TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, August 19, 2014

JAJI LEWIS MAKAME AFARIKI DUNIA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Marehemu mwenyekiti mstaafu wa tume ya Uchaguzi JAJI Lewis Makame enzi za  uhai wake alipokuwa amelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame, amefariki dunia katika Hospitali ya Ami Trauma Centre iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Jaji Makame alifariki jana mchana katika hospitali hiyo, alikokuwa amelazwa ambapo pia Rais Jakaya Kikwete, alimtembelea kumjulia hali. Taratibu za mazishi zilikuwa zikiendelea jana nyumbani kwake Masaki.
Historia fupi iliyopatikana, inaonesha kuwa Jaji Makame alikuwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza, ambapo baada ya kufanya mazoezi na kufanya kazi nchini humo, alirejea nchini Tanzania miaka ya 1960 na kutumikia Taifa mpaka alipofikia cheo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Mbali na cheo hicho, Jaji Makame pia alitumikia Taifa katika nafasi ya Mwenyekiti wa NEC na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-ECF).
Wakati akiwa Mwenyekiti wa NEC kwa takribani miaka 19, Jaji Makame aliweka historia ya kusimamia uchaguzi kadhaa wa vyama vingi nchini.
Alistaafu wadhifa huo baada ya mkataba wake kuisha Julai mwaka 2011. Nafasi yake ilichukuliwa na Jaji mstaafu Damian Lubuva.
CHANZO:HABARI LEO.(I.N)

Polisi, albino wapambana Dar 

Kamishna Suleiman Kova
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova
NA SHABANI MATUTU
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), waliokuwa wakizuia gari la polisi lililokuwa limebeba mtuhumiwa wa kutishia kuua albino kwa maneno.
Tukio hilo lilitokea jijini Dar es Salaam jana, ambako albino hao walivamia gari hilo na kuwataka askari polisi wamshushe ndani ya gari mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Ombeni Michael, ili wafahamu alikokuwa akipelekwa.
Vurugu hizo zilianza katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni, ambako albino hao walivamia wakati kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo ikiendelea katika mahakama hiyo.(I.N)
Baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo na dhamana kuwa wazi kwa mujibu wa sheria, watu hao wenye ulemavu waliamsha hasira ya kupinga kupewa dhamana kwa mtuhumiwa huyo.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 3, mwaka huu.
Mwekahazina wa Chama cha Albino Tanzania, Abdillah Omary, alilazimika kuandika barua mahakamani hapo kupinga hatua ya kupewa dhamana kwa mtuhumiwa huyo.
Pamoja na kuandika barua hiyo iliyopokewa na mahakama, ilibainika kuwa na upungufu wa kisheria na kutakiwa kuifanyia marekebisho.
Lakini ghafla mtuhumiwa huyo alipotolewa mahakamani na kuingizwa kwenye gari la polisi, alivamiwa na walalamikaji hao na kuanza kumshambulia.
Baada ya kuona walemavu hao wa ngozi wamewazidi nguvu, askari waliamua kuondoa gari na kuelekea katika kituo cha Buguruni, ambako waliomba msaada na baada ya muda waliwanya kwa mabomu ya machozi.
Akizungumzia kuhusu hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Albino Wilaya ya Temeke, Kasim Kibwe, alisema suala la kuwalinda ni dhahiri Serikali imeshindwa, hivyo kuomba msaada kutoka nje ya nchi.
Alisema hatua hiyo itawasaidia kulindwa wakati wote, kwani matukio ya watu wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa wakiongezeka kila siku.
"Inasikitisha kuona hapa nchini wanyamapori wanalindwa kwa nguvu kubwa kuliko sisi albino ambao ni binadamu, hali inayonifanya nifikirie kuwa mkimbizi nje ya nchi kuliko kuwa raia hapa nchini. Na hivi kuna uhusiano gani wa kuuawa kwa albino inapokaribia kipindi cha uchaguzi mkuu?" alisema Kibwe.
Kwa upande wake, Mwekahazina wa Chama cha Maalbino Taifa, Abdillah Omary, aliwataka albino wenzake kuwa watulivu katika kesi hiyo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Mary Nzuki, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo, huku akisema kuwa hali hiyo imechangiwa na mwili wa mwanamume mmoja aliyedhaniwa ni mlemavu wa ngozi kuokotwa amefariki dunia Tabata Kinyerezi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kamanda Nzuki alisema mwili huo kwa sasa upo katika uchunguzi unaowajumuisha viongozi wa Chama cha Albino Tanzania pamoja na wawakilishi wa Shirika la Under The Same Sun kubaini ukweli, na taarifa baada ya kukamilika zitatolewa wiki ijayo.
Alisema kuwa wakati wa tukio hilo, mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Mwenyeusi Issa (39), alidai kumsikia mtuhumiwa, Ombeni Michael (34) akitoa kauli ya kutishia kuwaua albino, huku akiwa anakunywa pombe baa.
CHANZO:MTANZANIA

