TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, November 28, 2014

UZALISHAJI WA MAFUTA KUENDELEA -OPEC 


Bei ya mafuta ulimwenguni imeendele kushuka kwa kiwango cha chini kwa kipindi cha miaka minne baada ya tamko la shirika la uzalishaji wa mafuta kwa wingi duniani OPEC ,kwamba halitaacha kuzalisha mafuta ili kuepusha kupanda kwa bei.
Kufuatia taarifa hiyo gharama ya mafuta ghafi imeshuka kwa dola elfu sabini na mbili za marekani,baada ya washirika kumi na mbili wa OPEC kuamua kuendelea na uzalishaji wa mafuta kwa mapipa elfu thelathini kwa siku.
Kwa muujibu wa mwandishi wa BBC wa masuala ya kiuchumi amesema kwamba muungano huo wa kikiritimba ili kudhibiti biashara ya mafuta hauna jipya,licha ya nchi kama Nigeria na Iran wangependa kusitisha uzalishaji ili bei ya mafuta ipande.
Saudi Arabia kwa kawaida hawako tayari kucheza mchezo wake wa asili wa kusawazisha soko la mafuta vinginevyo wazalishaji wote waamue kusitisha uzalishaji.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako.CHANZO:BBC

AJALI YAUA 11 TANGA 

 


Taswira kutoka eneo la Mkanyageni baada ya ajali hiyo mbaya iliyoua watu 11.

WATU 11 wanadaiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Mkanyageni mkoani Tanga baada ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ asubuhi hii.
Katika ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali.
Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN 
Chanzo:GPL

Thursday, November 27, 2014

Unamjua staa wa Soka Duniani ambaye amefunga ndoa hivi karibuni?

Wedding-Hands1 
Samuel Eto’o, moja kati ya wachezaji wakubwa wa  soka duniani  amefunga ndoa rasmi baada ya kuishi na mwanamke huyo ambaye walifunga ndoa ya kimila tangu mwaka 2007.
Eto’o amefunga ndoa na Tra Lou Georgette ambaye ana asili ya Ivory Coast na tayari wana watoto wanne.
Huenda kutokana na ustaa wake ungetarajia kuona tukio kubwa sana katika siku ya sherehe yao, lakini taarifa zinasema walifunga ndoa na kufanya sherehe ya kawaida sana katika mji wa Como, Italy siku ya jumatatu November 24.
Huenda katika sherehe hii cha thamani kubwa ikawa ni pete ya almasi ambayo Eto’o alimvisha mpenzi wake huyo Mwezi July, ambayo thamani yake ni Euro 500,000.
Samuel-Etoo-Georgette-600x600
samuel-etoo-wedding

Baada ya taarifa juu ya migogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki, unajua nini kimeamuliwa?

Margaret-Zziwa
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki EALA, Margaret Zziwa amesimamishwa kazi na Wabunge wa Bunge hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa amekuwa akiendeleza ubaguzi kwenye ajira, ufisadi na pia hana uongozi bora.
Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha BBC amekana madai hayo na kusema malumbano yanayoendelea ndani ya Bunge hilo yanatokana na siasa za chuki baina ya Wabunge na kusababisha Bunge hilo kutimiza majukumu yake.
Uchunguzi unafanyika ili kujua kama madai yaliyopelekea kumsimamisha yalikuwa na ukweli wowote.

Picha: Diamond Platnumz na Fally Ipupa kwa mara nyingine tena kwenye Mjengo wa BBA

.
Hii ni mara ya pili kwa msanii Diamond Platnumz kualikwa ndani ya jumba la BBA akiwa na mwanamuziki kutoka Congo, Fally Ipupa ambapo wameshiriki chakula cha mchana pamoja na washiriki waliobaki kwenye Jumba hilo, safari hii wasanii hao wameingia kwa ajili ya kuhamasisha ONE Campain ambayo inahusu kilimo, moja ya Project zilizowahi kufanywa na Kampeni hiyo ni ile nyimbo ya Cocoa na Chocolate ambayo wameshiriki pia mastaa wengine kibao kutoka Afrika.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
PBF_7282

U Heard ya Novemba 27 iko hapa, Steve Nyerere amjibu Linex kuhusiana na gari analodai kudhulumiwa

IMG_4502 
U Heard ya jana alisikika Linex ambaye alilalamika kudhulumiwa pesa kiasi cha milioni 11 na Nyamihela, ambaye alikutanishwa na muigizaji Steve Nyerere ambapo Linex alisema lengo lake ilikuwa ni kununua gari na Steve alimkutanisha na huyo jamaa kwa ajili ya kufanya biashara hiyo.
Leo amesikika Steve Nyerere ambapo amesema yeye aliwakutanisha Linex na Nyamihela baada ya Linex kumwambia kwamba anahitaji kununua gari, lakini baada ya hapo hakuwa na mawasiliano tena na Linex.
Steve amesema Linex alimtafuta baada ya kushindwana na Nyamihela na kumlalamikia Steve kwamba Nyamihela kamdhulumu pesa ambayo alimpatia ili amuuzie gari, japo Steve amesema kiasi cha pesa alichopatiwa Nyamihela ni milioni tatu na alimrudishia milioni moja kati ya pesa hizo.

