TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 11, 2014

A PROPOSED CHURCH BUILDING FOR GOOD NEWS INTERDENOMINATIONAL PROPHETIC FIRE MINISTRIES ( JENGO LINALO TARAJIWA KUJENGWA LA HUDUMA YA HABARI NJEMA)

 A MAN OF GOD, PROPHET STARFFORD GODSON JACOB, INVITES ALL THOSE MEN AND WOMEN OF GOD, TO CONTRIBUTE IN THIS SPECIAL ACTIVITY OF BUILDING THE CHURCH. IF YO FEEL BLESSED TO DO SO, PLEASE YOU MAY SEND YOUR CONTRIBUTION THROUGH THE FOLLOWING: EQUITY BANK AC 3001111174678 QUALITY CENTER BRANCH ( 2 Samuel 7: 5).
 for more details please contact the Prophet through +255757208288 / + 255713055459 
                   or 
E - M ail; gadsonstar@yahoo.com



  MTU WA MUNGU NABII STARFFORD GODSON JACOB, ANAWAKARIBISHA WATU WOTE WA MUNGU WA KIKE NA WA KIUME, KUCHANGIA KATIKA UJENZI WA KANISA. KILA ANAYEJISIKIA KUMTOLEA MUNGU ANAWEZA KUCHANGIA KUPITIA AKAUNTI NAMBA: 3001111174678 EQUITY BANK TAWI LA QUALITY CENTER NYERERE ROAD ( 2 samweli 7:5).
kwa mawasiliano zaidi piga simu +255757208288 / + 255713055459 
        au 
kwa barua pepe: gadsonstar@yahoo.com

MTU WA MUNGU NABII STARFFORD GODSON JACOB AKIOMBA KABLA YA KUANZA KUHUBIRI ( A MAN OF GOD, PROPHET STARFFORD GODSON JACOB PRAYING BEFORE START DELIVERING THE MASSAGE)


Wednesday, February 5, 2014

ZITTO AIBUKA NA DVD

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
WAKATI Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akijipanga kuanza ziara katika mikoa kadhaa nchini kujibu mapigo ya tuhuma dhidi yake zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ziara ya Operesheni M4C Pamoja Daima, mbunge huyo ameibuka na DVD inayowananga viongozi wa CHADEMA.
Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa DVD hizo zitasambazwa kwenye mikoa na maeneo yote atakayofanya mikutano ya hadhara mbunge huyo, kama moja ya harakati na mikakati ya kujisafisha na tuhuma za usaliti zinazomkabili ndani ya chama.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa DVD hizo zinatengenezwa kwenye kampuni moja iliyopo eneo la Kariakoo ambayo imepewa tenda ya kuchapa nakala 10,000 na kampuni nyingine zaidi ya tatu, nazo zimepewa tenda ya kuchapa DVD hizo kwa idadi tofauti.
Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba katika jaradio la DVD hizo kuna rangi ya njano, nyeupe, bluu nyepesi, bluu nzito pamoja na bendera ya taifa.
Rangi zilizotumika kwenye jaradio hilo hazina uhusiano na rangi za bendera ya CHADEMA wala chama chochote cha siasa nchini.
Mbali ya jaradio hilo kupambwa na rangi hizo, pia limepambwa na picha kadhaa za mikutano aliyopata kuifanya mwanasiasa huyo katika maeneo mbalimbali na nyakati tofauti nchini, huku picha kubwa ikimwonyesha Zitto akiwa amevalia suti huku akitabasamu.
Jaradio hilo pia limezungukwa na maandishi mbalimbali ambayo yanasomeka:
‘Uadilifu, Uzalendo na Uwajibikaji, ndio silaha yetu katika kutetea wanyonge na maskini wote wa Tanzania, tuungane kwa pamoja.’  ‘Tanzania Kwanza’
Maandishi mengine makubwa yanamtambulisha mbunge huyo ambayo  nayo yanasomeka:
‘Zitto Zuberi Kabwe, Mtetezi wa Wanyonge, Tumaini la Maskini wa Tanzania”
Jaradio hilo pia limeweka mawasiliano ya mbunge huyo ya simu ya mkononi, barua pepe, Facebook na Twitter.
Hakuna maelezo yanayoonyesha kama DVD hizo zinauzwa au zinatolewa bure.
Ndani ya DVD
DVD hizo ambazo nakala tunayo, zinaonyesha picha ya mikutano ya hadhara ya mbunge huyo aliyoifanya mkoani Kigoma mara baada ya Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA kumvua nyadhifa zake na Mahakama Kuu kushikilia hatima ya uanachama wake baada ya kukabiliwa na tishio la kuvuliwa uanachama.