 

Uamuzi mgumu CCM katika Kamati Kuu leo

Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM inakutana leo mchana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete huku ikitarajiwa kufanya uamuzi mgumu wa mchakato wa Katiba.
Kikao hicho kinaketi mara ya pili katika muda mfupi, baada ya hivi karibuni kukaa jijini Dar es Salaam na kueleza kuridhishwa na mchakato huo.(I.N)
Hata hivyo, safari hii kikao hicho kinaketi kukiwa na maswali lukuki ambayo hayajapata majibu: Je, Bunge la Katiba liendelee au livunjwe? Je, lisitishwe kwa muda kupisha maridhiano au la? Je, kuna umuhimu wa maridhiano? Kuna ulazima wa kuwapo Ukawa bungeni?
Akizungumzia kikao hicho, mtaalamu wa sayansi ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema jambo kubwa litakalojadiliwa katika kikao hicho ni kauli tofauti zilizotolewa na wananchi kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya.
"Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba ameshauri yafanyike maridhiano kwanza na wapo wanaCCM waliomuunga mkono. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema naye ameonyesha wasiwasi wake, Ukawa na Jukwaa la Katiba Tanzania nao wamesema yao. Nadhani kuna jambo CCM wameliona na wanataka kuliweka sawa," alisema Dk Makulilo.
Aliongeza, "Kujua nini wataamua ni ngumu lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa ni wazi kuwa wanakutana kuona nini kifanyike."
Kwa upande wake Bashiru Ali alisema, "Tangu mwanzo mchakato wa Katiba haukuwa katika ilani ya CCM, sasa unaweza kujiuliza wanakwenda kujadili nini wakati hata katika mikakati yao ya miaka 10 na 20 ijayo hakuna mpango wa kuandika Katiba."
Habari zilizozagaa mjini Dodoma zinadai kikao hicho pia kinaweza kupendekeza kuwashughulikia wanachama wake waliotoa kauli zinazopingana na msimamo wa chama hicho.
Miongoni mwa waliotoa kauli zinazopingana na chama hicho ni Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba kutokana na matamshi yake ya kuhoji uhalali wa vikao vya Bunge la Katiba kuendelea bila uhakika wa akidi.
Mbali na Mwigulu pia wabunge kadhaa wa CCM akiwamo, Esther Bulaya (Viti Maalumu), Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ridhiwani Kikwete (Chalinze) nao wamekaririwa kwa nyakati tofauti wakitoa misimamo inayokinzana na chama chao kuhusu uhalali wa Bunge la Katiba kuendelea bila kuwapo maridhiano na Ukawa.
Hata hivyo, habari nyingine zinasema iwapo kuna mpango huo, Mwigulu anaweza kuondolewa kutokana na utaratibu wa chama hicho kuwaondoa kwenye sekretarieti wajumbe wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa serikalini.
Chanzo chetu kinasema ikiwa hilo litatokea kwa sababu ya Mwigulu kuteuliwa Naibu Waziri wa Fedha, basi mpango huo hautamwacha nyuma Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje, Dk AshaRose Migiro ambaye pia hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba.
CHANZO:MWANACHI

