TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, June 5, 2014

BRAZIL YATETEA MAANDALIZI YAKE 

140604115528 brazil dima 512x288 bbc nocredit 82aea
Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea jinsi ambavyo taifa lake limetayarisha Kombe la Dunia litakaloanza juma lijalo jijini Sao Paulo.
Alisema kuwa michezo hiyo itakuwa yenye ufanisi mkubwa ijapokuwa kumekuwepo na kukosolewa kwa kuchelewa kwa nyanja na miundombinu mbalimbali.

Aliwaambia wanahabari kuwa matatizo ya aina ile ni ya kawaida kila mahali.
Bi Rousseff ambaye huenda akakumbwa na maandamano mapya ya kupinga serikali, alisema kuwa hawataruhusiwa kuvuruga mashindano hayo
''Kila mahali duniani, miradi mikubwa ya uhandisi mara kwa mara hutatizika," bi Rousseff aliwaambia wanahabari kutoka katika mataifa ya kigeni katika makazi ya rais jijini Brasilia.
Alisema kuwa hakuna anayeweza kutengeneza reli za chini ya ardhi isipokuwa labda Uchina.
Hayo aliyasema kuhusu kuchelewa kwa miradi ya miundombinu, jambo ambalo limewakera wananchi wengi wa Brazil waliotarajia kunufaika kutokana na kuboreswa kwa miundombinu hiyo.
Mifumo ya usafiri katika miji ya Cuiaba, Salvador, Recife na miji mingine mingi haijakamilishwa kwa kuwa juhudi zote zilielekezwa katika kukamilika kwa nyanja za kandanda zitakazotumika katika mashindano hayo.
Rais huyo alitaja kuchelewa huko kama ''gharama ya demokrasia yetu.''
Akizungumzia maandamano ya kupinga Kombe la Dunia la hivi majuzi- ambayo baadhi yaligeuka kuwa vurugu- rais alisema kuwa ingawa maandamano yaliambatana na demokrasia, maelfu ya polisi na askari zaidi watatumiwa kuhakikisha kuwa haitavuruga Kombe la Dunia.
''Tunawahakikishia watu wote usalama," alisema.
'Uangalifu wa karibu'
Uwanja wa Sao Paulo
Zaidi ya watu milioni moja waliingia mitaani wakati wa michezo ya Confederation kuandamana kupinga ufisadi na kile wanachodhani ni matumizi ya kupindukia katika kutayarisha Kombe la Dunia.
Maandamano hayo ambayo mwanzo yalianza kama makusanyiko madogo ya watu waliopinga kuongezeka kwa naulikatika usafiri wa umma ulianza kuwa baada ya polisi kutumia mbinu nzito kuwatawanya waandamanaji.
Bi Rousseff alisema kuwa vikosi vya usalama vitafanya kazi kwa uangalifu wakati huu.
Kikundi kidogo chenye waandamanaji wanaopinga serikali kililenga mechi ya kirafiki iliyokuwa ikichezwa baina ya Brazil na Panama katikati ya jiji la Goianiasiku ya Jumanne.
Waandamanaji hao waliokusanyika karibu na uwanja walikemea gharama kubwa ya michezo hiyo huku wakisema kuwa pesa nyingi ingetumiwa kugharamia huduma za umma ili kupunguza kukosekana kwa usawa.
Michezo hiyo itaanza tarehe 12 mwezi Juni huku wenyeji Brazil wakichuana na Croatia jijini Sao Paulo.
CHANZO BBC

ENGLAND YABANWA NA ECUADOR

140605013007 mechi ya england  512x288 bbc a748e
Katika mechi za kirafiki kwa maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, England ilitoka sare ya 2 - 2, dhidi ya Ecuador katika mechi iliyochezwa huko Miami. Timu ya England iliongozwa na Frank Lampard.
Raheem Sterling ambaye huchezea kalbu Liverpool, alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United.

Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki itakayofuata.
Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda mapumziko.
Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.
CHANZO BBC

MMILIKI WA NYIMBO ZA BOB MARLEY AAMULIWA 

140605004209 bob marley 512x288 bbc 5ae7d

Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.

Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.
CHANZO BBC

G7 WAKUTANA BRUSSELS BILA URUSI

140604214835 g7 brussels 512x288 pa nocredit d4af3
Na Hudugu Ng'amilo
Viongozi wa mataifa tajiri ya magharibi wanaokutana mjini Brussels wamesema kuwa wako tayari kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi iwapo itaendelea kuvuruga amani mashariki mwa Ukrain.
Taarifa ya pamoja ya mataifa ya G7 imesema kuwa Mambo yanayofanywa na Urusi nchini Ukrain hayawezi kubalika kamwe na lazima yakomeshwe.

Huu ndio mkutano wa kwanza wa viongozi hao tangu waifukuze Urusi kama mwanachama.
Urusi ilibumburushwa kutoka G7 kwa kosa lake kubwa zaidi, kuinyakua Crimea kutoka Ukrain.
Viongozi wa mataifa hayo ya G7 wanakutana sasa kwa mara ya kwanza tangu wakati huo.
Lakini huku wakikutana mapigano yamechacha kati ya serikali ya Ukrain na majeshi yanayo unga mkono Urusi mashariki mwa Ukrain.
Urusi imeendelea kukana kuhusika na mapigano hayo. Miongoni mwa mikutano iliyopangwa Alhamisi hii, waziri mkuu wa Uingereza Davin Cameron atakutana na rais Obama mjini Brussels, ambapo kwa upana zaidi watazungumzia Urusi. Kisha baada ya mkutano huo, David Cameron ataelekea Paris Ufaransa kwa mkutano wa faragha na rais wa Urusi Vladmir Putin.
D-Day barani Uropa
Katika wiki hii mataifa ya Uropa yamekuwa yakiadhimisha siku ya kuikomboa bara Uropa kutoka utawala wa ki Nazzi katika vita vya pili vya dunia miaka 70 iliyopita.
Huku hayo yakitokea, juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi miongoni mwa mataifa ya magharibi kumaliza uhasama kati yao na Urusi.
G7 wamepongeza uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Ukrain na wameirai Urusi kumpokea na kushirikiana na rais mpya wa Ukrain Petro Poroshenko. Pia wameonya kuwa hawatasita kuiwekea Urusi vikwazo zaidi iwapo itakataa kusaidia kurejesha uthabiti Ukrain.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa miaka 17 ambapo G7 inakutana bila Urusi.
CHANZO BBC

