TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, January 19, 2014

SAMPLE ZA BATIKI ZIPO SOKONI KWA WALE WANAOHITAJI TUWASILIANE KWA NAMBA 0756 335051/0656 507130



MATUKIO YA PICHA YA MKUTANO WA INJILI ULIOKUWA UKIFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MAJOHE KWA WALIOBA
Mchungaji Salome kutoka Kigamboni akihubili katika viwanja hivyo

Nabii Godson wa kanisa la Habari Njema na Mchungaji Neema wakiwa wanasikiliza mahubiri

Watu waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza mafundisho


Watu wakisikiliza mafundisho





Nabii Godson akiombea maji ambayo watu walikuja nayo mkutanoni kwa ajili ya maombezi ya kufunguliwa matatizo mbalimbali





Mama akitoa ushuhuda baada ya kupokea uponyaji wa mguu uliokuwa ukimsumbua na kujikuta mzima baada ya maombezi
Shuhuda zikiwa zinaendelea mama huyo alikuwa akisumbuliwa na tumbo sasa anaendelea vizuri

Mama huyo nae alikuwa akisumbuliwa na tumbo nae amepokea uponyaji baada ya maombezi

Saturday, January 18, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO MKOANI DODOMA 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sehemu ya jengo la Kituo cha Polisi cha kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa ambayo imeporomoka kufuatia mafuriko yaliyokikumba kijiji hicho kufuatia mvua kubwa zianazoendelea kunyesha mkoani Dodoma januari 17, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko yaliyokikumba kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa Januari 17, 2014. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mpwapwa, Gregory Tewu na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua daraja ambalo lilizibwa na maporomoko ya maji yaliyoambatana na magogo , mawe na udongo na kusababisha mafuriko katika kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa januari 17,20134.(P.T)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko katika kijiji cha Fufu wilayani Chamwino, Dodoma, Januari 17, 2014.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema nchimbi na kulia kwake ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea vijiji vya Chipogoro na Fufu katika wilaya za Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma na kukagua maeneo mbalimbali ambayo yaliathiriwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kati ya Januari 2 hadi Januari 11, mwaka huu.
Akiwa katika kijiji cha Chipogoro tarafa ya Rubi, Waziri Mkuu alikagua kituo cha polisi na nyumba zilizobomolewa, choo cha zahanati na kukagua eneo la barabara inayojengwa ya kutoka Dodoma hadi Iringa katika eneo lenye matatizo ya makaravati kuziba.
Kwenye kijiji cha Fufu katika tarafa ya Makangwa ambacho kiko umbali wa kilometa 30 kutoka Chipogoro, Waziri Mkuu alikagua maeneo ya makazi yaliyoathiriwa kwa mafuriko na kukagua baadhi ya nyumba zilizobomoka kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwapa pole.
Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo leo (Ijumaa, Januari 17, 2014), mara baada ya kupokea taarifa za maafa ya mafuriko hayo, Waziri Mkuu alimtaka Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha anasimamia wakandarasi wa barabara hiyo ambayo ujenzi wake bado haujakamilika na kuainisha maeneo korofi ili yafanyiwe marekebisho haraka.
“Nimekagua matundu katika daraja moja pale Chipogoro na kuona ni madogo, mtaalamu anasema uchafu ulioziba ndiyo umesababisha maji yasipite. Mimi si mhandisi na hizi ni mvua za kwanza tu, sasa yakija maji mengi zaidi ya haya hali itakuwaje?, alihoji Waziri Mkuu.
“Hata hapa Fufu, kuna mahali nimeona maji yanaonyesha yalikuja kwa kasi kubwa lakini upenyo wa kuingia kwenye makaravati na kutokea upande wa pili ni mdogo sana... barabara hii ni mkombozi lakini kama haitazingatia uhalisia wa maeneo itakuwa ni balaa,” alionya.
Alimtaka pia awasimamie wakandarasi hao ili wanapoweka matoleo ya maji wahakikishe upande wa pili barabara maji hayo yanakwenda kwenye mikondo ya mto na siyo kuyaacha tu yasambae kiholela na kuishia kwenye makazi ya watu au mashamba yao.
Waziri Mkuu aliahidi kutoa mifuko ya saruji 2,600 na mabati 1,560 ambapo kila kijiji kitapata mifuko 1,300 na mabati 780 ili kuwasaidia wakazi waliobomolewa nyumba zao waweze kujenga nyumba za kisasa.
Alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuwashirikisha wadau wengine katika mkoa huo ili waone wanawezaje kuchangia upatikanaji wa mabati mengi zaidi kwa ajili ya nyumba zilizoezuliwa.
Kuhusu chakula cha msaada, Waziri Mkuu alimtaka Dk. Nchimbi aandae makisio ya mahitaji ya chakula yaliyopo na kuyafikisha Ofisi ya Waziri Mkuu ambako kuna Idara inayosimamia maafa ili waletewe chakula hicho haraka kwa sababu kipo.
Alisema anakubaliana na ushauri uliotolewa kuhusu suala la ujenzi wa mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kupunguza kasi ya maji yanayoporomoka kutoka milimani lakini akasema Serikali imeanza na ujenzi wa Bwawa la Kidete lililoko wilayani Kilosa tangu yaliyopotokea mafuriko wilayani humo.
Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Alfred Msovella, alisema nyumba 129 zilibomoka, vyoo 78 vimebomoka kikiwemo cha zahanati ambapo wakazi 1,390 wamepoteza vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula, magodoro, vyombo vya ndani na mifugo.
Bw. Msovella ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alisema hivi sasa, wakazi hao wanahitaji mahema 400, magodoro 381, madaftari ya wanafunzi na dawa za matibabu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Bi. Fatma Salum Ally akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Fufu, alisema jumla ya nyumba 26 zilibomolewa na mali kama vyakula, samani, vyombo vya nyumbani na bidhaa za biashara kuharibika.
Alisema eneo la kijiji cha Fufu ni tambarare na liko chini ya safu za milima na maji ya mvua yanayoporoka kutoka milimani, huondoka polepole. “Hata hivyo, hali hii ya mafuriko imechochewa na ujenzi wa barabara kuu kwa kiwango cha lami ambapo tuta la barabara mpya na vidaraja vidogo vilivyowekwa vimekuwa kizuizi cha maji mengi yanayotoka milimani na hivyo kuongeza tatizo la mafuriko,” alisema.
Mikutano hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Gregory Teu ambaye pia ni mbunge wa Mpwapwa pamoja na mbunge wa Mtera, Bw. Livingstone Lusinde.

