutokana na kuwa nchi mwenyeji wa michuano, baada ya Morocco iliyokuwa imepewa nafasi ya kuandaa kutaka michuano hiyo kuahirishwa kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola ambao umeziathiri nchi za Afrika Magharibi, hususan Liberia, Sierra Leone na Guinea.
Vigogo wa soka barani Afrika, Nigeria na Misri hazitaonekana katika fainali hizo. BBC

Ujerumani haioni matumaini katika mzozo wa Ukraine 

Steinmeier und Lawrow in Moskau 18.11.2014
Frank Walter Steinmeier (kushoto) na Sergei Lavrov mjini Moscow
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier alisema Jumanne (18.11.2014) haoni sababu za kuwa na matumaini kuhusu mzozo unaoendelea Ukraine kutokana na machafuko kuongezeka mashariki mwa nchi hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov hapo jana, Steinmeir alionya kuhusu hali ya kutisha inayoendelea nchini Ukraine. Alizitolea mwito pande zote zinazohusika katika mzozo wa Ukraine kuuheshimu mkataba wa makubaliano uliofikiwa katika mkutano wa mjini Minsk nchini Belarus uliofanyika Septemba 5 mwaka huu ambao kwa kiwango kikubwa unaonekana kusuasua.(P.T)
Steinmeier alisema itakuwa hasara kubwa kuachana na mkataba huo ambao umefaulu kusitisha mapigano mengi, lakini umeshindwa kuepusha kuzuka machafuko ya hapa na pale katika maeneo muhimu. "Hata kama tuna shaka kama mkataba unafanya kazi katika kila kipengele, hata kama tutaripoti vipengele muhimu vimekiukwa katika wiki zilizopita, itakuwa hasara kubwa kuukataa mkataba huu. Lazima tufanye juhudi kujaribu kutafuta kilichokwenda kombo baada ya mkataba kusainiwa ili tuendeleze kazi ya kuvitekeleza vipengele hivyo."
Steinmeier alikwenda Moscow akitokea Kiev ambako alikutana na waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk. Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani alitaka kwa haraka kuwekwe eneo lisiloruhusiwa mapigano kati ya majeshi ya serikali ya Ukraine na waasi wanaoegemea Urusi mashariki mwa Ukraine kuuokoa mkataba wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov aliunga mkono mwito wa Steinmeier na kusisitiza umuhimu wa kuutekeleza kikamilifu mkataba wa Minsk. "Lengo kuu ni kuzuia mzozo wa kijeshi kusini mashariki mwa Ukraine, kuweka eneo la kuzitenganisha pande mbili na kuondoa silaha nzito. Lakini tutatafakari njia za kuleta uthabiti wa muda mrefu Ukraine bila kusahau umoja wa taifa, maelewano na maridhiano. Na hatupaswi kuyasahau mageuzi ya katiba yaliyosainiwa na Ukraine mjini Geneva Aprili 17."
Misimamo tofauti yajitokeza
Tofauti zilijitokeza kati ya Steinmeier na Lavrov katika mkutano na waandishi wa habari huku wote wakionekana kutotulia mara kadhaa. Ingawa viongozi wote walisisitiza umuhimu wa mkataba wa Minsk, Lavrov alisema mdahalo kati ya pande zinazohasimiana Ukraine unapaswa kuzingatia uchaguzi wa Novemba 2 ulioandaliwa na waasi katika maeneo wanayoyadhibiti katika hatua ya kukaidi uchaguzi wa bunge uliofanyika siku chache kabla.
Lavrov alisema hakuna mbadala wa ushirikiano kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya akiongeza kuwa Urusi haipaswi kulaumiwa kwa mahusiano mabovu na umoja huo kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.
Steinmeier alikutana pia na rais wa Urusi, Vladimir Putin, lakini ikulu ya Kremlin haikutoa maelezo yoyote kuhusu mazungumzo kati ya viongozi hao. Waziri Steinmeier ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka Ulaya kuzuru Moscow tangu mwezi Julai mwaka huu, katika ishara inayoonyesha namna gani uhusiano kati ya mataifa ya magharibi na Urusi ulivyovurugika tangu kumalizika kwa vita baridi kutokana na mzozo mashariki mwa Ukraine.
Mwandishi:Josephat Charo/AFPE/RTRE
Mhariri:Daniel Gakuba
Chanzo:DW

Taarifa nyingine kuhusu Cosby baada ya kukabiliwa na tuhuma za kubaka

 images ii Kwa zaidi ya wiki moja sasa kama umekuwa mfuatiliaji wa vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa kumekuwa na taarifa kuhusu tuhuma za kubaka zinazomkabili mchekeshaji wa Marekani, Mzee Bill Cosby.

