TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, February 4, 2013

MICHAEL WAMBURA ATUPWA TENA UCHAGUZI TFF

TAARIFA KWA UMMA  UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)

04/02/2013
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF  na Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:

1.       TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD

(a)                 Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI INAYOGOMBEWA
S/N0.
JINA
MWENYEKITI WA TPL BOARD
1.
Hamad Yahya Juma
2.
Yusufali Manji


MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD
1.
Said Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management  Committee)

1.

Kazimoto Miraji Muzo

2.
Omary Khatibu Mwindadi
(b)                Mwombaji uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board  Ibara ya 28(2)  kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.
2.       SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

(a)     Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
S/No.
JINA
RAIS WA TFF
1.
Athumani Jumanne Nyamlani
2.
Jamal Emily Malinzi

MAKAMU WA RAIS WA TFF


2.
Ramadhan Omar Nassib           
3.
Wallace Karia
MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)

           
1.
Kalilo Samson
2.
Salum Hamis Umande Chama


Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)
1.
Jumbe Oddessa Magati
2.
Mugisha Galibona
3.
Samwel Nyalla
4.
Vedastus F.K Lufano


Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
1.
Epaphra Swai



Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)


1.
Elley Simon Mbise
2.
Omar Walii Ali  


Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)
1.
Ahmed Idd Mgoyi
2.
Yusuf Hamis Kitumbo


Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)


1.
Blassy Mghube Kiondo
2.
Seleman Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)


Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)
1.
David Samson Lugenge
2.
John Exavery M. Kiteve
3.
Lusekelo E. Mwanjala


Kanda ya 8 (Ruvuma, Njombe)
1.
James Patrick Mhagama
2.
Stanley W. D Lugenge


Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)
1.
Athuman Kingome Kambi
2.
Francis Kumba Ndulane
3.
Zafarani Mzee Damoder


Kanda ya 10 (Dodoma,  Singida)
1.
Hussein Zuberi Mwamba
2.
Stewart Ernest Masima


Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)


1.
Riziki Juma Majala
2.
Twahil Twaha Njoki


Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
1.
Davis Elisa Mosha
2.
Khalid Abdallah Mohamed
3.
Kusianga Mohamed Kiata


Kanda ya 13 (Dar es salaam)
1.
Alex Crispine Kamuzelya
2.
Juma Abbas Pinto
3.
Muhsin Said Balhabou   

(b)    Waombaji uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i)                   Ndg. Omary Mussa Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(ii)                 Ndg. Michael Richard Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya  Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.

             Pia Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa  Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati  ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).  

(iv)               Ndg. Abdallah Hussein Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.

(v)                 Ndg.  Mbasha Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu)  hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.

(vi)               Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF  kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.

(vii)              Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3  inayotaka awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia  hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.

(viii)            Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.

(ix)               Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na.  7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF  kuhusu mabadiliko ya Katiba.

(x)                 Ndg. Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na  Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake na  vyeti vya elimu havikubaliani.


(xi)               Ndg. Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa  hakuhudhuria usaili.

(xii)              Ndg. Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa  alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania  (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

(xiii)            Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF. 

3.       Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board.

4.       Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.

Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
MAJAMBAZI WAVAMIA NYUMBANI KWA WAZIRI
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba

























WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa lengo la kufanya uhalifu. Hata hivyo majambazi hao ambao walimfunga kamba mlinzi wa nyumba hiyo na...
kuingia ndani, hawakufanikiwa kuiba chochote. Naibu Waziri Makamba aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana wakati yeye akiwa safarini jimboni kwake Bumbuli ila familia yake ilikuwapo nyumbani hapo.
Makamba alisema baada ya majambazi hao kuingia ndani, walimfunga kamba na kumziba mdomo mlinzi.
“Ujambazi huo ulitaka kufanyika nyumbani kwangu Masaki karibu na Ubalozi wa Afrika Kusini. Mimi sikuwepo nyumbani. Walivamia chumbani mke wangu akabonyeza kengele iliyopiga kelele ndio wakakimbia, baada ya majirani kuwasili eneo la tukio, wakatokomea kusikojulikana,” alisema Makamba na kuongeza:
“Waliingia kwenye ofisi yangu ya pale nyumbani na kupekua. Lakini cha ajabu ni kwamba sebuleni kulikuwa na Ipad na laptop (kidadavuzi mpakato) lakini hawakuvichukua.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyella alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu hao walitaka kufanya ujambazi, lakini hawakufanikiwa.
Kamanda Kenyella alisema tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri ya kuamkia jana, lakini majambazi hao hawakufanikiwa kutimiza azima yao.
“Walimfunga kamba mlinzi na kufungua dirisha, kisha kuingia ndani. Lakini hawakufanikiwa kuchukua chochote,” alisema Kamanda Kenyella.
Kamanda Kenyella alieleza kuwa majambazi hao hawakufanikiwa kuiba chochote kwa kuwa wakazi wa eneo hilo, walisikia purukushani na kupiga kelele zilizosababisha watu hao kutokomea.
“Haijulikani walikuwa wangapi kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewaona, lakini katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa,” alisema Kamanda Kenyella.
Alisema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi Kinondoni, inaendesha msako wa kuwatafuta watu hao ili kuweza kuwatia nguvuni na kuwafikisha mahakamani.
TIKETI ZA MCHEZO KATI YA TAIFA STARS NA CAMEROON KUANZA KUUZWA FEB 5





















