TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, January 15, 2014

Mlipuko waua 17 Maiduguri,Nigeria 

Watu kumi na saba wamefariki mwenye mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, limekiri kufanya shambulizi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi mshukiwa mmoja amekamatwa.
Mlipuko huo ulitokea karibu na soko moja mjini humo. Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa waliwaona watu wakitoroka kutoka eneo hilo nguo zao zikiwa na damu.
Kundi la Boko Haram, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara Kaskazini mwa Nigeria likiishinikiza serikali kukubali sheria za kiisilamu kutumika katika eneo hilo ambako wakazi wake wengi ni waumini wa kiisilamu.
Miili ilionekana ikiwa imetapakaa kote huku shahidi mmoja akiambia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na milipuko mingine midogomidogo.(P.T)

Wednesday, January 8, 2014

CHADEMA KUMPINGA ZITTO MAHAKAMA YA RUFANI 

zittokabwe1 e192c
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kiko katika harakati za kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, uliompa ushindi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe. (HM)
Zitto ambaye pia ni Mbuinge wa Kigoma Kaskazini, juzi aliibuka mshindi katika maombi yake ya kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake, hadi kesi ya msingi kuhusu suala hilo itakapokuwa imesikilizwa.
Kadhalika, chama hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano na Uenezi, John Mnyika kimesema kinaendelea na utekelezaji wa uamuzi wa Kamati Kuu wa kutompa Zitto ushirikiano wa aina yoyote.
Wakili wa Chadema, Peter Kibatala, alisema jana kuwa japo wanauheshimu uamuzi wa Mahakama, hawajaridhika nao na kwamba wanakusudia kwenda Mahakama ya Rufani kuupinga.
"Ingawa uamuzi huu ni Interlocutory (uamuzi usiomaliza kesi), lakini sisi hatukuridhika nao. Hatukuridhika na uamuzi wa kutupilia pingamizi letu la awali, hati ya kiapo na hata amri yenyewe ya zuio la muda," alisema Wakili Kibatala na kuongeza:
"Kuna namna nyingi za kufanya kupinga uamuzi huo, kama vile kukata rufaa, kuomba marejeo au namna nyinginezo. Kwa hiyo kwa sasa tunaangalia namna bora ya kwenda Mahakama ya Rufani bila kuathiri matakwa ya kisheria."
Wakili Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema kuna haja ya kuiomba Mahakama ya Rufani kuuchunguza uamuzi huo kwa kuwa una athari si kwa Chadema tu, bali hata vyama vingine dhidi ya wanachama wake.
Kauli ya Mnyika
Mnyika kwa upande wake alisema kutompa ushirikiano Zitto ni uamuzi wa Kamati Kuu ambao ulitokana na hatua yake ya kwenda mahakamani kwa masuala ya chama, kinyume cha matakwa ya Katiba ya Chadema na Kanuni zake.
Mnyika alikuwa akirejea taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baada ya kikao hicho akiwataka viongozi wa ngazi zote za chama hicho, wanachama, mashabiki na wapenzi wake, kutoshiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yote ya nje, ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake.
Ushindi wa Zitto
Katika maombi hayo namba 1 ya 2014, Zitto kupitia kwa Wakili Albert Msando, Zitto aliiomba Mahakama itoe zuio hilo la muda kwa CC ya Chadema, hadi kesi yake ya msingi namba 1 ya 2014 aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Awali, mawakili wa Chadema, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.
Katika uamuzi wake juzi, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
Maombi hayo ya Zitto yaliyotolewa uamuzi juzi yalitokana na kesi ya msingi aliyofungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema.
Katika kesi hiyo anaiomba mahakama ikizuie chama hicho, wakala wake na vyombo vyake vya uamuzi kumchukulia hatua zozote au kumjadili kuhusiana na uanachama wake, hadi hapo rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la chama hicho kupinga kuvuliwa nyadhifa, itakaposikilizwa.
Pia aliiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za CC za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Kesi hiyo ya msingi imepangwa kutajwa mahakamani hapo Februari 13, mwaka huu. Chanzo: Mwananchi

