TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, April 23, 2013

JK AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA  KIKRISTO
zz 27152
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam

MKUTANO WA CHADEMA MKOANI IRINGA
cdm1 6de2b
umati mkubwa  wa  wananchi  waliofika  kusikiliza mkutano  wa Chadema  Leo Iringa mjini
cdm2 b6b27
Katibu mkuu wa chadema Dk. Slaa Akihutubia katika mkutano wa wabunge chadema waliosimamishwa bungeni,
IMG 2382 7b7c4
katibu  mkuu  wa Chadema Dkt Slaa (kushoto) akiwa na mbunge wa jimbo la Ubungo Jonh Mnyika katika mkutano wa  wabunge wa chadema waliofukuzwa  bun
WATAKAO JIFUNGUA NYUMBANI KUTOZWA FAINI
2 f4702
Viongozi wa Tarafa za Mahuta na Namikupa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, wamesema watatoza faini kati ya Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa wajawazito watakaojifungulia nyumbani.Hatua hiyo
inakuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa wilaya hiyo wa kuhakikisha wajawazito wote wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Wakizungumza katika kikao maalumu kilichoitishwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa wilaya hiyo, Scholastica Sowani mwishoni mwa wiki, viongozi hao wakiwamo watendaji wa kata na vijiji, watumishi wa zahanati walisema hatua hiyo inaweza kuwa na mafanikio.
Kwa mujibu wa Sowani tarafa ya Litehu wameweza kufikia asilimia 100 ya wajawazito wote kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya, pamoja na mikakati mingine baada ya kuweka faini ya Sh10,000 kwa watakaojifungulia nyumbani.
"Kikao hili kimeshirikisha kata za Nahyanga, Lukokoda, ambapo tatizo la wajawazito kujifungulia nyumbani ni kubwa na hadi sasa wilaya tumefikia asilimia 75 ya wajawazito wanaojifungulia hospitali, kituo cha afya au zahanati" alisema mratibu huyo:CHANZO MWANANCHI
UPELELEZI KESI YA LWAKATARE UMEKAMILIKA
1 73ee8
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, amesema upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatale na
mwenzake Joseph Ludovick umekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mulungu alisema kwa sasa jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.
Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu. Watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.
Kuhusu kesi ya kumwagiwa tindikali Kada wa CCM, Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Igunga Septemba 2011, alisema tayari watuhumiwa wawili wamekwishafikishwa mahakamani.
Mulungu alisema kuhusu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na matukio mengine yaliyotokea Zanzibar, upelelezi bado unaendelea na kwamba upo katika hatua mbalimbali. Aliwataka watu kuwa na subira:CHANZO MWANANCHI.
KOCHA KIM ATANGAZA YOUNG TAIFA STARS

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.
soma zaidi.

Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
"Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao," amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).
Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).
AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT Ruvu.
Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
FA UINGEREZA YAMFUNGULIA MASHTAKA SUAREZ
R 107fd
Suarez akimng'ata Ivanovic uwanjani:
Chama cha soka nchini Uingereza, FA kimenuia kumpa adhabu kali mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwa kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mchezo wa jumapili baina ya Liverpool na Chelsea,mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.
FA imesema mwamuzi wa mchezo huo hakukiona kitendo hicho uwanjani lakini marejeo ya picha za mchezo huo zilionyesha Suarez alimng'ata Ivanovic,kitendo ambacho kinachukuliwa kama vurugu mchezoni na adhabu yake ni kufungiwa mechi tatu lakini adhabu hiyo haitoshi kwa tukio alilolifanya Suarez.
Suarez amepewa muda wa mpaka saa 12 jioni jumanne ya April 23, awe amekubali au kukataa kosa hilo kabla ya tume ya kudhibiti maadili haijakutana hapo siku ya jumatano kutoa hukumu stahili kwa kosa hilo.
Mwenyewe Suarez aliisha kiri kufanya kosa hilo na kumuomba Ivanovic msamaha kwa njia ya simu na kuwaomba mashabiki wa soka wamsamehe kwa kosa hilo.
Klabu yake ya Liverpool imempa adhabu ya kumpiga faini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay.
Mwaka 2010, Suarez wakati akiichezea Ajax ya Uholanzi alimng'ata begani kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal na kufungiwa mechi saba na chama cha soka nchini Uholanzi kwa kosa hilo.
Itakumbukwa Suarez tayari amekwishawahi kufungiwa kutocheza mechi nane za mashindano nchini Uingereza na faini ya paundi elfu 40 kwa kosa la kumtolea lugha ya kibaguzi beki wa Manchester United Patrice Evra mwaka 2011
:CHANZO BBC
MAN U YATWAA UBINGWA KWA MARA 20 KATIKA HISTORIA YA LIGI KUU UINGEREZA
MN c852e
Magoli matatu ya Robin Van Persie yaliifanya Manchester United kutwaa Ubingwa wa 20 katika Historia ya ligi kuu ya Uingereza:
DD 8c711
Mashabiki wa United wakiwa na jezi zenye maana ya kombe la 20

SW 925e9

Van Persie na Rio Ferdinand wakicheza gangnam kusheherekea ubingwa:CHANZO BBC.

