TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, December 1, 2014

Thierry Henry kurudi Arsenal?

titi enzi hizo
Nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ameiaga timu yake ya New York Red Bulls aliyokuwa anaichezea baada ya mkataba wake kuisha .
Henry ameichezea Red Bulls kwa muda wa miaka minne na nusu na inadhaniwa kuwa huenda akatangaza kustaafu soka baada ya kuwa kwenye mchezo huo kwa karibu miaka 20 .
Henry ambaye katika ubora wake aliwahi kuzichezea timu za As Monaco , Juventus , Arsenal na Fc Barcelona ukiachilia mbali timu ya taifa ya Ufaransa alinukuliwa akisema kuwa angependa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Arsenal ambako inaaminika kuwa atajiunga na benchi la ufundi chini ya kocha wake wa zamani Arsene Wenger .
henry
Moja ya ishara zilizowapa watu sababu ya kuamini kuwa huenda kuna mpango wa nyota huyo kurejea Arsenal ni kitendo chake cha kubadili picha ya ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo alitoa picha inayomuonyesha akwia amevalia jezi ya New York Red Bulls na kuweka picha ya uwanja wa nyumbani wa Arsenal The Emirates Stadium .
Timeline ya ukurasa rasmi wa facebook wa Thiery Henry ikionyesha uwanja wa Emirates unaotumiwa na Arsenal .
Timeline ya ukurasa rasmi wa facebook wa Thiery Henry ikionyesha uwanja wa Emirates unaotumiwa na Arsenal .
Henry hadi leo anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya England katika historia ya ligi hiyo na amewahi kutwaa mataji karibu yote kluanzia kombe la dunia na kombe la ulaya akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa , Ligi za England na Hispania pamoja na ligi ya mabingwa barani ulaya .
Kocha wa klabu ya Girondins Bordeaux Willy Sagnol ambaye aliwahi kucheza na Henry kwenye timu ya taifa ya Ufaransa amemkaribisha nyota huyo kujiunga naye kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ufaransa ofa ambayo Henry bado hajakubali au kutoa tamko la kuikataa .
titi
Henry alijiunga na New York Red Bulls wakati mkataba wake na Fc Barcelona ulipomalizika na amekuwa moja kati ya wachezaji walisaidia kupandisha umaarufu kwenye ligi ya Marekani maarufu kama MLS .

Mchezaji bora wa Afrika huyu hapa 

FBL-WC-2014-MATCH54-GER-ALG
Kituo cha habari cha Uingereza  BBC kimemtaja nyota wa timu ya taifa ya Algeria Yacine Brahimi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Brahimi ambaye anachezea klabu ya Ureno ya Fc Porto anakuwa raia wa kwanza wa Algeria kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa na BBC kila mwaka .
Yacine Brahimi ametwaa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika .
Yacine Brahimi ametwaa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika .
Brahimi ametwaa tuzo hii kufuatia uwezo aliouonyesha kwa mwa huu akiwa na timu yake ya taifa hasa kwenye michuano ya kombe la dunia ambako Algeria walifanikiwa kufika hatua ya 16 bora .
BBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka ambapo kwa miaka miwili iliyopita kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure amekuwa akitawala .
yacine

Tuzo ya Ballon d’OR kwa hawa hapa.

FIFA Ballon d'Or Gala 2012
Orodha ya wachezaji watatu waliongia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Ballon’Dor inayotolewa kwa mchezaji bora wa dunia imetajwa hii leo .
Orodha hiyo imewajumuisha wachezaji watatu ambao ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo  , nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, na Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo  mwaka jana.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo mwaka jana.
Mchezaji ambaye anatetea tuzo hii hadi sasa ni Cristaino Ronaldo ambaye aliitwaa kwa mwaka 2013 na kwa jinsi mambo yanavyokwenda ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo mwakani .
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon'Dor.
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon’Dor.
Mshindi wa tuzo hii atatangazwa kwenye hafla itakayofanyika huko Zurich januari 12 ambapo tuzo mbalimbali zitatolewa .
neur
Kipa wa Ujerumani Manuel Neur atawania tuzo hiyo dhidi ya Lionel Messi na Cristaino Ronaldo.

