TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, June 2, 2015

Balozi Liberata Mulamula akabidhiwa rasmi Ofisi 


 Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula alikuwa Balozi  wa Tanzania nchini Marekani na Mhe.  Haule kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani leo tarehe 01 Juni, 2015.(P.T)


 Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule.

 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Lugaganya na  Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula  (hayupo pichani)
Balozi Mulamula akizungumza huku Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya, (kulia kwa Balozi Mulamula), Mhasibu Mkuu Bw. Paul Kabale (wa tatu kutoka kushoto), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mambo ya Nje, Bw. Mathias Abisai na Afisa Habari wa Mambo ya Nje Bw. Ally Kondo.Picha na Reginald Philip

Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria 

Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria
Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto.
Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali.
Walioshuhudia wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ndiposa likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.
Mmoja ya waliokuwa wakishughulika kuwanusuru waliojeruhiwa amesema magari mengine 12 nayo yalishika moto.
Mwandishi wa BBC aliyeko Nigeria anasema mikasa ya ajali zinazohusu magari ya kubeba mafuta hutokea mara kwa mara nchini humo.
Miaka mitatu iliyopita ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliwaua zaidi ya watu 100 huko Niger Delta katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.BBC

Yemen: video ya mateka wa Ufaransa yarushwa hewani 

Maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa Isabelle Prime, Sanaa, Machi 9 mwaka 2015.
Maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa Isabelle Prime, Sanaa, Machi 9 mwaka 2015.
Na RFI
Video ambayo ameonekana mateka wa Ufaransa Isabelle Prime imerushwa hewani Jumatatu wiki hii. Isabelle Prime alitekwa nyara Februari 24 mwaka huu katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Video hiyo imethibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, ambayo imehakikisha kwamba idara zote za serikali " zimesimama kidete " kuhakikisha kuwa mateka huyo anachiliwa huru.
Katika video hiyo ya sekunde ishirini na moja, Isabelle Prime ameonekana akivalia nguo nyeusi, huku akiikaa sakafuni, na akiwaomba marais wa Ufaransa François Hollande na wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi, msaada ili aweze kuachiliwa huru. "Tafadhali mnisafirishe Ufarnsa haraka iwezekanavyo ”, amesema mateka huyo.
“ Hii ni video ambamo ameonekana Isabelle Prime ”, naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Alexandre Giorgini amesema, akithibitisha uhalali wa video hiyo, ambayo Rfi hakipendelea kuirusha hewani kwenye tovuti yake.
“ Idara zote za serikali ambazo zina uwezo zimesimama kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa raia huyo wa Ufaransa na mkalimani wake wanaachiliwa huru “, amesema Alexandre Giorgini,
Rais wa Ufaransa aliomba kuachiliwa huru kwa mateka huyo baada ya kutekwa nyara Februari 24 katika mji wa Sanaa. Ni kwa mara ya kwanza picha za mateka huyo zinawekwa hadharani tangu kutekwa kwake nyara.
Isabelle Prime mwenye umri wa miaka 30, alitekwa nyara akijielekeza kazini kwake, akiwa ameambatana na mkalimani wake Chérine Makkaoui. Watu waliohusika na kisa hicho walikua walijificha nyuso zao

Mama Tunu Pinda azindua Taasisi ya Manjano Foundation


Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.
Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .
Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake.
Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi. (DK)

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar.

Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch.

Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) akiwa na mtoa mada katika halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda

Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 

Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation.

Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bondo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.

Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda. 