Kituo cha NBS ambacho kilikuwa kikifanya kazi na mzee huyo, kimesitisha kuirusha show yake kutokana na tuhuma hizo zinazomkabili kwa mujibu wa msemaji wa kituo hicho, Rebecca Marks.
Tuhuma hizo zilitolewa na mwanamitindo ambaye pia ni mtangazaji wa Televisheni, Janice Dickinson ambaye amesema mwaka 1982 Cosby alimnywesha pombe kabla ya kumfanyia kitendo hicho.
Mwanamke huyo amesema alishindwa kuripoti Polisi baada ya kufanyiwa kitendo hicho kwa kuwa alihisi hakuna ambaye angeweza kumuamini.
Mwanasheria wa Cosby amepinga madai hayo japo Cosby  mwenyewe hajazungumzia lolote mpaka sasa.

Kauli ya Raisi wa Simba kuhusu usajili wa Mnigeria Emeh Izechukwu

IMG_8912.JPG
Siku chache baada ya dirisha la usajili kufunguliwa kumekuwepo na tetesi za usajili kumhusu mshambuliaji wa kinigeria Emeh Izuchukwu kurudi Msimbazi.
Lakini Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba hawana nafasi ya kusajili ya mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel Okwi, Amisi Tambwe na Paul Kiongera wanawatosha.
Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo vya habari vimekuwa vikiwahusisha washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na Mganda Danny
Sserunkuma kusajiliwa na Simba.
Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni mchezaji wao wa zamani, ameomba mwenyewe kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika hawana nafasi ya mchezaji
wa kigeni.
“Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba hatujazungumza nao,”amesema Aveva

Good news nyingine, inahusu miundombinu za usafiri Tz

Behewa
Good news Tz zinaendelea kusikika, kila mmoja ni mtumiaji wa vyombo vya usafiri lakini baadhi ya kero ambazo tumekuwa tunakutana nazo ni kama vile foleni, uchakavu wa vyombo vyenyewe, na miundombinu duni.
Katika taarifa ya kituo cha ITV, kuna taarifa ya kuhusu kuwasili kwa mabehewa mapya 50 ya treni, akizungumza wakati wa kuwasili mabehewa hayo Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi amesema; “…Rai yangu kubwa kwa Watanzania na wafanyakazi TRL, mali hizi zinazoletwa ni za kwetu tuwe watu wa pamoja kulinda mali hizi kwa namna moja au namna nyingine. Kila Mtanzania Reli inakopita awe ni mmoja wa kushiriki katika ulinzi wa Reli hii kwa sababu tunaamini kabisa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Reli ambao umeanza sasa hivi unatupeleka katika matokeo makubwa ambao faida yake itapatikana kwa Tanzania wakulima kwa kusafirisha mizigo…”– Shaban Mwinjaka
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRL amesema; “… Leo kuna hizi behewa 50 baada ya muda mfupi katika mwezi huu unaokuja wa Desemba kutakuwa na behewa 50 zingine kati ya hizo 274, mwezi huo huo Desemba kuna 50 zingine, mapema mwakani kuna behewa 174… baadaye kutakuwa na Locomotive mpya na kadhalika. Kuna miradi kama 12 ambayo TRL inatekeleza sasa hivi katika program ya BRN, hizi behewa 274 ni sehemu tu lakini kuna Locomotive mpya, mabehewa ya abiria mapya ambayo nayo mwanzoni mwa Desemba yatafika tutakutana, tutayaona…”–Mhandisi Kipalo Kisamfu

Wednesday, November 19, 2014

Louis van Gaal kayatoa ya moyoni…. anataka nani ashinde Ballon d’Or 2014? Ronaldo na Messi je?

Screen Shot 2014-11-20 at 3.53.45 AM
Wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2014 walishatangazwa ambapo list hiyo pia inawahusisha mastaa wa soka kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, huku list hiyo ikiwa pia na wachezaji wa Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Baada ya ushindi wa Ronaldo na Messi kuchukua headlines sana kocha wa Manchester United Louis van Gaal (63) ameamua kuyatoa ya moyoni na kusema mwaka huu Ronaldo na Messi hawatakiwi kuchukua hiyo tuzo bali ni halali ikachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani.
Wajerumani wanaowania tuzo hiyo ni Mario Gotze, Toni Kroos, Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger.
Screen Shot 2014-11-20 at 4.04.25 AMAnasema ‘Naamini Ujerumani inafaa kuchukua hii tuzo, mara nyingi imekua tu ni wachezaji maarufu/wanaofahamika ndio wanashinda hii tuzo, kitu kikubwa kushinda ni kombe la dunia ndio maana naamini itachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani sababu kiukweli wanastahili
Screen Shot 2014-11-20 at 3.50.45 AM
Umeonaje mawazo ya Van Gaal? ungependa nani ashinde Ballon d’Or ya 2014 mtu wangu? naomba niachie maoni yako kwenye comment hapa chini.