Baada ya ishu ya Escrow, haya ni majibu mawili ya Waziri Mkuu Pinda ikiwemo kujiuzulu

question_mark_20166
Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.
Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?Mbowe.
Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…
Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Baada ya majibu hayo, Mbowe alipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa Waziri Mkuu; “…Pamoja na kwamba jambo hili litajitokeza baadaye katika mijadala ya leo, bado haiondoi ukweli kwamba una wajibu wa kulijibu swali langu. Naomba kwa heshima sana nikuulize tena kwa mara nyingine, taifa limepata fedheha kubwa sana kutokana na sakata hili, nchi nzima inasikiliza tatizo hili…“– Mbowe.
…Una heshima kama kiongozi wa Serikali lakini heshima ambayo itakuwa imethibitishwa zaidi kama utaamua kujiwajibisha mwenyewe ili kuweka heshima yako na heshima ya Serikali, je kwa mara nyingine huoni ingekuwa vema kama basi utujibu kama unafikiri bado zile fedha ni za umma kama hutaki ku-declare kujiuzulu katika hatua ya sasa?”– Mbowe.

Wednesday, November 26, 2014

Novemba 26 Bungeni Tz, ishu ya Escrow na agizo la Mahakama kuzuia mjadala wa Ripoti ya CAG

investigation
Wakati Kikao cha Bunge kikiendelea Dodoma leo, miongozo bado iliendelea kuombwa na baadhi ya Wabunge kuhusiana na suala ambalo limechukua siku kadhaa sasa kwamba Mahakama ilitoa agizo la kuzuia Bunge kujadili kuhusiana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali CAG, leo Novemba 26 Wabunge Suleiman Nchambi, Esther Bulaya, Tundu Lissu, Ole Sendeka na Joshua Nassari waliomba mwongozo kuhusiana na hilo.
Mbunge Nchambi alianza kwa kuuliza; “… Watanzania waelewe wazi sisi wabunge wa Chama cha Mapinduzi tunayo dhamira ya kujadili jambo hili Bungeni na kwa kuwa CHADEMA wameonyesha waziwazi kupitia mjumbe wao kuwa wanapinga suala hili, naomba mwongozo wako kwanini wakati tunajadili suala hili zito tusijadili pia suala hili zito la mjumbe wa CHADEMA kwenda kupinga kujadiliwa hoja hiyo hapa Bungeni…
Tundu Lissu akajibu hoja hiyo; “… Anaitwa Gabriel Mnyele, mkazi wa Mpanda ni mwana-CCM na wasiofahamu mimi nimesoma naye… Wakili wa Pan African Power Solutioms anafanya kazi kwenye kampuni moja ya uwakili na Mabere Marando, isipokuwa Wakili Mabere Marando hajahusika kwa namna yoyote ile na kesi iliyopelekwa Mahakamani...”
… Kilichotokea jana kwa Mahakama Kuu kutoa amri kuzuia mjadala Bungeni, ni jambo ambalo halijawahi kutokea tangu Mahakama kuu ya Tanganyika ianzishwe mwaka 1922…“– Tundu Lissu.
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu amejibu haya kwenye miongozo iliyoombwa na Wabunge hao; “… Taarifa ya kiti ambayo ndiyo taarifa rasmi bado Bunge halijapokea  barua yoyote ya kukataza mjadala wa Escrow kujadiliwa Bungeni. Hii miongozo mingine nitaijibu jioni.
Baada ya hapo Bunge liliahirishwa, na kupitia mtandao wa Twitter na Instagram, Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe ameandika kwamba Ripoti hiyo itasomwa leo jioni katika kikao cha Bunge hilo.
Instagram : “Ripoti tayari inasubiri kuwasilishwa“– @zittokabwe
Twitter : “Taarifa ya PAC kusomwa saa kumi na moja jioni Leo“– 
Zitto Ripoti II Zitto Ripoti

Malalamiko ya kukatwa muda wa hewani kwenye simu kwa huduma ambayo hujaitumia yamefika tena Bungeni

phone
Kumekuwa na malalamiko kwa watumiaji wengi wa simu za mkononi kutokana na kukatwa gharama za huduma ambazo hawajaziomba, ikiwemo kuunganishiwa miito ya simu na nyinginezo.
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza Bunge jana Novemba 25, ilihojiwa kuhusiana na suala hilo ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia alitolea majibu pamoja na suala la baadhi ya maeneo kuwa na matatizo ya mtandao.
… Katika makubaliano kati ya Serikali na kampuni mpya ya simu ya Viatel, ambayo imekubali kujenga minara na kupeleka mawasiliano katika maeneo yote ambayo hayana mawasailiano nchini, tumewapa orodha ya Vijiji elfu nne ambavyo havina mawasiliano kote Nchini au vina mawasiliano ni hafifu, na tumekubaliana tumewekeana mkataba kwamba maeneo yote hayo ikiwemo maeneo ya jimbo na Nyag’wale yatapata mawasiliano kabla ya mwezi Novemba mwaka huu…“– January Makamba.
“... Kuhusu miito ambayo inaingiziwa kwa wateja bila ridhaa yao, Serikali inatambua kwamba hili ni tatizo na sisi kama Wizara tumewaandikia barua na tumezungumza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ambayo ina wajibu wa kusimamia jambo hili kuhakikisha kwamba halifanyiki lakini na maslahi ya watumiaji wa simu yanalindwa, kwa hiyo tutaendelea kulifuatilia kuhakikisha kwamba Sheria inazingatiwa ili watumiaji wasidhulumiwe…”– January Makamba