MESSI BORA, HATA ASIPOPATA TUZO

article-2274726-17648C8F000005DC-173 634x5371 21a9d
MLINZI wa kulia wa Barcelona, Dan Alves amedai kuwa anaamini Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi kwa sasa ulimwenguni hata kama hatapata tuzo ya mwanasoka bora wa dunia. (HM)

Mastaa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Franck Ribery wa Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, lakini Alves anaamini kuwa haitabadilisha lolote na Messi ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi wa zama hizi.
"Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia inachosha kidogo kwa sababu imehamishwa mahala pake. Imepelekwa katika eneo la mawazo ya watu, nje ya uwanja wa soka. Lakini kama tukitazama mambo ya uwanjani nadhani Lionel anawasukuma wengine katika nafasi ya pili," alisema Alves.
Kwa misimu minne mfululizo, Messi amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa dunia na ingawa msimu huu hapewi nafasi kubwa kutokana na kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, lakini bado amechaguliwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo. Chanzo: mwanaspoti

MORSI ACHELEWA KUWASILI MAHAKAMANI MISRI

Taarifa kutoka Misri zinasema kiongozi aliyepinduliwa nchini humo, Mohammed Morsi, amechelewa kuwasili mahakamani leo mjni Cairo.
Inasemekana kuwa hali mbaya ya anga imeizuia helikopta iliyotarajiwa kumsafirisha hadi katika mji mkuu huo anakokabiliwa pamoja na maafisa wengine wa utawala wake na tuhuma za kuchochea mauaji ya waandamanji mnamo mwaka 2012 alipokuwa madarakani.
Awali vikosi vya usalama viliimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo ,Morsi akitarajiwa kuwasili mahakamani.
Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake wanashutumiwa kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuvunja gereza.
Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa . Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni Rais na alifungwa kinyume na matakwa yake.(P.T)

Tuesday, January 7, 2014

Meno ya tembo 81 yakamatwa Tanzania 

130303065644 elephants ivory 304x171 reuters nocredit1 93ca2
Watu wawili wanashikiliwa na polisi nchini Tanzania baada ya kukamatwa na shehena ya meno ya tembo katika bandari ya Dar es Salaam, waliyokuwa wakisafirisha kiharamu maafisa wa nchi hiyo wamesema. (HM)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha amesema meno hayo yapatayo 81 yana uzito wa kilo 303.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya tembo ni mapya ikiwa na maana yametokana na tembo 41 waliouawa ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Naibu Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema mauaji ya tembo yameongezeka nchini humo baada ya operesheni ya kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni Tokomeza" kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za binadamu.
Mapema wiki hii Naibu Waziri huyo amesema tembo wapatao 60 wameuawa kati ya mwezi Novemba na Decemba ikilingalishwa na tembo wawili waliouawa mwezi Octoba. Chanzo: bbcswahili

Sudan mbili zajadili ulinzi wa mafuta

Sudan na Sudan Kusini zimejadili swala la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya mafuta Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.
Marais wa nchi hizo mbili wameanza mazungumzo ya kupeleka kikosi cha ulinzi ili kulinda visima vya mafuta Kusini ambako waasi wamezusha vurugu kwa karibu wiki nne sasa.
Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.
Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.
Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.(P.T)

MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE AVAMIWA, APIGWA, ATUPWA UNUNIO

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya cha hicho, Joseph Yona akitolewa eneo la tukio. (Picha na Millard Ayo)
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona (33), amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio Kawe jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanadai walisikia kelele za mtu kupigwa saa tisa usiku.
Mwenyekiti huyo anadai alichukuliwa nyumbani kwake Mtoni Kwa Aziz Ally na watu wasiojulikana waliokuwa na gari kama la polisi wakidai wananipelekea kituoni kabla ya kuanza kunishambulia kisha kunitupa.


TASWIRA KUTOKA NJE YA MAHAKAMA KUU DAR KABLA YA HUKUMU YA ZITTO

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Polisi wakiwadhibiti wafuasi wa Zitto na wale wanaompinga nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar kabla ya hukumu…
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Polisi wakiwadhibiti wafuasi wa Zitto na wale wanaompinga nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar kabla ya hukumu kutolewa.
Wafuasi wa Zitto wakiwa na mabango.
Wanaompinga Zitto wakiwa na mabango yao nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Polisi wakituliza vurugu nje ya Mahakama Kuu leo.
 