Unamjua mtaalamu wa IT mwenye umri mdogo kuliko wote Duniani?

Ayan Qureshi.
Ayan Qureshi.
Wazazi wengi Afrika wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba na vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri mdogo zaidi duniani.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.

Umesikia kuhusu meno ya tembo yaliyopotea mikononi wa Serikali?

satao-killed-ivory-poaching-attack-kenya
Kuhusu vita dhidi ya biashara haramu ya meno ya tembo, mataifa mbalimbali yamekuwa yakikemea biashara hiyo lakini bado wapo watu ambao wameendelea kuifanya.
Maafisa Wanyamapori watano wamesimamishwa kazi ili kupisha upelelezi kufanyika kufuatia kupotea kwa meno ya tembo kwenye mazingira ya kutatanisha yakiwa katika sehemu ya ulinzi mkali wa Serikali, Uganda.
Akizungumza na AFP mkurugenzi wa Uganda Wildlife Authority, Raymond Engena amesema wameomba msaada wa Kikosi cha Askari wa Kimataifa (Interpol) kufanya upelelezi kufuatia agizo la Rais Museveni la kutaka wahusika wote kukamatwa kutokana na upotevu huo.
Meno hayo yana uzito wa kilo 1,335 yana thamani ya Dola Mil. 1.1 za Uganda ambapo imesemekana baadhi ya maofisa hao wamekuwa wakiyachukua meno hayo kwa ajili ya kutumia kuwatega wafanyabiashara wa meno hayo lakini hawayarudishi baada ya kuyafanyia kazi hiyo.
china-ifaw-ivory-01
Ripoti zinaonyesha idadi ya tembo 35,000 wamekuwa wakiuawa Afrika kila mwaka kutokana na biashara hiyo kuonekana kuwa na soko kubwa nchi za Asia.

Baada ya Mabasi ya Mwendokasi, Kivuko cha Mv. Dar, hii ni nyingine kuhusu usafiri Dar

 MagufuliBaada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “… Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya South Korea imekubali kutufadhili kujenga flyover nyingine pale.. na barabara yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita 7.2 na barabara itaanzia Coco Beach, itapita baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital na kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli Hassan Mwinyi…
“.. Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna mradi wa BRT ambao una-involve kilometa zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi unaisha chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic count ya magari yanayopita pale kwa siku yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja elfu kwa hiyo hawawezi wakaya-accommodate magari yote yanayoweza kupita sehemu hiyo…”– Dk. Magufuli

Monday, November 17, 2014

Ndio utajiuliza ilikuaje mpaka jamaa akaiba gari la Polisi kwenye mazingira haya.

Police car
Wakati flani nilipoitembelea Afrika Kusini niliambiwa na mwenyeji wangu kwamba wizi wa magari unafanyika hata barabarani, unaweza ukawa umesimama kwenye mataa ukisubiri uruhusiwe lakini ghafla watakuja majambazi na silaha wanazuziba kwa mbele kisha wanachukua gari na kuondoka nalo.
So inaelekea wizi wa magari unaweza kuwa ‘kipaji’ kwa hawa ndugu zetu wa Afrika Kusini manake kuna kijana mmoja wa miaka 19 huko Northern Cape alifanya kitendo cha kujiamini zaidi pale alipoiba gari la Polisi, yaani ingekua ni gari binafsi linalomilikiwa na askari ingekua afadhali ila hili aliloiba ni gari la Polisi kabisa na nembo zake.
police 4
Ishu imetokea Jumamosi ya November 15 2014 na unaambiwa Polisi walianza kumsaka mtu huyu na kufanikiwa kumpata baadae yeye pamoja na gari ambapo baada ya kukamatwa alikua anatarajiwa kufikishwa Mahakamani Jumatatu ya November 17 2014.
Ilikuaje mpaka akafanikiwa kuliiba? ……alipata hiyo nafasi baada ya Polisi kwenda kwenye eneo la tukio kulikotokea ajali kwa hiyo baada ya Polisi wote kushuka huku funguo za gari zikiwa zimeachwa sehemu yake ndio jamaa akapiga gia.
police 2

Sasa hivi kivuko sio Kigamboni tu hata Dar – Bagamoyo wameletewa hiki kipya.

