TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, December 20, 2013

MATUKIO YA PICHA YA IBADA KATIKA KANISA LA HABARI NJEMA LILILOPO MAJOHE KWA WALIOBA
Waumini wakiwa kwenye Ibada wakimuabudu Mungu

Ibada inaendelea

Mchangaji Godson akiwa anaongoza waumini wapya sala ya toba walioamua kumpa Yesu maisha yao katika ibada ya Jumapili

Mchungaji wa katavi akiwa anahubiri neno la Mungu
Maombezi yakiwa yanaendelea





Maombezi yakiwa yanaendelea , Pia wote mnakaribishwa katika Kongamano la mwisho wa mwaka la kuona baraka za Mungu linaloendelea huko Majoe katika kanisa la Habari Njema kwa mawasiliano jinsi ya kufika huko 0754335051/0713055459

Thursday, December 19, 2013

KAGAME ASHTUSHA MSIBA WA MANDELA 

 paul20kagame1 42102

*Alitua ghafla na kwenda kumuaga Mandela
*Aondoka bila kumpa mkono wa pole Rais Zuma
KATIKA hali isiyotarajiwa, Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumatano iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kufika ghafla jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuaga mwili Mzee Nelson Mandela na kuondoka mara moja. (HM)

Pamoja na kuwasili ghafla bila taarifa Pretoria, Kagame alikwenda moja kwa moja katika majengo ya Union Buildings na kwenda kuaga mwili huo kisha alielekea uwanja wa ndege na kuondoka.
Aliondoka saa chache baada ya kuuaga mwili wa shujaa Mandela na kuelekea Rwanda ambako alikwenda kuongoza Mkutano Mkuu wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF), ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.
Habari za ndani zimesema kuwa Kagame ambaye alikuwa na ulinzi mkali, aligoma kwenda kusalimiana na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Kuja ghafla kwa Kagame na Rais Omar al Bashir wa Sudan katika kumuaga Mandela kulizua maswali mengi, kwa vile Rwanda ilitangaza kuwa Rais Kagame hatahudhuria mazishi hayo na badala yake itatuma ujumbe wa viongozi wa juu wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.
Serikali ya Afrika Kusini awali ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Rwanda, Pierre Habumuremyi, Katibu Mkuu wa RPF Francois Ngarambe, ndio wangeongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazishi hayo.
Clyson Monyela, Naibu Mkurugenzi Mkuu na Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mahusiano alisema kuwa Serikali awali ilipokea jina la Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa RPF, lakini baadaye waliambiwa kuwa Kagame amewasili mwenyewe na ujumbe wa watu wachache.
Monyela alisema walipokea orodha ya maraisi wengi wa Afrika wakiwamo kutoka Kenya, Uganda, Congo DRC na Burundi lakini hawakupokea jina la Kagame ingawa alitokea ghafla na wala hakwenda kumpa pole Zuma, ila alituma ujumbe kwa Rais Zuma na wananchi wa Afrika Kusini.
"Hatukupokea jina la Rais Kagame kwa vile Serikali ya Afrika Kusini haina tabia ya kumualika mtu kwenye msiba wala mazishi, hiyo ni tabia ya wananchi wa nchi hii," alisema.
Msemaji huyo alisema kuwa hakuna hata Rais au kiongozi yoyote aliyealikwa katika msiba na mazishi hayo, na ilikua ni utashi wa kiongozi kuthibitisha kuwa atahudhuria.
Rais Kagame katika muda wa hivi karibu amekuwa na ugomvi wa chini chini na maraisi Zuma, Kikwete na Banda kutokana nchi hizo wanachama wa jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika (SADC) kupeleka askari wao nchini Congo kuwaondoa waasisi wa kikundi cha M23 wanaosaidiwa na nchi za Uganda na Rwanda.
Naibu Mkurugenzi huyo wa habari aliongeza kuwa Kagame alikwenda katika majengo ya Makao Makuu ya nchi hiyo na alisalimiana na Mchungaji Jesse Jackson wa Marekani.
"Siwezi kujua walizungumza nini lakini walikutana, wakakumbatiana na kuzungumza, ila kwenye misa ya kitaifa ya kumuombea Mandela pale katika viwanja vya FNB hakuhudhuria," alisema Monyela.
Hata hivyo, taarifa ndani zimedai kuwa mke wa Rais Kagame aligoma kuhudhuria mazishi hayo na kuaga mwili huo kutokana na kutoridhishwa na uhusiano wa nchi ya Rwanda na Afrika Kusini.
Kuna taarifa kuwa kulikua na kutokuelewana katia ya Rais Kagame na familia yake kutokana na nia yake ya kuhudhuria mazishi hayo.
Hata hivyo Serikali ya Rwanda kama zilivyo nchini nyingine duniani zilishusha bendera yake nusu mlingoti kuomboleza kifo cha Mandela.
Mandela alifariki Alhamisi wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na viongozi wengi duniani akiwamo raisi wa Marekani Barack Obama walihudhuria ibada maalumu na kuaga mwili wake.
Hata hivyo Kagame aliandika barua kwa familia ya Mandela na ilikabidhiwa familia hiyo na balozi wa Rwanda nchini humo.
Wakati marehemu Mandela alipochaguliwa kuwa Rais wa kwanza mwafrika nchini Afrika Kusini mwaka 1994, Rwanda ilikua katika machafuko ya mauaji ya wenye kwa wenye kati ya Wahutu na watusi. Chanzo: Mtanzania