Matokeo Champions League  

Papa ataka majadiliano na IS 


Baba mtakatifu Francis ametaka milango ya majadiliano na kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam iwe wazi ,ingawa hali ni mbaya na ya kutatiza katika maeneo wanako tekeleza mashambulio yao.
Papa Francis ameyasema hayo wakati akirejea mjini Rome, Italia,baada ya kulitembelea bunge la muungano wa jumuiya ya Ulaya lilifanyika katika mji wa Strasbourg, Papa pia amesisitiza makubaliano ya kimataifa kutokomeza ugaidi yalikuwa muhimu.na hakuna ulazima wa nchi kupigana na ugaidi ikiwa peke yake nguvu ya pamoja ni muhimu sana.
Akilihutubia bunge hilo ,alishusha mvua za lawama kwa muungano huo kuwa una hatia kwa kuweka sheria zilizokuwa kali na za kuumiza, hasa katika suala la wahamiaji na kuonya kuwa Mediterranean isifanywe kuwa kaburi la wahamiaji wanaosafiri kwa boti kutokea upande wa kaskazini mwa Africa.CHANZO:BBC

Deegbe aliacha kazi Benki na kujiajiri 


Makala ya Ndoto ya Afrika inaeleza habari kuhusu Wajasiriamali wanane kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika kila mmoja akieleza changamoto alizozipata alipokua akianza.Hivyo, katika mfululizo huu utapata fursa ya kujifunza katika kufikia ndoto, ndoto zao, na kama waliweza kuzisimamia.CHANZO:BBC
Mjasiriamali Deegbe,hutoa elimu kwa wengine ili kutimiza malengo yaoMbali na kutokua na elimu katika soko la viatu, Fred Deegbe, ambaye alikua mfanyakazi wa Benki,aliamua kubadili mwelekeo, aliungana na rafiki yake na kuanzisha kampuni yao iitwayo, Heel The World (HTW) Kampuni kubwa ya kutengeneza viatu yenye makazi yake, Accra Ghana, hiyo ilikua mwaka 2011, na mwaka mmoja baadae Deegbe aliacha kazi ya Benki na kuweka nguvu zake katika kazi yake hii mpya.
Mjasiriamali huyu mdogo anataka kututhibitishia kuwa viatu vyenye ubora vinaweza kutengenezwa nchini mwake.
Heel The World, ambayo ina waajiriwa saba wa kudumu, ina mtandao wake maalum kwa ajili ya shughuli zote za kutangaza soko na biashara yake hii inategemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa, katika shughuli za kutafuta masoko.
Ni jinsi gani unaweza kukuza biashara yako kushindana na Soko la bidhaa kutoka China?
Deegbe anasema: Bidhaa za China siku zote hazinitii hofu, na sababu kubwa, nimejiwekea kanuni mimi na ninaofanya nao kazi, niliweka kanuni hizo tangu mwanzo kuwa:
-Ushindani ni mzuri wakati wote lakini ni rahisi kumudu, hivyo ninahakikisha Kampuni yangu mara zote inatengeneza bidhaa nzuri ili ziweze kupendwa kwa namna tunavyotaka.
-Moja ya mikakati niliyonayo tangu awali ni kulenga soko linalofaa.
bidhaa kutoka Heel The World-Nimetumia muda wangu na kuwekeza sana kwenye aina ya bidhaa na soko la bidhaa zangu.
-Tangu mwanzo wa Biashara yangu niliweka akilini kuwa bidhaa ya Kampuni yangu itakuwa ya kutengeneza kwa mkono kuliko mashine.
-Kuwafanya wateja kuwa marafiki. Hili ni suala muhimu sana, kupitia biashara hii, nasaidia pia viwanda vya hapa nyumbani.
Kwa sababu Watu hasa vijana wachache wana ajira na kuwa wanakosa elimu ya ujasiriamali tuna kitengo cha uwezeshaji kinachowasaidia Watu wanaotamani kuwa Wajasiriamali na wengine wanaotaka kuwa wajasiriamali wabunifu.
Tumeanzisha Semina tukishirikisha shule za sekondari, Vyuo vikuu pia Taasisi mbalimbali kama UT Bank.
Deegbe anasema bidhaa yake inakidhi viwango vya kimataifatunaajiri na kushirikiana na Watu wabunifu ambao tunaamini kuwa wanaweza kushidana kwenye Soko la Dunia.
Tumekua tukitoa mafunzo kwa Watu wanaotaka kujifunza kuhusu utengenezaji wa Viatu na kazi nyingine za ngozi, na kuwafundisha namna ya kupata wateja kwa mitindo ya aina mbalimbali ya bidhaa.
Kampeni ya kuwa washindi katika bidhaa zilizotengenezwa Ghana, Afrika:tunathamini bidhaa zetu wenyewe na tumekuwa tukizifanyia kampeni kwa miaka mingi kuwa hizi ni bidhaa za nyumbani.
Shanga zetu zimetengenezwa kwa vipande vya chupa na shaba nyeupe, vyupa hivyo vinatoka kwenye chupa xa Guinness ambazo hutupwa, na shaba kutoka kweye vyuma kutoka kwenye magari mabovu ya zamani.
Kulenga Soko:tunalenga Soko la bidhaa zetu kupitia mitandao ya kijamii pia kwa kuonana ana kwa ana na Wateja, ni biashara ambayo imekua kwa haraka na kwa mara zote tumetaka kuwapa Wateja wetu huduma bora na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Baada ya kulifikia Soko la nyumbani na kufanikiwa kwenye hilo, sasa tunadhamiria kupeleka bidhaa kwenye Soko la nje, na nimefanikiwa.Hatua hii inahitaji Ubora wa hali ya juu.

