TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, May 3, 2013

VILLABOAS BALE HANGO'KI SPURS KWA PAUNDI 60 MILLION
d1 c44c0

Gareth Bale
KOCHA Andre Villas-Boas hana shaka Gareth Bale ataendelea kuwa mchezaji wa Tottenham msimu ujao, akisema kwamba hata itolewe ofa ya Pauni Milioni 60 hatamuuza.
 
Nyota huyo wa Wales, ambaye leo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda England, amekuwa katika msimu mzuri, akitoa mchango mkubwa kwa Spurs.
Akiwa amefunga mabao 19 katika mechi 29 za Ligi Kuu England, Bale ameendelea kuzikuna klabu kubwa, zikiwemo Real Madrid na Bayern Munich ambazo zinaitaka saini yake kwa gharama yoyote.
 
Gwiji la Ufaransa, Zinedine Zidane, ambaye anafanya kazi kama Mshauri Maalum wa vigogo wa Hispania, Real amesema jana kwamba kiasi cha Pauni Milioni 48, ambazo Madrid waliliipa Juventus kumpata yeye zaidi ya muongo uliopita, kupata saini ya winga huyo.
 
Pamoja na hayo, Villas-Boas amejibu leo, akisema: "Hata kama kiwango hicho cha fedha kinamlenga mchezaji huyo, haijalishi kwetu, kwa sababu ni mchezaji wetu na mchezaji ambaye tunatakiwa kuendelea kuwa naye kuhakikisha tunatimiza malengo yetu na kuendeleza harakati. 
 
"Taarifa nilizonazo kutoka kwenye klabu klabu ni kwamba, mchezaji huyo yupo hapa kubaki, hata ikiwa tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa au la. Klabu lazima iendelee mbele kwa kuwashikilia wachezaji wazuri,".
CHELSEA YATINGA FAINALI EUROPA LEAGUE YAIPIGA BALSE FC 3-1
c1 92a3c
 
Victor Moses akifunga
  
c2 15f5e
 
 
Fernando Torres akifunga bao lake la tano katika mechi nane na la 10 katika Europa League msimu huu
 
 
c 72875
 
 
David Luiz akifunga kwa shuti la mbali
 
CHELSEA imefanikiwa kutinga fainali ya Europa League baada ya kuifunga mabao 3-1 FC Basle ya Uswisi jana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
 
Mabao ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na Fernando Torres dakika ya 50, Victor Moses dakika ya 52 na David Luiz dakika ya 59, wakati la kufutia machozi la Basle lilifungwa na Salah dakika ya 45,
Chelsea imetinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada ya awali kushinda ugenini 2-1 na sasa itamenyana na Benfica ya Ureno katika fainali, ambayo usiku huu imeifunga Fenerbahce mabao 3-1 hivyo kufuzu kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-2.
MOURINHO KUIHAMA REAL MADRID MSIMU UJAO

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho, amesema huenda asiwe kocha wa klabu hiyo msimu ujao.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka hamsini, ambaye amewahi kuongoza Chelsea, siku ya Jumanne, alishuhudia vijana wake wakiondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, licha ya kuilaza Borussia Dortmund ya Ujerumani, kwa magoli mawaili kwa yai.

Dortmund ilifuzu kwa fainali ya kombe hilo kwa jumla ya magoli manne kwa matatu.

Katika mechi ya raundi ya kwanza Dortmund, iliilaza Real Madrid kwa magoli manne kwa moja.

Kumekuwa ya ripoti kuwa kocha huyo kutoka Ureno, alikuwa akijiandaa kukihama klabu hiyo ya Real Madrid na kurejea nchini Uingereza. Chanzo: www.bbcswahil.com

Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya jana Morinho alisema , anafahamu kuwa anapendwa na mashabiki na vilabu vingi nchini Uingereza.

Hata hivyo amesema atasalia hadi mwisho wa msimu huu kabla ya kuamua hatma yake ya siku zijazo.

Mourinho alikihama klabu ya Chelsea, katika hali ambayo haikufahamika Septemba mwaka wa 2007, baada ya kutofautiana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA TFF
 
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.

FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA, Jerome Valcke.

Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT). 

“Matarajio yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.

“Lengo letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na FIFA.”

Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika barua FIFA kuomba iingilie kati.

Rais Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
  1. Kuunda vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
  2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
  3. Kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
  4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.

Katika kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.

Katika maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.

Hata hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.