wageni walikwa

Dunia yatazama Wakimbizi Nyarugusu, wa Mtabila warejea tena 

DSC_0015
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi ya mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na Kongo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team, Kigoma
WAKATI dunia kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahangika kutanzua changamoto za wakimbizi Nyarugusu, mkoani Kigoma imeelezwa kuwa idadi kubwa ya Wakimbizi waliorejeshwa nchini Burundi kutoka kambi ya Mtabila iliyoko Kigoma iliyofungwa rasmi Desemba, 2012 wameingia tena nchini na kujazana katika makazi ya muda ya Nyarugusu wakiomba hifadhi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Sospter Christopher wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekwenda kuangalia hali halisi ya kambi ya Nyarugusu na Wakimbizi akiambatana na Maofisa wa Umoja wa Mataifa akiwemo Mratibu wa Mashirika hayo nchini Alvaro Rodriguez.
Kurejea kwa wingi kwa Wakimbizi hao ni pigo kisaikolojia kwa watu ambao walirejeshwa nyumbani kwa kuonekana kwamba hali ni shwari na walikuwa wameanza kuishi maisha ya kawaida.
Mkuu huyo wa kambi alisema idadi hiyo ikichanganyika na wengine imafanya  kambi kuhemewa na kuonekana haja ya kutafuta eneo jingine la kupiga kambi kwa ajili ya Wakimbizi hao ambao mpaka mwishoni mwa wiki iliyopita walikuwa zaidi ya elfu 51.
“ Kwa sababu tunapokea idadi kubwa ya waomba hifadhi toka Burundi, tumekuwa tukiongeza idadi ya vituo vya mapokezi ili kukidhi mahitaji ya kuwapokea  wakati tukisubiri maelekezo toka ngazi za juu za kuwahamishia Migunga Hills eneo linalopendekezwa kufunguliwa kambi ya Nyarugusu B” alisema Christopher mbele ya Waziri Chikawe.
Alisema walianza kupokea waomba hifadhi hapo kambini kuanzia Aprili 29, 2015 kwa idadi ndogo kabisa ya watu 36, lakini idadi hiyo ilianza kuongezeka siku hadi siku na kufikia Mei 27 mwaka huu idadi yao ilifikia 48,333, idadi kubwa ikiwa wanawake na watoto.
Wakimbizi hao walikuwa wakipitia vituo vya Kigoma (27,638), Manyovu (4,439), Kilelema (1,603) na Kigadye (1,291).
Kambi hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 50,000 imeelemewa kwa sababu ya ujio mpya uliosababisha kuwepo kwa Wakimbizi zaidi ya 106,410.
Kuna matatizo zaidi ya milipuko ya wagonjwa kambi hii imechanganywa na  Wakimbizi wa Kongo watu ambao hawana utamaduni wa pamoja na kuonekana hatari ya kukabiliana kwa kutosikilizana.
 Aidha kambi hiyo pamoja na kuwahifadhi waburundi wapo pia Wakimbizi kutoka Kongo wapatao 54,706; Burundi,3261 ; Rwanda 72; Uganda 17; Sudan Kusini wanane; Kenya 7; Somalia 3; Ethiopia 1; Zimbabwe 1; na Ivory coast 1.
DSC_0072
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Alvaro Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (wa nne kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa taarifa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Akijibu  maswali ya waandishi wa habari walioambatana naye katika ziara hiyo kuhusu hali ya baadae ya Wakimbizi wa Kongo ambao wapo nchini kwa takribani miaka 19 sasa, Waziri Chikawe alisema kwamba serikali haina mpango wa kuwapa uraia kwa sasa ingawa Marekani imesema itawachukua Wakimbizi elfu 30 kuwapeleka kwao na kwingine duniani.
“hatuna mpango wa kuwapa uraia kwa sasa…” alisema Chikawe na kusema kwamba kwa kuondolewa kwa hao  wengine kutasaidia kupunguza idadi yao katika kambi hiyo.
Alisema kwamba ni lengo la serikali kuhakikisha kwamba kambi hiyo inapunguzwa ili kuweza kuchangia ipasavyo kwa hali bora ya Wakimbizi na kwamba mchakato wa kuwaangalia waomba hifadhi kama wanafaa kuwa Wakimbizi unaendelea.
Akizungumzia malalamiko ya upatikanaji wa chakula, Waziri Chikawe alisema kwamba si kweli kuwa kuna watu hawajapata chakula kwa siku saba la sivyo wangelikufa.
Alisema wengi wa Wakimbizi ni watoto na kwamba wanapoingia nchini wanapewa vyakula vikavu (kama biskuti)  lakini wakishafika kambini wanapewa chakula kilichopikwa na resheni ya siku 14 .
Alisisitiza kuwa kama kungelikuwa hakuna chakula watoto hao wasingeishi, labda kama wanataka kuongezewa chakula zaidi. (dk)
Kuhusu ujenzi wa kambi mpya Migunga alisema kwamba wataalamu wanaangalia barabara mbadala kwani iliyopo sasa pamoja na kuhitajika milioni 300 kuitengeneza lakini bado kila mvua itakapokuwa inanyesha itahitaji kutengenezwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika mahojiano na waandishi wa habari aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kufungua mipaka ili Wakimbizi waweze kuingia na kutoa eneo kwa ajili ya kambi mpya kutokana na ya sasa kujaa sana.
Aidha aliishukuru serikali ya Uingereza kwa kuwa ya kwanza kutoa misaada kwa ajili ya Wakimbizi hao na kutarajia nchi nyingine kama Marekani itafanya hivyo mapema ili kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuhudumia waomba hifadhi.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez amesema wanafanya kila linalowezekana ili kupunguza idadi ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu kwa kuwapatia eneo jingine la kujihifadhi.
Alisema kwa kuwatoa hapo watasaidia shule zilizofungwa ambazo zinasomesha watoto kutoka kwa Wakimbizi wa Kongo kurejea madarasani kukamilisha mtaala wao.
DSC_0038
Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakati akitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
DSC_0143