Monday, November 24, 2014

Yanga SC yanasa straika aliyewaumbua Zamalek 

YANGA iko kwenye harakati za karibu sana za kumshawishi straika wa Uganda na AS Vital ya DR Congo, Yunus Sentamu atue Jangwani na wakimpata wana imani kwamba watakuwa wamemaliza kazi na tatizo sugu kwenye fowadi yao.
Mchezaji huyo mwenye miaka 20 ndiye mchezaji aliyefunga bao pekee la AS Vital lililoing'oa Zamalek ya Misri jijini Alexandria kwenye mechi ya kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwaacha Waarabu wengi midomo wazi.
Sentamu pia alifunga moja kati ya mabao mawili walipocheza na CS Sfaxien na kufuzu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika hivikaribuni. Ni miongoni mwa wachezaji wanaothaminiwa sana kwa sasa nchini Uganda kiasi cha kufanya kocha wa nchi hiyo, Sredejovic Milutin 'Micho' awasahau Hamis Kiiza wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba.
Yanga imeanza kupambana kimyakimya kumpata straika huyo hata kabla ya Kocha Marcio Maximo kusitisha mkataba wa Mbrazil Geilson Santos 'Jaja' na kutangaza kumleta kiungo mkabaji Emerson Rouqe wa Brazil.(P.T)
Straika huyo wa AS Vita yupo katika orodha ya CAF ya wachezaji wanaowania tuzo ya uchezaji bora Afrika kwa upande wa wachezaji wanaocheza ndani.
Habari za ndani ya kamati ya Usajili ya Yanga, zinasema Sentamu ni kati ya washambuliaji wanaotakiwa sana ili kuwa na straika mmoja mkali wa Afrika ambaye ni mtu wa kazi na mwenye uzoefu kuliko kujaribujaribu na kuingia hasara kila mara.
"Viongozi wanafanya kazi ya kutafuta straika wa maana mwenye uwezo wa kufunga ili kuonyesha kwamba bado Afrika ina wachezaji wazuri tofauti na fikra za kocha (Marcio Maximo)," alidokeza kiongozi huyo na kuongeza kwamba endapo huyo akitua huenda safari ikamkumba Hamis Kiiza au wakaachana na Emerson anayekuja nchini kesho Jumanne na Maximo.
Si Yanga pekee wanamtaka mchezaji huyo kwani CS Sfaxien ya Tunisia nao wameingia kwenye kinyang'anyiro lakini Yanga wamegundua kwamba mchezaji huyo ameambiwa kwamba Tanzania kuna fedha na anataka kucheza karibu na nyumbani.
Awali wakati ishu ya Sentamu inaanza, Yanga kulikuwa na malumbano kwenye kamati ya usajili kwani baadhi ya viongozi wanataka kusajili mchezaji kutoka nje ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na usumbufu wanaoupata kutoka kwao mara kwa mara na kwamba wengi wao wana viwango vinavyofanana na wachezaji wa Tanzania.
Bado Yanga ipo katika kuhakikisha pia inamnasa kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke ambaye amerudi Mbeya baada ya kutokamilika kwa mazungumzo ya kwanza jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Ili Sentamu asajiliwe katika kikosi cha Yanga, ni wazi klabu hiyo itabidi iachane na mmoja wa wachezaji wake wa kigeni kati ya Hamis Kiiza (Uganda), Haruna Niyonzima au Mbuyu Twite wote wa Rwanda lakini Kiiza ndiye yupo katika wakati mgumu kwani tayari Maximo anaonekana hamhitaji kikosini mwake.
Chanzo:Mwanaspoti

 

Kiemba aanza kupiga kazi Azam 


Amri Kiemba
AMRI Kiemba ataanza mazoezi kwenye kikosi chake kipya cha Azam FC leo Jumatatu, lakini ametoa la moyoni kwa kusema, yaliyomtokea Simba hayamuumizi kichwa na anayachukulia kama sehemu ya changamoto na sasa ametua kwa Bakhresa kila kitu amemwachia Mungu ili aamue hatma yake.
Lakini akaenda mbali na kuwaambia mabosi wake wa sasa, yeye hajui kuchagua, wampe jezi yenye namba yoyote ile iliyopo au watakayoona inamfaa ataivaa.
Kiemba amekwenda Azam kwa mkopo na dau la Sh10 milioni akitokea Simba.(P.T)
Mchezaji huyo ameliambia Mwanaspoti kuwa: "Tukijaaliwa kesho (leo) nitaanza mazoezi rasmi. Binafsi nimejiandaa vizuri lakini siwezi kutoa ahadi nyingi kila kitu nimemwachia Mungu aamue."
"Unajua wakati mwingine binadamu tunakosea, unasema nitafanya hiki na hiki lakini utambue kuwa yote yanapangwa na Mungu kikubwa naomba ushirikiano,"alisema Kiemba ambaye amebakiza miezi sita Simba na amekwenda kwa mkopo Azam kwa miezi sita.
"Unaweza kukuta, hata hicho kilichonitokea Simba, ilipangwa tu ili kifanyike hiki kilichofanyika."
Akizungumzia sakata lake Simba, Kiemba alisema:
"Yote nayachukulia kawaida tu kuwa ni sehemu ya changamoto za maisha, ndivyo ilivyokuwa imepangwa, sitaki kuyazungumzia sana kwa undani."
Hadi kutua kikosini hapo, Kiemba alikuwa amesimamishwa na uongozi wa Simba kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu. Alisimamishwa pamoja na wachezaji wenzake, Shaaban Kisiga 'Marlone' na Haroun Chanongo.
Chanzo:Mwanaspoti