Iraq yabaini wanajeshi hewa 


Uchunguzi wa idara ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini Iraq umebaini kuwepo kwa wanajeshi hewa 50,000 katika orodha ya malipo ya mishahara.
Askari hao wajulikanao kama askari mizimu yaani Ghost soldiers hawajawahi onekana kazini japo kuwa mishahara yao ilionekana kuendelea kulipwa kwa watu wasiojulikana.
Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Iraq ofisi yake imechukua hatua kuhusiana na tatizo hilo na tayari malipo ya mishahara hiyo ya skari hewa imekwisha simamishwa.
Vitendo vya rushwa ndani ya jeshi la Iraq vinatajwa kuchangia kurudisha nyuma vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiislam IS Kaskazini na Magharibi mwa taifa hilo.
                                                                                                      CHANZO:BBC

Siku ya kupiga vita dhidi ya ukimwi duniani 

Bango linalotahadharisha tatizo la Ukimwi nchini Afrika Kusini na wito kwa kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
Bango linalotahadharisha tatizo la Ukimwi nchini Afrika Kusini na wito kwa kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
Na RFI
Vita dhidi ya Ebola visipelekei kusahau kupambana dhidi magonjwa yanayoathiri afya ya watu kama ukimwi. Kufuatia siku ya kupiga vita dhidi ya ukimwi duniani, ripoti kadhaa zinaonyesha takwimu za kutia moyo, ikiwa ni pamoja na ile ya milioni 15, kwa mfano.
Hii ni idadi ya watu ambao wanaweza kunufaika kutokana na matibabu katika mwaka 2015. Hata hivyo, vita dhidi ya VVU viko mbali kufaulu.(P.T)
Iwapo takwimu zinaonyesha maendeleo ya kweli katika mapambano dhidi ya Ukimwi, takwimu hizo huficha mara nyingi ukweli wa hali ya mambo. Maambukizi mapya, ambayo ni takwimu muhimu kwa kupungua kwa Ugonjwa huo zimepungua kwa theluthi tatu tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini pia kukosekana kwa usawa kunaonekana kuko juu. Katika nchi nyingi kusini mwa Sahara barani Afrika, lengo la kupunguza idadi ya maambukizi haliwezi kukamilika.
Uchunguzi wa mwaka huu unaonyesha kuwa dunia imefikia hatua ya mageuzi katika kufikia mwanzo wa mwisho wa Ukimwi. Iwapo mafanikio makubwa yamewezesha nchi 26 kupunguza nusu ya maambukizi yao mapya, wanapaswa kujua kwamba kwa upande mwingine, watu waliotengwa au kubaguliwa, wameendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi.
Ni vema kuelewa kwamba huduma bora pamoja na kufanya vipimo mara kwa mara bila kusahau kuendelea kupata tiba vinapaswa kupewa kipaumbele Kaskazini na Kusini ili kukomesha maambukizi mapya kwa lengo la kupiga vita Ukimwi. Zoezi la kuhamasisha na kutoa taarifa kwa vijana wanaoishi kusini mwa Sahara barani Afrika linabakia kuwa suala muhimu katika kupambana dhidi ya Ukimwi.
Tangu kuzuka kwa virusi vya Ebola vinavyoendelea kushuhudiwa Afrika Magharibi sekta ya Afya imeendelea kukabiliana na mdororo wa mfumo wa matibabu , kwa sababu hata kama upatikanaji wa huduma bado unawezekana, wafanyakazi wa afya kwa kiasi kikubwa wameathirika. Mbio dhidi ya muda zilianza ili janga la Ukimwi lisiendelei kupata nafasi katika mataifa hayo.

POLISI WAPAMBANA NA WAANDAMANAJI HONG KONG


Polisi wakielekea kuwakabili waandamanaji mjiini Hong Kong.

Polisi wakimtia nguvuni mmoja wa waandamanaji.

Mmoja wa waandamanaji akipewa kichapo na piolisi.

POLISI mjini Hong Kong nchini China na waandamanaji wanaodai demokrasia wamepambana katika eneo linalozunguka makao makuu ya serikali.
Ili kutuliza maandamano hayo, polisi wamelazimika kutumia maji ya pilipili huku wakiwa wamejihami kwa silaha ili kuwatawanya waandamanaji.
Takribani watu 48 wanashikiliwa na polisi kutokana na maandamano hayo ambayo yamechukua miezi miwili hadi sasa.
Madai ya waandamanaji hao ni kutaka kuwa na uhuru wa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na Beijing.
Chanzo: BBC

Diamond aungana na wasanii wa Afrika kurekodi wimbo wa kupinga Ugonjwa wa Ebola

.
.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wa Afrika watakaosikika kwenye wimbo wa pamoja wa kampeni  ya kupinga ugonjwa wa Ebola ‘Africa Against Ebola’ wasanii walioshiriki katika kampeni hiyo akiwemo, Iyanya, Donald,Banky W,Kcee,Mafikizolo,Sean Tizzle na wengineo.
Hizi ni baadhi ya picha ambazo Nov 31 Diamond na Wasanii wa Afrika wameshoot  video ya wimbo huo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..

Zawadi ya gari kwenye birthday sio bongo tu, Lil Wayne kampa mwanae haya mawili

Lil Wyne 1
Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba mtoto huyu wa miaka 16 wa hiphop staa wa kitambo duniani, Lil Wyne….. Reginae Carter anaweza kuweka stika kwenye gari lake aina ya BMW alilozawadia ikisoma >>> ‘gari langu jingine ni Ferrari
Sherehe ya kutimiza kwake miaka 16 ilifanyika Atlanta Marekani ikiambatana na tamasha dogo ambalo Nicki Minaj aliimba “Moment 4 Life” na “Flawless (Remix) kwenye stage na kushuhudiwa na baadhi ya mastaa akiwemo T.I, Tiny, Kandi Burruss, Fantasia na Jacob Latimore.
wyne 2
Birthday girl mwenyewe ambae ni msanii chini ya lebo ya Young Money alichukua time yake kwenye stage na kuimba single yake ya ‘mind going’
wyne 3
wyne 4
wyne 5
wyne 6
wyne 7
Wyne 8
Wyne 9
wyne 10
Rg 1
rg 2
rg 3
rg 4
rg 5
rg 6

Safari hii ni wanne waliotolewa #BBA_Hotshots, Unajua kura zinamuweka kwenye nafasi ipi Idris?

DSC06323
Goitse.
Siku ya 56 ripoti ikufikie kutoka ndani ya jumba la Big Brother Africa #BBA9_Hotshots kwamba November 30 2014 ni washiriki wengine wametolewa kwenye jumba hilo na kufanya game iendelee kunoga…………. ulikuwa mbali na TV yako usiku wa tukio hili? nimekuandikia ripoti yote hapa.
Goitse mshiriki wa kutoka Botswana, Ellah mwakilishi kutoka Uganda, Sheillah mwakilishi wa Botswana na Trezagah kutoka Msumbiji ndio washiriki walioyaaga haya mashindano Novemba 30 2014.
Idadi ya washiriki waliobakia ni nane tu akiwemo Idris kutoka Tanzania ambapo kwa mujibu wa ukurasa wa Big Brother matumaini yaliyopo kwamba ikiwa msimamo wa kura ukiendelea poa kama hali ilivyo huenda neema ikawa kwa mshiriki huyo akarudi na ushindi.
DSC06321
Ellah.
DSC06331
DSC06334
Idris.
Sheillah.
Sheillah.
Trezagah.
Trezagah.
DSC06338

Nakukutanisha na mapacha wasio na birthday moja

twins
Mapacha wenyewe ndio hawa ambapo wote ni wa kike.
Kwa kawaida mapacha wanazaliwa siku moja wakiwa wametofautiana muda mfupi sana na mara nyingi huwa inakuwa ni sekunde au dakika toka wakati anapozaliwa mmoja mpaka wakati anakozaliwa mwingine na hii ni kwa sababu kibaiolojia haiwezekani kwa watoto wawili kutoka tumboni kwa wakati mmoja.
Lakini Uingereza imeweka rekodi hii ya kuwa na watoto mapacha ambao siku zao za kuzaliwa ziko kwenye tarehe mbili tofauti yaani kama mmoja amezaliwa tarehe 1 mwingine amezaliwa tarehe 2.
Huko Bolton watoto Scarlett na Robbyn wameweka rekodi hii baada ya mama yao kujifungua watoto wawili kwenye tarehe mbili tofauti, ilianza kama utani wakati ambapo mama huyo aliingia kwenye maumivu ya uchungu wa kuzaa saa chache kabla ya kuingia kwa siku mpya ambayo kwa mahesabu ya kidunia huanza saa sita usiku.
Hawa ni mapacha ambao mwaka 2013 walivunja rekodi ya kuzaliwa katika nchi mbili tofauti, mmoja alizaliwa England na mwingine Scotland ambapo wa pili alizaliwa dakika 100 baada ya wa kwanza kuzaliwa.
Hawa ni mapacha ambao mwaka 2013 walivunja rekodi ya kuzaliwa katika nchi mbili tofauti, mmoja alizaliwa England na mwingine Scotland ambapo wa pili alizaliwa dakika 100 baada ya wa kwanza kuzaliwa.
Kabla ya kufika kwa saa sita kamili usiku majira kama ya 5 na dakika 45 usiku mama huyo alijifungua mtoto mmoja huku akingojea kujifungua mwingine kwani alifahamu fika amebeba mapacha.
Mtoto mwingine alikuja kuzaliwa dakika 18 baada ya saa sita usiku kupita na hivyo kufanya ionekane kuwa watoto mapacha Robyn na Scarlett wamezaliwa kwenye tarehe za siku mbili tofauti mmoja akiwa amezaliwa saa tano usiku kabla ya siku mpya kuanza na mwingine akiwa amezaliwa baada ya saa sita usiku saa chache baada ya siku mpya kuanza.