Tiketi kwa ajili ya pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon (Indomitable Lions) zinaanza kuuzwa kesho (Febaruari 5 mwaka huu) katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Viingilio katika pambano hilo litakalochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni ni sh. 5,000 (viti vya kijani), sh. 7,000 (viti vya bluu), sh. 10,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B na sh. 30,000 VIP A.  Vituo vitakavyouzwa tiketi hizo kuanzia saa 2 asubuhi ni
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Oilcom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.
 Vilevile tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi, na milango itafunguliwa saa 8 kamili mchana.
 Wakati huo huo, kundi la kwanza na la pili la wachezaji wa Cameroon tayari limetua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Cameroon chini ya Kocha Jean Paul Akono itafanya mazoezi kesho saa 11 jioni Uwanja wa Taifa. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager yenyewe itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa leo saa 11 jioni.
 12,984 WASHUHUDIA SIMBA, JKT RUVU ZIKITOKA SARE
Watazamaji 12,984 walikata tiketi kushuhudia mechi ya namba 99 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
 Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 ambapo jumla ya sh. 73,532,000 zilipatikana. Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 17,443,752.45 ambapo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,216,745.76.
 Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,869,704.64, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 5,321,822.78, Kamati ya Ligi sh. 5,321,822.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,660,911.39 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,069,597.75.
 UCHAGUZI FRAT SASA KUFANYIKA FEB 14
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) uliokwama kufanyika mara mbili, sasa utafanyika Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla ya tarehe ya uchaguzi. Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.
 Wagombea ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.
 Abdallah Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi wanawake yupo Isabela Kapera.
 Wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.

Sunday, February 3, 2013

JK AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na viongozi wengine wa chama wakijiandaa tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.
























Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa  sherehe kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Chama cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani Humo.
JENGO LA PPF TOWER LATEKETEA KWA MOTO
Picha ya jengo la PPF ikionesha moshi mkubwa unaofuka kutoka kenye jengo hilo.Shukurani ya picha: A, rafiki wa M.C.na Subi
----
Taarifa zinasema kuwa,hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo  juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi  wa  jengo hilo  walishuhudia moshi mzito  ukitoka ndani ya  jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi ghorofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo.
 Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo  kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.

Saturday, February 2, 2013

KILIMO NA UJASILIAMALI NI MUHIMU
Wafanyabiashara wakiwa na bidhaa zao Morogoro Msavu

Maharage mabichi hayo yakiwa sokoni hapo




Kijani  inavyopendeza kwa mabili hayo yanayoonekana ni mahindi yakiwa yametoa mbelewele

Hiyo ndio kazi yetu tukiwa nje ya Jiji la Dar ni kutunza mashamba na kulima

Friday, February 1, 2013

JK AKAMILISHA USAILI WA KITAMBULISHO CHA TAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya Ijumaa, Februari Mosi, 2013.

WEMA SEPETU ACHUKUA FOMU YA KUSHIRIKI BIG BROTHER AFRICA


Taarifa kutoka ofisi za DSTV jijini Dar es Salaam zinadai kuwa aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu alikuwa katika ofisi hizo kuchukua fomu za kushiriki shindano la Big Brother Africa mwaka huu.

Wema ni miongoni mwa mastaa nchini wanaopendekezwa zaidi kuiwakilisha Tanzania mwaka huu. Mwingine anayependekezwa zaidi ni Khaleed Mohamed aka TID

WOLPER AELEZA SIRI YA UREMBO WAKE
 
 Msanii wa filamu Tanzania Jackline Wolper hatimaye amefichua siri ya urembo wake kitu kinachomfanya aendelee kuonekana kuwa  mrembo na kubaki na mvuto wake wa asiri

Akizungumza na Pro-24 ,Wolper alijikuta akiweka wazi anachokifanya ili kuendelea kubaki na urembo huo huku akisisitiza kuwa mazoezi ya viungo vya mwili na kutokunywa bia ni siri kubwa ya urembo wake

Wolper hakusita kuweka wazi kuwa yeye ni mtu wa kula mbogamboga,samaki, maziwa na matunda kwa wingi huku akipata muda wa kupumzika ili kujenga mwili wake bila ya kusahau kunywa maji kwa wingi kwani hayo yanamfanya ngozi yake iendelee kuwa yenye mvuto