Jeshi la Kenya kuwasaka wauaji Mandera mpakani mwa Somalia

Bus lililotekwa na wapiganaji wa Al shabab kabla ya kuwaua abiria 28 wasiokuwa waislamu,Mandera mpakani mwa Somalia
Bus lililotekwa na wapiganaji wa Al shabab kabla ya kuwaua abiria 28 wasiokuwa waislamu,Mandera mpakani mwa Somalia
Na Martha Saranga Amini
Mshauri wa juu wa raisi Uhuru Kenyata Abdikadir Mohammed ametoa wito kwa wakenya wote wa imani zote kuungana pamoja dhidi ya wahalifu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia mauaji ya alfajiri ya jana kutekelezwa na wapiganaji wa kiislamu kutoka somalia ambao waliteka basi moja na kuwaua abiria ambao hawakuwa waislamu.(P.T)
Tayari maafisa wa jeshi la Kenya KDF wamewasili Mandera eneo la mpakani mwa somalia kuwasaka waliotekeleza mauaji hayo na kuhakikisha ulinzi baada ya abiria 28 kuuawa mapema jana.
Kundi la Al-Shabab limesema shambulizi hilo lililenga kulipa kisasi kufuatia mauaji ya waislamu ambayo kundi hilo limedai kutekelezwa na majeshi ya kenya katika mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali ya kenya imesema imeanza kuwatambua wahalifu hao na itahakikisha inafikisha mbele ya sheria.
Waziri wa mambo ya ndani Joseph Olellenku amesema kuwa kambi iliyokuwa inamilikiwa na wapiganaji hao huko mandera imeshambuliwa na jeshi la kenya.
Chanzo:RFI

MABAKI YA MH 17 KUREJESHWA UHOLANZI


Mabaki ya ndege ya MH 17
Shirika la ulinzi la ulaya,limearifu kwamba mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Malaysia yaliyookotwa huko mashariki mwa Ukraine hatimaye yanarejeshwa Uholanzi.
Mkuu wa shirika hilo Michael Bociurkiw ameiambia BBC mabaki yaliyokusanywa na timu ya uchunguzi kutoka Ujerumani, ambao wamekwisha ingia katika ardhi inayo dhibitiwa na serikali ya Ukraine na mabaki hayo yatasafirishwa kwa ndege kutoka katika mji wa Kharkiv.BBC
Timu hiyo ya watafiti wa Kijerumani inaongoza timu ya watafiti wa kimataifa kufuatia ajali hiyo ya ndege iliyotokea mwezi July kutokana na maombi maalumu ya serikali ya Ukraine.
Ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa Amsterdam na idadi kubwa kati ya abiria 298 ya waathirika wa tukio hilo ni Wajerumani .
Juhudi za uchunguzi huo zinakwamishwa na mgogoro unaoendelea huko Mashariki mwa Ukraine kati ya Urusi na nchi hiyo mgogoro ambao unaungwa mkono na askari wa majeshi ya nchi hiyo.

 

UCHAGUZI WA RAIS TUNISIA

Tunisians queue outside a polling station in La Marsa, Tunisia, Sunday Oct. 26, 2014.  (photo credit: AP/Hassene Dridi)
Raia wa Tunisia katika zoezi la upigaji kura
Wananchi wa Tunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu kutokea vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011.
Mapinduzi hayo yalisababisha vuguvugu hilo la mabadiliko kutabakaa katika nchi nyingine za Kiarabu.
Miongoni mwa wagombea katika kinyang'anyoro hicho ni mwanasiasa mkongwe Beji Essabsi, aliyewahi kushika nafasi muhimu wakati wa utawala kabla ya kutokea mapinduzi.
Bwana Beji Caid Essabsi anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo ameahidi kurejeha kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.
Mpinzani wake wa karibu ni Rais wa mpito wa sasa Moncef Marzouki ambaye amejenga jina lake kama mpigania haki za binadamu na kama msimamizi wa moyo wa mapinduzi na anayetamani mabadiliko. Waziri wa Ulinzi wa Tunia Ghazi Jeribi amesema ana matumaini nchi itasonga mbele kidemocrasia.BBC