WAGANDA WAHOJI FIFA OKWI KWENDA YANGA

UGANDA-VS-ANGOLA-181 fcd9e
Uongozi wa Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) umendika barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutaka kujua uhakika kuhusiana na mshambuliaji Emmanuel Okwi kuuzwa Yanga. (HM)

Taarifa zinasema katika mtandao wa MTNfootball kwamba OKwi alijiunga na Yanga kwa kitita cha sola 100,000 lakini Fufa kupitia bosi wake, Edgar Watson imetaka kujua uhalali kuhusiana na uhamisho wake.
Fufa kupitia Watson imetaka kujua kama ni sahihi kwa kuwa kwamba ni sahihi Okwi aliyepelekwa SC Villa kwa mkopo akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia kama anaweza kucheza Yanga.
Okwi alidumu SC Villa kwa miezi miwili akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uganda na kufanikiwa kufunga mabao matatu.
Lakini Mkurugenzi we SC Villa, Edgar Agaba ameiambia MTNFootball.com, Okwi alikuwa mchezaji huru kabla ya kwenda kujiunga na Yanga.
Okwi amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na kusababisha vurugu kubwa hasa Simba wanapinga kwa kuwa wanahitaji kulipwa fedha zao dola 300,000 kutoka Etoile du Sahel. Chanzo: Salehe Jembe

SERIKALI YAFAFANUA KUCHELEWA KWA AJIRA ZA WALIMU NCHINI

mulugo_d38b5.jpg
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu walimu waliomaliza masomo yao na kutopangiwa vituo vya kazi kuwa muda wa kufanya hivyo bado.
Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge jana mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kuwa Serikali haijawasahau wala kushindwa kuwaajiri walimu waliomaliza masomo yao.
"Ni kweli wengi hawajapangiwa vituo vya kazi, lakini ndugu zangu Watanzania hebu muwe mnakumbuka kuwa ni muda gani huwa tunawapangia ajira walimu, mbona muda bado,"alihoji Mulugo.
Alisema kuwa muda wa kuwapangia walimu huwa ni kati ya Februari Mosi hadi Machi 30 mara baada ya wizara kupata vibali kutoka Utumishi.
Kuhusu walimu kupangwa na wengine kuachwa, alisema inatokana na bajeti ambayo wanakuwa wamepewa kutoka utumishi ambayo lazima inakuwa na ukomo wa idadi ya watu wanaotakiwa.(P.T)
Hata hivyo alisema kuwa walimu ambao walimaliza na wana sifa za kufundisha wanapaswa kuwa na subira kwani kumbukumbu zao zipo na kwa vyovyote lazima Wizara itawaangalia.
Kuhusu taarifa iliyotolewa kuwa wako wanafunzi wa darasa la saba, ambao hawajui kusoma Kingereza kwa kiwango cha darasa la pili, alikataa kuzungumza kwa mada ni kuwa hana taarifa na utafiti huo.
"Siwezi kuzungumzia jambo ambalo utafiti wake umefanywa na watu wengine kwa malengo yao wenyewe, naomba wazungumze wao," alisema.
Mjini Morogoro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu, bado kuna changamoto nyingi ikiwamo ya upungufu
wa vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia kama vitabu vya kiada.
Dk Kawambwa aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini na kuwa changamoto zilizopo zinahitajika kutatuliwa ili kiwango cha elimu kiendelee kukuwa na kuongeza uelewa kwa wanafunzi. Alitaja changamoto nyingine kuwa ni ufaulu mdogo katika masomo ya sayansi, hisabati na lugha unaosababishwa na upungufu wa walimu, madarasa ya awali na msingi.
Chanzo:Mwananchi

MAN UNITED WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA LIGI, SPURS NJE LICHA YA ADEBAYOR KUFUNGA 

article-2526023-1A2FC18B00000578-500_634x393_f96bb.jpg
Raha ya bao: Ashley Young (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dhidi ya Stoke City
Na BIN ZUBEIRY
KOCHA David Moyes ameendelea kupambana baada ya jana kuiongoza Manchester United kushinda mabao 2-0 dhidi ya Stoke City katika Kombe la Ligi England.
Ushindi huo wa United jana ulitokana na mabao ya Ashley Young dakika ya 61 na Patrice Evra dakika ya 78.
article-2526024-1A2FC12600000578-769_634x439_13a0d.jpg
Katika mchezo mwingine, mshambuliaji Emmanuel Adebayor alirejea uwanjani na kufunga bao moja wakati timu yake, Tottenham Hotspur ikifungwa 2-1 na West Ham United, mabao ya Jarvis dakika ya 80 na Maiga dakika ya 85.
Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.
Adebayor akishangilia bao lake ambalo hata hivyo halikuweza kuinusuru Spurs na kipigo
Nayo Manchester City iliifunga 3-1 Leicester na kufikisha jumla ya mabao 75 katika mechi 25 za mashindano yote msimu huu.
article-2525815-199D593100000578-596_634x494_a8818.jpg
Free-scoring: Sergio Aguero (centre) and Alvaro Negredo (left) are combining effectively in

RAIA WAWILI ,ASKARI WAUAWA MORO,KITUO CHACHOMWA MOTO

mwema_5b367.jpg
Watu watatu, akiwamo askari polisi wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuzuka mapambano kati ya polisi na raia katika Kijiji cha Igwati, Tarafa ya Malinyi Wilaya ya Ulanga, Morogoro.
Diwani wa Kata ya Malinyi, Said Kila aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Leon Chikwita, Andrew Likomoka na Edson Kidunda.
Alisema mmoja wa majeruhi Idelfonce Malenga (35), hali yake ni mbaya baada ya kupigwa risasi shavuni. Majeruhi wawili majina yao hayakufahamika mara moja.
Diwani Kila alisema mauaji hayo yalitokea baada ya kundi la wakulima kuvamia Kituo cha Polisi Malinyi kushinikiza kuachiwa kwa wenzao watatu waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mfugaji mmoja wa kijiji hicho hivi karibuni.
"Baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa wenzao walifika kituo cha polisi ambako, hawakuwakuta watuhumiwa hao kwani walikuwa wamehamishiwa kituo kingine," alisema diwani huyo.(P.T)
Alisema katika jitihada za kulinda kituo, polisi walitoa tahadhari mbalimbali za kuwataka wananchi hao kutawanyika ikiwamo kupiga mabomu ya machozi, lakini waliendelea kukaidi amri hiyo na badala yake walizidi kujikusanya na kukivamia na kisha kukichoma moto pamoja na gari la askari lililokuwapo. Katika shambulizi hilo, ndipo mauaji hayo yalipotokea.
Chagonja eneo la tukio
Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kwenda kuongeza nguvu katika operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususan, Kata ya Malinyi kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
Chanzo cha mgogoro
Mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wa Igwati ulianza Desemba 13, mwaka huu wakati kundi la wananchi lilipomkamata mfugaji huyo na kumpeleka katika ofisi za kijiji.
Ilidaiwa kuwa baada ya kumfikisha, mtendaji wa kijiji alimfungia mtuhumiwa huyo ofisini kwake na kuanza kuhoji sababu za wananchi kumkamata jambo ambalo linaelezwa kwamba liliwakera na kuanza kumshambulia hadi kuikimbia ofisi na kumwacha mfugaji huyo ambaye alishambuliwa na kuuawa.
Kitendo cha kukamatwa na kupigwa hadi kuuawa kwa mfugaji huyo kinadaiwa kuwa kilikuwa cha kulipiza kisasi baada ya wafugaji kuvamia nyumbani kwa Mjumbe wa Kamati ya Mazingira, Victoria Marietha na kumjeruhi vibaya kisha kufariki dunia katika Hospitali ya Lugala, Malinyi alikokuwa akipatiwa matibabu.

WACHEZAJI RAJA CASABLANCA WAGOMBEA VIATU VYA RONALDINHO 

 article-0-1A2FF25400000578-150 634x4321 97f14

Wachezaji wa Casablanca wakisaka viatu vya Ronaldinho (HM)
article2 6bf4e
article3 9fcaa
MARA tu baada ya kutolewa katika Klabu Bingwa ya Dunia a FIFA, wazi Ronaldinho alitaka kurejea chumba cha kubadilishia nguo cha Atletico Mineiro kujiliwaza.
Lakini alilazimika kubaki uwanjani baada ya kuvamiwa na wachezaji wa Raja Casablanca, waliomsalimia na kumuomba viatu vyake vya Nike!
Timu hiyo Morocco iliendeleza wimbi lake la ushindi nyumbani kwa ushindi wa mabao 3-1, wakimtoa nishai Mbrazil huyo ambaye alifunga bao zuri la mpira wa adhabu- katika jitihada zake za kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu alipofika fainali akiwa na Barcelona mwaka 2006. Chanzo: binzubeiry

Wednesday, December 18, 2013

AU YATAKA SUDAN KUSINI KUACHA MAPIGANO

130524092249_zuma_africain_union_304x171_reuters_nocredit_96fa1.jpg
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AU, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameelezea kusikitishwa na hali ilivyo Sudan Kusini, kufuatia kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, siku ya Jumapili.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu na kuchapishwa katika gazeti la Sudan Tribune, mwenyekiti huyo amesema ana wasiwasi hasa na hali ya usalama wa wananchi.
Mapigano yalizuka katika mji wa Juba, Jumapili jioni kati ya vikundi vyenye silaha katika kambi ya jeshi na mapigano hayo yaliripotiwa kuendelea Jumanne, huku milioni ya bunduki ikisikika katika maeneo yote ya mji wa Juba mbali na kuhakikishiwa na serikali ya Sudan Kusini kuwa imedhibiti hali hiyo.
Dlamini-Zuma ameitaka serikali ya Sudan Kusini na makundi mengine yanayohusika katika mapigano hayo kujizua na aina yoyote ya kuendelea kwa mgogoro huo.
Pia amezitaka pande zinazohusika na mgogoro huo kutafuta suluhisho la amani kutokana na tofauti zao, "kwa kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu na uhalali wa kikatiba", akisema AU iko tayari kusaidia kutafuta suluhisho la hali ya sasa.
Wito wa AU umekuja wakati Marekani ikizitaka pande zinazohusika katika mgogoro wa Sudan Kusini kujizuia na ghasia na kutafuta suluhisho la amani.
Mjumbe maalum wa Marekani Donald Booth alitumia mawasiliano ya Twitter siku ya Jumatatu akitaka kuwepo kwa hali ya utulivu, akisema migogoro ya kisiasa lazima imalizike kwa njia ya mazungumzo na sio vurugu.(P.T)
Rais Salva Kiir amemshutumu naibu wake wa zamani, Riek Machar, kwa kuchochea jaribio la kutaka kuiangusha serikali yake.
Mawaziri kadha wa zamani wamekamatwa, wakihusishwa na jaribio hilo, ambapo mawaziri wengine hawajulikani walipo.
Bwana Kiir ametangaza amri ya kutotembea ovyo usiku katika mji wa Juba, ambapo maeneo mengi yenye pilikapilika za kibiashara, yamekimbiwa kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo, mazingira ya jaribio hilo hayako bayana, huku kukiwa na taarifa zinazokinzana na kauli rasmi ya serikali kuhusu tukio hilo, zikidai kuwa msuguano wa uongozi katika chama tawala, SPLM katika wiki za karibuni ulisambaa hadi katika jeshi, SPLA, na kuchochea mapigano kati ya wafuasi wa Bwana Kiir na Machar.
Jumatatu, walinzi wa rais waliizingira nyumba ya Bwana Machar katika eneo la Amarat, na kuharibu sehemu kubwa ya nyumba hiyo. Hakuwa nyumbani wakati huo na mpaka sasa hajulikani alipo.
Maafisa wa afya wanasema watu wapatao 26 wamethibitika kufariki dunia katika hospitali ya Juba, wakati zaidi ya watu 113 wametibiwa kutokana na majeraha ya risasi.