Wolper alisisitiza kuwa katika maisha yake hutumia kula nyama nyeupe na kuepuka nyama nyekundu ili aendelee kubaki hivyo alivyo na kuepuka kuwa mnene na kutoka kitambi kama baadhi ya wanawake wengine wanavyokuwa

NUNGWI MASHUA YAZAMA NA WATU 11 KUTOONEKANA

























  Kama ingekuwa nchi kavu tungesema eneo la nungwi ni sawa na eneo hatari kama vile mlima kitonga au sekenke,kwani mchana wa leo limetokea lingine la kutokea hukohuko nungwi…

Jahazi la clouds fm likafanya juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa kaskazini unguja.. ACP ahmad khamis abdallah amezungumza jinsi ajali hiyo ilivyotokea
"ajali imetokea baina ya Nungwi na Tanga, na tayari tmeshapokea badhi ya watu, tumepokea 21 ambao ni wazima, hakuna maiti iliyopatiokana mpaka sasa, na waliokuwemo kwenye chombo walikua jumla ya watu 32, khiyo ni kusema watu 11 mpaka sasa hawajapatikana." amesema Ahmad Khamis
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI NA ASKALI WENZAKE WAMTIBUA HAKIMU

























Askari waliomleta mahakamani mtuhumiwa askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)  wa mauwaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi,   wamemtibua Hakimu aliyeagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani hapo kwa kudharau mahakama hiyo.

Tukio  hilo lilitokea leo  majira ya saa 5.35 lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo. Askari  watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa  kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .

Mahakama ikiwa  bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi  wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani  huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza  kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.

Wakati hakimu  huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku  hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria  waMahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha  na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa  bila utaratibu wa mahakama hebu  mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona  wanafanya fujo mahakamani  hao.
Pamoja na jitihada za mwanasheria wa  serikali Adolf Maganda kuwaita  kwa  sauti,  askari hao  kuwataka  kumrudisha  ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo  bali  walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda naye mahabusu. 

Baada ya dakika kama 5 hivi, ndipo mwanasheria  huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambaye hata  hivyo hakwenda kusimama  kizimbani na badala  yake alikwenda upande wa  kushoto wa mahakama ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama  kuanza na kuketi katika  kiti huku akiwa bado amevaa miwani na kofia  yake.

Kutokana na  tukio  hilo, Hakimu  huyo alilazimika  kuwahoji askari hao  watatu kwa vurugu  hizo  walizozifanya kwa kuwauliza swali moja  pekee , ikiwa wanaona walichofanya ni  sahihi, ambapo askari hao waliosema, “samahani mheshimiwa”.

Mwendesha mashtaka  wa Jamhuri, Adolf Maganda aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena  kwa kesi hiyo ambayo awali ilikuwa imetajwa Januari 27, 2013 lakini mtuhumiwa alishindwa kufika Mahakamani kutokana na ugonjwa. Mahakama  hiyo  imeahirisha  kesi hiyo  hadi  Februari 14 mwaka huu.

Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa  bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Ten  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  zilipozuka vurugu kati ya  Askari Polisi na wafuasi wa  CHADEMA.
MTANGAZAJI WA RADIO NCHINI AKAMATWA NA MADAWA YA KULENYA KENYA



















Hivi karibuni mamlaka nchini Kenya zilikamata madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 5.44.

Msemaji wa mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA) Kennedy Onyonyi amesema madawa hayo yalikamatwa yakiwa na mtanzania Saraphia Peter Shirima, Jan. 23 alipokuwa akijaribu kuvusha madawa hayo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.


Mamlaka hiyo imesema Saraphia sio mwanafunzi bali ni mtangazaji wa radio nchini Tanzania.Onyonyi alisema mtangazaji huyo ana kibali cha kuishi nchiini Sweden kwa miaka miwili kitakachoisha ” Nov. 28, 2014.

Madawa hayo yana gharama ya dola za kimarekani 150,000 ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akiyasafirisha kuyapeleka Budapest, Hungary.
RIHANA ATAJA SABABU ZILIZOMFANYA ARUDIANE NA CHRIS BROWN
Rihanna amefunguka mengi kuhusu uhusiano wake na Chris Brown na kuweka wazi kwanini aliamua kumpa second chance.

“Niliona  ni muhimu zaidi kwa mimi kuwa na furaha, “ aliliambia jarida lijalo la Rolling Stone. “Sikutaka kuacha mtazamo wa mtu yeyote hata kama ni kosa, ni kosa.”

Katika toleo hilo litakalotoka kesho, Rihanna ameelezea vitu vilivyobadilika kati yao.

“Unatuona tukitembea sehemu, tukiendesha sehemu, tukiwa studio, tukiwa club, na unadhani unajua. Lakini ni tofauti sasa. Hatuna majibizano kama ya zamani tena. Tunaongea kuhusu mambo. Tunathaminiana. Tunajua fika tunachokataka sasa na hatutaki tukipoteze.”