MBRAZIL EMERSON KUZIBA PENGO LILILOACHWA NA JAJA YANGA 


Geilson Santana Santos ‘Jaja’.
KLABU ya Yanga inatarajia kumsajili kiungo mkabaji mpya kutoka Brazil Emerson De Oliveira Neves Rouqe kuziba nafasi hiyo iliyoachwa na mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’ aliyekatisha mkataba wake na klabu hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Jaja akishangilia bao lake alilofunga kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Yanga na Thika United ya Kenya.
Taarifa kutoka Mtandao wa klabu hiyo umesema Emerson De Oliveira Neves Rouqe '24' atawasili nchini Jumanne mchana kwa ajili ya majaribio na endapo atafuzu moja kwa moja atajiunga na kikosi cha mabingwa hao mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara.GPL(P.T)
Kabla ya kuamua kuja Tanzania, Emerson alikuwa akiichezea timu ya Bonsucesso FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Brazil, msimu uliopita alikuwa akicheza soka la kulipwa nchini Poland katika timu ya Piotrkow Trybunalski FC iliyopo Ligi Daraja la pili nchini humo.
Jaja mfungaji wa mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC, kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Septemba 14 alisaini mkataba wa miaka miwili na Yanga akitokea timu ya Itabaina FC na ameichezea timu hiyo kwa miezi minne na kufunga mabao matano katika mechi zote alizoichezea timu hiyo zikiwemo za mashindano na kifariki.
Jaja aliifungia Yanga bao la kwanza ilipocheza mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu kwenye uwanja wa Gombani Pemba dhidi ya Chipukizi na kisha alifunga bao lake la pili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Thika United ya Kenya lakini mashabiki na baadhi ya viongozi wa Yanga hawakuwa wakifuraishwa na kiwango chake.
Mshambuliaji huyo alionekana kuwapa matumaini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga mabao mawili safi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya bingwa mtetezi Azam FC huku bao la pili akilifunga kwa ustadi mkubwa na kuwaziba mdomo mashabiki waliokuwa wakimdhihaki baada ya hapo mechi za Ligi Kuu zilianza na ukame wa mabao ukatawala sana kwake ikiwa ni pamoja na kukosa mkwaju wa penalti katika mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Staa huyo aliibuka tena katika mechi ya nne ya Ligi dhidi ya Stand United ya Shinyanga kwa kufunga bao lake la kwanza katika ligi na la mwisho baada ya hapo mashabiki hawakuwa wakifurahia anapopewa nafasi uwanjani na kocha raia mwenzake wa Brazili, Marcio Maximo.

Friday, November 21, 2014

Pale ambapo Wabunge wanaamua kuruka ukuta kuingia Mjengoni

PIC.24.-FRACAS-AT-THE-NATIONAL-ASSEMBLY-IN-ABUJA11-600x324 
Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge ….!!
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.
PIC.25.-FRACAS-AT-THE-NATIONAL-ASSEMBLY-IN-ABUJA1-600x390
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.
Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo.

Ulishawahi kufikiria Bus linaweza kutumia kinyesi cha Binadamu kutembea?stori iko hapa

bio bus
Unaweza usiamini ama kufikiria kuwa kinyesi cha binadamu kina thamani kiasi cha kutumika kama mbadala wa mafuta katika gari lakini unaambiwa Basi la kwanza Uingereza linalotumia nishati hiyo limeingia barabarani.
Basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria40 ‘Bio bus’ linatumia gesi itokanayo na kinyesi cha binadamu na takataka nyingine zinazozalishwa kwenye kiwanda kilichopo kusini Magharibi mwa nchi hiyo kuweza kutembea.
Katika Gazeti la UHURU limeandika kuwa tanki moja la gesi hiyo lililozalishwa kutokana na kinyesi cha watu inatosha kuendesha gari hilo kwa umbali wa kilomita305.
Basi hilo rafiki wa mazingira ambalo watengenezaji wake wanasema litaboresha hewa, linaendeshwa kwa nishati ambayo ni ya kawaida,kinyesi cha binadamu ambacho ni miongoni mwa majitaka mengine.
Watengenezaji hao walisema gari hilo la aina yake litaboresha hali ya hewa na kuthibitisha kumbe kuna thamani katika kinye si cha binadamu.
gesiiii
Zipo taarifa kuwa siku si nyingi kinyesi cha binadamu kitaanza pia kuzalisha nishati kwa ajili ya simu za mkononi baada ya wataalam kutoka chuo kikuu cha East Anglia cha nchini humo.
Gesi hiyo inazalishwa katika mtambo wa majitaka wa Wessex Water,unaendeshwa na kampuni ya nishati ya Geneco na ugunduzi ,huo unaweza kuzalisha nishati kwa ajili ya teknolojia inayobebeka kama vile simu za mkononi na hata kompyuta mpakato.
Watetezi wa nishati hiyo wanasema basi hilo ambalo linatarajia kusafirisha abiria 10,000 kwa mwezi,linaonyesha thamani ya takataka na linaonyesha mustakabali mwema katika sekta ya usafiri wa umma.

Rais kutoa msamaha kwa wafungwa Waandishi wa Habari

pingu
Waandishi wa habari watatu walioshtakiwa kwa kuandika habari za kichochezi huenda wakaachiwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais.
Waandishi wa Habari hao Peter Greste raia wa Australia, Mohammed Fahmy mwenye asili ya Canada na Baher Mohammed wanashikiliwa Misri ambako walihukumiwa kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kukisaidia chama cha Muslim Brotherhood na kueneza habari za kupendelea upande wa Kikundi hicho.
Mohammed Fahmy, Peter Greste, Baher Mohamed
Rais wa Misri, Abdi Fatah El Sisi amesema msamaha huo utatolewa kama hakutakuwa na athari yoyote kwa nchi hiyo kiusalama.
Waandishi wawili kati yao walihukumiwa kifungo cha miaka 10, mmoja wao akihukumiwa kifungo cha miaka 7.