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakikagua sehemu wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi wa Waomba hifadhi hao wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.
DSC_0148
Muonekano wa moja ya chumba cha kulala familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu ambapo kifika muda wa kulala wanatandika mkeka chini katika vumbi hilo jekundu na kupata usingizi.
DSC_0097
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa Waomba hifadhi wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo  wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma walipotembelea kambi hiyo kukagua kambi hiyo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
DSC_0129
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati walipotembelea kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa juma lililopita.
DSC_0084
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akigawa vifaa vya matumizi ya nyumbani ambavyo ni Blangeti, Mkeka, Kontena la kuhifadhi chakula na dumu la maji la lita 10 kwa mmoja wa Waomba hifadhi waliowasili siku ya ziara ya kutembelea kambi ya Nyarugusu mwishoni mwa juma wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (mwenye shati jeupe).Kulia ni Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
DSC_0112
Waomba hifadhi  na familia zoa wakiwa katika foleni ya kupokea vifaa hivyo.
DSC_0107
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na Waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo akiwa ameambatana na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na Mwakilishi wa shirika la kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR).
DSC_0235
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wakinamama anayeishi kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakati wa ziara maalum ya kutembelea maeneo hayo iliyohusisha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
DSC_0244
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez  na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M) (katikati) ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
DSC_0177
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Mh. Mathias Chikawe alipotembela katika chumba maalum kichotumika kufanya usajili kwa Waomba hifadhi na familia zao kwa ajili ya kupewa hati ya kuwa Wakimbizi kamili kama watatimiza vigezo vinavyohitajika. Aliyeketi kulia ni Msajili wa Waomba hifadhi, Ndalo Charles Bogohe.
DSC_0188
Zoezi la usajili likiendelea kwa familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
DSC_0170
Wakinamama wakiandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama walivyokutwa na kamera ya modewjiblog
DSC_0052
Sehemu ya familia za Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Geita wakiendelea kujipanga baada ya kuwasili kwenye eneo hilo.
IMG_0586
Moja ya familia za waomba hifadhi ikiwa imejipumzisha mara baada ya chakula cha mchana huku nyuso zao zikionekana kuwa na furaha na matumaini mapya.
DSC_0058
Hili ni eneo ambalo Waomba hifadhi  kutoka nchini Burundi wa kambi ya Nyarugusu wakiteka maji safi kwa matumizi yao.
DSC_0340
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati wakielekea kukagua vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mapendo ambayo yamegeuzwa kuwa nyumba za kulala Waomba hifadhi, kutokana na uhaba wa makazi ya kuishi kwenye maeneo ya kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika msafara huo.
DSC_0327
Baadhi ya Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakiwa wamempumzika huku wengine wakipata chakula cha mchana kama walivyokutwa na kamera ya modewjiblog.
DSC_0329
Kinababa nao hushiriki kuandaa chakula cha mchana kwa familia zao kama huyu aliyekutwa na kamera ya modewjiblog.
IMG_0630
DSC_0335
Eneo la shule ya msingi Mapendo katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu ambalo kwa sasa linatumika kuhifadhi Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili nchini wakitokea Burundi kupitia mji wa Kigoma.
DSC_0350
Madawati ya wanafunzi katika shule ya msingi Mapendo yakiwa nje ya madarasa yakitumika kuanikiwa nguo na huku wakati wa msimu wa mvua yakinyeshewa.
DSC_0379
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakibadilishana mawazo na wasimizi wa kambi hizo za Nyarugusu wakati wa ziara ya siku moja wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
DSC_0279
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa ameambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakikagua eneo jipya litakaloitwa Nyarugusu B lililotolewa na serikali kwa ajili ya Waomba hifadhi wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma ambalo liko mbioni kutengenezwa na kukamilika ndani ya miezi 3 ijayo.
DSC_0302
Eneo jipya la kambi ya Nyarugusu B ambalo limetengwa na serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa ajili ya makazi ya Waomba hifadhi wanataotenganishwa Burundi na Congo mara tu baada ya kukamilika.
IMG_0642
Muonekano wa eneo jingine la makazi ya Waombahifadhi ndani ya kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
IMG_0644
IMG_0666
Amani na upendo itawale kati yetu……ndivyo wanavyosema kwa pamoja baadhi ya watoto waomba hifadhi wakifurahia picha pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Burundi: waandamanaji wakata tamaa baada ya mkutano wa Dar es Salaam 