Kwa mujibu wa DVD hizo, katika moja ya mikutano ya mkoani Kigoma, Zitto anasikika akiuambia umati wa wafuasi wake waliofurika kumsikiliza akieleza chanzo cha mgogoro wake na CHADEMA ni msimamo wake wa kuhoji hesabu za fedha za vyama vya siasa, kikiwemo CHADEMA na kumuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uhakiki.

Kama ambavyo amepata kukaririwa mara kwa mara, Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) anasema CHADEMA ilimtaka awajulishe kwanza kabla ya kumuagiza CAG kufanya ukaguzi ili kutoa fursa ya kuweka hesabu zao vizuri.

DVD hiyo pia inamuonyesha Zitto akisema sababu nyingine ya ugomvi wake na CHADEMA ni dhamira yake ya kutaka kuwania uenyekiti wa CHADEMA, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wafuasi wake, baadhi wakiwa na mabango ya kumsifia, Zitto anasema hajawahi kupewa fedha na CCM kuisaliti CHADEMA na kuongeza kwamba atakuwa wa mwisho kutoka ndani ya chama hicho alichojiunga nacho akiwa na umri wa miaka 16.

Dk. Kitila Mkumbo naye yumo

DVD hiyo pia inamuonyesha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la CHADEMA, Dk. Kitila Mkumbo, akieleza sababu za yeye kutaka kujiuzulu kabla ya Kamati Kuu kuamua kumvua uanachama.

Dk. Kitila pia anaonekana  kwenye DVD hiyo akielezea waraka ulioandikwa na Samson Mwigamba ambao ulinaswa ukielezea mikakati ya kutaka kuung’oa uongozi wa Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti.

Kwa kifupi maelezo ya Dk. Kitila ni  yale aliyopata kuyatoa siku yeye na Zitto walipofanya mkutano na vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam wakitetea waraka huo kwamba haukuwa wa uasi kama ilivyotafsiriwa na CHADEMA.

Wiki iliyopita gazeti hili liliibua mkakati  unaodaiwa kufadhiliwa na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kutaka kumtumia Zitto kupambana na CHADEMA waziwazi.

Katika mkakati huo CCM inadaiwa kutaka kukodisha helikopta ya kumpeleka Zitto katika mikoa minne kwa gharama ya sh milioni 50, mara tu baada ya CHADEMA kuhitimisha Operesheni yao ya M4C Pamoja Daima.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vilivyo karibu na Zitto na CCM, yeye na chama hicho sasa wana adui mmoja – CHADEMA; na wameamua kujibu mapigo baada ya kuridhika kwamba kwa vyovyote Zitto amekwisha kupoteza uanachama wake katika CHADEMA.

Nia yao ni kumtumia Zitto kuleta mpasuko katika CHADEMA, na kufunika mjadala wa mgogoro wa CCM, kero za wananchi na mchakato wa Katiba mpya.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA – Naibu Katibu Mkuu Bara, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Baraza Kuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – anatarajia kutumia helikopta yenye uwezo wa kubeba watu wanne, ambayo inadaiwa kukodishwa na wapinzani wa CHADEMA.

Kwa mujibu wa habari hizo, lengo la ziara ya Zitto ni kujibu mapigo ya CHADEMA, hasa katika maeneo ambayo baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho wamepita na kuzungumzia hatima yake kisiasa, hasa walipojibu maswali ya wananchi kuhusu sakata lake kuvuliwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, na hatimaye Zitto kwenda mahakamani kuzuia chama kujadili uanachama wake.

Katika kesi ya msingi, Zitto aliyewahi kuwa maarufu akiwa kiongozi wa CHADEMA, anaomba arudishiwe nyadhifa zake zote, na apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ili aweze kukata rufaa Baraza Kuu.
CHANZO NI TANZANIA DAIMA

WHO YAONYA KUHUSU WIMBI LA SARATANI

999_928f6.jpg
Uraibu wa pombe na sigara husababisha saratani
Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa saratani kote duniani.
Shirika hilo limesema nusu ya ugonnjwa wa Saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili kufanyika ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi, ulevi na uvutaji sigara.
Watu milioni kumi na nne wanajulishwa kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha miongo miwili ijayo.
Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa Saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu.
Taasisi hiyo imesema serikali zinahitajika kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu matumizi ya pombe na sukari kama vile kuongeza bei na marufuku ya matangazo ya kibiashara ya bidhaa hizo.
CHANZO:BBC

NINI HATMA YA KESI YA KENYATTA ICC? 

KESNYATA_185c0.jpg
Pande zinazohusika katika kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Mjini The Hague zimekuwa na kikao cha kujadili mstakabali wa kesi hiyo.
Kiongozi wa mashtaka wa ICC Fatou Bensouda amekiri kuwa bado hana ushahidi wa kutosha kuwezesha kesi hiyo kuendelea.
Mawakili wanaomwakilisha Rais Kenyatta wanataka kesi hiyo kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007 itupiliwe mbali.
Bensouda amesema kuwa bado kuna maswala yanayozua utata na ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina. Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa kiasi cha kujiondoa katika kesi hiyo.
Viongozi wa mashitaka ICC wanasema kuwa Kenyatta aliongoza ghasia hizo lakini kesi dhidi yake imefanywa dhaifu kutokana na baadhi ya mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo.
Mawakili wa Kenyatta wanatuhumu upande wa mashitaka kwa kusisitiza kutaka taarifa kuhusu akaunti ya benki ya Rais Kenyatta kuona ikiwa kuna pesa zozote zilizotolewa kwa lengo la kutumika wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/08
Wakili wa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi amesisitizia mahakama kuwa kutupiliwa mbali kwa kesi kutawakosesha waathiriwa haki. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi katika siku chache zijazo.
Rais Kenyatta alifikishwa ICC kutokana na tuhuma kuwa alikuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007/2008. Anakabiliwa na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.
Kadhalika Kenyatta alishitakiwa pamoja na makamu wake William Ruto kwa tuhuma sawa. Kesi dhidi ya Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Watu 1,200 walipoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 huku maelfu wakilazimika kutoroka makwao. Wote wamekanusha mashitaka.
Kesi yenyewe ilitarajiwa kuanza Jumatano, lakini ikaahirishwa kwa mara ya nne mwezi jana wakati ambapo wendesha mashitaka waliposema kuwa shahidi mwingine alijiondoa kwenye kesi huku wakiomba mahakama kuwapa muda zaidi kutafuta ushahidi. CHANZO BBC SWAHILI

MLEMAVU AFAIDI MKONO WA KIELECTONIKI

mkono_18778.jpg
Mfumo wa mkono wa kieletroniki
Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa binadamu.
Italia
Katika tukio linalopigiwa upatu kuimarisha hali ya walemavu katika siku za usoni, madaktari huko Italia wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki na neva za mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya fataki na hivyo kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa kielektroniki .
mkono2_de0a9.jpg
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
'' tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa wetu kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki kuekelea majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti .
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Dennis hakuficha furaha yake alisema mkono huo umebadilisha kabisa hali yake.
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''

KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014, CHANGAMOTO, FURSA KWA BIDHAA

Na Shaffih Dauda
Mwaka 2014 umetawaliwa na tukio kubwa zaidi la kimichezo nalo ni kombe la dunia. Ni wakati wa makampuni yenye misuli mikubwa na hata washirika na wadhamini kujipanga kwa ajili ya kwenda sawa na kipyenga kitakachopulizwa rasmi jijini Sao Paulo nchini Brazil. Chapa kama Adidas, Coca-Cola, Visa, Continental na McDonald zimewekeza paundi bilioni 5.5, kwa ajili tu ya kushiriki kupata haki ya kufanya biashara kwenye michuano hiyo, inayoandaliwa kila baada ya miaka minne na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.
Ni wakati wa kujiuliza sasa ni zipi changamoto na fursa zitakazozikumba chapa hizi nchini Brazil? Kombe la dunia ni nafasi kwa bidhaa mpya pia washirika wa kibiashara kupata nafasi ya kuwasiliana na asilimia 50 ya watu wote duniani, kwani mashabiki zaidi ya bilioni 4 watawasha televisheni zao kuangalia michuano hiyo, pia ulimwengu wa digitali pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni nafasi kwa bidhaa kupata umaarufu ingawa kutakuwa na ushindani kwenye kupata nafasi. Nani atawika? Hilo ni swali muhimu sana kwetu.
Brazil ni nchi ambayo itatawaliwa na rangi za kila aina kutoka kila kona ya dunia, pamoja na ushabiki uliotukuka wa mchezo wa soka nchini humo, na ni muda pia wa bidhaa kufikia malengo ya kibiashara kwa kuwa huo ni muda wa thamani.
Adidas kwenye ubora wametumia njia zote kukabiliana na wapinzani wao NIKE, ambayo ni bidhaa maarufu katika bara la Amerika kusini. Mnamo mwezi Disemba Adidas walizindua mpira maalum utakaotumika kwenye kombe la dunia uliopewa jina la BRAZUCA, ambapo kampuni hiyo kubwa kwa kuzalisha vifaa vya michezo yenye makazi yake nchini Ujerumani, ilifanya utafiti kwa kuwahoji wakazi zaidi ya milioni moja nchini Brazil, ili kufahamu namna walivyoupokea huo mpira, lakini pia kampuni hiyo ya Adidas iligawa mpira mmoja mmoja kwa kila mtoto aliyezaliwa ile siku ya uzinduzi. mmmhh mambo hayo! Wananchi wa Brazil ni moja ya wateja lakini kwa upande mwingine watatumika kama njia ya kutangaza bidhaa, na makampuni mengi yanategemea kufaidika na michuano hiyo kwa kuitumia kama ngazi kwa kuwa karibu na wananchi kupitia mitandao ya kijamii pia na biashara za kutembeza mitaani. Mitandao ya kijamii ni njia nzuri na bora kwa mashabiki kufuatilia michezo kwa kubadilishana uzoefu kupitia Twitter, Facebook and YouTube. Coca-Cola kama wadhamini wa michuano ya kombe la dunia, wameshaanza kutumia nafasi ya kufanyika kipindi cha kiangazi kwa kutumia ziara ya kombe la dunia wakijihusisha na mashabiki moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram jambo ambalo linamvuto kwa mashabiki wa soka.
Pamoja na kufanya mitandao ya kijamii ni vyema kwa mameneja bidhaa kutumia fursa kama ilivyokuwa kwa (Super Bowl 2013 ) na Adidas (2012 kwenye michuano ya Olympic ) kufanikisha kuwatumia walaji kama mabalozi kupitia idadi zao kwenye mitandao ya kijamii.. Walaji watakuwa na uwezo wa kuangalia video kwa mahitaji ya Brazil, na kutokana na mazingira kumetoa fursa kwa technolojia kuweza kumsaidia mlaji kupata fursa ya kushuhudia matukio . Wadhamini wengine wa Kombe la dunia la FIFA 2014 ni kampuni ya VISA, wameikuza technolojia yao ya digitali kwa walaji kupitia bidhaa yao ‘Go World’ inayofanana na ile ya kampeni ya michuano ya Olympic 2012.
VISA ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube, kwa maudhui maalum ya video zinazoonyesha maisha halisi ya watu, pia mashindano ya mbio kuendana na matakwa ya walaji. Sasa katika hili itasaidia sana kujenga imani ya watu juu ya VISA. Moja ya changamoto kwa bidhaa ni wananchi kukosa imani na bidhaa husika kutokana na umaarufu wao, kwenye kujikita katika tasnia ya michezo. Changamoto ya kombe la dunia la Fifa 2014 kwa washirika wa kibiashara, ni kutafuta nafasi ya kujikita kwenye nyoyo za watu ili kupata nafasi ya kuzungumza kutakakopelekea kupata uhuru wa kujitawala kibiashara kwa muda mrefu, na bidhaa kupata fursa mpaka siku ya fainali

WAZIRI MKUU ARUHUSU ULEVI ASUBUHI

UK_d7d4a.jpg
London, England. Waziri Mkuu, David Cameron amebatilisha uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuamuru uongozi wake ufikirie upya wazo la kuruhusu baa kufunguliwa mapema kwa biashara ya pombe wakati wa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Italia, Juni 14 mwaka huu.
Uamuzi wa Cameroon ni baada ya wamiliki wa baa kunyimwa kibali cha kubadili muda wa kufungua biashara zao katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Watu walio karibu na ofisi ya Cameroon wameeleza kuwa kiongozi huyo ameamuru pande zote zinazohusika wakiwamo wamiliki wa baa, polisi na mamlaka za miji wakae pamoja ili kuhakikisha baa zinafunguliwa wakati wa mchezo huo dhidi ya Italia.
Awali, Wizara ya Mambo ya Ndani ilipinga maombi ya Chama cha Wauza Bia na Wenye Baa waliotaka muda wa kufungua biashara zao utazamwe upya wakati wa mchezo huo kwa masilahi ya nchi. chanzo, MWANANCHI
Hata hivyo, katika majibu yake kupitia mtandao wa kijamii, Twitter, Cameron alisema: "Nimeamuru agizo hilo liangaliwe upya wakati wa mechi zote za England wakati wa fainali za Kombe la Dunia, tunahitaji mawasiliano ya pande zote zinazohusika."
Wamiliki wa Baa waliomba muda wa kufungua biashara ubadilishwe kutoka Saa 5: 00 hadi 7:00, Juni 14 wakati wa mchezo huo na kuendelea ili mashabiki kufuatilia mchezo huo. Waziri wa Mambo ya Ndani, Norman Baker alipinga pendekezo hilo na kuacha jukumu hilo kwa mmiliki mmoja mmoja kwenye mamlaka za miji ili kutoa leseni kwa gharama ya Pauni 21 kwa kila mmoja.

Sunday, February 2, 2014

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA

epl_4f3e9.png

ARSENAL YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 2-0 

afc_14387.jpg
Washika bunduki wa London maarufu kama ''the gunners'' wameitandika timu ya crystal palace magoli 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa Jumaapili katika uwanja wa Emirates Stadium, magoli hayo ya Arsenal yalifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, kwa matokeo hayo Arsenal ipo kileleni katika msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 55, wakati timu hiyo bado ikisubiri mchezo kati ya Manchester city na Chelsea utakaochezwa leo hii katika uwanja wa ''Etihad Stadium'' ili kumpata kinara atakesimama kileleni kwa pointi nyingi zaidi, Arsenal imeizidi timu ya Manchester City pointi mbili tu hivyo kama Manchester city watashinda, Arsenal itashika nafasi ya pili katika msiamo kwa kuwa Manchester City itakuwa na pointi 56.

MAANDAMANO YAUA WATU WAWILI MOMBASA 

 MOMBASA2_ab9f6.jpg


Watu kama wawili wanaarifiwa kuwa wameuwawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika mji wa Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaohusishwa na wanaharakati Waislamu wenye siasa kali.
Polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji na kuwakamata watu 100.
Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuliwa na watu wasiojulikana katika miezi ya karibuni.
Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi. CHANZO BBC SWAHILI

Catherine Panza; mama anayetarajiwa kuleta amani CAR 

 panza_bf7a7.jpg

Kadiri siku zinavyokwenda dhana ya mwanamke kutokuwa na umuhimu kwenye jamii nyingi za Kiafrika inapotea kutokana na kundi hilo kuanza kuaminika na kupewa madaraka makubwa maeneo husika.
Awali, ilikuwa vigumu kwa wanamke kuwa na madaraka ya kutawala nchi, hasa katika Bara la Afrika, lakini sasa hali ya kujiamini, upendo na nguvu za ushawishi walizonazo ndani yao zimeanza kulibeba kundi hili la jamii.
Miongoni mwa wanawake hao waliofanikiwa kuchomoza barani Afrika ni Catherine Samba Panza, aliyechukua jukumu zito la kuiongoza nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambayo katika siku za karibuni imekuwa ikisifika kwa migogoro na machafuko yanayosababisha raia wengi kupoteza maisha kila kukicha.
Licha ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke katika CAR, Samba pia anaweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kuingia madarakani, wakati nchi ikiwa kwenye machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Inawezekana jambo hili likashtua watu wengi hata kujiuliza namna mwanamke huyu alivyopata ujasiri na kujitosa kuongoza katika nchi iliyokithiri umwagaji wa damu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lakini, ukweli utabaki kuwa ni imani,upendo na busara wanazokuwa nazo wanawake wengi, ndizo zilizowafanya viongozi wa makundi ya wapiganaji kukubali kumweka madarakani Catherine, wakiamini kwamba uongozi wake utaleta amani nchini humo.
Kudhihirisha hilo, katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa kiongozi CAR, rais huyo aliyaita makundi ya wapiganaji kama watoto wake na kutaka kuweka silaha chini ili kurudisha hali ya amani Jamhuri ya Afrika ya Kati.
"Niwaombe wanangu wekeni silaha nchini na kutanguliza uzalendo, sihitaji tena kusikia habari za mauaji ya watu wasio na hatia,"alisema Rais Catherine.
Kauli hiyo ya Catherine(59), Meya wa zamani wa mji wa Bangui, inaonyesha wazi namna wanawake wanavyokuwa wanyenyekevu katika kuhakikisha amani inatawala kwenye jamii yake.
Tofauti na siasa, Catherine ambaye ni mama wa watoto watatum, ana taaluma ya sheria inayoaminika kuwa silaha kubwa katika uongozi wake na ndiyo moja ya sababu iliyofanya makundi ya wapiganaji kumkubali bila kipingamizi.
Raia wa nchi hiyo pia wametokea kumkubali na kumwamini Catherine,kutokana na kuchoshwa na utawala uliotangulia, unaoonekana kushindwa kutafuta suluhu ya migogoro iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa mwaka 2003,mama huyu alikuwa mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki biashara mbalimbali nchini humo ikiwemo kampuni ya bima. chanzo MWANANCHI

MABASI YA MWENDO KASI YAKIWA MAJARIBIONI DAR 

mwendokasi_9b89b.jpg


Moja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.
mwendokasi1_37785.jpg