Wednesday, January 15, 2014

Picha kutoka kwa Beyonce jinsi alivyosherekea birthday ya mwanae Blue Ivy

1
Blue Ivy ametimiza miaka 2 tangu azaliwe na siku ya birthday yake Beyonce na Jay Z  walikodi Zoo kwa ajili ya kusherekea pamoja na marafiki zao.
Beyonce kupitia mtandao ame-upload hizi picha wakiwa na rafiki zao wakisherekea miaka miwili ya mtoto Blue Ivy.
2
3
4
5
6
7
8
9
10

Namna ambavyo Tbs walivyoendesha operesheni kataza kuuza nguo za ndani za mitumba

IMG_5870
Januari 15 wafanyabiashara wa nguo za ndani wa soko la Karume hawakuimaliza vizuri siku hii baada ya Shirikia la Viwango Tanzania[Tbs]kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini kuendesha operesheni ya Kataza kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba).
IMG_5913
Afisa Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida ameongea na waandishi wa habari mara baada ya kukamata kwa marobota hayo ya nguo za ndani ambapo amesema wamekamata nguo hizo za ndani kwa sababu walishazipiga marufuku kuuzwa hapa nchini kwa kukosekana kwa viwango vinavyotakiwa lakini wafanyabiashara hao wamekua wakikaidi agizo hilo na kuendelea kuuza.
IMG_5873              
    Wafanyabiashara wa Karume wakiishuhudia hali hiyo.
Marobota ya nguo za ndani jana yalipakizwa kwenyemagari ya polisi na yalielekea kituo cha polisi cha msimbazi kwa ajili ya kuteketezwa kwa moto.
IMG_5904                                             Baadhi ya nguo za ndani zilizokamatwa.
IMG_5901