Mtoto huyo anaangalia jinsi askari polisi wakiondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za mji wa Bujumbura, Mei 30 mwaka 2015.
Mtoto huyo anaangalia jinsi askari polisi wakiondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za mji wa Bujumbura, Mei 30 mwaka 2015.
Na RFI
Baada ya mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika Jumapili Mei 31 jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, raia katika wilaya za mji wa Bujumbura, nchini Burundi, hasa waandamanaji wamekata tamaa kufauatia uamzi wa marais hao.
Suala muhimu la awamu ya tatu ya Rais Pierre Nkurunziza halikuchukuliwa uamzi katika mkutano huo au hata kujadiliwa na marais hao wa nchi za Afrika Mashariki. Watu wamechukizwa na jambo hilo na wako tayari kuendelea na maandamano.
Katika wilaya za mji wa Bujumbura kunakofanyika maandamano kama Cibitoke na Nyakabiga, raia wamekata tamaa. Lakini pia wamekua na hasira, baada ya mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.(P.T)
Wakaazi wa wilaya hizo walikua na matumaini kuwa viongozi hao kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki wangemtaka rais Pierre Nkurunziza kuacha kuwania awamu ya tatu. Suala la kuahirishwa kwa uchaguzi kwa mwezi mmoja na nusu halina mabadiliko yoyote katika msimamo wao.
" Tumekataa tamaa moja kwa moja, kwa sababu hawakusema chochote kuhusu awamu hii ya tatu ya rais Nkurunziza. Marais wa kanda hii hawana uwezo wa kumshawishi Nkurunziza kuacha kuwania awamu ya tatu. Tunahitaji jumuiya ya kimataifa kutusaidia ili tuweze kukabiliana na mgogoro huu ", amesema raia mmoja aliyehojiwa na RFI.
" Hatukua na matumaini makubwa kuhusu mkutano huo. Tuna machungu kutokana na uamzi huo. huo ni usaliti wa moja kwa moja. Tutaendelea kuandamana, tutaendelea na harakati zetu. Lakini ukweli hatimaye utashinda ", wamesema raia wangine wa mji wa Bujumbura.
Serikali ya Burundi imekaribisha mapendekezo ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuahirisha Uchaguzi kwa angalau mwezi mmoja na nusu ili kukabiliana na hali ya kisiasa nchini humo.
Hata hivyo upinzani unasema umesikitishwa na mapendekezo ya marais hao waliokutana mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam na wameapa kuendelea na maandamano makubwa jijini Bujumbura leo Jumatatu.
Pacifique Nininahazwe kiongozi wa maandamano amesema kuwa wamesikitishwa kuwa viongozi hao wameshindwa kumwambia rais Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu.
Uchaguzi wa wabunge nchini Burundi umepangwa kufanyika tarehe tano mwezi huu, huku ule wa urais ukifanyika tarehe 26.
Itafahamika kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakushiriki mkutano huo na aliwakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Alain Nyamitwe. Hata rais wa Rwanda Paul Kagame alisusia mkutano huo, akibaini kwamba viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wamekua wakipigana chenga kuhusu uamzi mabo unapaswa kuchukuliwa dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Unicef : Dola za Marekani Milioni 500 zahitajika Iraq 

Mpiganaji wa Islamic State akibebelea bendera ya kundi lake, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.
Mpiganaji wa Islamic State akibebelea bendera ya kundi lake, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.
Na RFI
Mashirika mbalibali ya kibinadamu yanapanga kuzindua mchango wa kutafuta Dola za Marekani Milioni 500 kukabiliana na hasara iliyosabishwa na wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq.
Mchango huu unasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto Unicef.
Mwakilishi wa Unicef nchini Iraq Philippe Heffinck, amesema hali ya kibainadamu nchini humo ni mbaya sana na shirika hilo linahitaji fedha hizo ili kuendelea kuwasaidia zaidi ya watu Milioni 8 waliothirika.
Haya yanajiri wakati huu Marekania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa jijini Paris nchini Ufaransa kujadili namna ya kuendeleka kukabiliana na Islamic State nchini Iraq na Syria.(P.T)