Tuesday, June 3, 2014

LISU ARUSHA KOMBORA LINGINE KWA MAWAZIRI 

lissupx b4f46
Na Hudugu Ng'amilo
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Binilith Mahenge, jana walituhumiwa kutumia vibaya nafasi zao kwa kuweka fedha nyingi za miradi ya maji katika maeneo wanakotoka, huku sehemu zenye matatizo ya huduma hiyo zikitengewa fedha kiduchu.
Ilielezwa bungeni jana kuwa Profesa Maghembe ambaye ni Mbunge wa Mwanga, Kilimanjaro, wizara yake imetenga Sh1.4 bilioni kwa ajili ya miradi ya maji, ambazo ni zaidi ya mara saba ya Sh190 milioni zilizotengwa kwa ajili hiyo katika Wilaya ya Ikungi, Singida.
Akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji jana, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alihoji kile alichokiita upendeleo wa wazi katika ugawaji wa fedha za maji, unaoipa kipaumbele baadhi ya mikoa wanakotoka mawaziri.
Pia aliitaja Wilaya ya Makete, Njombe anakotokea Dk Mahenge ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji kuwa imetengewa Sh1.9 bilioni na kusema: "Upendeleo wa aina hii haufai kwa sababu utaleta matatizo na siyo haki hata kidogo."
"Profesa Maghembe atueleze sababu za kutenga bajeti hii kwa upendeleo, huku mikoa isiyokuwa na vyanzo vya maji, mito ya kudumu na mabwawa ya maana imepewa bajeti kidogo ikilinganishwa na ile yenye mifumo mizuri ya maji," alisema Lissu.
Alisema licha ya Profesa Maghembe katika hotuba yake kutaja mikoa ya Dodoma, Singida, Simiyu na Shinyanga kuwa inakabiliwa na upungufu wa maji, imetengewa kiasi kidogo cha fedha, huku mikoa inayopata mvua za kutosha na vyanzo vya uhakika vya maji ikitengewa mabilioni ya fedha.
"Dodoma imetengewa Sh7.2 bilioni, Singida Sh3.2 bilioni, Shinyanga Sh3.2 bilioni na Simiyu Sh2.8 bilioni, wakati mikoa yenye vyanzo vya maji na mvua za kutosha imetengewa fedha nyingi; mfano ni Tanga Sh10.7 bilioni, Kilimanjaro Sh6.3 bilioni, Mbeya Sh9.2 bilioni na Mtwara Sh7.5 bilioni," alisema.
Lissu alisema hali hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa mawaziri hao wanatumia mamlaka yao kujipendelea na kuhoji kama huo ndiyo utaratibu wa Serikali ya CCM... "Kama utaratibu wa mgawanyo wa fedha ndiyo huu sisi tunaotoka mikoa yenye ukame tutapataje maji?"
Jana Profesa Maghembe aliendelea kuwa katika wakati mgumu, baada ya kuandamwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alimwita kuwa ni mzigo kutokana na kutokutolewa kwa fedha za miradi ya maji.
Mnyika alionyesha kushangazwa na wabunge wenzake kuunga mkono bajeti ya wizara hiyo, licha ya kuwa ndogo na fedha za miradi zimekuwa hazitolewi kama inavyotakiwa.
"Kwa kufanya hivi sidhani kama tunamsaidia Profesa Maghembe ambaye ni CCM. Fedha zilizotengwa mwaka jana kuisaidia wizara hii hazijatoka na za bajeti hii hazitatoka kwa kiwango cha kuwezesha utekelezaji. Namna bora ya kumsaidia ili viongozi wa CCM wasiendelee kumwita mzigo ni kuikataa bajeti hii ili Serikali irudi mezani na kujiuliza."
Mnyika alisema kuwa hata ahadi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa Serikali itaongeza Sh80 bilioni kwa wizara hiyo kabla ya Mei 31 mwaka huu nayo haijatekelezwa na kusisitiza kuwa wabunge wakiipitisha bajeti hiyo watakuwa wameuziwa mbuzi kwenye gunia.Alisema kuwa hata miradi ya maji jijini Dar es Salaam ambayo Profesa Maghembe aliahidi kuwa itakamilika mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde alisema Profesa Maghembe amechota mabilioni ya fedha na kuyapeleka katika miradi ya maji kwenye jimbo lake la uchaguzi wakati maeneo mengine ameyaacha licha ya kuwa yana kipaumbele na kwamba anatumia miradi ya Serikali kujinufaisha kisiasa.
"Ukitaka takwimu zote ninazo hapa, idadi ya watu kwako ni wachache kuliko hata kwangu lakini kwa vipindi viwili mfululizo umekuwa ukijitengea mabilioni ya fedha, wewe ni mzigo kabisa," alisema Silinde.
Mwandosya amtetea
Wakati akijibu hoja za wabunge, Profesa Maghembe hakugusia tuhuma hizo na badala yake Profesa Mwandosya alimtetea akisema miradi hiyo katika wilaya za Same, Mwanga na Korogwe ilianza wakati yeye (Mwandosya) akiwa Waziri wa Maji... "Si kweli kwamba Profesa Maghembe anapendelea jimbo lake kwa sababu hakuwa waziri wa wizara hiyo wakati mradi huo unaanzishwa. Wananchi wa Same, Mwanga, Korogwe na Simanjiro wana haki ya kupata maji kama wananchi wa sehemu nyingine yoyote. Mwacheni waziri atekeleze majukumu yake ili watu hawa wapate maji".
Alisema mradi wa maji wa Same, Mwanga na Korogwe ni muhimu sana kwa sababu utakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 400,000 ambao hawapati maji kabisa.
Alisisitiza kuwa yuko tayari kubeba lawama juu ya mradi huo na si Profesa Maghembe, kwani waziri huyo anafanya kazi nzuri ya kutekeleza mradi huo ambao ulikuwapo hata kabla hajapelekwa katika wizara hiyo.
CHANZO MWANANCHI.

Monday, June 2, 2014

Habari mpya kuhusu Chris Brown na kesi zake mahakamani

brown
Licha ya video yake ya Loyal kuendelea kumuweka pazuri kwenye soko lake la muziki,  bado kwenye maisha binafsi ya Chris Brown mambo yake hayapo vizuri.
Siku ya May 9 Chris Brown alihukumiwa siku 131 kwenda jela kwa baada ya kwenda tofauti na masharti aliyopewa kutokana na kesi ya Rihanna.
Chris Brown hivi sasa ameachiwa huru baada ya kukaa jela siku 108 na miezi michache ijayo kesi yake nyingine ambayo ilitokea Washington D.C itaanza kusikilizwa.

Taarifa ya kuwasili kwa Taifa Stars na walivyopongezwa kwa ushindi

9s4a0125
Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.
Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.

Wazungu noma, Wametengeneza hii ndege inayotumia nguvu ya jua, tayari imeanza kuruka

solar
Ndege inayoendeshwa kwa kutumia nguvu ya jua ya Solar Impulse 2 aircraft ambayo ni ya pili katika mfululizo wa ndege za aina hiyo zinazotengenezwa nchini Uswizi leo imeanza safari yake ya kwanza kutoka katika kiwanja chake Magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa watengenezaji, Ndege hiyo ambayo kwa asilimia kubwa inategemea nguvu ya jua ilipaa angani kwa takribani saa mbili na dakika 15 na kufanikiwa kuruka umbali wa mita 2400.
solarimpulse
Kabla ya kufanya majaribio ya toleo hilo la pili, marubani wa ndege hiyo André Borschberg na Bertrand Piccard walitumia muda mwingi katika toleo la kwanza la ndege kama hiyo iliyopaa Ulaya hadi Moroco na kupitia nchini Marekani mwaka 2010 kwa muda wa saa 26 bila kutua.
Baada ya muda mrefu wa majaribio na maandalizi, Watengenezaji hao na marubani wamefanikiwa kuirusha ndege ya pili leo kwa kutumia jua pekee ambapo ilitua saa mbili baadae.
sol2
Solar Impulse 2 ni kubwa zaidi ya ile ya kwanza lakini ina uzito mdogo ukilinganisha na baadhi ya magari.
Viti vya ndege hiyo vinaweza kulala ambapo sehemu ngumu zaidi itakuwa ni kukatisha katika bahari za Atlantic na Pacific safari inayoweza kuchukua siku tano mchana usiku.
Sasa jiulize ikianza kutumika kupandisha abiria utakuwa tayari kupanda?

BUNGE LAONGEZWA MUDA KUJADILI VAT,ARDHI 

makinda_b04e9.jpg
Dodoma. Bunge limeongeza muda wa vikao kwa siku tatu zaidi ili kutoa nafasi kwa wabunge kujadili Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambao unalenga kuondoa misamaha ya kodi.
Kwa mujibu ya ratiba ya awali, vikao vya Bunge vilivyoanza Mei 6, mwaka huu vilikuwa vimalizike Juni 27, mwaka huu lakini sasa ratiba hiyo imesogezwa hadi Juni 30, mwaka huu.
Wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Anne Makinda alikaririwa akisema kuwa Bunge litaongeza muda ili kujadili muswada huo na ripoti ya kamati teule iliyoundwa kuchunguza migogoro ya ardhi nchini.
"Kwa mujibu wa kanuni zetu, hatuingizi kitu kingine katika Bunge la Bajeti zaidi ya bajeti, lakini tunaangalia uwezekano wa kuongeza muda baada ya bajeti kwa siku chache kwa sababu ya mambo yanayotakiwa kufanyika. Naambiwa kuwa Serikali inataka kuleta sheria inayohusiana na VAT."
Hivi karibuni akiwa bungeni, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alitishia kukusanya sahihi za wabunge kumwondoa Spika Makinda iwapo muswada huo hautawasilishwa katika Bunge hili la bajeti ili kufuta misamaha ya kodi.
Mbunge huyo alisema katika bajeti iliyopita, nchi ilipoteza Sh1.5 trilioni kwa misamaha ya kodi kiwango ambacho ni sawa na kile kilichopungua katika Bajeti ya Serikali mwaka jana.
"Kama hawajaleta muswada kiofisi, mimi siwezi kufanya chochote lakini nimesikia kuwa Serikali inataka kuleta muswada huo," alisema Makinda.
Kuhusu ripoti ya migogoro ya ardhi nchini, Makinda alisema kuongezwa kwa siku hizo kutawawezesha wabunge kuijadili.
Alisema kamati ya Bunge iliyopewa kuchunguza migogoro hiyo ilikwenda mbali zaidi na kuona vitu vingi yakiwamo matatizo yaliyopo katika mfumo.
Kamati hiyo teule iliundwa Novemba 9, mwaka jana na Makinda, kuchunguza migogoro inayowahusisha wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Wajumbe waliounda kamati hiyo ni Profesa Peter Msola aliyekuwa Mwenyekiti na wajumbe Jenista Mhagama Magdalena Sakaya, Joseph Selasini na Christopher Ole Sendeka.
Kamati hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza kasoro zilizopo katika matumizi ya ardhi na kupeleka mapendekezo bungeni, ambayo yatapunguza na kuondoa migogoro ya muda mrefu yanayoendelea kati ya wakulima, wafugaji, wawekezaji na watumiaji wengine wa ardhi.(E.L)

MAREKANI IMEKOSEA KUWAACHILIA TALIBAN WA 5

140602011947 bergdahl parents 304x171 ap 3530c
Na Hudugu Ng'amilo
Serikali ya Afghanistan imeghadhabishwa na makubaliano ya Marekani kukubali kuwaachia huru wanamgambo watano wakuu wa Taliban, ili kuachiwa huru kwa mwanajeshi mmoja wa Marekani.
Wafungwa hao kutoka gereza la Guantanamo walikabidhiwa Qatar...

Wengi walielezea ghadhabu kwa hatua hii. Kwa upande wa Afghanistan wanasema kuwa katika mpango kama huu, kwa mujibu wa sheria za kimataifa wafungwa hawastahili kukabidhiwa kwa nchi ya tatu. Lakini hilo sio sababu kubwa ya kuwatia matumbo joto.
Afghanistan hasira ya kubwa ni kuwa wafungwa wale wameachiliwa. Sasa wanawasiwasi kuwa mashambulio yatazidi. Watarudi kujiunga na kundi lao kwa maana kuwa serikali inajitahidi kupiga vita Al Qaeda ilhali Marekani inawaachilia, tena watano kwa ajili ya mwanajeshi wao mmoja.
Kwanza kabisa hao walioachiliwa sio wafungwa wa hivi hivi tu, ni mibabe walioshutumiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Al Qaeda. Kwa hiyo wadau wengi katika jamii yakimataifa wanahofia.
Bila shaka hii ni hatua kubwa nyuma katika kukabili Ugaidi na hasa Kundi hilo la AL Qaeda. Wadau wengi wana wasiwasi ni ujumbe gani hatua hii itatuma kwa magaidi wengine. Wafungwa sio hawa tu, Je Marekani itaendelea kufikia makubaliano na magaidi kama hawa ?
Bowe Bergdahl ameachiliwa
Taliban walimteka mwanajeshi mmoja wa Marekani (Bowe Bergdahl) ambaye inaaminika walimzuilia nchini Afghanistan kwa zaidi ya miaka 5.
Sasa wamekuwa wakidai kuwa wanataka viongozi wao waliokamatwa waachiliwe. Marekani imejaribu njia zote, na la kushangaza ni kuwa wamekiri wazi kuwa wameshindwa kumuokoa na ikabidi wafikie makubaliano na hao wanamgambo.
Sasa Bowe yupo hospitalini Ujerumani, anapokea matibabu na itachukua muda mrefu kabla ya kurudishwa nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa ameathriika kisaikolojia na lazima kwanza atibiwe.
Chini ya sheria ya kimataifa hakuna ruhusa kwa yeyote kufanya mashauriano na watekaji nyara au hata kulipa ridhaa yoyote kwa watekaji nyara.
Kwa hiyo mashirika makubwa yakimataifa au hata nchi na serikali zinaposikia mfanyikazi wao ametekwa au mwnajeshi, kawaida ni kutafuta mbinu za kumuokoa.
Huwa hawazungumzii kuwa wamelipa ili aachiliwe. Na japo kun abaadhi ya mashirika au nchi ambao wameshukiwa kulipa, hakuna anayekiri. Kukubali matakwa ya watekaji nyara ni kinyume na sheria za kimataifa
Ni sababu hii imemfanya rais Barack Obama akemewe hata na wanasiasa kutoka nchini mwake hasa wa Republican. Japo wanasema kuwa wamefurahi mwanajeshi wao ameachiliwa, wengi wanashuku gharama itayowafika ya kuwaachilia wafungwa watano wa Taliban. 
CHANZO BBC

WANANAWAKE WABAKWA GEREZANI - DRC

120601190230 women drc 304x171 afp 86619
Na Hudugu Ng'amilo
Utafiti uliofanywa na shirika moja la misaada Uingereza umeonesha kuwa ubakaji unatumiwa tena kwa kiasi kikubwa gerezani kama adhabu kwa wanawake wanaojihusisha na masuala ya siasa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Utafiti huo uliofanywa na "Freedom from Torture" umegundua kuwa zaidi ya nusu ya wanawake wote walio fanyiwa uchunguzi walikuwa wamebakwa na magenge.
Shirika hilo ambalo huwasaidia waathiriwa wa ubakaji umewafanyia uchunguzi wanawake 34. Ubakaji umekuwa ukitumika kwa miaka mingi kama silaha katika vita vya mashariki mwa DRC lakini shirika la ''Freedom from Torture'' linasema kuwa sasa wanawake magerezani kote nchini humo wanabakwa kama njia moja ya kuwaadhibu na kuwanyamazisha kutozungumza au kuchangia siasa za nchi hiyo.
Wanawake hao waliofanyiwa uchunguzi wanajumuisha wachuuzi, wasomi na hata wataalamu mbali mbali kati ya miaka 18 na 62 kote nchini humo.
Takriban hao wote walitiwa nguvuni kwa kujihusisha na masuala ya haki za binadamu au kampeini za kisiasa, au hata jamaa katika familia yao alihusika na siasa.
Zaidi ya nusu ya wanawake hao wanasema wamebakwa na magenge hata wanaofika kumi. Shirika hilo sasa linataka serikali ya DRC kufanya hima kutekeleza azimio la umoja wa mataifa dhidi ya kuwatesa watu.
CHANZO BBC

Huyu ndie kijana anayetaka kurusha ndege dunia nzima akiwa peke yake.