unnamed (14)
Foleni za Dar es salaam na matatizo yake imekua sio stori mpya tena ila ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka pamoja na hiki kivuko ndio habari ya mjini ambapo leo kuna stori imetoka ikiwa ni good news kuhusu hiki kivuko kipya.
Kwenye Blog ya issamichuzi.blogspot.com kuna taarifa kuhusu kutua kwa kivuko cha Mv. Dar es Salaam ambacho kitakuwa kinafanya safari kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama inavyoonekana kwenye hizi picha.
Waziri wa Ujenzi John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wakisubiri kivuko hicho kushushwa bandarini Dar.
Waziri wa Ujenzi John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wakisubiri kivuko hicho kuwasili bandarini Dar.
Kivuko cha Mv Dar es Salaam kikiwasili Dar leo Novemba 17.
Kivuko cha Mv Dar es Salaam kikiwasili Dar leo Novemba 17.
Kivuko III
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri Magufuli wakipewa maelekezo na Injinia Japhet Masele.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri Magufuli wakipewa maelekezo na Injinia Japhet Masele.

Wabunge walipoingilia kati Wasichana wanaovaa nguo fupi kuchaniwa mavazi hadharani.

Woman 1
Kutoka Kenya kikubwa kilichotawala mitandao na vyombo vya habari kwa mfululizo tangu wiki iliyopita ni kuhusu tukio la wanaume kuwachania nguo hadharani wanawake ambao wanawatuhumu kuvaa vibaya, leo katika taarifa ya habari kituo cha Citizen TV imeripotiwa taarifa kuhusu mwendelezo wa habari inayohusiana na tukio hilo.
Dress Kenya
photo (1)
Wabunge wamekuwa watu ambao mara nyingi tumezoea kuwaona wakitetea maslahi ya watu wanaowaongoza, leo kwenye taarifa ya kituo hicho Wabunge wanawake Kenya pamoja na wanawake wengine wameandamana kulaani kitendo kinachofanywa na wanaume hao kuwachania nguo wasichana.
…Sisi kama jamii lazima tuwe tunatetea haki za akina mama, au haki za kila mmoja, uwe mwanaume uwe mwanamke.. Kitendo cha kumvua mwanamke nguo sijui niseme ni hujuma au niseme vipi.. Kwa sababu kama tutaendelea kuwa hivyo tutakuwa kama India, India walianza hivyo hivyo.. Kisha wakaanza ‘kuwa-rape’ akina mama..
“… Kati ya wanawake watatu at least mmoja amedhulumiwa na mwanaume lakini hawazungumzi, na hata wakizungumza wanafikiri hawatasikilizwa.. Kwa hivyo leo hii niko hapa kuwaambia hao wanaume kwamba mtashikwa na mtachukuliwa hatua…
Kwa upande wa wanaume ambao wanawafanyia vitendo hivyo wasichana wamesema haya; “… Tunapinga nguo fupi maana yake kinyume.. Maadili ya Waafrika ni kwamba avae kinadhifu.. Halafu dini zote hakuna dini inayokubali mwanamke avae nguo fupi ama mini-skirt fupi…
Kampeni ya kulaani kitendo hicho imepewa  jina la My Dress My Choice.
Hizi ni baadhi ya picha zilizowekwa na Standard Digital zikionyesha maandamano hayo.
Dress III
Dress IV
Dress V

Unajua sala aliyoifanya Mike Sonko pamoja na ujumbe alioutoa kwa wanaowachania nguo wasichana?

Sonko 
Jina la Mbunge wa Jimbo la Makadara Kenya, Mike Sonko sio jina geni, wengi tunamfahamu kutokana na vitu vingi ambavyo amekuwa akifanya ikiwa ni pamoja na aina ya maisha anayoishi na amekuwa akisifiwa kutokana na namna ambavyo amekuwa akiwajibika kwa wananchi wake anaowaongoza.
Stori kutoka Kenya ambayo imetawala vyombo vingi vya habari ni kuhusiana tukio la msichana kuchaniwa nguo na wanaume hadharani kutokana na kuvaa vibaya.
Ujumbe aliouandika Sonko kutokana na tukio ulianza na sala hii; “…. Namuomba Mungu awasamehe wanaume wanaowachania nguo wasichana.. Namuomba awaeleweshe wote kwamba wasichana wa karne ya 21 wako kidijitali sana na tofauti…
…. Namuomba atutawale sote na kuirejesha amani kati ya wanaume hao na wanawake waliochaniwa nguo.. Leta amani kwa wasichana waliochaniwa nguo wakidhania mavazi hayo yanasababisha waaibishwe kwa kujua ama kutokujua…”– Sonko
Sonko II
Baada ya sala hiyo, Sonko alitangaza kutoa zawadi ya fedha kiasi cha shilingi 100,000/= za Kenya kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa wale wote waliohusika kufanya kitendo hicho cha kikatili katika mitaa ya Nairobi.