UBALOZI WA UFARANSA LIBYA WASHAMBULIWA
v e27c6
Bomu limelipuka nje ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Libya Tripoli, na kuwajeruhi walinzi wawili huku ikisababisha uharibifu mkubwa:CHANZO BBC
WAMASAI WATETEA ARDHI YAO TANZANIA
00 6c17a
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi mjini Arusha hasa katika eneo la Loliondo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Serengeti imekodishwa kwa kampuni ya uwindaji ya Emirati iitwayo Ortello.
000 bfff0

 :CHANZO BBC
DKT. SHEIN KUTEMBELEA MIKOA YA ZANZIBAR 
0 271df
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein amesema kuwa ataendelea kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuulinda Muungano wa Serikali mbili uliopo.
Kauli hiyo ameitoa katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.
Dkt Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa kuna kila sababu ya kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu wake na kwamba Muungano uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya kuendeleza mashirikiano ya kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.
Amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kupata taarifa za matukio mbali mbali pamoja na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo zinazohusu CCM.
Aidha amewataka viongozi wa CCM kuwa na mashirikano mazuri katika kukiimarisha Chama na kuhakikisha kwamba kinapata ushindi katika kila uchaguzi unaokuja.
Dkt. shein amesema kuwa ana imani na Chama chake kuibuka mshindi katika chaguzi kutokana Chama hicho kuchagua uongozi makini ambao utahimili vishindo vya uchaguzi ujao.
Katika hatua nyingine Dkt Shein aliwataka Wananchi kuendelea kujishughulisha na harakati zao za kujiletea maendeleo na kuepuka kuvunja sheria za nchi.
"Serikali inataka amani na utulivu kwa Wananchi wake sambamba na kuimarisha maendeleo kama Malengo ya Mapinduzi yalivyoelekeza na kwa njia hiyo hatuna budi kuyaenzi Mapinduzi" alieleza Makamo Mwenyekiti wa CCM.
Katika ziara hiyo Makamo Mwenyekiti amezindua Tawi jipya la CCM la Vikokotoni, Kikwajuni SACCOS BANK pamoja na kutoa kadi 270 kwa wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi.

SERIKALI YAFUNGA KIWANDA CHA NONDO CHA METRO JIJINI DAR ES SALAAM KWA KUZALISHA NONDO ZISIZO NA VIWANGO VYA UBORA VINAVOTAKIWA

Inspekta wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Yona Afrika  akizugumza  na Meneja wa Kiwanda cha nondo cha Metro cha  jijini Dar es Salaam, Onesmo Ngondo mara baada ya TBS  kukifungia kiwanda hicho kwa muda usiojulikana , kutokana na kuzalisha nondo  zisizo na  viwango vya ubora vinavyotakiwa

SAKATA LA JUMA NATURE KUTOLEWA KWENYE INTERVIEW....NATURE AFUNGUKA

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku katika kipindi cha burudani cha  televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena. Kilichotokea  kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika kupitia ukurasa wake wa facebook.... 

JUMA NATURE AKAFUNGUKA:
hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa
 ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo,
kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi
 kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa 
kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka 
kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa
 kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview

RAIS TENGA ATOA MIPIRA YA DOLA 30,000

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa mipira zaidi ya 1,200 yenye thamani ya dola 30,000 za Marekani kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na vituo 21 vilivyo hai vya kuendeleza vijana (academies).
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) lilimpa Rais Tenga fedha hizo ikiwa ni shukrani kwake kwa kushughulikia mgogoro wa uongozi wa mpira wa miguu nchini Kenya uliodumu kwa miaka miwili; ambapo nchi hiyo kutokana na mgogoro huo ilikuwa na vyama viwili (KFF na FKL).
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mipira hiyo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam leo (Aprili 22 mwaka huu), Rais Tenga amesema amefanya hivyo kwa vile anaamini kuwa mipira ndiyo kitu muhimu katika kuinua mchezo huo mahali popote.
“Dhamira yangi si kushukuru kwa hafla hii, bali kutoa sababu kwa nini nimefanya hivi. Ninaamini kwa kuanzia mipira ndiyo muhimu, pili kwa kufanya hivi itaonekana kweli mipira imegawiwa,” amesema Rais Tenga.
Amesema amesema mpira wa miguu kwa Tanzania unahitaji sana watu wa kujitolea, na yeye amefanya hivyo kwa kujitolea kutokana na ukweli shughuli anazotumwa na FIFA ni za kujitolea.
Rais Tenga ambaye pia alitumwa na FIFA kutatua matatizo ya uongozi wa mpira wa miguu katika nchi za Uganda, Zambia na Sudan Kusini amesema anaamini anapata fursa hizo kutokana na kuwa kiongozi wa TFF, na kwa kuwakumbuka waliomchagua ndiyo maana hakusita kupeleka fedha hizo kwenye mipira.
Amesema moja ya ndoto zake wakati anaingia kuongoza TFF mwaka 2004 ameshindwa kutimiza ni kusaidia mipira, kwani uwezo wa kununua mipira kwa wanaocheza katika ngazi ya chini hasa watoto haupo.
“Hizi kelele zote za maendeleo ya mpira wa miguu ni kwa sababu shuleni hakuna vifaa. Nia yangu ilikuwa shule zote zipate mipira, lakini hiyo ni moja ya ndoto nilizoshindwa kutekeleza. Vipaji haziwezi kupatikana kama watoto hawachezi.
“Tunashukuru sana kwa Serikali kurejesha mpira shuleni. Hata nitakapoondoka madarakani nikipata nafasi nitaendelea kuomba mipira kwa ajili ya shule,” amesema Rais Tenga.
Vyama vya mikoa ambavyo jumla ni 32 (Tanzania Bara na Zanzibar) kila kimoja kimekabidhiwa mipira 25 (kumi saizi namba tano, 15 saizi namba nne kwa ajili ya vijana). Kwa academies ambazo ni 21 kila moja imepewa mipira 25 (minane saizi namba tano, na 15 saizi namba nne).
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almasi Kasongo, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) Nassib Mabrouk na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Riziki Majala.

WALIMU WAPIGWA MAWE NA WANAFUNZI WA SHULE YA MIZENGO PINDA KWA MADAI KUWA NI WACHAWI

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda  kata ya Kibaoni  Wilayani Mlele mkoani Katavi, wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu hao baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi, Joseph Myovela, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2:30 usiku shuleni hapo baada ya kuzuka kwa tafrani iliyodumu kwa zaidi ya saa 1:30.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kilitokana na mwanafunzi mmoja aitwaye Jofley Pinda kushikwa na ugonjwa wa mapepo uliomfanya aanguke chini ambapo tukio hilo lilitokea mchana wa saa saba.
Alisema wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja Alico Kamyoge (36) ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa mapepo

Myovela alisema  ilipotimia muda huo wa saa mbili wanafunzi hao walijikusanya na kuandamana hadi kwenye jengo la utawala na kuanza kulishambulia kwa mawe na matofali na kuvunja mlango na dirisha la jengo hilo.

Alieleza baada ya kufanya uharibifu kwenye jengo la utawala walielekea kwenye ofisi ya mwalimu wa taaluma ambapo waliharibu mtandao wa mawasiliano kwenye Computer.

Wanafunzi hao ambao muda wote walikuwa na hasira walielekea nyumbani kwa mkuu wa shule, huku wakiwa na matofali na mawe walipofika na kumkosa mkuu washule aliyekuwa amekwenda kwenye matembezi ya jioni walianza kushambulia nyumba yake kwa mawe na tofali na kuharibu mlango na madirisha.
Kaimu kamanda Myovela alisema  kundi hilo lilielekea nyumbani kwa mwalimu wao wa taaluma Bonifasi Nsalamba ambapo walimkuta akiwa anajiandaa kuingia ndani ya nyumba yake akitokea matembezini.

Ndipo walipoanza kumshambulia kwa mawe katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimzomea kuwa mchawi huyo mshirikina ..

Alisema katika shambulio hilo wanafunzi walimjeruhi mwalimu Bonifasi na kumsababishia majeraha katika mwili wake na aliweza kutibiwa katika zahanati ya kibaoni na kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoa wa katavi limetoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine  za mkoa huo waachane na kuamini imani za ushirikina na polisi inaendelea na uchunguzi  wa tukio hilo ili kuwabaini waliohusika na
waweze kuchukuliwa hatua.

UPELELEZI WA KESI YA VITENDO VYA KIGAIDI VYA LWAKATARE WAKAMILIKA


Jeshi la Polisi nchini limekamilisha upepelezi kuhusu kesi inayomkabili Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi vinvyzomkabili. Jalada la kesi hiyo linaandaliwa kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, DDP kwa hatua zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mghulu akizungumza na wanahabari leo hii, amesema upelelezi huo umezingatia matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyofanyika hapa nchini.
Kuhusu kumwagiwa tindikali kada wa CCM bwana Musa Tesha, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Iguga mwezi Septemba wa mwaka 2011, tayari watuhumiwa wawili wamekwisha kufikishwa mahakamani na upelelezi upo katika hatua za mwisho. Endapo watabainika watuhumiwa wengine, nao watafikishwa mahakamani kwa muda muafaka.