“Kutokana na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.

Rais Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, May 2, 2013

CCM WAMVAA MKUU WA MKOA WA ARUSHA.....WANADAI AMEMUONGEZEA UMAARUFU GODBLESS LEMA


VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Wabunge hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka 
za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.

“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.
“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.


Mbunge mwingine ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema alichokifanya Mulongo ni sehemu ya tatizo kubwa la viongozi wa serikali kujihusisha na ukereketwa wa kisiasa.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi, tena hakumtaja jina, kwamba anapendwa kubebwa, alisema mwacheni abebwe. Alisema vile kuwazuia polisi kukabiliana na watu wanaopenda kumbeba kiongozi huyo.

“Mkuu wa Mkoa Arusha na wengine wanaokabiliana na wapinzani kwa nguvu kubwa bila sababu, hii inawaongezea umaarufu,” alisema mbunge huyo kutoka moja ya majimbo ya kanda ya kati.


Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya CCM ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alilaani jinsi mkuu wa mkoa huyo alivyojikoroga katika kushughulikia mzozo wa Chuo cha Uhasibu Arusha.


“Niliposoma ujumbe wa simu ya mkononi wa Lema ambao alidai umetoka kwa Mkuu wa Mkoa, nilishangaa sana. Sijui kwanini amefanya vile,” alisema kigogo huyo.


Aprili 24 mwaka huu, Mulongo aliliamuru Jeshi la Polisi mkoani Arusha kumkamata Lema kwa madai kuwa aliwachochea wanafunzi wa chuo hicho cha IAA kumzomea na kumrushia mawe.

Lema alizingirwa nyumbani kwake na maofisa wa polisi kitengo cha upelelezi na wale wa doria Ijumaa saa 5.30 usiku kisha kuchukuliwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuwekwa rumande siku tatu hadi Jumatatu wiki hii alipofikishwa mahakamani.


Hata hivyo, madai ya Mulongo kuwa Lema alichochea wanafuzni hao yanakinzana na ushahidi wa video unaoonesha kuwa mbunge huyo alitumia kila aina ya ushawishi kuwasihi wasiandamane kufuatia mwenzao Elly Kago (22) kuuawa na watu wasiojulikana jirani na chuo.

Mapema kabla ya kukamatwa, Lema aliitisha mkutano na waandishi wa habari akidai kutishiwa na Mulongo kupitia ujumbe wa maandishi wa simu.


“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonyesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
Atisha waandishi


Wakati CCM wakiendelea kumlalamikia Mulongo kwa hatua zake dhidi ya Lema, kiongozi huyo jana aliwageukia waandishi wa habari wa Arusha akiwataka wawe makini kipindi hiki, akidai kuwa nao wanatumika na wanasiasa.


Akihutubia katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi, alisema kuwa ikibainika wanatumika nao watafikishwa katika vyombo vya sheria.


“Mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, hivi hivi wakawa hawanielewi na ikafika wakati wakanielewa kwani kuna miongoni mwao tulitaka kuwafikisha katika sheria, lakini tukayaacha kwa kuwa sisi ndio walezi,” alisema.

Mulongo aliongeza kuwa vitu ambavyo vinaandikwa si kweli kabisa, na kwamba wataendelea kufuatilia kwani baadhi ya waandishi wanashirikiana na wanasiasa kuwachafua viongozi wa serikali.

Alisema baadhi ya waandishi mkoani Arusha wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ushabiki wa kisiasa na kuandika mambo ambayo hawana uhakika nayo.


“Unapoingia katika mkakati wa kudhalilisha kiongozi wa serikali unakuwa umeiweka roho yako rehani, kuweni makini,” alisema.


Aidha alivionya vyama vya wafanyakazi mkoani Arusha kutoruhusu kutumiwa na watu kwa malengo ya kisiasa na pia waajiri waache kufanya kazi bila kufuata taratibu na sheria.



TANZANIA DAIMA
SIKU NIKIFA RUGE MUTAHA NA KUSAGA WASIHUDHURIE MAZISHI YANGU LADY JAYDEE

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.


Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
 
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
 
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.  
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.

Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.  
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.

Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
 
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
 
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
 
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
 
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
 
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

Wednesday, May 1, 2013

DOTNATA AWEKEWA TEGO LA SUMU KWENYE JUICE
Husna-Poshi-533-K

Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.
Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.
 
Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.
 
“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.
 
Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
 
“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. 
 Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”
CHEKA AENDELEZA UBABE
Picture 1442 2263f
Bondia Cosmas Cheka kushoto akipambana na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba siku ya mei mosi Cheka alishinda kwa ponti mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Picture 1613 4e039
UEFA:BAYERN,DOTMUND FAINALI WEMBLEY
b1 b06d5
Bayern watinda fainali kwa kishindo baada ya kuitwanga Barcelona 7-0 katika michezo yote miwili, wa kwanza 4-0 na wa pili 3-0.

b2 65928
Robben (haonekani) shuti lake likitinga nyavuni

b3 78840
Kipa wa Barca, Victor Valdes akilalamika baada ya Pique kujifunga

b4 5d06d
Thomas Muller wa Bayern akifunga bao la tatu

b 921b6
Arjen Robben (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Nou Camp
 
 Itakuwa fainali ya Wajerumani watupu Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Wembley wiki tatu zijazo Jumamosi, ikiwakutanisha Bayern Munich na Borussia Dortmund.
 
Hiyo inafuatia Barcelona iliyomkosa Lionel Messi aliyekuwa benchi kutandikwa mabao 3-0 nyumbani usiku huu, baada ya awali kuchapwa 4-0 Ujerumani, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 7-0.
 
Barcelona walionekana kabisa kuzidiwa uwezo na mapema tu walionekana hawawezi kupanda mlima huo. Mabao ya Bayern ambao tayari ni mabingwa wa Ujerumani, wakiivua taji Dortmund, yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 49, Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 72 na Thomas Muller dakika ya 76. Chanzo: Binzubeiry.
 
RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI MBEYA

8E9U2311Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi wengine kuimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa maadhimisho ya Sikuukuu ya Wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa TUCTA Nicolaus Mgaya, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mhe.Gaudensia Kabaka, Kaimu Rais wa TUCTA Bibi Nortubunga Maskini, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Mh.Abdulrahman Kinana.
8E9U2015Baadhi ya wafanyakazi wakishiriki katika maandamano  yaliyofanyika wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi  katika Uwanja wa michezo  wa Sokoine mjini Mbeya(picha na Freddy Maro)
MIKOA 18 YAPATA MABINGWA WA MIKOA
10 ad9baMikoa 18 kati ya 27 ya kimpira tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu tatu za juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014). Ligi ya FDL ina jumla ya timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu ni Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa na Morani FC ya Manyara.

Mabingwa waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Wengine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Kila klabu inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
MTANZANIA AOMBEWA ITC ACHEZE NORWAY
Shirikisho la Mpira wa Miguu Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili aweze kucheza mpira nchini humo.
NFF inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini Norway.
AZAM YAENDELEA KUJINOA MOROCCO
Timu ya Azam ambayo iko jijini Rabat kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabati ya huko inaendelea vizuri na mazoezi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi wa Azam FC, Jaffer Idd maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Mei 4 mwaka huu). Jaffer Idd anapatikana kwa namba +212671146092.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MADRID YAFA KIUME SANTIAGO BERNABEU YAIPIGA DOTMUND 2-0
r1 08cb6
  Sergio Ramos akishangilia bao lake la pili lililowapa Madrid Matumaini makubwa
  r6 6e08a
 Robert Lewandowski akichungulia moja ya mashuti yake kama unaingia kimiani ama la
   r7 a0a0a
Mourinho akionekana amepaniki sana 

Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Daah! Ali manusura vijana wa Mourinho waione Wembley mwaka huu baada ya kuwafunga nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani, Borrusia Dortmund mabao 2-0 usiku huu katika dimba la Santiago Bernabeu.

Matokeo hayo yameitupa nje Real Madrid kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza nchini ujerumani ambapo Mourinho alipiga kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 na baada ya kushinda leo kwa mabo mawili Madrid wanatoka kwa wastani wa mabao 4-3.
NITAGOMBEA URAIS MWAKA 2015
05 840fa
Na Francis Godwin,Iringa
HUKU hali ya mambo ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kuwa si shwari kutokana na makada wake kuendelea kupigana vikumbo ikiwa ni sehemu ya harakati mbio za urais mwaka 2015 , waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe ameibuka na kutoa ya moyoni kuwa atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015 iwapo wananchi wataona anafaa na watamtaka agombee nafasi hiyo.