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika mlango wa kuingia Mahakama Kuu leo.
Ulinzi mkali nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu.

Sunday, January 5, 2014

HATIMAYE LEWANDOSKI AJIUNGA NA BAYERN MUNICH KWA MKATABA WA MIAKA MITANO

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski atajiunga na klabu ya Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni wa mwa msimu huu, mabingwa wa Ujerumani wametangaza.
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Lewandowski alitangaza nia yake ya kuondoka Westfalenstadion pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu, na akawa anahusishwa na kujiunga na wapinzani wao Bayern.
Lewandoski, 25, alijaribu kulazimisha kuuzwa kipindi cha kiangazi kilichopita lakini Dortmund waligoma kumuuza na kusisitiza lazima amalize mkataba wake.
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alitangaza dili la Lewandoski, akisema: "Tuna furaha uhamisho huu umekamilika kwa mafanikio.
"Robert Lewandowski ni mmoja ya washambuliaji bora ulimwenguni, atakiongezea ubora kikosi chetu cha FC Bayern."(P.T)

Jenerali wa Sudan Kusini auwawa Bor

Mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Sudan Kusini.
Mapigano makali yamezuka nje ya mji mkuu wa Sudan Kusini wa Bor na Jenerali mmoja wa jeshi la Sudan Kusini ameuwawa.
Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya serikali vinazidi kuelekea karibu na mji wa Bor ambapo kumekuwa na mapigano ya kutegeana baina ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi vinavyomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Mwandishi wetu amesema pia ameshuhudia miili ya watu ikiwa chini na vifaru vikiwa vimelipuliwa vibaya pembezoni mwa barabara.
Pande pinzani nchini humo zinataraji kuanza mazungumzo ya ana kwa ana mjini Adis Ababa kujaribu kumaliza wiki tatu za mapigano.
Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Sudan kusini Nial Deng Nial amesema kuwa ni muhimu kwamba viongozi kuzungumzia kuhusu kusitishwa kwa vita.(P.T)

HAYA NDIYO MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA 

Katibu Mkuu anaanza kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kuanza press akiungana na John Mnyika pia Katibu Mkuu anasema kuwa atasoma neno kwa neno kutokana na umuhimu wa hoja yenyewe! Ameanza kusoma na kusema kamati kuu ilikuwa ni ya dharura iliyokuwa na lengo la kuwajadili Wanachama watatu Dr. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samsoni Mwigamba.
Dr Slaa anaonyesha kabrasha lenye nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa mabadiliko 2013, mashtka ya watuhumiwa na nyaraka nyingine muhimu. Sasa Dr. Slaa anasoma mashtaka yote 11 ya Watuhumiwa kama walivyokabidhiwa kwa maandishi
Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.
Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.(P.T)
Dr. Kitila Mkumbo alikataa kuzungumzia vifungu vya katiba walivyodai vimevunjwa kwa madai kuwa tayari wana malalamiko kwa msajili tayari. Aidha Dr. Kitila Mkumbo alishindwa kuithibitishia Kamati Kuu kwa ushahidi kuhusu madai ya taarifa ya fedha ambazo yeye na Zitto walishiriki, pia alishindwa kuonyesha ushiriki wa M/Kiti katika manunuzi ya vifaa mbalimbali vya Chamazikiwemo pikipiki za Chama.
H...ivyo Kamati Kuu imeamua kuwavua Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo kuanzia tarehe ya jana baada ya maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu. Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.
Dr. Slaa anasema malengo ya waraka wa mabadiliko hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa Viongozi wa Chama.
Mwisho
Chama kinawatangazia Wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na Washirika wake kwa jina la Chama.