Thursday, November 20, 2014

Baada ya Shy-Rose Bhanji kudaiwa kumpiga mbunge mwenzake, hiki kimesemwa bungeni

1 (1) 
Kumekuwa na taarifa kuhusu kuwepo migogoro mbalimbali inayohusisha Wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo Mbunge Shy-Rose Bhanji amehusishwa sana kwenye vichwa vya habari.
Kwenye kikao cha Bunge November 20 2014 Dodoma Hatibu ambae ni mbunge wa Zanzibar aliuliza >>> “… Sisi wabunge wa bunge hili ndiyo wapiga kura wa kuwachagua wawakilishi wetu wa kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki, kumekuwa na taarifa za kulipaka Taifa hili matope kulitia aibu kutokana na  baadhi ya wawakilishi wetu, Wabunge wetu wa Afrika Mashariki kutokana na matendo wanayoyafanya kule..
…Ni lini hasa kinachoendelea pale na hatua gani zilizochukuliwa kuhusu ukosefu wa nidhamu uliojitokeza kwa mbunge Shyrose Banji wazi wazi na bili hali hakuna taarifa yoyote, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo wako…”– Hatibu.
Baada ya swali waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akawasha kipaza sauti na kutoa haya majibu “…Naomba nitoe taarifa kwamba kinachotokea katika Bunge la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa  spika mwenyewe, hilo ndiyo chanzo cha matatizo mengi, kwa hiyo  wabunge  wa Bunge la  Afrika Mashariki wamegawika kataka makundi mawili, kuna kundi linalotaka Spika lazma aondolewe, na wengine wanadai wanamtetea abaki…
EA..
Sasa katika kundi ambalo wanataka  abaki imeonekana Tanzania ndio kikwazo, kwa sababu ili upate uamuzi ndani la Bunge la Afrika Mashariki  katika suala lolote lazima upate akidi inayotosheleza kutoka  kila nchi, sasa wabunge wa Tanzania ambao mwanzoni waliunga mkono hoja ya kumuondoa yule Spika wamefuta hilo na wamekubaliana aendelee kwa hiyo imeleta chuku kiasi Fulani…“– Sitta.
 “…Katika tukio ambalo limetokea juzi na nasema hivi kwa sababu  Naibu Waziri wangu yuko kule kwa hiyo ni jambo halisi, kilichotokea sio kama kinavyoelezwa Mheshimiwa Shyrose Banji ambaye anahesabika ni mfuasi mkubwa wa Yule Spika kiasi kwamba wenzie wanamuona kama kibaraka vile, alikuwa anapita katikati ya Wabunge wengine kuwahi usafiri kwa bahati mbaya akamgonga Mheshimiwa Ndelakindo Kessy, Mheshimiwa Ndelakindo akahamaki na kwa kusaidiwa na  baadhi ya Wabunge  wengine wa Uganda akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa kwa madai kwamba amefanyiwa makosa ya jinai wanaita ‘assaults’…“– Sitta.
“>…Ikabidi aitwe ‘Sergeant at Arms’ wa Bunge la EALA ambaye alikwishaanza jitihada za kulifanya jambo lile liishie ndani ya Bunge na katika jitihada hizo alifika mbali kidogo akawezesha Wabunge wetu hao wawili waweze kusikilizana na ninavyotoa taarifa hivi sasa ni kwamba jana suala hili limekwisha na haliendelezwi na Polisi tena…
“– Sitta.
Hivi ndivyo Waziri Sitta alimalizia kujibu suala hilo; “…Sasa yale mengine yaliyosema kwamba alifanya mambo ya hovyo Mheshimiwa yule tena kama miezi miwili iliyopita, bado yako mikononi mwa tume ya Bunge la Afrika Mashariki hadi hapo watakapolishughulikia hatuwezi kufanya kitu chochote, na tukishapata taarifa ya tume ya Bunge la Afrika Mashariki basi mimi nitatoa taarifa kwa Mheshimiwa Spika ili sasa sisi kwa wote kama jimbo la uchaguzi La Wabunge hao tuone ukweli ni upi na tujue hatua ya kuchukua..”– Sitta.

Na hii imfikie kila shabiki wa Manchester United!

Manchester-United
Club hii imeripotiwa kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Victor Valdez baada ya kufanya nae mazoezi kwa muda wa karibu mwezi mzima.
Valdez ambaye aliihama Barcelona baada ya mkataba wake kuisha msimu uliopita alikuwa karibu kujiunga na Liverpool lakini jeraha baya la goti alilopata katikati ya msimu uliopita  lilizuia usajili wake kwenda Anfield.
Victor Valdez yuko mbioni kukamilisha usajili wake na Manchester United .
Victor Valdez yuko mbioni kukamilisha usajili wake na Manchester United .
Katika kipindi hiki kocha wa Manchester United Louis Van Gaal alimpa kipa huyo nafasi ya kufanya mazoezi na United hali ambayo ilimuweka karibu na usajili ndani ya klabu hiyo .
Usajili wa Valdez ulithibitishwa na kipa namba moja wa United David De Gea ambaye alizungumza na waandishi wa habari na kuwathibitishia kuwa United imemsajili Valdez.
De Gea aliwaambia waandishi kuwa United haijamsajili Valdez kama mbadala wake.
De Gea aliwaambia waandishi kuwa United haijamsajili Valdez kama mbadala wake.

Hawa ni wanawake pekee waliopo kwenye listi ya watu Matajiri zaidi Afrika.

Isabela dos Santos
Isabela dos Santos
Unajua kwamba kwenye listi ya matajiri 50 Afrika kuna wanawake wawili wanaoingia kwenye listi ya matajiri hao?
Jarida la Forbes lilitoa listi ya matajiri hao ambapo Aliko Dangote mfanyabiashara kutoka Nigeria anaongoza kwenye listi hiyo.
Wanawake hao wawili ni Isabel dos Santos ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos amewekeza kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kampuni za mitandao ya simu za mkononi ni mwanamke tajiri zaidi ambaye ameingia kwenye listi hiyo, pamoja na Folorunsho Alakija ambaye ni mfanyabiashara na mwanamitindo wa Nigeria.
Folorunsho Alakija
Folorunsho Alakija

Umesikia taarifa ya ajali mbaya iliyotokea Mahakamani?

bigstock-police-line-22737392-750x375
Mtoto wa mwanamke mmoja amefariki wakati mama yake alikuwa anapandishwa kizimbani baada ya kukamatwa akiuza bidhaa barabarani kinyume na Sheria.
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili amegongwa na gari na kufa katika Makao Makuu ya Halmashauri ya jiji la Kampala KCCA, ambapo mama yake Madina Namakula alifikishwa Mahakamani Kampala, Uganda, kusomewa shitaka lake ambapo wakiwa Mahakamani hapo ndipo mtoto huyo alipopata ajali hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa Polisi wamesababisha kifo cha mtoto huyo.
Mtoto huyo amezikwa leo Kampala, Uganda.

Mapya kuhusu huduma za chakula Mgahawa wa Bunge

Mjengo 
…Naomba mwongozo wako kwamba kinachoendelea katika viwanja hivi vya Bunge pale Kantini,  kuna mabadiliko makubwa sana yamefanyika kwa watoa huduma kiasi kwamba kwanza hata huduma zao na kauli zao kwa wateja wao sisi wabunge sio nzuri..“, Hiyo ilikuwa kauli ya mwongozo wa Mbunge Martha Mlacha alipopewa nafasi kutoa mwongozo wake katika kikao cha Bunge leo Dodoma.
…Lakini kitu ambacho.. ninachokuomba mwongozo  kwamba Bunge hili.. hapa mahali hapa.. ndiyo chimbuko na kisima cha watetea haki za Watanzania wote, wakiwemo vibarua, wafanyakazi na watu wengine na kwamba kama kuna kampuni inachukua ama kufanya biashara kwenye eneo fulani ikakuta wafanyakazi maeneo yale, inabidi wafanyakazi wa eneo lile wachukuliwe na kampuni ile inayokuja pale…”– Mlata.
…Kumetokea sintofahamu naomba mwongozo wako, hivi sasa vijana thelathini waliokuwa wanafanya kazi katika kwenye kantini ile wanarandaranda mitaani wanakutana na sisi wabunge wakituomba tuwasaidie hata hela ya kula, naomba mwongozo wako ni nini kimetokea?..”– Mlata.
Akijibu mwongozo huo Naibu Spika; “… Hili ambalo ameliongea Mheshimiwa Mlatha ni jambo la ndani.. ni jambo la kwetu sisi wenyewe, niwahakikishieni waheshimiwa Wabunge kwa kifupi sana kwamba jambo hili liko mikono salama ya tume ya huduma za Bunge, mabadiliko hayo ni kwa nia njema watumishi waliokuwa pale wengi wao wamekuwa deployed tayari maeneo mengine ya kazi..“– Ndugai.
…Nawapa majibu ya uhakika, zaidi ya robo tatu wameshakuwa deployed tayari na tulikuwa na kamati ya tume jana wala sio juzi na tumelizungumzia jambo hili , wako vijana wachache ambao bado hawajachukuliwa, na hao wachache watachukuliwa watapangwa katika maeneo mengine ya shughuli. Kwa hiyo liko mikono salama kabisa…“– Ndugai.

Mwingine aliyehukumiwa kwa kosa la kuzamisha Meli kwa uzembe

Prisondoor460
Wiki moja baada ya Nahodha wa Meli iliyozama kuhukumiwa kifungo cha miaka 36, na wenzake 13 hukumu ya miaka 30 kila mmoja, kumbe kuna watu wengine ambao wana hatia kutokana na kupatikana na hatia ya uzembe uliopelekea meli kuzama na kuua watu 300.
South Korea Sinking Ship
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayomiliki Meli hiyo ya Mv. Sewol, Kim Han-Sik,  amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuruhusu meli hiyo kupakia mizigo kuzidi uwezo wake.
Kim Han-Sik
Kim Han-Sik
Mbali na mkurugenzi huyo, wengine 9 wamehukumiwa miaka 6 kila mmoja na mmoja kati ya watuhumiwa ameachiwa huru kwa kukutwa bila hatia.