Rais Obama asifu majeshi ya Iraq na kurd 

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga hatua kubwa kulitwaa tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Amesema wamethibitisha kwamba wanauwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya Marekani, ambayo tayari yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo linalokaliwa na wapiganaji wa kiislamu.
Ripoti zinasema kuwa mapambano katika juhudi za kudhibiti maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaendelea.
Katika hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti wa bwawa hilo.
Wakati huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao .
Papa Amesema ni halali kuzuia kile alichokiita dhuluma ya kichokozi. Lakini ametahadharisha kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa lazima ifanyiwe tathmini. kusimamisha na kwamba hakusema. Mwandishi wa BBC MJINI Roma Italia anasema papa Fransis hajaonesha kuunga mkono mashambulio ya anga yanayofanywa hivi sasa na Marekani dhidi ya wapiganaji hao wa kiislamu.

CHELSEA YAANZA LIGI KUU KWA KUIKANDAMIZA BURNLEY 3-1  1408395163253_lc_galleryImage_Chelsea_s_Ivorian_striker

Tembo: Didier Drogba akipiga shuti kujaribu kufunga goli baada ya kuingia katika dakika za lala salama 
MBWATUKAJI Jose Mourinho ameanza ligi kuu England ‘Swafii’ kabisa baada ya kufanikiwa kuingoza ugenini Chelsea kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu mpya ya Burnley.
Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa Scott Arfield,  lakini mshambuliaji mpya wa Chelsea, Diego Costa alifungua akaunti ya mabao katika mechi za ligi kuu baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 17.

Akaunti ya magoli: Diego Costa akifunga bao lake la kwanza la ligi kuu 
 Wakati Burnley wakiwa na matumaini ya kuongeza bao, Mjerumani, Andre Schurrle aliifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika 21 na Branislav Ivanovic akahitimisha karamu ya mabao katika dakika ya 34.
Tatizo kubwa kwa Burnley ni kwamba wachezaji wake hawajawahi kukutana na kitu kama hiki, hivyo kujikuta wakizidiwa maarifa kimbinu na kiufundi.

Hadi beki yumo: Ivanovic akifunga goli la tatu
Mabingiwa hao wa The Championship, mara kwa mara waliambiwa ligi ni ngumu lakini sio ngumu kama hivi leo.(P.T)
Katika mechi ya leo, Didier Drogba alianzia benchi na kucheza mechi ya kwanza tangu arudi Chelsea, lakini alishawahi kucheza mechi ya kwanza kabisa miaka ya nyuma.
Mlinda mlango, Thibaut Courtois naye alimkalisha kwenye ‘gogo; mkongwe Petr Cech.

 Mambo kutoka kwa Mjerumani: Andre Schurrle akiifungia Chelsea bao la pili
 Kikosi cha Burnley: Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Taylor (Kightly 70), Marney, Jones, Arfield, Ings (Sordell 82), Jutkiewicz (Barnes 70).
Wachezaji wa akiba: Wallace, Gilks, Long, Dummigan.
Kadi ya njano: Sordell.
 Kikosi cha Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Schurrle (Willian 78), Oscar (Mikel 82), Hazard (Drogba 84), Costa.
Wachezaji wa akiba: Cech, Luis, Zouma, Torres.
Kadi ya njano: Costa.
Mwamuzi: Michael Oliver (Northumberland)
Chanzo: http://shaffihdauda.com

Polisi walaumiwa kwa mauaji Kenya


Tangu shambulizi la Westgate, harakati za kudhibiti ulinzi zimekuwa zikikosolewa
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limewalaumu polisi wa kupamba na ugaidi nchini Kenya kwa kufanya mauaji ya kiholela.
Human Rights Watch inasema kuwa pia imepata ushahidi wa watu kutoweka kwa lazima, kushikwa bila sababu na kudhulumiwa kwa washukiwa.
Shirika hilo pia linasema kuwa watoa misaada wa kimataifa wanastahili kusitisha misaada yao kwa polisi wa kupambana na na ugaidi kikosi kilichobuniwa baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi mwaka 1998.
CHANZO:BBC

Watu weusi wabaguliwa Korea kusini 


Tangu kuanza kwa ugonjwa wa Ebola kumekuwapo na malalamiko ya watu wanaotoka Barani Afrika kutengwa kwa kutopewa huduma za kijamii nchini Korea ya kusini ikiwamo kutoruhusiwa kuingia katika Migahawa na usafiri wa umma kwa madai ya kuwa huenda wana virusi vya Ebola.
Aidha, baadhi yao wamedai watu weusi wanaposimamisha TAXI hazisimami kutokana na hofu ya virusi hivyo vya Ebola.
nimezungumza na Kijana RWEHUMBIZA KALANGALI,ambaye ni mwanafunzi anayesoma huko Korea Kusini, na hapa anaeleza hali ilivyo.
CHANZO:BBC

Saturday, August 16, 2014

Wahamiaji haramu wakamatwa Mkoani Njombe

Baadhi ya wakazi wa mjini Makambako Mkoani Njombe waliojitikeza kuwaangalia wahamiaji hao( kulia) na waliokaa ni raia wa Ethiopia mara baada ya kukamatwa na kufikishwa katika ofisi za uhamiaji za Makambako.
Pasipoti Nne za Baadhi ya Wahamiaji Hao Waliokamatwa Mjini Makambako
Naibu Kamishna uhamiaji mkoa wa Njombe Bi. Rose Mhagama akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.(Picha na Mathias Canal)(P.T)

 

Ratiba ya Michezo ya leo ligi kuu nchini Uingereza 

SN-BPL-PRfcfEVIEW-640x360_2a533.jpeg
14:45 Manchester United Vs Swansea City
17:00 Leicester City Vs Everton
17:00 Queens Park Rangers Vs Hull City
17:00 Stoke City Vs Aston Villa
17:00 West Bromwich Albion Vs Sunderland
17:00 West Ham United Vs Tottenham Hotspur
19:30 Arsenal Vs Crystal Palace
Hizi ni saa za afrika ya mashariki (P.T)

PATASHIKA LA LIGI KUU ENGLAND NI LEO

article-2725958-208DCEFD00000578-103_634x823
 Kazi yapamba moto: kocha Louis Van Gaal tayari kuanza maisha mapya Man United
LIGI kuu nchini England inaanza kutimua vumbi leo hii na Louis Van Gaal anaanzisha patashika dhidi ya Swansea City katika uwanja wa Old Trafford.
Kocha huyo wa Kiholanzi mwenye miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda mechi tano na sare moja katika mechi za maandalizi ya msimu na sasa mashabiki wengi wana hamu ya kuangalia mafanikio yake katika ligi.(P.T)
Swansea ni moja ya timu nane zilizoingia katika rekodi ya kushinda mechi Old Trafford msimu uliopita ambapo Man United ilikuwa inaongozwa na kocha David Moyes aliyefukuzwa mwishoni mwa msimu kutokana na kuvurunda.
Msimu wa 2013/2014, United pia ilikabiliana na Swansea katika mchezo wa ufunguiz wa ligi kuu wakiwa mabingwa watetezi na kushinda mabao 4-1 katika uwanja wa Liberty.
Katika mechi ya leo, Wayne Rooney ataiongoza kwa mara ya kwanza Man United tangu achaguliwe kuwa nahodha jumanne timu ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Valencie.
Kwa upande wa Luke Shaw hataweza kucheza mechi ya leo kwasababu ya kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
1408135236305_wps_3_MANCHESTER_ENGLAND_MAY_11
Watabakiza ndoo?: Manchester City waanza kutetea ubingwa wao waliotwaa msimu uliopita baada ya kuwazidi kete Liverpool
Katika mechi nyingine, Aserne Wenger aliyemaliza ukame wa miaka tisa bila kutwaa kikombe baada ya kuibuka mabingwa wa kombe la FA msimu uliopita na kuanza vizuri msimu kwa kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuifunga Manchester City 3-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, ataanza ugenini dhidi ya Crystal Palace isiyokuwa na kocha mkuu baada ya Tony Pulis kutimka kufuatia kutofautiana na wamiliki wa klabu hiyo juu ya sera ya usajili..
Mshambuliaji mpya Alexis Sanchez aliyesajiliwa kwa paundi milioni 30 kutokea Barcelona anatarajia kuwemo katika kikosi cha Asernal kitakachoongozwa na nahodha mpya, Mikel Arteta.
Katika mechi nyingine, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itachuana na Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho.
Liverpool, wataanza kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itakabiliana na Burnley iliyopanda msimu huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester City na keshokutwa Burnley v Chelsea.

TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI  0114

Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.
02
03
Waandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakimsikiliza Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman (hayupo pichani) katika Mkutano wake na wandishi leo.(P.T)
04
05
Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo upande (JWTZ) Luteni  Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo.
06
Mmoja wa uwanja utakaotumika katika mashinda hayo, uliopo Bregedi ya Nyuki Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Chanzo:shaffihdauda.com

Monday, August 11, 2014

JK AOMBWA KUSITISHA BUNGE LA KATIBA 

BungeKatibaz_aa762.jpg
JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata), limemuomba Rais Jakaya Kikwete asitishe Bunge Maalumu la Katiba, lakini pia limevionya vyama vya siasa nchini kuhusiana na vitisho vya kuwashughulikia wanachama wao kuhusiana na Bunge hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, alisema kauli ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kwamba watawashughulikia wanachama wao, ambao ni wajumbe wa Bunge hilo si nzuri na kusisitiza kwa hali ilivyo sasa kuna haja Rais Kikwete asitishe Bunge Maalumu la Katiba.(MM)
"Yatosha tu kusema kwa sasa nchi imegawanyika vibaya kuhusu mchakato wa Katiba mpya na ulipofikia, haikuwa mshangao kushuhudia wajumbe watatu kutoka kundi la Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) wakitinga bungeni na kujiandikisha ili kuendelea na vikao vya Bunge, akiwemo Mwatuka (Clara) kutoka CUF.
"Wengine ni waheshimiwa Leticia Nyerere, John Shibuda na Said Arfi, wote kutoka Chadema na Chiku Abwao pia wa Chadema, ambaye baada ya kusoma upepo kuwa Ukawa wamesusia kiukwelikweli amekanusha na kwamba alikuwa na shughuli zake binafsi mjini Dodoma na wala hakufika kushiriki vikao vya Bunge.
"Vyama vyao vya CUF na Chadema vimeahidi kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa kukiuka maamuzi ya vikao halali vya kichama, lakini jambo moja dhahiri ni kuwa hawa ni wahanga tu wa tatizo kubwa zaidi la mpasuko wa kitaifa," alisema Kibamba.
Alisisitiza kuwa suala la kuchukuliana hatua au kushughulikiana si zuri na halileti tatizo la ufumbuzi uliopo kwani hata Ukawa wenyewe wamegawanyika, CCM nao wamegawanyika na jambo la msingi ni kutafuta ufumbuzi wa kitaifa kwani kuna mpasuko mkubwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba, kijamii na hakuna maridhiano ya kitaifa.
"Kuna wajumbe wamechelewa kufika Dodoma kwa kuwa wanaamini Bunge Maalumu halipaswi kuendelea kwa hali hii, aidha hata miongoni mwa wajumbe wa CCM kuna mpasuko wa waziwazi kati ya wanaoamini kuwa Bunge Maalumu halipaswi kuendelea kwa sasa kwa kuwa theluthi mbili haitaweza kufikia maridhiano yanayohitajika ili Katiba mpya iweze kuandikika," alisema.
Alisema kuna wajumbe zaidi ya wanne wa CCM wametoa sauti kuhusiana na Bunge hilo na kwamba wapo wengi na ni ishara kuwa CCM nako kuna mpasuko.
Alidai kuwa CCM imegawanyika katika makundi matatu kuhusiana na mchakato huo na kuyataja kuwa ni kundi la wanaoondoka madarakani, kundi la wasio na upande ambao wapo kimya na kundi la wanaotaka madaraka.
"Pia hata miongoni mwa wana Ukawa kumetokea mpasuko kati ya wale wanaoamini kuwa hakuna haja ya kushiriki Bunge Maalumu, ambalo hatima yake hakutazaliwa Katiba mpya na wale wanaoamini kuwa wana haki ya kimsingi ya kushiriki vikao Bunge Maalumu la Katiba na kupata posho zao kama wale wa CCM," alisema.
Pia alieleza kuwa kuna wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete ambao wameduwaa na hawajui la kufanya.
"Tunashauri kuwa mchakato wa kuandika Katiba mpya uahirishwe hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili uanze tena Januari 2016 na kwamba ili kuokoa gharama za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, chaguzi hizi mbili zifanyike siku hiyo hiyo moja ya Uchaguzi Mkuu," alisema.
Pia Kibamba alieleza kitendo cha Ukawa kushindwa kurejea bungeni kinaunyima mchakato wa Katiba uhalali wa kisiasa na kisheria na kwamba upande wa wajumbe wa Zanzibar wanafanya kukosekana kwa theluthi mbili inayohitajika. 
CHANZO:HABARILEO

MISS ETHIOPIA NDIYE MISS AFRICA USA, JOY KALEMERA AWA WANNE 

 

Miss Ethiopia akifurahia taji la kuwa Miss Africa katika mashindano hayo yaliyofanyika Rockville, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Mshiriki wa Tanzania, Joy Kalemera ameshika nafasi ya 4 kati ya washiriki 20 walioingia fainali hizo.
Washiriki watano waliopata nafasi ya kuingia tano bora kutoka kushoto ni Miss Tanzania aliyeshika na 4, Miss Uganda aliyeshika na 2, Miss Ethiopia aliyeshinda, Miss Guinea aliyeshika namba 3 na Miss Nigeria aliyeshika namba 5.(MM)
Washindi namba 2 mpaka 4 wakiangalia Miss Ethiopia akivishwa taji, kushoto ni miss Cameoon aliyekua Miss Africa USA msimu uliopita.
Washiriki wote 20 katika picha ya pamoja.
 Miss Ethiopia akipata picha ya pamoja na washindi namba 2 na 3 ambaye ni Miss Uganda na Miss Guinea.
Miss Ethiopia katika picha ya pamoja na mshindi namba 2 Miss Uganda.
Miss Ethiaopia akipata picha na wageni akiwepo Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

PROFESA TIBAIJUKA AKUTANA NA WADAU WA MJI WA KIGAMBONI

Waziri Tibaijuka akifunga majadiliano juu ya mradi huo.
Waziri Tibaijuka akiwa ameshikana mikono na mbunge was Kigamboni Faustine Ndungulie na baadhi ya madiwani na viongozi wengine kuonyesha maridhiano namna mradi utakavyotekelezwa.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Usanifu Miji na Uendelezaji Hellenic Mpetuta akitoa mada namna mji mpya utakavyopangiliwa katika mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kivukoni Dar es Salaam
(Awadh Ibrahim wa Mjengwa  blog/Kwanza jamii radio)

Pichaz za Rais Uhuru Kenyatta na Akon nchini Marekani

akon 12
President Uhuru Kenyatta wa Kenya ni miongoni mwa Marais wachache wenye umri mdogo kulinganisha na Marais wengi ambapo amekua akienda sawa na baadhi ya mahitaji au tabia ya vijana wengi ikiwemo kujumuika na Wasanii wakubwa hata wa Kenya kama Jaguar ambae huwa mara nyingi anakuwepo kwenye hafla za Ikulu.
Uhuru na Akon 1
Hapa walikutana wakati wa mapumziko kwenye hili kongamano.
Hizi picha zake za Marekani kwa mujibu wa ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich, ni kwamba mmoja wa Waandaaji wa mkutano wa Brook Business uliowakutanisha pamoja marais wa afrika na wakuu wa kampuni za kimataifa ni mwimbaji Akon.
Akon mwenye asili ya Senegal aliezaliwa miaka 41 iliyopita ni miongoni mwa wakali wachache kutoka Afrika ambao waliweza kupenda na kuingia kwenye chati za muziki wa dunia.
Pamoja na umaarufu na utajiri wake alioupata akiwa anaishi mpaka sasa nchini Marekani, Akon bado ameendelea kuikumbuka Afrika na hata kwenye baadhi ya interview zake na anachoandika kwenye mitandao ya kijamii, anasisitiza watu kuwekeza Afrika.
Uhuru na Akon 2