Lembeli ataka Watanzania waamue mkweli 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amesema anawaachia Watanzania waamue mkweli kati ya kamati yake na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.Kauli hiyo ya Lembeli inafuatia taarifa ya gazeti moja la kila siku (Siyo Mwananchi), iliyomnukuu Nyalandu akisema ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyowang'oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.
Nyalandu anadaiwa kutoa kauli hiyo alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma na Manyara kuhusu mgogoro wa mipaka kati wanavijiji na Hifadhi ya Tarangire.
Pia, mgogoro huo unahusisha Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani.
Nyalandu alikaririwa akisema kutokana na taarifa hiyo kueleza wapo watu waliobakwa wakati siyo kweli. Tanzania imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora kutokana na ukiukwaji haki za binadamu.
Hata hivyo, Lembeli alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na kauli hiyo alijibu: "Sijaisoma hiyo habari ila nimeisikia tu, kama ni kweli ametoa kauli hiyo (Nyalandu) basi ni hatari."
Lembeli alisema anawaachia Watanzania kupima mkweli kati yake, kamati yake na Waziri Nyalandu katika jambo hilo.(P.T)
"Kwa sasa niko kijijini kwangu huku jimboni, lakini nitafafanua zaidi nitakaporejea Dar es Salaam," alisema.
Ripoti hiyo ya kamati ndogo ya uchunguzi iliyoongozwa na Lembeli ndiyo iliyosababisha mawaziri wanne kuwajibika, kutokana na kuibuliwa kwa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Mawaziri waliong'olewa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Mathato David na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alijiuzulu kabla.
Atangaza ubabe
Lembeli alikazia kwa kusema hawezi kuishi kwa kuhofia vitisho vya maisha, kwa madai ya taarifa yake ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyosababisha kung'olewa kwa mawaziri wanne.
Akihutubia mkutano wa hadhara Kata ya Igunda, Lembeli alisema haogopi vitisho hivyo na ataendelea kutetea masihali ya umma.
Awali, Diwani wa kata hiyo, Tabu Katoto wakati akimkaribisha, alimpa pole mbunge huyo kwa kazi ngumu na lawama aliyoifanya mwaka jana kwa faida ya taifa, hali ambayo Lembeli alisema inampa wakati mgumu kutokana na watu wenye akili ndogo kumpa vitisho. vya maisha yake.
Chanzo:Mwananchi

Mlipuko waua 17 Maiduguri,Nigeria 

Watu kumi na saba wamefariki mwenye mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, limekiri kufanya shambulizi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi mshukiwa mmoja amekamatwa.
Mlipuko huo ulitokea karibu na soko moja mjini humo. Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa waliwaona watu wakitoroka kutoka eneo hilo nguo zao zikiwa na damu.
Kundi la Boko Haram, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara Kaskazini mwa Nigeria likiishinikiza serikali kukubali sheria za kiisilamu kutumika katika eneo hilo ambako wakazi wake wengi ni waumini wa kiisilamu.
Miili ilionekana ikiwa imetapakaa kote huku shahidi mmoja akiambia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na milipuko mingine midogomidogo.(P.T)

Wednesday, January 8, 2014

CHADEMA KUMPINGA ZITTO MAHAKAMA YA RUFANI 

zittokabwe1 e192c
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kiko katika harakati za kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, uliompa ushindi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe. (HM)
Zitto ambaye pia ni Mbuinge wa Kigoma Kaskazini, juzi aliibuka mshindi katika maombi yake ya kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake, hadi kesi ya msingi kuhusu suala hilo itakapokuwa imesikilizwa.
Kadhalika, chama hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano na Uenezi, John Mnyika kimesema kinaendelea na utekelezaji wa uamuzi wa Kamati Kuu wa kutompa Zitto ushirikiano wa aina yoyote.
Wakili wa Chadema, Peter Kibatala, alisema jana kuwa japo wanauheshimu uamuzi wa Mahakama, hawajaridhika nao na kwamba wanakusudia kwenda Mahakama ya Rufani kuupinga.
"Ingawa uamuzi huu ni Interlocutory (uamuzi usiomaliza kesi), lakini sisi hatukuridhika nao. Hatukuridhika na uamuzi wa kutupilia pingamizi letu la awali, hati ya kiapo na hata amri yenyewe ya zuio la muda," alisema Wakili Kibatala na kuongeza:
"Kuna namna nyingi za kufanya kupinga uamuzi huo, kama vile kukata rufaa, kuomba marejeo au namna nyinginezo. Kwa hiyo kwa sasa tunaangalia namna bora ya kwenda Mahakama ya Rufani bila kuathiri matakwa ya kisheria."
Wakili Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema kuna haja ya kuiomba Mahakama ya Rufani kuuchunguza uamuzi huo kwa kuwa una athari si kwa Chadema tu, bali hata vyama vingine dhidi ya wanachama wake.
Kauli ya Mnyika
Mnyika kwa upande wake alisema kutompa ushirikiano Zitto ni uamuzi wa Kamati Kuu ambao ulitokana na hatua yake ya kwenda mahakamani kwa masuala ya chama, kinyume cha matakwa ya Katiba ya Chadema na Kanuni zake.
Mnyika alikuwa akirejea taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baada ya kikao hicho akiwataka viongozi wa ngazi zote za chama hicho, wanachama, mashabiki na wapenzi wake, kutoshiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yote ya nje, ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake.
Ushindi wa Zitto
Katika maombi hayo namba 1 ya 2014, Zitto kupitia kwa Wakili Albert Msando, Zitto aliiomba Mahakama itoe zuio hilo la muda kwa CC ya Chadema, hadi kesi yake ya msingi namba 1 ya 2014 aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Awali, mawakili wa Chadema, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.
Katika uamuzi wake juzi, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
Maombi hayo ya Zitto yaliyotolewa uamuzi juzi yalitokana na kesi ya msingi aliyofungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema.
Katika kesi hiyo anaiomba mahakama ikizuie chama hicho, wakala wake na vyombo vyake vya uamuzi kumchukulia hatua zozote au kumjadili kuhusiana na uanachama wake, hadi hapo rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la chama hicho kupinga kuvuliwa nyadhifa, itakaposikilizwa.
Pia aliiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za CC za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Kesi hiyo ya msingi imepangwa kutajwa mahakamani hapo Februari 13, mwaka huu. Chanzo: Mwananchi

MESSI BORA, HATA ASIPOPATA TUZO

article-2274726-17648C8F000005DC-173 634x5371 21a9d
MLINZI wa kulia wa Barcelona, Dan Alves amedai kuwa anaamini Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi kwa sasa ulimwenguni hata kama hatapata tuzo ya mwanasoka bora wa dunia. (HM)

Mastaa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Franck Ribery wa Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, lakini Alves anaamini kuwa haitabadilisha lolote na Messi ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi wa zama hizi.
"Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia inachosha kidogo kwa sababu imehamishwa mahala pake. Imepelekwa katika eneo la mawazo ya watu, nje ya uwanja wa soka. Lakini kama tukitazama mambo ya uwanjani nadhani Lionel anawasukuma wengine katika nafasi ya pili," alisema Alves.
Kwa misimu minne mfululizo, Messi amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa dunia na ingawa msimu huu hapewi nafasi kubwa kutokana na kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, lakini bado amechaguliwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo. Chanzo: mwanaspoti

MORSI ACHELEWA KUWASILI MAHAKAMANI MISRI

Taarifa kutoka Misri zinasema kiongozi aliyepinduliwa nchini humo, Mohammed Morsi, amechelewa kuwasili mahakamani leo mjni Cairo.
Inasemekana kuwa hali mbaya ya anga imeizuia helikopta iliyotarajiwa kumsafirisha hadi katika mji mkuu huo anakokabiliwa pamoja na maafisa wengine wa utawala wake na tuhuma za kuchochea mauaji ya waandamanji mnamo mwaka 2012 alipokuwa madarakani.
Awali vikosi vya usalama viliimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo ,Morsi akitarajiwa kuwasili mahakamani.
Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake wanashutumiwa kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuvunja gereza.
Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa . Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni Rais na alifungwa kinyume na matakwa yake.(P.T)

Tuesday, January 7, 2014

Meno ya tembo 81 yakamatwa Tanzania 

130303065644 elephants ivory 304x171 reuters nocredit1 93ca2
Watu wawili wanashikiliwa na polisi nchini Tanzania baada ya kukamatwa na shehena ya meno ya tembo katika bandari ya Dar es Salaam, waliyokuwa wakisafirisha kiharamu maafisa wa nchi hiyo wamesema. (HM)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha amesema meno hayo yapatayo 81 yana uzito wa kilo 303.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya tembo ni mapya ikiwa na maana yametokana na tembo 41 waliouawa ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Naibu Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema mauaji ya tembo yameongezeka nchini humo baada ya operesheni ya kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni Tokomeza" kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za binadamu.
Mapema wiki hii Naibu Waziri huyo amesema tembo wapatao 60 wameuawa kati ya mwezi Novemba na Decemba ikilingalishwa na tembo wawili waliouawa mwezi Octoba. Chanzo: bbcswahili

Sudan mbili zajadili ulinzi wa mafuta

Sudan na Sudan Kusini zimejadili swala la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya mafuta Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.
Marais wa nchi hizo mbili wameanza mazungumzo ya kupeleka kikosi cha ulinzi ili kulinda visima vya mafuta Kusini ambako waasi wamezusha vurugu kwa karibu wiki nne sasa.
Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.
Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.
Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.(P.T)