Familia ya soka yampoteza gwiji Eusebio 

 

Eusebio kushoto enzi zake akiwa na Pele Mwaka 1966 katika mechi kati ya Ureno na Brazil.
Eusebio da Silva Ferreira
Gwiji wa soka kutoka taifa la Ureno, Eusebio amefariki dunia.
Alikuwa na miaka 71 na kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Eusebio alizaliwa nchini Msumbiji kama Eusebio da Silva Ferreira na anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani.
Aliitumikia klabu ya mjini Lisbon,Benfica FC kwa miaka 22 ambapo uwezo wake wa mbio na kasi, kuutumia vyema mguu wake wa kulia na mbinu za kimpira kulimpa umaarufu sana nchini Ureno na kubatizwa jina la The Black Pearl or the Black Panther.
Wakati wa uchezaji wake alifunga mabao 733 katika mechi 745, pia alifunga mabao tisa kwenye michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1966 na kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo na kuisaidia Ureno kushika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.(P.T)

MATUKIO PICHA MAPOKEZI MWILI WA DR WILIAMU MGIMWA 

 

unnamed_4ec2a.jpg
Mwili wa marehemu ukishushwa katika uwanja wa ndege wa nduli iringa
unnamed1_3161e.jpg
Jeneza likifunikwa kwa bendera ya Taifa mara baada ya kushushwa katika ge
unnamed2_6f0ab.jpg
maofisa wakinyanyua jeneza tayari kwa ajili ya kupakiwa kwenye gari uwanjani hapo
unnamed3_7f1a6.jpg
Mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye gari
unnamed4_24a6e.jpg
Madiwani wa mkoani iringa wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu
unnamed5_babac.jpg
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye ukumbi wa siasa ni kilimo tayari kwa kuagwa na wakazi wa iringa
unnamed6_aee1b.jpg
Askofu Ngalalekumtwa akimuombea marehemu
unnamed7_9cc96.jpg
Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu
unnamed8_4eacb.jpg
Umati wa wananchi wa Iringa wakiwa na huzuni wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu
unnamed9_0ce99.jpg
Wananchi wa Iringa walijitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa marehemu
Picha na Mnyalu (P.T)

Saturday, January 4, 2014

SIMBA SC YASHIKWA NA KCC AMAAN, NGOMA DROO 

Kipa wa KCC, Magoola Omar akiruka juu kupangua mpira kichwani kwa mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki jioni hii Uwanja wa Amaan
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
SIMBA SC imegawana pointi na KCC ya Uganda baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa ujumla timu zote zilitoshana nguvu na maarifa kwa dakika zote 90 za mchezo huo, huku makipa wote, Ivo Mapunda wa Simba na Magoola Omar wa KCC wakistahili sifa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.
Mabeki wa KCC walimdhibiti vizuri winga machachari wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano 'Messi' leo, wakati pia beki Mkenya, Donald Mosoti Omwanwa aliiongoza vyema safu ya ulinzi ya Simba SC.(P.T)
Matokeo hayo yanazifanya Simba SC na KCC ziendelee kukabana kileleni, kila timu ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili.
Mapema jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, wenyeji KMKM nao walitoshana nguvu na AFC Leopard ya Kenya kwa sare ya 0-0 pia.
Mechi za Kundi B zitahitimishwa Januari 5, kwa Simba kumenyana na KMKM na KCC na Leopard.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi C, Ashanti ikimenyana na Spice Stars na Azam FC na Tusker ya Kenya Uwanja wa Amaan, wakati Uwanja wa Gombani, Pemba Clove Stars itamenyana na URA ya Uganda na Mbeya City na Chuoni.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid 'Baba Ubaya', Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Zahor Pazi dk89, Amri Kiemba/Said Ndemla dk50, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk67, Uhuru Suleiman/Ramadhani Chombo dk48 na Haroun Chanongo/Edward Christopher dk78.
KCC; Magoola Omar, Saki Mpima, Kavuma Habibu, Kawooya Fahad, Kiiza Ibrahim, Senkumba Hakim, Waswa Herman, Masiko Tom, Tony Odur, Stephen Bengo/Gadafi Kiwanuka dk 58 na Wadri William.

Mazungumzo kuhusu Sudan Kusini yaanza 

Mazungumzo ya kupatanisha pande mbili zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita, yameanza mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje nchini Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika Mashariki wananuia kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota kwa takriban wiki tatu.
Hata hivyo mazungumzo ya ana kwa ana yangali kuanza kati ya pende zinazozozana yangali kuanza.
Waakilishi kutoka pande zinazozozana wanakutana na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa vingozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa ana.(P.T)
Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais Salva Kiir na yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais Riek Machar
Wakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.
Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita.