TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 5, 2013

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA PAMOJA WA SADC NA ICGLR PRETORIA, AFRIKA KUSINI 

abnc_e0728.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Waterloof Air Force Base jijini Pretoria, Afrika ya Kusini Jumatatu Oktoba 4, 2013 tayari kuhudhuria mkutano wa pamoja wa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na za maziwa makuu (ICGLR) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Pretoria, Afrika ya Kusini
pre2_98843.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa pamoja wa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na za maziwa makuu (ICGLR) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, usiku wa kuamkia leo Oktoba 5, 2013(P.T)
pre3_d6880.jpg
Meza kuu katika mkutano wa pamoja wa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na za maziwa makuu (ICGLR) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Pretoria, Afrika ya Kusini
pre4_10f1d.jpg
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakiwa katika mkutano wa pamoja wa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na za maziwa makuu (ICGLR) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Pretoria, Afrika ya Kusini

Monday, November 4, 2013

LOWASSA : MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA HAUNA MENO

 lowassapx_add09.jpg

Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema ana shaka kama Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now), utafanikiwa kutokana na Kitengo cha Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo kilicho chini ya Ofisi ya Rais (PDB) kukosa meno.
Akichangia mjadala wa hoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015, Lowassa alisema tatizo kubwa linaloikabili nchi ni viongozi kushindwa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
"Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo mengi lakini hakuna utekelezaji," alisema Lowassa wakati akichangia mjadala huo uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, wiki iliyopita.
Mbunge huyo wa Monduli (CCM), Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje alisema itakuwa vigumu kwa PDB kutekeleza wajibu wake wakati hakina meno ya kusimamia utekelezaji wa mipango ya Serikali.
Kitengo cha PDB kinachoongozwa na Omar Issa kiliundwa mwaka huu na kutengewa kiasi cha Sh29 bilioni na kulalamikiwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika wakati wa kikao cha Bunge cha Bajeti 2013/14.(P.T)
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuinua uchumi kutoka wa chini hadi kufikia wa kati ifikapo mwaka 2025.
"Nataka mjiulize maswali machache. Je, hawa PDB wana meno?" alisema Lowassa na kuongeza:
"Tunazungumza lakini mjue kuwa 'discipline' (nidhamu) ya wenzetu wa Malaysia ni tofauti na hapa kwetu. Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua bila kutekeleza." Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge, Lowassa aliitaka Serikali kuwa na mipango michache ambayo itakayoweza kuifuatilia kwa ukaribu na kuitekeleza. Alipendekeza kuwa ajira, elimu na kuendeleza reli kuwa vipaumbele muhimu.
"Kinatakiwa chombo ambacho kinaweza kufanya uamuzi mgumu unaotekelezeka kwelikweli. Bila kuwavika joho la kufanya uamuzi ili kuwarahisishia utekelezaji wa kazi yao na wakawa na 'function' itakuwa ni kazi bure. Ni uamuzi mzuri kuanzisha mpango huu lakini msipoangalia itakuwa kazi bure. Lazima wawe na meno ya kuuma mkishakubaliana mambo yafanyike."
Kila mtu analalamika
Lowassa alisema sasa Tanzania imekuwa nchi ya kila mtu kulalamika, kuanzia viongozi hadi wananchi.
"Wananchi na viongozi wote wanalalamika haiwezekani kukawa na jamii ya aina hii, lazima awepo mtu mmoja anayefanya uamuzi na anayechukua hatua. Bila kuchukua hatua tutaendelea kulalamikiana tu" alisema.
Mpango wa Matokeo Makubwa uliingizwa nchini kwa kurudufiwa kutoka Malaysia, ambayo ilipopata uhuru mwaka 1957 ilikuwa katika kiwango sawa na Tanzania katika maendeleo ya kiuchumi lakini sasa ina rekodi ya juu kiuchumi barani Asia. Mpango huu pia unatekelezwa Nigeria na Rwanda na umeonyesha mafanikio makubwa katika nchi hizo.
Katika kutekeleza mpango huo, Serikali imeanza na wizara sita; Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Kilimo, Chakula na Ushirika, Maji, Uchukuzi, Fedha na Nishati na Madini.
Ajira
Akizungumzia suala la elimu, Lowassa alisema: "Huwezi kuzungumza mipango bila kuzungumza ajira, kuna Watanzania wengi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita wapo mitaani na hawana ajira. Tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi."
Alisema katika mkutano wa Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwaka huu, walizungumzia mdororo wa uchumi kwa nchi za Ulaya na moja ya nchi hizo ambayo ni Hispania, ilieleza jinsi ilivyoweza kujinasua kwa kuweka kipaumbele cha ajira.
"Hispania walitoa mfano kuwa walikuwa na ukosefu wa ajira kwa asilimia 50, waliamua katika bajeti yao kujikita katika kuzalisha ajira. Kila mwekezaji aliyekwenda katika nchi hiyo alipewa masharti ya kuwekeza katika ajira ya vijana. Kimsingi tunatakiwa kuwa na takwimu za kujua tumezalisha ajira ngapi ndipo tutajua uchumi wetu unakua kwa kiasi gani," alisema.
Lowassa alisema baada ya miaka mitatu nchi hiyo imetoka kuwa miongoni mwa nchi zisizo na ajira na kusisitiza kuwa mipango mingine ni migumu kutekelezeka kama nchi haitakuwa na ajira.
Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu kutokana na kitendo chao cha kuwapa ajira wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu baada ya kuwapatia matrekta na mashamba.
Elimu
Lowassa alisema kuna tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania. "Nilitegemea wahusika wangepata taarifa ya Tume ya Serikali kuchunguza kushuka kwa kiwango cha elimu ili kujua matatizo yaliyopo katika elimu na nini cha kufanya."
Mwanzoni mwa mwaka huu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliunda tume ya watu 15 kuchunguza sababu za idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne kuvurunda katika matokeo ya mtihani huo mwaka 2012.
Tume hiyo tayari imeshakamilisha kazi na kukabidhi ripoti hiyo serikalini, lakini mpaka sasa bado haijawekwa hadharani.
"Haitoshi kumchukua mwanafunzi aliyemaliza chuo kikuu wakati akienda katika soko la ajira wakati shahada yake hamsaidii, mtu ana shahada lakini kazi hakuna."
"... Kunatakiwa kufanyika mjadala nchi nzima kuzungumza juu ya matatizo na nini kifanyike. Nchi isipokuwa makini katika hili itaachwa katika ushindani uliopo sasa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)."
Awafagilia Magufuli, Mwakyembe
Akizungumzia uendelezaji wa Reli ya Kati alisema pamoja na juhudi zinazofanywa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kujenga barabara, alisema zinaharibika kwa kasi kutokana na kuzidi kwa kiwango cha uzito wa malori.
"Reli ya Kati inatakiwa kuangaliwa kwa haraka maana malori yanayotembea katika barabara yatapungua kwa kuwa mizigo itakuwa inachukuliwa na treni," alisema. Licha ya kusifu kazi inayofanywa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe Lowassa alisema foleni jijini Dar es Salaam zinashusha uzalishaji, kwani watu wengi wanatumia muda mwingi barabarani kuliko kufanya shughuli za maendeleo.
"Serikali haiwezi kukaa hivi hivi, 'this is a disaster' (hili ni janga), mtafute njia ya kuangalia mnafanyaje kumaliza foleni ya Dar es Salaam, jambo hili lifanyike sasa," alisema.
Uamuzi mgumu
Lowassa alisema pia Tanzania haitakiwi kuendelea kulumbana na Uganda, Rwanda na Kenya zinazotaka kuitenga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), badala yake ichukue uamuzi mgumu wa kushirikiana na nchi nyingine.
"Wao wameamua kuanzisha ushirikiano na Sudan Kusini, Tanzania inaweza kuanzisha ushirikiano na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) ambako ni kuzuri zaidi na kikubwa kinachotakiwa kufanyika ni kuifufua Reli ya Kati," alisema.
Chanzo:Mwananchi

MAKABILIANO YAPAMBA MOTO DRC 

131031134004_drc_bunagana_refugees_304x171_bbc_nocredit_eba27.jpg
Watu wote wa mji wa Bunagana Mashariki mwa DRC, wametoroka mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo la mpaka wa Uganda na DRC, amesema kuwa makombora yaliyorushwa na wanajeshi yalisababisha vifo vya watu wanne.
Majeshi ya serikali siku ya Jumatatu yalikataa mazungumzo na waasi wa M23 waliokuwa wameahidi kusitisha vita kwa ajili ya kufanya mazungumzo na serikali ya DRC.
Karibia watu laki nane wametoroka makwao tangu mgogoro huu wa kisiasa kuanza Machi mwaka 2012.
Wiki jana , mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Martin Kobler, alisema kuwa kundi la M23 sio tisho tena kwa jeshi la DRC.(P.T)
Siku moja baada ya kauli yake bwana Kobler, wanajeshi wa serikali waliukomboa mji wa Bunagana uliokuwa kombe kuu ya waasi hao, kwenye mpaka wa Uganda na DRC.
Hata hivyo, mapigano mapya yalizuka Jumatatu na hali ni tete sana mpakani mwa nchi hizo mbili huku wakaazi wakikimbilia usalama wao.
Wakimbizi wamefahamisha Bahizi kuwa ni wanajeshi wa serikali ya DRC waliosalia mjini Bunagana, huku maelfu ya wakaazi wakiwa wamekimbilia usalama wao na kuingia Uganda.
Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa waasi hao nao wanaonekana kujibu mashambulizi dhidi yao kwa ukali mno ikilinganishwa na hali ilivyokuwa siku za awali.
Lakini wanajeshi sasa wameweza kukomboa mji muhimu wa Mbuzi ulio juu milimani karibu na mji wa Bunagana, baada ya kuushambulia kwa roketi na vifaru.
Waasi saba walikamatwa kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
"Ushindi, ushindi," wanajeshi waliokuwa katika mji jirani wa Ntamugenga walisikika wakisema, baada ya kupata habari kuwa mji wa Mbuzi umekombolewa.
Wanajeshi wa serikali sasa wanalenga maeneo matatu yaliyo milimani ambako waasi wengi wangali wamejificha.

Sunday, November 3, 2013

NAMNA TULIVYO SHEHEREKEA KOMUNIO YA MTOTO ELIZABETHI

Mtoto Elizabethi akiwa katikati na wapambe wake

Mzaa chema Caren akiwa na watoto wake hapo
Watu wakiwa wamependeza kwenye ukumbi mambo yalikuwa mazuri kweli kweli

Zoezi muhimu la kufungua champeni likifanyika hapo kama mnavyowaona watu walivyopendeza wakiwa tayari kwa ufunguzi

Caren and Francisca

Caren, Francisca na Beatrice full shangwe
Hapana chezea Dayana ameng'aaaje
 
Dada huyu mkabidhi shughuli yako uone itakavyong'ara ni mpambaji maarufu Jijini, kwa mambo ya misosi ndio usisema chakula akipika kwenye shughuli lazima utake ukirudie tena kula kwa utamu namba zake za simu 0652711024 anti Latifa  mtwangie uone kazi

Huo ndio wakati muafaka hapo tumbo linapata kitu chake

Tabasamu la ukweli rafiki yangu maisha ni raha tupu

Chezea sherehe wewe hasa ikiwa ya shoga mwenyewe utaingia botique

Mambo ndivyo yalivyokuwa hapo , Pongezi nyingi kwa shost Carren kwani tulijiachiaje kwenye sherehe ya mtoto wentu?

ZITTO ARUDI NA SIRI YA MABILIONI YA USWISI 

Zitto-Kabwe_bec88.jpg
*Apanga kuanika aliyobaini Ulaya, ashtushwa na fedha zilizofichwa visiwa vya Uingereza
*Asema ni zaidi ya zile za Uswisi, ayageukia makampuni asema nayo yamo, aonya yakiachwa
MIEZI 12 tangu serikali iazimie kuunda timu maalumu kuchunguza sakata la vigogo wanaodaiwa kuficha fedha haramu nje ya nchi, hususani katika mabenki ya Uswisi, upepo wa suala hilo sasa unaweza kubadilika wakati wowote, baada ya muasisi wa hoja hiyo, Zitto Kabwe, kupanga kuibua mazito aliyodai kubaini katika uchunguzi wake Ulaya.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alirejea nchini jana akitokea katika nchi za Ulaya, baada ya kumaliza kazi ya kuongoza jopo la wataalamu kutoka Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo (Eurodad), kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi.(P.T)
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao akiwa nchini Ufaransa siku tatu zilizopita, Zitto alisema; "Huu uchunguzi ni mkubwa. Ni jambo kubwa sana. Nikimaliza kazi nitafanya press conference (mkutano na waandishi wa habari) ili kila Mtanzania aweze kujua, uchunguzi wa suala hilo ni mkubwa, hivyo kila Mtanzania anatakiwa kujua kinachoendelea," alisema Zitto kwa kifupi.
Gazeti hili lilipotaka kujua ni mambo gani hasa ameyabaini ambayo yanaigusa Tanzania moja kwa moja, likiwemo suala la idadi ya vigogo wanaotajwa kuficha fedha chafu nje ya nchi, Zitto bado alisisitiza azma yake ya kukutana na waandishi wa habari, huku akitoa angalizo kuwa inatupasa kuwa makini.
Nikimaliza kazi nitafanya 'press conference' siku ambayo nitatangaza ili kila Mtanzania aweze kujua, ninarudi Novemba 2. Uchunguzi ni mkubwa sana na lazima tuwe makini sana," alisema.
Alisema akiwa huko alikutana na watu waliokuwa wanafanya kazi kwenye mabenki ya Uswisi na Mauritius, ambao alisema kuwa wana taarifa nyeti sana.
Zitto, ambaye wakati anawasiliana na gazeti hili alikuwa mjini London, nchini Uingereza, alisema akiwa hapo alikutana na mchunguzi mwingine kwa ajili ya akaunti za visiwa vya Jersey, Isle of man, Guarnsey, Cayman na kisiwa cha British Virgin, ambako imebainika kuna fedha nyingi zaidi kuliko zile za Uswisi.
Alibainisha kuwa fedha za watu binafsi ni chache kuliko makampuni makubwa yanavyokwepa kodi nchini.
Watu binafsi ni rahisi kuwashughulikia na kurejesha fedha zilizopatikana kwa wizi, rushwa na biashara ya madawa ya kulevya. Kazi kubwa ipo kwa makampuni ya kimataifa ambayo yanakwepa kodi zaidi ya dola 546 milioni kila mwaka," alisema Zitto.
Katika kushughulikia suala hilo la utoroshwaji wa mabilioni ya fedha nchini, Zitto alisema kuwa ni vyema makampuni nayo yasisahauliwe.
Akili za watu wengi sasa ni kwa watu binafsi, lakini tusipokuwa makini tutayaacha makampuni yakiendelea kunyonya rasilimali zetu na kutolipa kodi," alisisitiza Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Kwa upande wa kampuni za madini, alisema tangu mwaka 2001 mpaka 2011 zimeuza nje ya nchi madini ya dola 11.3 bilioni, lakini wamelipa kodi dola 440 milioni, ambayo ni chini ya asilimia nne ya mauzo yao yote.
Kwa mujibu wa maelezo yake, idadi hiyo ni mbali na makampuni ya simu na sekta nyingine ambapo ametilia shaka serikali kupoteza fedha nyingi kwa mtindo huo.
Inaelezwa kuwa takwimu za mtiririko wa fedha haramu zinazofichwa nje zikitokea Afrika ni mara mbili ya kiasi cha fedha za msaada zinazotolewa kwa bara hili.
Shirika la Kimataifa la Fedha la Global Financial Integrity, linakadiria kuwa kiasi cha dola trilioni 1.4 zilihamishwa kutoka Afrika katika kipindi cha miongo mitatu (1970 mpaka 2009).
Katika kipindi hicho, mikopo ya Afrika ilikuwa chini kuliko fedha haramu zinazohamishwa.
Inakadiriwa kuwa kila mwaka, Afrika inaingia hasara ya dola bilioni 50 katika ukwepaji wa kodi.
Hatua hiyo ilisababisha Nicholous Shaxson kuandika katika kitabu chake "Treasure Islands" kwamba; huwezi kuelewa umaskini barani Afrika pasipo kujua jukumu la Kodi ya Bandari.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa na Sh 12.7 trilioni).
Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwa muda mrefu amekuwa akipigia kelele suala hilo ambapo Novemba 9 mwaka jana, katika mkutano wa Bunge aliwasilisha hoja binafsi ya kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza serikali hatua dhidi ya raia wa Tanzania walioficha fedha na mali haramu nje ya nchi.
Hata hivyo, Bunge liliazimia serikali ifanye uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu, jambo ambalo haijaweza kulitekeleza mpaka sasa.
Gazeti hili lilimtafuta Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, kujua ilikoishia ripoti hiyo ya uchunguzi unaofanywa na serikali. Alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda, katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge kilichofanyika kabla ya kuanza kwa shughuli za Bunge linaloendelea sasa mjini Dodoma, aliikumbusha serikali kuhusu kuleta ripoti hiyo.
"Spika katika kikao cha Kamati aliagiza serikali ilete taarifa, hivyo siwezi kujua, lakini kama ni taarifa tu ya serikali muda huo utapatikana," alisema Joel.
Alipoulizwa iwapo pia Zitto anaweza kuwasilisha taarifa yake ya Eurodad katika Bunge hili, alisema haitawezekana, kutokana na utaratibu wa Bunge kuwa mwisho wa kuwasiliswa hoja ni siku moja kabla ya kuanza kwa Bunge.
"Sidhani, kwa utaratibu wetu hoja zinatakiwa ziwasilishwe siku moja kabla ya kuanza, labda kama ataleta na atakabidhi kwa Katibu wa Bunge kwa ajili ya Bunge lijalo," alisema Joel.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye mara kadhaa amekaririwa akisema kuwa ripoti kuhusu mabilioni ya fedha ipo tayari, alipotafutwa mara kadhaa na gazeti hili kujua lini itafikishwa bungeni, ameonekana kutopenda kuweka wazi suala hilo.
Zitto aliteuliwa mwezi uliopita kuongoza jopo la wataalamu kutoka Eurodad, ambao ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki, kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi.
Mashirika hayo yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea.
Uchunguzi huo uliofanywa katika nchi za Ulaya, ulianza Oktoba 20 na ulitarajiwa kukamilika Novemba 5, mwaka huu kwa kuandika ripoti yake.

KERRY AZURU MISRI

kerry e5013
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili Misri Jumapili kituo cha kwanza katika ziara yake ya kidplomasia kwa siku 9 Mashariki ya Kati na Ulaya. Ziara ya Kerry huko Cairo imefanywa siku moja kabla ya kesi dhidi ya rais aliyetimuliwa madarakani Mohammed Morsi kuanza kesho Jumatatu. (HM)

Morsi alitimuliwa madarakani na majeshi mwezi Julai na kushtakiwa kwa makosa ya kuchochea mauaji ya waandamanaji waliokuwa nje ya kasri ya rais mwezi Desemba.
Utawala wa rais Obama umedhibiti baadhi ya msaada wa kila mwaka kwa jeshi la Misri ambao ulikuwa wa takriban dola bilioni 1.3 kutokana na umwagaji damu nchini humo na msukosuko wa kisiasa.
Kerry atakwenda Saudi Arabia baadaye leo Jumapili kwa mazungumzo na viongozi wa Saudia kuhusu Misri, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria na majadiliano juu ya program ya nuklia ya Iran.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani baadaye atakwenda Bethlehem ambako atakutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmud Abbas.Pia atazuru Jordan,Milki ya nchi za Kiarabu, Algeria,Morocco na Poland. Chanzo: voaswahili
KUTANA NA PASTOR STARFFORD GODSON JACOB WA HUDUMA YA GOOD NEWS FOR ALL NATIONS 'INTERDENOMINATIONATIONAL' 'HABARI NJEMA KWA MATAIFA YOTE' ILIYOPO MAJOHE KWA WALIOBA , AMBAPO MUNGU AMEKUWA AKIMTUMIA KWA NJIA YA PEKEE KUWAFUNGUA MATEKA WALIOFUNGWA KWA KAMBA ZA MINYORORO YA ADUI.
Mzee Jumanne akiongozwa sala ya toba na Mchungaji baada ya kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake

Mchungaji Starfford akiwa madhabahuni kwenye Ibada ya Jumapili  akiwafundusha waumini wake neno la Mungu

Waumini wakiwa wameguswa na ujumbe wa Bwana uliotoka madhabahuni




Family Mulaba kwaya ikiwa inatumbuiza wakati wa ibada ya Jumapili


Matendo ya Mungu ni ya ajabu mzee huyo unayemuona hapo pichani  amefika hapo kanisani kwenye ibada akiwa na tatizo la kupooza miguu kwa muda wa miaka minne , lakini kwa msaadawa mke wa alifikishwa hapo kanisani na kufanyiwa maombi hatimaye amefanikiwa kunyanyuka hapo kwenye kiti kama anavyoonekana

Kama mnavyomuona mzee wa kupooza kwa miaka minne akiwa amesimama mwenyewe huku mchungaji akiwa ameshika mkono kumpongeza kwa yale mungu aliyomtendea katika maisha yake

Waumini wakiwa na furaha kuona yale Mungu aliyemtendea mzee huyo.

Hakika Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini na kumwamini pale unapompa maisha yako lazima afanye kitu tofauti katika maisha yako.Ukitaka kutyaona hayo yote fika kwenye Ibada zetu siku ya Jumapili ibada inaaza saa 2asubuhi hadi saa 7 mchana . kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo . 0713 055 459 / 0754 33 5051 wote mnakaribishwa nyumbani mwa Bwana.

Friday, November 1, 2013

RIPOTI YAONYESHA WIZI WA FEDHA WA KUTISHA

bot_59b7b.jpg
Taasisi za Fedha nchini zimepoteza kiasi cha Sh34.4 bilioni kuanzia kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi Oktoba mwaka huu kutokana na wizi wa fedha katika taasisi hizo,ripoti mpya imebainisha.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Kenya,Tanzania na Uganda umebainisha kuwa,Taasisi za Fedha za Afrika Mashariki zimepoteza zaidi ya Sh471 bilioni sawa na (USD 30 milioni) kwa mwaka.
Hata hivyo benki hizo ziliweka wazi upotevu wa Sh126.9 bilioni tu ambao ni robo ya upotevu huo wa zaidi ya Sh471 bilioni kwa kile kinachodaiwa kuhofia kupoteza wateja.
"Taasisi za fedha zinapoteza fedha nyingi kutokana na teknolojia na watendaji wa ngazi za juu kuhusika kwa kiwango kikubwa lakini hazitaki kukiri kwa sababu ya kuhofia kukosa wateja," alisema Robert Nyamu, Mkurugenzi wa Delloite, Afrika Mashariki.(P.T)
Msemaji wa Benki Kuu ya Tanzania,Loy Nabeta hakuwa tayari kuzungumzia upotevu huo na kusema kuwa ni suala linalohitaji majadiliano ya kina na utendaji wa ngazi za juu.
Wimbi la wizi wa fedha katika benki lilianza kupata umaarufu mwaka 2010 na Oktoba 2012 hadi Februari 2013, inakadiriwa kuwa jumla ya Sh700 milioni zimeibwa katika benki mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Ripoti hiyo ya Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2013 iliyotolewa na Kampuni ya Uchunguzi wa Huduma ya Delloite imebaini kuwa watendaji wa ngazi za juu wanahusika zaidi na uhalifu huo ukilinganisha na watendaji wa ngazi za chini.
"Wanapofanya uhalifu hujua namna ya kuuficha na kuujadili na wasimamizi wa ndani bila kubainika.Wanajua mbinu na mifumo yote ya kifedha na wanatumia fursa hiyo kuiba," alisema Nyamu.
Watendaji waliotajwa kuhusika zaidi na wizi huo wa fedha ni wale wa ngazi za juu wakiwamo wakurugenzi watendaji, ofisa operesheni, wakurugenzi wa fedha, vitengo vya teknolojia na wakuu wa vitengo wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa fedha ukilinganisha na wafanyakazi wa kati na ngazi za chini.
Wizi unaofanyika zaidi katika nchi za Afrika Mashariki unatajwa kuwa ni wa fedha halali ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya uhalifu wa aina zote wa kifedha.
Hata hivyo Nyamu alisema watendaji wa ngazi za chini wanaweza kufanya uhalifu wa kiasi kikubwa cha fedha iwapo wanajua namna ya kufanya hivyo.
Mtaalamu wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM), Dk Eliamani Sedoyeka alisema ni kweli kuwa watu wa ngazi za juu wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa kifedha kwa sababu wanaelewa kwa undani mfumo unavyofanya kazi na kutolea mfano i wizi wa Benki ya Stanbic .

MAKINDA AAMUA ‘UGOMVI’BAINA YA LUKUVI, ABWAO

abc_066bf.jpglukuvi1_cb7d2.jpg
Spika wa Bunge, Anne Makinda jana aliingilia kati mvutano baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi baada ya kubanwa na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Chiku Abwao.
Hali hiyo ilijitokeza pale Lukuvi alipolazimika kutumia nafasi yake ya uwaziri kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Abwao kuhusu mpango wa serikali wa kufikisha maji Isimani. "Mheshimiwa Waziri, Jimbo la Isimani wananchi wake wana matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji na wamekuwa na maisha magumu,hivyo wanahitaji msaada huo, je Serikali inatoa kauli gani kuhusu kuwasaidia wananchi hao," aliuliza Abwao.(P.T)
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema shida waliyonayo wananchi wa Isimani ni sawa na maeneo mengine nchini .
Baada ya majibu hayo, Lukuvi alilazimika kusimama ghafla na kuwasha kipaza sauti,ili kusawazisha jibu la swali hilo ambalo lililenga moja kwa moja katika jimbo lake,Baadhi ya wabunge walianza kupiga kelele za kumtaka Lukuvi asizungumze kwa kuwa swali lilimlenga moja kwa moja.

ZITTO, LEMA KATIKA VITA YA MANENO

zittokabwe_742a7.jpg
Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.
Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.
Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.
Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
"Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema".(P.T)
Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.
Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.
"Mimi sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011," aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.
Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.
"Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee," alisema Zitto.
Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine wa umma.
"Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine," alisema Lema na kuongeza:
"Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600".
Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.
"Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili, ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,"alisema Lema.
Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.
"Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000 ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata Sh10,000,"alisema

KABILA ANYOOSHA MKONO WA DIPLOMASIA 

kabila_620b0.jpg
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewataka wapiganaji wa makundi yote ya waasi mashariki mwa nchi yake kuweka silaha zao chini, baada ya kile kinachoaminika kuwa ni kusambaratika kwa kundi la M23.
Akihutibia taifa hapo jana (tarehe 30 Oktoba) kwa njia ya redio na televisheni, mara tu baada ya jeshi la serikali kuuteka mji wa Bunagana, Rais Kabila alilipongeza jeshi hilo na wale Umoja wa Mataifa kwa kulirejesha eneo la Rutshuru mikononi mwa serikali.
Hata hivyo, Rais Kabila akasema pamoja na ushindi huo wa kijeshi, diplomasia na mazungumzo baina ya Wakongomani yataendelea.(P.T)
"Ninasisitiza wito wangu kwa wapiganaji wa kundi lililofurushwa kwenye mitaa ya Nyiragongo na Rutshuru kutua silaha zao chini kwa ikhari yao wenyewe kulingana na pendekezo la Nchi za Maziwa Makuu. Kinyume cha kufanya hivyo tutalazimika kuwapokonya silaha kwa nguvu. Wito wa aina hiyo hiyo unatolewa pia kwa makundi mengine ya wapiganaji ya kitaifa, kusitisha hatua zote za kijeshi kutasababisha wao na wengine kufaidika na mpango wa kuingizwa katika maisha ya kawaida." Amesema Rais Kabila.
Kabila azionya nchi jirani, makundi ya kigeni
Katika hotuba hiyo ya kwanza tangu taarifa za kusambaratika kwa kundi la waasi wa M23 mashariki kwa nchi hiyo, Rais Kabila aliyatahadharisha pia makundi ya wapiganaji ya kigeni yalioko nchini huko Kivu.
"Kuhusu makundi yaliosalia ya kigeni yakiwemo FDLR, LRA, ADF/Nalu na FNL yanayoendelea kutaabisha wakaazi wa Kivu ya Kusini na Kivu ya Kaskazini, ninayatahadharisha kutua chini silaha haraka sana. Vyenginevyo, makundi hayo yatapokonywa silaha kwa nguvu na yatachukuliwa hatua kama tunayoendesha hivi sasa."
Katika hatua nyengine, Rais Kabila ametumia hotuba hiyo kuzionya nchi jirani,ambayo hakuzitaja jina, kwamba amani ya kudumu ya Kanda la Maziwa Makuu itatokana na utekelezwaji wa Mkataba wa amani wa Addis Ababa.
"Kwan nchi jirani, ninaziambia mara nyingine kwamba njia muafaka ya kuleta amani na ustawi wa ukanda huu, ni utekelezwaji wa dhati na kwa nia nzuri kwa Mkataba wa Amani wa Addis Ababa na vile vile Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ninawahimiza kutekeleza wajibu wao kulingana na mkataba huo."
Anyoosha mkono wa diplomasia
Rais Kabila amesema ijapokuwa ushindi wa kijeshi umepatikana, lakini juhudi za kidiplomasia na kisiasa zitaendelea.
"Mtizamo wetu ni ule wa kutafuta suluhisho la mzozo wa Kongo kwa njia tatu: ya kijeshi, ya kisiasa na kidiplomasia. Na ndilo tunalofanya sasa. Ushindi wa kijeshi huko Kivu hauwezi kuvunja juhudi zingine za kisiasa na kidiplomasia."
Kufuatia ushindi wa jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa M23, Rais Kabila aliwapongeza wanajeshi na kusema wameungwa mkono na taifa nzima.
Vile vile, aliwapongeza wanajeshi wa Tanzania katika kazi wanayoifanya kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa na kutoa heshima zake na rambirambi za pole kwa familia ya wanajeshi wa Kongo na wale wa Tanzania waliopoteza maisha yao kwenye uwanja wa mapambano.
Rais Kabila alitoa wito wa kutokueko na ulipizaji kisasi baina ya Wakongomani.
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo/DW Kinshasa
Mhariri: Mohammed Khelef

NAHODHA,MAOFISA JWTZ WAMUAGA MLIMA

mlimapx_050d7.jpg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha jana aliwaongoza maofisa wa JWTZ katika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Luteni Rajab Ahmed Mlima.
Marehemu Luteni Mlima, aliuawa akiwa katika Uwanja wa Mapambano na wanagambo wa Kundi la Waasi wa M23, katika Milima ya Gavana, karibu na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Viongozi wengine walioshiriki katika kutoa heshima zao za mwisho kwa ofisa huyo, ni pamoja na waziri wa zamani katika wizara hiyo Profesa Philemon Sarungi, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na viongozi mbalimbali wa Serikali.(P.T)
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa heshima hizo, Waziri Nahodha alisema Serikali inatoa pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, kwa kumpoteza mtu shujaa aliyekuwa akitetea roho za watu.
Alisema hata hivyo, Serikali haitarudi nyuma katika masuala ya ulinzi wa amani, na kwamba itaendelea kutoa msaada wa ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi hapo amani itakapopatikana.
"Kwa kweli tumepata pigo kubwa la kuondokewa na shujaa wetu, lakini sisi kama Serikali hatutarudi nyuma kwenye masuala ya ulinzi wa amani hadi pale tutakapoona amani imepatikana,"alisema Nahodha.
Waziri huyo alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kutoa msaada kwa familia ya marehemu Luteni Mlima, kwani hilo ni jukumu lake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Ndomba, alisema Luteni Mlima amefariki kishujaa wakati akilinda amani na kwamba siku zote jeshi litatambu mchango wake.

MUGABE ANAWEZA 'KUTUSIWA'AU KUKOSOLEWA

120927121136_mugabe_un_304x171_reuters_nocredit_35956.jpg
Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe imebatilisha sheria inayosema kuwa ni uhalifu kumtusi Rais wa nchi.
''Viongozi wa mashitaka hawapaswi kuwa na tamaa sana ya kuwashitaki watu wanaomkosoa Rais Mugabe katika kumbi za ulevi na maeneo mengine ya kijamii,'' iliamua mahakama ya kikatiba.
Angalau watu 80 wameshitakiwa chini ya sheria hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei, mwanaharakati Solomon Madzore alikamatwa baada ya kudaiwa kumuita Mugabe 'Punda anayechechemaa.'(P.T)
Alikanusha kosa la kumtusi Rais.
Chini ya kifungu cha 33 cha sheria ya uhalifu nchini Zimbabwe, mtu anaweza kufungwa jela hadi mwaka mmoja au kutozwa faini ya dola 100 kwa kumtusi Rais.
Sheria hiyo ilipingwa na watu kadha nchini humo akiwemo mkaazi mmoja wa mji wa Bulawayo Kusini mwa nchi, Tendai Danga, aliyekamatwa miaka miwili iliyopita kwa madai ya kumtusi Mugabe wakati alipozozana na polisi ndani ya baa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Harare, Brian Hungwe, majaji tisa waliotoa uamuzi huo, walikubaliana kwa kauli moja kuwa sheria hiyo inahujumu uhuru wa kujieleza na kuifanya vigumu kwa serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wao.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimpa waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa hadi tarehe 20 Novemba kukata rufaa.
Mwezi Agosti mahakama ilimwachilia huru mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 26 Takura Mufumisi, aliyeshitakiwa kwa kuwa na nia ya kutumia bango la karatasi lenye picha ya Mugabe kama karatasi ya kujipangusia chooni ndani ya baa moja.
Katika kura ya maamuzi iliyofanyika mwezi Machi, wananchi walipitisha katiba mpya ambayo inawapa uhuru zaidi wa kujieleza.
Watu wengi wamepongeza uamuzi wa mahakama wakiamini kuwa sheria ilikuwa imemlinda rais dhidi ya kukosolewa.

ICC YAAHIRISHA KESI DHIDI YA RAIS KENYETTA

 131013152443_addis_union_africaine_african_union_uhuru_kenyatta_12102013_304x171_reuters_nocredit_0143d.jpg

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imeahirisha kesi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mahakama hiyo hadi tarehe 5 mwezi Februari mwaka 2014.
Uamuzi huo umefikiwa hii leo ikiwa siku moja kabla ya upande wa mashitaka kuashiria kuwa hawatapinga ikiwa kesi hiyo kuahirishwa kwa mwaka mmoja hadi Novemba mwaka 2014
Pia unakuja huku juhudi za kidipmolasia za viongozi wa Afrika kushinikiza baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zikishika kasi kulitaka baraza hilo kukubali kesi dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto kuakhirishwa.(P.T)
Rais Kenyatta alikuwa ameiomba mahakama hiyo kuakhirisha kesi dhidi yake hadi Februari mwaka ujao huku upande wa mashitaka ukitaka ukahirishaji kutozidi Februari tarehe tatu mwaka 2014.
"Majaji wamekubaliana na upande wa mashitaka kuahirisha kesi dhidi ya Rais Kenyatta hadi Februari mwaka 2014 ili kuupatia upande wa mashitaka muda wa kutosha kufanya uchunguzi zaidi kutokana na tuhuma dhidi ya upande wa mashitaka kutoa taarifa zisizo za kweli, '' majaji walisema katika uamuzi wao.
Upande wa utetezi nao ulitaka tarehe ya kesi hiyo kuahirishwa ili majaji waweze kushughulikia baadhi ya malalamiko yao, kuhusu Kiongozi wa mashitaka kuhujumu mfumo wa kesi dhidi ya Kenyatta. Malalamiko hayo waliyawasilisha Oktoba tarehe kumi na kuwasilisha ombi la kutaka kesi dhidi ya Rais Kenyatta kufutiliwa mbali.

MAMBO YALIVYOKUWA TAIFA LEO BAADA YA POLISI KULIPUA MABOMU SIMBA NA KAGERA 

Nimesikitishwa sana na vitendo vya kihuni vilionyeshwa na wachezaji na baadhi ya wapenzi wa Simba jana pale Neshno.
Simba wanastahili adhabu ikiwemo kufidia uharibu ule wa viti vya kukalia. Na adhabu hiyo isichelewe...
Maggid.
aa_a428f.jpg
haya ni mabomu ya machozi ambayo yalirushwa ili kudhibiti vurugu hizo
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam jana uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu hizo zikitoka 1-1.
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung'oa viti na kuvitupia uwanjani.
bb_4adda.jpg
hapa mashabiki wakikimbia baada ya vurugu hizo kuanza kutokea na mabomu kuanza kurushwa
cc_58045.jpg
Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mohamed Theofile wa Morogoro aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, ambao walishindwa kuumudu kabisa, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
dd_2fa72.jpg
hivi ni baadhi ya viti vilivyong'olewa na mashabiki
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri ya Betram Mombeki na kumpiga chenga beki Salum Kanoni, kabla ya kumchambua kipa Hannington Kalyesebula.
Kagera ilipata pigo mapema dakika ya 22 kipa wake Agathon Anthony kuumia katika harakati za kuzuia shambulizi la Tambwe na nafasi yake ikachukuliwa na Mganda, Kalyesebula.
Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza, ingawa Simba SC ndiyo waliotengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.
Kipindi cha pili, Simba SC iliendelea kusukuma mashambulizi mengi langoni mwa Kagera, lakini washambuliaji wake walikosa umakini wa kutumia nafasi.
Kagera nayo iliendelea kushambulia na kwa ujumla mchezo ulizidi kunoga kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele kutokana na ushindani mkali.
Wakati refa wa akiba, Hussein Kalindo wa Kinondoni, amekwishaonyesha dakika nne za nyongeza, Kagera ikafanya shambulizi langoni mwa Simba na Daudi Jummane akaangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Simba SC, Joseph Owino na refa akaamuru penalti.
Beki wa zamani wa Simba SC, Salum Kanoni akaenda kumchambua vizuri kipa Abuu Hashimu kuisawazishia Kagera dakika ya 90+2.
Simba SC; Abuu Hashim, Nassor Masoud 'Chollo', Issa Rashid, Joseph Owino, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betram Mwombeki, Amisi Tambwe na William Lucian.
Kagera Sugar; Agathon Anthony/Hannington Kalyesebula dk22, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Ernest Mwalupani, Malegesi Mwangwa, Zuberi Dabi/Juma Mpola dk46, Benjamin Asukile/Adam Kingwande dk46, George Kavilla, Themi Felix, Daudi Jumanne na Paul Ngwai.
ee_e08bb.jpg
Hapa askari wakimdhibiti mmoja ya mashabiki (P.T)