Pia waziri Membe alisema kuwa hali ya nchi inavyokwenda kwa sasa si shwari kutokana na baadhi ya wabunge wa CCM na vyama vya upinzani kuendelea kuzungumza ovyo ovyo juu ya chama na serikali jambo ambalo ni hatari zaidi kwa Taifa.
Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusu mbio hizo za Urais .
mtandao huu ulifanya mahojiano hayo mjini Iringa baada ya kumalizika kwa kongamano la wana vyuo vya elimu ya juu mkoani Iringa kongamano lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic ambako alikuwa mgeni rasmi waziri Membe alisema kuwa pamoja na kauli yake ya kwanza kwa Taifa kuwa muda bado kufika wa kufanya hivyo .
Waziri huyo alisema kuwa mbali ya kuwa muda wa kutangaza kuwania nafasi hiyo bado haujafika na chama chake kina utaratibu wa kutangaza mara baada ya muda kufika ila kwa mtazamo wake kama alivyopata kuueleza umma awali alipozungumza na vyombo vya habari juu ya mbio hizo za urais ,alisema kuwa anaheshimu sana taratibu za chama .
" Naomba kurudia tena mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea Urais ....ila nasema hivi natagemea sana ushauri wa watanzania iwapo wataniona nafaa na kunitaka nigombee nitapima mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka nigombee basi nitachukua fom na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu " alisema waziri Membe
kuwa kama wananchi watasema jaza fom na nikaona ni sauti ya wengi nitajaza fomu ya kuwania kiti cha urais
Pia alisema kuwa hadi sasa hali ya nchi inazidi kwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza mambo bila kuthathimini na kuwa mbaya zaidi hata baadhi ya wabunge wa CCM nao wamekuwa si msaada kwa chama kutokana na mambo wanayozungumza dhidi ya serikali na chama.
Kuhusu mwenendo wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sasa waziri Membe alisema kuwa kwa upande wake amepata kukaa bungeni zaidi ya miaka 15 toka bunge la spika Pius Msekwa hadi sasa chini ya spika Anne Makinda ila anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo bila kuzingatia kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari zaidi.
Alisema kuwa bunge linalotazamwa na watanzania ni lazima liwe bunge lenye mfano wa kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza ila kwa sasa ndio maana bunge linaendelea kupoteza mwelekeo wake .
"Bunge linapoteza mwelekeo kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wakifikiri wakisema ovyo na kutumia lugha kali katika kuzungumza basi wao ndio wanaonekana ni wabunge bora kitu ambacho hakipo ....kwani kuwa mbunge ni pamoja na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura wako bungeni"
Waziri Membe alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kutotumia busara katika kujadili mambo bungeni si ubunge mzuri na watambue wazi kuwa wananchi wao wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kama hivyo wanachokifanya ni kuwawakilisha wananchi ama kujiwakilisha wao.
"Nawaomba wabunge kuwa wazalendo na kuwawakilisha wananchi waliowatuma badala ya kuligeuza bunge kama sehemu ya kuonyesha ujuzi wa kuzungumza ovyo ....nasema tuwaogope wananchi mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila mbunge kwa sasa wananchi wanakusikiliza na kunakutazama ila muda ukifika watakuacha"
Alisema kuwa wabunge wengi ni vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika na kuangalia kuwa amefanya nini katika jimbo lake na watakupima kwa kazi uliofanya na sio ukali wako bungeni.
Aidha waziri Membe alisema kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi katika majimbo yao na pia wamekuwa msaada kwa chama na serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa msaada mkubwa wa kusukuma mbele maendeleo ya Taifa ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao wa kusema ovyo.

NHIF YASHIRIKI KWENYE MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU
0 835b4
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe.Dr Hamid Nassoro akipata ufafanuzi wa huduma zilizotolewa na NHIF wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kwa wote ambayo yaliyoadhimishwa kitaifa mkoani Lindi hivi karibuni,anayetoa maelezo kulia mwenye miwani ni msimamizi wa ofisi ya NHIF Lindi Fortunata Raymond

02 8ff49
Afisa wa NHIF mkoa wa Lindi Laurent Hoja akishiriki kuchangia damu kwenye benki ya damu salama ili iweze kusaidia wananchi wenye mahitaji

JK AKUTANA NA MORGAN TSVANGIRAI IKULU , DAR
jk a5d98
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu wa nchi ya Zimbabwe Bwana Morgan Tsvangirai ikulu jijini Dar es Salaam. Chanzo: Freddy Maro