MACHAR: SIHUSIKI NA JARIBIO LA MAPINDUZI 

271_Dr.RiekMachar_356b1.jpg
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar aliyekimbilia mafichoni amekataa madai kuwa amehusika katika jaribio la mapinduzi.
Ameiambia BBC kuwa wa kulaumiwa kwa machafuko yaliyotokea katika mji mkuu wa Juba ni rais Salva Kiir ambaye anadai kuhusika kwake.
Machar ambae alifarakana na Rais Salva Kiir mnamo mwezi wa Julai alimshtumu kwa "kuchochea mapigano ya kikabilai" ili kuficha udhaifu wake..
Rais Kiir amesema kikundi cha wanajeshi wanaomuunga mkono Bwana Machar kilijaribu kutwaa madaraka kwa nguvu usiku wa Jumaapili lakini walishindwa.
Alisema mapigano hayo yalianza pale watu waliovalia mavazi ya kijeshi walipofyatua risasi katika mkuano wa chama kinachotawala cha (SPLM).
Lakini Bw Machar aliiambia BBC: "Hakukuwepo jaribio lolote la mapinduzi."
Rais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa Gerard Arud amesema kuwa mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini ambao umechukua mrengo wa kikabila unaweza kugeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Bwana Arud ameiambia BBC kwamba umoja wa mataifa umepata habari kwamba mamia ya watu tayari wamepoteza maisha yao tangia jaribio la mapinduzi lifanyike siku ya jumapili,ijapokuwa amesisitiza kuwa sio raia wanaolengwa.
Ameiambia BBC kwamba takriban raia elfu 20 wamepewa hifadhi katika makao ya umoja wa mataifa katika mji wa Juba na kwamba wanakumbwa na uhaba wa chakula na madawa.(P.T)

KIINGILIO MECHI YA MTANI JEMBE 5,000/- 

2n_c23ba.jpg

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Desemba 21 mwaka huu) ni sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 40,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja katika vituo mbalimbali, mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Vituo ambavyo tiketi hizo zitauzwa keshokutwa (Ijumaa) ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi hiyo itachezeshwa na Ramadhan Ibada (Kibo) kutoka Zanzibar, ambapo atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba, na Simon Charles kutoka Dodoma. Mwamuzi wa akiba ni Israel Nkongo wa Dar es Salaam wakati mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha.(P.T)
TANZANITE YAWASILI JOHANNESBURG KUIVAA BATSESANA
Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi tisa cha timu ya Tanzania ya wasichana chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili leo jijini Johannesburg tayari kwa mechi dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Batsesana).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Canada.
Tanzanite imefikia Millpark Garden Court Hotel tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini.
Wachezaji wa Tanzanite walioko katika kikosi hicho ni Amina Bilali, Amina Hemed, Amisa Hussein, Anastaz Katunzi, Anna Mwaisula, Belina Nyamwihula, Donisia Minja, Fatuma Maonyo, Happiness Mwaipaja, Latifa Salum, Maimuna Kaimu, Najiat Idrisa, Neema Kiniga, Rehema Rhamia, Sada Hussein, Shelda Mafuru, Stumai Athuman, Tatu Salum, Theresa Kashilim na Vumilia Maarifa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Monday, December 16, 2013

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI 



Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org(P.T)

 Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
 Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho

MAAFA -UKAME

 unnamed_e4467.jpg

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa - Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba akieleza umuhimu wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo kwa Wilaya ya Kishapu, Shinyanga jana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kishapu (watatu kushoto) Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Bw. Octavian Mangosongo. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu).
Vijana Kutumika Katika Kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Ya Ukame.
Na. Mwandishi Maalum
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imesema itawatumia vijana walioko shuleni na nje ya shule katika Mradi wa kuzijengea uwezo jamii wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. Kauli mbiu ya Mradi huo ni " Athari za Ukame Zinapunguzika, Jamii ikielimishwa."
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo jana wilayani Kishapu, Mkurugenzi Wa Idara Ya Uratibu Wa Maafa, Ofisi Ya Waziri Mkuu, Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba alisema lengo la kujumuisha vijana walioko shuleni na nje ya shule, ni kuwajengea utamaduni wa kutambua viashiria na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ili waweze kukabiliana na maafa yanapotokea na hatimaye kuwaanzishia miradi midogo midogo ya ufugaji na Kilimo kwa ajili ya kipato na kujikimu na maisha.(P.T)
"Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi yameleta athari nyingi ikiwemo ukame, kupitia mradi huu ulioanza kutekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Same kwa Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Kishapu kwa Mkoa wa Shinyanga vijana na akina mama wataelimishwa juu ya upandaji wa miti na kilimo cha mazao yanayohimili ukame hususan mihogo na viazi vitamu." Alisema Rioba
Rioba alifafanua kuwa katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame mradi utaainisha na kutoa mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu. Pia mafunzo kwa wataalam kuhusu matumizi ya vifaa vya kukusanyia takwimu na mawasiliano yatatolewa pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo utaboreshwa.

SUDAN KUSINI YATIBUA JARIBIO LA MAPINDUZI

59D9A9A4-69A8-4F4C-8E86-9FF0663BC5F3_mw1024_n_s_f229c.jpg
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer.
Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo.
Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.
Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)

ANDY COLE AWAPA NAFASI U-17 WA TANZANIA

colepix_282d6.jpg
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Andy Cole amewaasa vijana walio chini ya miaka 17, kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.
Cole ambayo yuko nchini, alisema: "Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao.
Naomba nichukue nafasi kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio."
Katika hafla hiyo, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel iliipiga tafu timu ya taifa ya vijana ya U-17 kwa kuikabidhi mipira 100 ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuendeleza soka ya vijana nchi.(P.T)
Mbali na hayo, Airtel iko katika mkakati mmoja na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema: Uwekezaji katika michezo ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa."
Alisema kuwa kampuni yake inakabidhi mipira 100 kama sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kusaidia maendeleo ya michezo.
"Tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine na kuhakikisha tunapata mabalozi wazuri wa kutuwakilisha mashindano ya kimataifa."
Naye Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa aliwashukuru Airtel kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa kampuni zingine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo.

Sunday, December 15, 2013

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA NELSON MANDELA, AONGEA KIJIJINI QUNU AFRIKA KUSINI

unnamed_6_03326.jpg
unnamed_4_825a3.jpg
unnamed_5_afc9d.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013
unnamed_3_80f5c.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi ya Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika.
PICHA NA ISSA MICHUZI WA IKULU(P.T)