matt3
Vijana wengi wenye umri wa miaka 19 wanajipanga kwa ajili ya likizo ya majira ya joto. Lakini ni tofauti wa kijana Matt Guthmiller kutoka jijini Las Vegas nchini Marekani  anatarajia kutumia likizo yake hiyo kwa kurusha ndege dunia nzima akiwa yeye mwenyewe yani peke yake.
matt2
Guthmiller anatarajia kurusha ndege ya 1981 Beechcraft A36 Bonanza kwa matarajio ya kuwa rubani wa kwanza mwenye umri mdogo kurusha ndege dunia nzima peke yake.
Anasema ameguswa na kijana mwenye umri wa miaka 21 Jack Wiegand ambaye alikamilisha safari yake ambapo sasa anashikilia rekodi ya kitabu cha Guinness.
matt
Safari hiyo inatarajia kufanyika kwa takribani siku 40 au saa 160 za kusafiri angani ingawa anapanga kusimama katika vituo 20 katika mabara matano na kuweka kila anachokifanya katika mitandao ya kijamii.
Ingawa rubani huyo mdogo mipango yake ni kupata nafasi katika kitabu cha rekodi za dunia, Guthmiller anasema safari yake hiyo itawahamasisha vijana wengine kufuata ndoto zao.

Uamuzi wa Mahakama kuhusu yule jamaa aliemshambulia Brad Pitt red carpet

Screen Shot 2014-06-02 at 9.16.26 AM
Movie mpya ya Angelina Jolie ( Maleficent) ni movie ambayo siku inaonyeshwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita kulitokea ishu ya Brad Pitt ambae ni mume wa Angelina Jolie kuvamiwa na kupigwa usoni na mtu yuleyule ambae amekua akihusishwa kuvamia mastaa kwenye red carpet kama Will Smith.
Screen Shot 2014-06-02 at 9.09.35 AM
Angelina kwenye movie yake mpya ya Maleficent
Brad hakuumia na badala yake aliendelea kukutana na mashabiki mbalimbali waliojitokeza huku aliemvamia akikamatwa na kupelekwa polisi ambapo taarifa mpya kuhusu huyu jamaa aliemshambulia Brad, ni kwamba atakua chini ya uangalizi kwa miaka mitatu na pia ameonywa kuwa anatakiwa kukaa mbali na shughuli za mastaa kwa umbali wa mita 457.
Show ambazo hatakiwi kujisogeza ni pamoja na uonyeshwaji wa movie pamoja na utolewaji wa tuzo na pia katika uangalizi wa miaka mitatu, Sediuk anatakiwa kufanya kazi za kijamii kwa siku 20.
Screen Shot 2014-06-02 at 9.28.25 AM
Sediuk pia ameonywa kukaa mbali kabisa na Angelina Jolie pamoja na Brad, vilevile atatakiwa kwenda kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

Mtoto wa Pele amehukumiwa kwenda jela aisee

 dogopele 

Edson Cholbi do Nascimento maarufu kama Edinho ni mchezaji soka mstaafu aliyecheza kama mlinda mlango katika klabu ya Santons ambayo Pele alicheza miaka ya 90.

Unaambiwa mtoto wa Pele mwenye umri wa miaka 43 alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutiwa nguvuni na sasa hivi uamuzi uliotolewa na Mahakama ulitolewa mjini Praia Grande katika jimbo la Sao Paulo unamuweka Edinho kwenye kifungo cha miaka 33 jela.
Kisa cha kuhukumiwa miaka hiyo ni kutokana na kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya pamoja na kuwa na uhusiano na wauzaji wakubwa wa dawa hizo nchini Brazil.

Taarifa rasmi ya Yanga kuhusu uwenyekiti wa Manji na kocha Maximo

1908319_739353366128611_8170079415409113241_n 
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay  Dar es salaam huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya anga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ili kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha wanachama kilichomuomba Manji kuendelea na uongozi ambapo mwenyekiti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama,  wameazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF