TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 30, 2014

ISRAEL YASEMA HAMAS ILIWAUWA VIJANA WAKE

Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.
Benjamini Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu
Israel imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.
Katika kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema yamefanywa na wanyama.
Netanyahu amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.
Hamas imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah
Mwandishi wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege za Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .
Kulikuwa na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha mawaziri cha usalama .
Mji wa Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo zimekuwa zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.
vifo vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.
CHANZO BBC

HOFU KUWA SYRIA INA SILAHA ZA KEMIKALI 

Syria imeshindwa kutimiza makataa ya mwisho yaliyotolewa na jamii ya kimataifa kuitaka iharibu silaha zake za kemikali hivi leo.
Rais Bashar al Assad alikamilisha zoezi la kutoa silaha zilizotambuliwa rasmi juma lililopita, hii ikiwa ni miezi kadhaa baada ya siku ya mwisho iliowekwa na jamii ya kimataifa.
Bado kuna wasiwasi kwamba huenda Syria bado imehodhi zana zaidi za kinuklya.
Silaha hizo zitahariobiwa katika meli ya Marekani ya MV cape Ray katika eneo lisilojulikana ndani ya bahari ya Mediterenean.
Shughuli hiyo itachukua takriban siku sitini lakini bado kuna wasiwasi kuhusu kuwepo kwa silaha za kemikali ndani ya Syria.
Mwishoni mwa juma, usalama zaidi uliwekwa katika bandari ya Gioia Tauro nchini italy.
Vilevile vizuizi vya ukaguzi vimewekwa katika bandari hiyo.Kati ya tarehe moja na tatu mwezi July,kilomita moja ya eneo ambalo ndege hazifai kuruka litawekwa.
Makasha yaliojaa vifaa vya kutengeza silaha hatari duniani ndani ya meli moja ya Denmark Ark Futura yatafunguliwa na vifaa hivyo kuingizwa katika meli ya MV Cape Ray.
Lakini shirika la kukabiliana na silaha za kemikali duniani limekiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba rais Bashar Al Asaad bado anaficha vituo vya siri vya kemikali,na kuna wasiwasi zaidi kuhusu madai ya utumizi wa gesi ya klorine na wataalam wa kijeshi wameonya kuwa makundi yenye itikadi kali nchini Syria yanamiliki silaha za sumu.CHANZO BBC,(A.I).

HIZI NDIZO ATHARI ZA KUTAZAMA TV


Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia
mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.
"Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo.
"Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo."
Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa kutumia tarakilishi na muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao walioshiriki, ambao walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao asilimia 67 walikuwa wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2. mwishowe, vifo 97 viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na mishipa na moyo, 46 kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na sababu nyinginezo.
Utafiti huo ulionyesha hatari kubwa ya kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa washiriki walioripoti kutazama runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku ikilinganishwa na wale waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.

Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu
Hatari hii mara mbili zaidi ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa ya vigezo vingine vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao hawakupata ushirikiano kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia tarakilishi au kuendesha gari na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema kutokana na sababu zote.
Pia waliongezea kuwa utafiti zaidi unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni athari zipi zilizopo kati ya kutumia tarakilishi na kuendesha gari katika viwango vya vifo, na pia kutathmini taratibu za kibayolojia zinazoweza kueleza uhusiano huo.
"Watu wanapoendelea kuzeeka, tabia za kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama runinga, na hili litasababisha mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuzeeka," Martinez-Gonzalez alisema.
"Matokeo ya utafiti wetu yanapendekeza watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya viungo, waache kukaa tu kwa muda mrefu, na wapunguze kutazama televisheni kwa zaidi ya saa mbili kila siku."
BBC

POLISI WAWILI WAUAWA KARIBU NA IKULU YA MISRI


Maafisa wawili wa polisi waliuawa wakitegua mabomu yaliyokuwa yametegwa karibu na ikulu ya rais
Mabomu mawili yamelipuka karibu na Ikulu ya Rais mjini Cairo, nchini Misri na kuwaua maafisa
wawili wa polisi.
Bomu la kwanza lilimuua afisa wa polisi na kuwajeruhi wengine watatu.
Bomu la pili lililipuka maafisa wa polisi walipokuwa wanajaribu kulitegua na kumuua polisi mwingine.
Wapiganaji wa kiisilamu wanadaiwa kutega mabomu hayo katika eneo hilo wiki jana.
Shambulizi hili limetokea katika siku ya maadhimisho ya maandamano ambayo yalisababisha jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Muhammad Morsi.
Mkuu wa ulinzi wa mjini Cairo ameambia BBC kuwa mkuu wa idara ya kutegua mabomu Generali, Alaa Abdel Zaher, alikuwa miongoni mwa wale waliojeruhiwa.
Wakati huo huo, naibu mkuu wa ulinzi amesema kuwa wataalamu wa kutegua mabomu walitegua mabomu mengine mawili yaliyopatikana nje ya ikulu ya Rais.
Abdul Fattah al-Sisi.

Hata hivyo ratiba ya Rais Abdul Fattah al-Sisi haikubadilishwa kutokana na mashambulizi hayo.
Mashambulizi ya mara kwa mara yamesababisha vifo vya mamia ya watu wakiwemo maafisa wa usalama tangu Morsi kuondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Wapiganaji wa kiisilamu wameongeza mashambulizi katika kujibu operesheni ya kijeshi dhidi ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, ambapo zaidi ya watu 1,400 wameuawa na wengine 16,000 kujeruhiwa.
BBC

RAIS WA URUGUAY AWATUKANA MAOFISA WA FIFA


Rais Jose Mujica amesema maafisa wa FIFA wamuadhibu Suarez kwa unyonge wake
Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa''
au "a bunch of old sons of bitches".
Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.
Mchezaji huyo aliitaja adhabu hiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.
Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.
Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.
Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya muondoano.
Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa alitaka kujirekebisha.
Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.
Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.
BBC

RAISI KIKWETE KUFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII 

index

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kimataifa ya utalii yanayojulikana kama Swahili Tuorism Expo yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba mwaka huu.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Razaro Nyalandu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam alipozindua rasmi tovuti ya taarifa za maonyesho hayo inayojulikana kama Swahili Tourism Expo (S!TE).
 
Maonyesho hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
 
Waziri Nyalandu alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kupanua wigo wa sekta ya utalii ambapo nchi zote za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Sudan zinatarajiwa kushiriki lakini pia mataifa mbalimbali yataalikwa.
 
Alisema tayari 50% ya nafasi za maonyesho zimeshachukuliwa na kwamba mialiko kwa mataifa mbalimbali imeshatumwa ambapo ofisi yake itafuatilia kwa karibu mialiko hiyo na kuhakikisha nchi nyingi kwa kadri inavyowezekana zinashiriki.
 
“Kutokana na ukubwa wa tukio hili Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi lakini pamoja na TTB kupewa jukumu la kuratibu pia ofisi yangu itachukua jukumu la kipekee  kufuatilia mialiko iliyotumwa nchi mbalimbali kuhakikisha zinashiriki,” alisema Waziri.
 
Aliongeza kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuongeza biashara ya kitalii nchini ambapo baada ya hapo Tanzania inatarajiwa kupokea watalii zaidi ya milioni 2 kwani maonyesho hayo yataitangaza nchi husika kwa kiasi kikubwa.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Balozi Charles Sanga alisema maonyesho hayo yatakuwa chachu ya kukuza utalii wa ndani na kuwajengea tabia watanzania kutembelea vivutio tulivyonavyo.
 
Alisema tumekuwa tukipokea watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kujionea utajiri wa maliasili tulizonazo lakini idadi ya watalii wazalendo imekuwa ndogo sana ambapo pamoja na mambo mengine muamko na taarifa za vivutio hivi zimekuwa haziwafikii na hivyo maonesho hayo yatakuwa chachu ya kuongeza idadi ya watalii wa ndani.
 
“Maonyesho kama haya ni maarufu katika nchi za wenzetu na yamekuwa yanawasaidia sana katika kukuza sekta zao za utalii hivyo nasi tunaanza na litakuwa linafanyika kila mwaka,”
 
“Kupitia maonyesho haya sekta na biashara nyingi za kitalii zitapanuka lakini kubwa zaidi tunaamini baada ya hapo watanzania wengi watakuwa na taarifa za kutosha kuhusu maliasili tulizonazo na watahamasika na hatimaye kuongeza idadi ya watalii wa ndani ya nchi,” alisema Balozi Sanga.
 
Wizara ya Maliasili kupitia TTB imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa na mchango wa kipekee katika pato la taifa ambapo pamoja na maonyesho hayo pia ina mikataba mbalimbali ya matangazo na nchi mbalimbali duniani katika kuhakikisha taarifa za vivutio vyetu zinawafikia watu wengi zaidi.(A.I)

WANARIADHA WAAHIDI KUILETEA HESHIMA TANZANIA

RTE1
RTE3
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand.(A.I).

WAZIRI WA NCHI AZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI 

???????????????????????????????
???????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dr. Eng. Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Julius Ningu (wa kwanza kulia) wakiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani Mr.  Hans Koeppel kwa ajili ya Mazungumzo jijini Dar es Salaam.CHANZO BBC,(A.I).

 

MARCIO MAXIMO AANZA KAZI YANGA

10259844_762529373768464_2298164036768070188_n
Wachezaji wa Yanga sasa kuanza mazoezi chini ya Maximo
KOCHA mpya wa Yanga sc, Mbrazil Marcio Maximo ameanza kazi leo kwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo .
Mkutano huo umefanyika makao makuu ya klabu ya Yanga, makutano ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es salaam.
Maximo alipata nafasi ya kuwaeleza mipango yake ya kazi na kuwataka wachezaji waelewe umuhimu wao katika kujenga mafanikio ya Yanga.
Kocha huyo aliyewahi kufanya kazi nchini kwa kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars, baada ya kukutana na wachezaji leo hii, sasa yuko tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza mwezi agosti mwaka huu.

Sunday, June 29, 2014

LIBYA:MSHUKIWA WA SHAMBULIZI MAHAKAMANI

Ahmed Abu Khatallah
Mmoja ya washukiwa wakuu wa shambulizi lililomuua balozi wa Marekani nchini Libya miaka miwili iliopita amefika mbele ya jaji katika mahakama moja ya kijimbo mjini Washington, Marekani.
Ahmed Abu Khatallah alikana mashtaka yote matatu ya ugaidi dhidi yake.
Mashtaka hayo yalisomwa kwake kupitia mkalimani.
Anashtakiwa kwa mauaji ya balozi Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine watatu wa Marekani katika shambulizi la ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.
Mshukiwa huyo alikamatwa na vikosi maalum na kusafrishwa kutoka Libya katika meli ya wanamaji wa Marekani.CHANZO BBC,(A.I).

 

VIJIJI VYASHAMBULIWA TENA NIGERIA

Shule ya Chibok ambapo wanafunzi wasichana walitekwa nyara Aprili
Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia vijiji kadha na makanisa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi wa huko walisema kuwa watu wengi wameuwawa na nyumba nyingi zimeteketezwa.
Mashambulio yamefanywa karibu na mji wa Chibok, ambako wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa nyara mwezi wa Aprili.
Mwandishi wa BBC Nigeria anasema katika kijiji kimoja cha Kautikari, wanamgambo wa kijiji walizidiwa nguvu walipojaribu kulinda kanisa.
Anasema jeshi halikuweza kufika katika vijiji hivyo vilioko mbali.CHANZO BBC,(A.I

ISRAEL YATEKELEZA MASHAMBULIZI GHAZA

Wanajeshi wa Israel
Israel inasema kuwa imetekeleza mashambulizi ya roketi katika eneo la Ghaza siku ya jumamosi ili kujibu shambulizi jengine la roketi kutoka kwa wapiganaji wa kipalestina.

Jeshi la Israel limesema kuwa limeshambulia kile ilichokitaja kama maeneo tisa ya ugaidi.

Awali roketi mbili zilipiga kiwanda kimoja katika mji wa Sderot nchini Israel na kukichoma mbali na kuwajeruhi watu wanne.

Mashambulizi hayo yanajiri wakati ambapo kuna wasiwasi huku wanajeshi wa Israel wakiendelea kuwasaka vijana watatu ambao walitoweka na wanaaminika kutekwanyara katika eneo la West Bank.
Israel inasema kuwa walitekwanyara na watu wa kundi la Hamas ambalo linadhbiti eneo la Ghaza.CHANZO BBC,(A.I).

FACEBOOK YAPINGA KESI KUHUSU DATA


Facebook inasema mahakama ilikiuka katiba
Mtandano wa kijamii wa Facebook umekata rufaa dhidi ya amri ya mahakama ambapo
ilitakiwa kuwasilisha data ya watu 400 waliouhusika na visa vya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Mtandao huo wa kijamii ulisema kuwa ombi hilo la mahakama lilihusisha idadi kubwa ya majina ya watu kuwahi kuombwa na shirika la kiserikali kutoka kwa mtandao huo
Picha na ujumbe wa faragha pamoja na taarifa nyinginezo kuhusu watu hao ziliwasilishwa kwenye mahakama mwaka jana, lakini mahakama ilitoa tangazo hili wiki hii.
Uamuzi wa mahakama ulitaja Facebook kama mhifadhi wa data za kidijitali.
Jaji wa kesi hiyo alisema maana ya kuwa mhifadhi ni kwamba Facebook inapaswa kutii agizo la mahakama la kutaka kufanysa msako.
Kesi halisi ilichunguza visa vya watu kadhaa kudai malipo kutoka kwa mfuko wa taifa kwa watu wenye ulemavu Marekani.
Lakini akaunti zao za Facebook zilionyesha wakiwa hawana ulemavu wowote.
Mtandao huo ulilazimishwa kuwasilisha taarifa kuhusu akaunti za watu 381 ambazo mahakama ilisema zilikuwa na ushahidi kuonyesha watu hao walifanya uhalifu.
Baada ya ombi lao la rufaa kupinga agizo hilo kukataliwa, Facebook ilitii amri ya mahakama na kuwasilisha taarifa hizo ingawa ilisisitiza kuwa agizo hilo lilikiuka katiba ya Marekani ambayo inazuia msako wowote usio na msingi.
Kesi hiyo imekuwa ikisikilizwa faraghani lakini tangu Facebook kukata rufaa jaji wa kesi hiyo aliamua kuendesha kesi hiyo hadharani.
BBC

SHEREHE ZA KUAGA WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA MKOANI MWANZA ZAFANA 

1
Meza Kuu katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza (katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja ambaye pia ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizofana katika Ukumbi wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza.
2
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza na Wageni Waalikwa (hawapo pichani) katika Sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza.

3
Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Mwanza wakimsikiliza Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake fupi katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba, Jijini Mwanza.(A.I)

Vikosi vya Iraq vyashindwa kuteka Tiqrit

mwanajeshi wa Isis
Ripoti kutoka Iraq zinaarifu kuwa vikosi vya serikali vilivyojaribu kuuteka mji wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa kisunni vimelazimika kurejea nyuma.
Walioshuhudia wanasema kuwa wanajeshi hao walilazimika kurudi katika mji wa Dijla ,yapata kilomita 25 kusini baada ya mashambulizi yao yalioshirikisha mizinga,magari ya kujihami na ndege kushindwa kufua dafu.
Hatahivyo kuna ripoti ya majeruhi wengi kutoka pande zote mbili.
Duru zimearifu kuwa vikosi hivyo vya serikali vinajitahidi kufika Tikrit kwa kuwa wapiganaji wa ISIS wametega vilipuzi vingi katika barabara kuu ya kuingia mjini humo.
Wakati huohuo Iraq inasema kuwa imepokea kundi la kwanza la ndege za kijeshi ilizoagiza kutoka Urusi ili kuisadia kukabiiana na wapiganaji wa dhehenu la kisunni ISIS ambao wameyateka maeneo mengi ya taifa hilo.BBC,(A.I).

Friday, June 27, 2014

Gavana akabiliwa na kesi ya mauaji Kenya 

GAVANA_66c7a.jpg
Gavana wa kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la mpeketoni.
Issa Timamy hata hivyo hatakiwi kujibu mashtaka hayo wakati huu.
Timamy alikamatwa Jumatano jioni na maafisa wa polisi na kuhojiwa kabla ya kuzuiliwa usiku katika kituo kimoja cha polisi. Alifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kadkalika Timamy anakuwa mwanasiasa wa kwanza wa ngazi ya juu kushtakiwa kuhusiana na mauaji hayo, ambayo ni mabaya zaidi tangu yale yaliyotokea katika eneo la Westgate Jijini Nairobi..(E.L).
Anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi, mauaji na kuwafnya watu kuhama makwao kwa lazima. Atasalia kizuizini hadi Juni thelathini huku uchunguzi ukiendelea. Wiki iliyopita, rais Uhuru Kenyatta alilaumu wanasiasa kwa kuchochea mauaji hayo.
Lakini kundi la Alshabab limedai kuhusika katika mashambulio hayo. Wengi wa waliofariki katika mashambulio hayo walikuwa watu wa jamii ya moja Kikuyu, kabila sawa na la rais Kenyatta.
Wakili wake na chama chake cha kisiasa kimewashutumu maafisa wa polisi kwa jinsi alivyokamatwa na kuhojiwa
Mamia ya wafuasi wa gavana huyo walifurika mahakamani kumuunga mkono gavana huyo huku baadhi ya wanasiasa wakilalamikia serikali kuhusu gavana huyo alivyokamatwa na kutendewa na polisi.
Mauaji ya Mpeketoni yalitokea tarehe 15 na 16 mwezi Juni ambapo watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito walienda nyumba hadi nyumba wakiwaua wanaume kutoka jamii moja.
Rais Uhuru Kenyatta aliwalaumu wanasiasa kwa kuwachochea wananchi kufanya mauaji hayo licha ya kundi la Al Shabaab kukiri kuyafanya.
Kenyatta alipuuza madai ya Al Shabaab , hasa kwa sababu ni watu wa kabila moja waliolengwa kwa mashambulizi hayo.
Polisi pia wamewakamata washukiwa 13 wa vuguvugu linalotaka kujitenga na Kenya na ambo wanatumuhiwa kwa mauaji hayo Mombasa.
Katika taarifa yake serikali ilisema kuwa wale waliokamatwa walikuwa wanapanga kufanya mauaji ya kikabila na kwamba walikuwa wanachama wa vuguvugu.(E.L)

Dk Salim: Sina mpango na urais 2015 

dk_24d53.jpg
Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hana mpango na hafikirii tena kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam jana, Dk Salim alisema alipowania nafasi hiyo mwaka 2005, hakuwa na ufahamu mzuri kuhusu mchakato huo lakini baadaye alibaini kwamba, mbali na rekodi ya utendaji, kuna mambo mengine yanayohitajika katika kinyang'anyiro hicho na kwamba hata watu wanaomfikiria na kutaja jina lake miongoni mwa wanaoweza kuwania tena nafasi hiyo, wanakosea.
"Sifikirii tena, hii ni zamu ya kizazi kingine. Ila nitaendelea kuisaidia nchi yangu katika nyanja mbalimbali kadri ya uwezo wangu," alisema.
Dk Salim ambaye mbali na uwaziri mkuu amewahi kushika nafasi nyingine mbalimbali kitaifa na kimataifa, alisema uzoefu alioupata katika kinyang'anyiro cha urais unatosha.(E.L).
Alipoulizwa kama uzoefu huo ni mbaya au mzuri kwake, alisema ni mchanganyiko.
Dk Salim aliwahi kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na kushindwa kutokana na kura ya veto ya Marekani, pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa Umoja wa Afrika (AU). Pia aliwahi kuwa Rais wa Bunge Kuu la UN mwaka 1979 na 1980.
Licha ya kujitokeza mara moja kuomba uteuzi wa CCM kuwania urais 2005, nyota yake katika nafasi hiyo ilianza kuwaka tangu mwaka 1985 akiwa Waziri Mkuu pale aliposhindanishwa katika Kamati Kuu ya CCM na aliyekuwa Waziri Mkuu, Rashidi Kawawa pamoja aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Ali Hassan Mwinyi ambaye alipitishwa kiitifaki na kushinda kiti hicho.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa alisimulia jinsi Mwinyi alivyopita, kwa sababu alikuwa Makamu wa Rais, hivyo wajumbe wa Kamati Kuu walikosa hoja na sababu za kumwacha na kumchukua Waziri Mkuu aliyekuwa chini yake kiitifaki.
"Makamu wa Rais ukimruka maana yake hatoshi, wakaona hawana maelezo hayo, ikabidi wamteue Mwinyi," alisema Msekwa.
Sifa za viongozi
Katika hatua nyingine, Dk Salim alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa viongozi hasa mtu anayekwenda kushika nafasi ya urais atakayekwenda sambamba na mahitaji ya kizazi cha sasa alichokiita cha 'dot com'.
"Hapa sizungumzii viongozi wa CCM au wa Chadema au chama kingine, nazungumzia viongozi wa nchi watakaoweza kufanyia kazi matatizo ya Watanzania.
"Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza kushughulikia matatizo hayo. Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo," alisema. Dk Salim alisema katika kipindi hiki, anahitajika kiongozi atakayekuwa juu ya tofauti za kisiasa, kidini, asili.
"Unajua hapa nchini kama ilivyo mahali pengine, ukiingiza mgawanyiko wa kidini wakati familia nyingi zina watu wa dini tofauti, wote wataathirika."
Viongozi na rushwa
Akizungumzia tatizo la rushwa, Dk Salim alisema ni kubwa na kadri linavyoongezeka, linakuwa adui wa uwajibikaji, demokrasia.
Alisema katika enzi za utumishi wake nje ya nchi, alikuwa akiona rushwa ilivyokithiri katika nchi mbalimbali, lakini hapa nyumbani pakiwa salama hadi akawa anasema Tanzania ina bahati, kauli ambayo hawezi kuisema sasa.
Dk Salim alibainisha kuwa uongozi unaoingia madarakani kwa rushwa hauwezi kuwa mzuri kwa nchi na athari zake zinaonekana hadi ngazi ya chini katika huduma za jamii kama mahakamani, polisi na hospitalini.(E.L)

OBAMA AOMBA PESA AWASAIDIE WAASI 

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.(P.T)

Wednesday, June 25, 2014

CAR:USALAMA WAZIDI KUZOROTA YASEMA U.N 

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri ya Africa ya Kati, Generali Babacar Gaye amesema kuwa usalama umezorota katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita na kuwa nchi hiyo inaweza kuathirika vibaya kutokana na hali hiyo.
Generali Gaye aliliambia baraza la usalama kuwa nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mashambulizi hatari na uasi wa wanamgambo wa kiislamu na wakristo.(P.T)
Zaidi ya watu 50 wameuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi katika siku chache zilizopita.
Afisa huyo wa umoja wa mataifa alitoa habari za kuhuzunisha kuhusu yanayofanyika katika nchi hiyo, mbele ya baraza la usalama.
"Takriban watu 20,000 wamezuiliwa katika maeneo machache", Generali Babacar Gaye alisema .
"wakiondoka, wanaweza kushambuliwa kabla hawajafika kwenye usalama".
Mji mkuu, Bangui, kwa sasa hauna idadi ile yake ya waislamu walio wachache kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa kikristo.
Waliobakia, wamezingirwa na watu waliojihami kwa silaha ambao wanawazuia kuondoka na pia kukata usambazaji wa vyakula na dawa.
Wanaojaribu kuwasaidia kupitia kusambaza huduma zozote zile, pia wanalengwa na wanamgambo hao.
Generali Gaye alisema kuwa ulinzi na usalama unahitajika eneo hilo.
Chanzo:BBC

MAREKANI YAANZA KUISAIDIA IRAQ VITANI 

Wanajeshi wa Marekani
Wizara ya Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa kundi la kwanza la wanajeshi wa Marekani waliotumwa kulisaidia jeshi la Iraq kupambana na machafuko ya waasi wa kisunni limeanza kazi.
Rais Obama alitangaza juma lililopita kuwa wanajeshi maalum 300, walitumwa Baghdad kuwapa mawaidha na kuwasaidia maafisa wa huduma za usalama, na kuwa takriban nusu ya idadi ya wanajeshi hao tayari imewasili Baghdad katika shughli hizo, na waliosalia wanatarajiwa kuwasili siku chache zijazo.
Wanajeshi 40 wa Marekani walio nchini Iraq ndio kikosi cha kwanza kilichotumwa nchini humo.(P.T)
Katika siku chache zijazo, wanajeshi wengine kutoka sehemu nyingine za eneo hilo watakua wakiwasili Baghdad.
Utawala wa Obama umekua na kibarua kigumu kueleza kuwa wanajeshi hao hawakua na nia ya kutumika kivita ila lengo lao haswa ni kutoa ujasusi kuhusu hali ilivyo nchini humo.
Serikali ya Iraq ilikuwa imeitisha msaada wa mashambulizi ya angani ya Marekani ili kujaribu kuzuia hatari ya ISIS.
Hata hivyo, rais Obama amesita kufanya chochote kitakacho sababisha shutma za Marekani kuegemea upande mmoja, katika mgongano huo wa kidini.
Mara kwa mara imekua akiitisha suluhisho la kisiasa kwa mgogoro huo, kupitia kwa serikali inayowasilisha vizuri matakwa ya wa Sunni na waKurdi walio wachache.
Hili lisisitizwa siku ya Jumanne na waziri wa mswala ya kigeni wa Marekani, John Kerry, alipoutembelea mji la kikurdi wa Irbl.
Chanzo:BBC

MULTCHOICE AFRICAYAKUTANA NA WADAU WAKE MAURITIUS 


Mtendaji Mkuu wa MultChoice Afrika,Nico Meyer akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.Hafla hiyo imekusanya wadau mbali mbali wa MultChoice barani Afrika,ambapo Kampini hiyo itakuwa ikinyesha mambo mbali mbali wanayojihusisha nayo kwenye vipindi mbali mbali vya Televisheni zao za DStV na GoTV.Picha zote na Othman Michuzi.

Meneja wa MultChoice kwa Ukanda wa Afrika Magharibi,Bi. Wangi Mba-Uzoukwu nae alipata wasaa wa kuzungumza machache wakati wa tafrija hiyo ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.

Aki akiingia kwenye kipindi hicho kwa mbwembwe (J M)

Muigizaji wa Filamu toka Nigeria,Ritha Dominic akijibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wadau mbali mbali wa filamu za Kinigeria waliopo ukumbini hapo.

Msanii Nassib Abdul a.k.a Diamond ni mmoja kati ya wasanii saba kutoka barani afrika walioshiriki kutuna na kuimba wimbo wa Africa Rising,pichani ni katika sehemu alioimba Diamond ilipokuwa ikionyeshwa kwenye ukumbi wakati wa kuuzindua wimbo huo.
CHANZO: MICHUZI

FASTJET YAINGIA ZIMBABWE

fastjet 2 8a847

KAMPUNI ya ndege ya Fastjet imezidi kupanua huduma zake kwa kuongeza masafa yake kwenda nchini Zimbabwe mara mbili kwa wiki ikitokea Dar es Salaam na kufikia njia ya tatu ya kimataifa baada ya zile za Zambia na Afrika Kusini.
Akizungumzia uzinduzi huo, Mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo, Ed Winter, alisema wamefikia hapo baada ya kupiga hatua kimafanikio katika maeneo ya huduma zake kwenye maeneo ya awali.
"Pamoja na huduma zetu kufanikiwa, katika maeneo yetu ya huduma hapo awali, bado tunatambua mahitaji muhimu ya Watanzania na wananchi wa nchi jirani kiuchumi, kwamba wanahitaji kufika kwa wakati katika masoko yao ya kibiashara," alisema.
Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Zimbabwe, Dk. Orbet Mpofu, alisema nchi yake imepokea kwa furaha taarifa za Fastjet kuichagua Zimbabwe kuwa sehemu yake muhimu ya kutolea huduma zake, na kwamba itakuwa faraja na mafanikio makubwa ya kibiashara.
"Itakuwa hatua moja nzuri sana ya kiuchumi baina ya wafanyabiashara wa Zimbabwe na Tanzania, kwa hiyo sisi tunawakaribisha sana Fastjet kwani tumekuwa tukisikia sifa nzuri kuhusu huduma nzuri na bei nafuu mnazotoa," alisema Dk. Mpofu.
Alisema kuwa Zimbabwe inalenga kufanya mazungumzo ya kina na Fastjet ili kuona kama itawekeza nchini humo katika nyanja ya usafirishaji na uchukuzi.
CHANZO TANZANIA DAIMA

MAXIMO :KUJA YANGA ,APISHANA NA JUMA KASEJA

maximo 163f9

KOCHA mpya wa Yanga, Marcio Maximo amezungumza moja kwa moja na Mwanaspoti jijini hapa jana na akatamka maneno mazuri kwa mashabiki wa Yanga.
Mbrazil huyo amesema kwamba anakuja Dar es Salaam kesho Jumatano(leo) kuitengeneza Yanga imara na itakayobadili soka la Tanzania.
"Huu ndio wakati muafaka kwangu kuifundisha Yanga, nataka niitengeneze Yanga kwa masilahi ya nchi nzima, siendi Tanzania kwa ajili ya Yanga pekee naenda kwa ajili ya Taifa, nataka kufanya kitu cha kipekee kabisa.
"Yanga ni sehemu ambayo imetulia sana kwa sasa, nimekuwa nafuatilia sana. Najua. Nimepata ofa za China, Dubai na klabu moja ya madaraja ya chini Uingereza, lakini nimeamua kuziacha zote hizo niende Tanzania kwa Yanga,"alisisitiza Maximo.
Kocha huyo aliiambia Mwanaspoti jijini hapa kwamba kuna mambo machache anamalizana na Yanga kisha atazungumza kwa kina zaidi kuhusiana na kila kitu kupitia Mwanaspoti pekee.
Apishana na Kaseja
Wakati Maximo, akitua nchini kesho Jumanne, kipa wa timu hiyo Juma Kaseja yupo zake majuu anapiga dili.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka wa mmoja wa marafiki wa kipa huyo, zinasema Kaseja alitimka nchini wiki mbili zilizopita ambapo alianzia Oman ambako aliongozana na Meneja wake Abdulfatah Saleh.
Baada ya kutoka Oman sasa kipa huyo yupo Marekani ambapo kwa mujibu wa Abdulfatah ambaye alizungumza na Mwanaspoti jana Jumapili, kipa huyo atakuwa huko kwa wiki nzima na atarejea Jumapili wakati ambapo tayari Maximo atakuwa ameshaanza kazi na wachezaji wengine wa Yanga kwenye Uwanja wa Bandari.
"Tupo Marekani mimi na Juma (Kaseja), kikubwa tumekuja kupumzika baada ya kumaliza majukumu yetu," alisema Abdulfatah
Yanga wanakutana rasmi leo Jumatatu kwa matayarisho ya msimu mpya wa Ligi lakini kabla ya mazoezi kutakuwa na kikao cha mabosi wa juu na mazoezi yataanza rasmi kesho.
Ingawa Ajenda za kikao hicho zikiwa siri Mwanaspoti linafahamu kuwa mambo matatu yatazungumzwa ambayo ni nidhamu, mikakati mipya ya uongozi huo pamoja na taarifa za ujio wa Maximo.

Tuesday, June 24, 2014

Iraq:Kiwanda kikuu cha mafuta chatekwa 

Wapiganaji wa kisunni wamekuwa wakiteka miji nchini Iraq na kuwaacha maelfu bila makao
Wapiganaji wa Kisunni nchini Iraq wameteka kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini humo katika eneo la Baiji Kaskazini mwa Baghdad.
Kiwanda hicho kilikuwa kimezingirwa kwa kipindi cha siku kumi huku vikosi vya serikali vikizuia shambulizi la waasi mara kadhaa.
Msemaji wawaasi hao amesema kuwa kiwanda hicho sasa kitapewa usimamizi wa makabila yanayoishi katika eneo hilo na kwamba mapambano ya kuuteka mji mkuu wa Baghdad yataendelea.
Utekaji nyara wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Baiji ni muhimu sana kwa waasi hao iwapo watasimamia maeneo ambayo wameyateka kufikia sasa, hasa kwa kutoa umeme kwa mji wa Mosul.
Wakati huo huo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, ameahidi msaada mkubwa kwa jeshi la Iraq wakati wapiganaji wa Kisunni wakiendelea na mashambulizi yao nchini humo.
Alisema Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki na viongozi wengine wameahidi kuunda Serikali ya Umoja inayowashirikisha wote ifikapo mwisho wa mwezi.(P.T)

Kiwanda cha mafuta ambacho kimedhibitiwa na waasi wa kisunni
Daktari Zuhair Al-Naher, msemaji wa Serikali ya Iraq ambaye pia ni mwanachama wa chama tawala cha Waziri Mkuu Nouri al-Maliki, Islamic Dawa Party, anasema kuwa anaamini kuwa Bwana Maliki ataunda Serikali ya kuwashirikisha wote.
Bwana Kerry alikuja Baghdad kwa mambo mawili.
Kwanza kabisa kumshinikiza Waziri Mkuu Nouri al-Maliki na viongozi wengine wa kisiasa kuwa wanapaswa kuwa na Serikali mpya, pana inayofuatia uchaguzi mkuu uliofanywa Aprili. Mamlaka yanapaswa kugawiwa Wasunni na Wakurdi walio wachache na sio kwa Washia ambao ni wengi pekee.
Pili Bwana Kerry alitaka kuhakikishia Serikali ya Iraq kuwa Marekani itasaidia wanajeshi wa taifa hilo wanapendelea kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la ISIS.
Chanzo:BBC

Monday, June 23, 2014

WATU HAWA HAWANA HAMU NA SOKA BRAZIL 

Mchezaji wa Brazil Neymar

Walimkosa nyota wa Brazil, Neymar akiangua kilio wakati wimbo wa taifa wa nchi hiyo ulipokuwa unapigwa katika mechi yao ya pili dhidi ya Mexico.
Wala hawana habari kuhusu penalti iliyozua utata katika mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia.
Hutowapata mitaani wakiwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga kombe la dunia , ingawa baadhi wanawaunga mkono maandamano hayo.
Hawa ni raia wa Brazil ambao hawana muda na kombe la dunia.
Badala ya kutizama soka kwa dakika 90 katika runinga zao, wanaona afadhali kuoka keki, kucheza baharini , kumtembeza Mbwa na kutizama vipindi wanavyovipenda kwenye televisheni au bora zaidi walale.
Victor Pavan, mwanafunzi mwenye miaka, 18,Sao Paulo
"hili sio jambo la kisiasa. Mimi sipendi soka hata kidogo. Nilipokuwa mdogo, nilijaribu kucheza , lakini sikufana katika soka. Sasa mimi huwaambia watu tu kwamba sipendi soka wala sina muda na mchezo huo.
Sio rahisi kuwa raia wa Brazil sasa hivi hasa kama hupendi soka. Kwa sababu tu kwamba mimi ni mwanamume, kila mtu anadhani kuwa napaswa kufurahikia soka. Sijali wala sina muda wa soka. Hata siungi mkono timu yoyote ya nyumbani.
Mpenzi wangu ambaye ni shabiki wa klabu ya,Corinthians - anapenda sana soka.
Huwa naudhiwa sana nikisikia wati wakiongea kuhusu soka kwa muda mrefu. Mpenzi wangu anatazama mechi zote za kombe la dunia wakati mimi naona afadhali kuunga mkono filamu.
Wakati Brazil inapocheza, hata huwa siangalii ukurasa wangu wa Facebook kwa sababu kila mtu anaongea kuhusu kombe la dunia.
Hata siungi mkono nchi hii kuwa mwenyeji wa kombe la dunia. Yaani hili gumzo lote kuhusu kome la dunia linanichukiza kweli.
Lakini najaribu kabisa kutozungumzia kwa sababu kila mtu ana kitu ambacho anakipenda.''

Lucas Kanyo, Mbunifu mwenye umri wa miaka 39, kutoka Sao Paulo

''Sijatazama mechi hata moja ya kombe hili la dunia na sitazama.
Jumatatu wakati ambapo Brazil itacheza, mimi nitakwenda zangu kazini kama kawaida.
Wakati ambapo Brazil ilicheza dhidi ya Mexico Jumanne, nilihisi kuumwa, na kwa hivyo nikaamua tu kulala. Nililala mechi ilipokuwa inachezwa.
Sio rahisi kujiepusha na soka Brazil kwa wakati huu.
Ninapoingia kwenye Taxi, dereva anasikiliza mechi kuptia kwa redio. Nilishangaa sana nilipoamka , sikusikia milio ya fataki kwa sababu Brazil ilitoka sare tasa, lakini kwangu mimi nilihisi vizuri kwa sababu nilipumzika.
Kwa upande mmoja napenda kelele zote barabarani, msongamano wa magari na hayo yote hayanisumbui kwa sababu mimi hutumia baiskeli yangu.
Na kwa kweli, nilikuwa napenda kombe la dunia hadi, mwaka 1998 ambapo Brazil ilishindwa na Ufaransa mabao matatu kwa nunge. Baada ya hapo sijawahi kupenda tena soka.''

Roberta Milazzo, Menaja, mwenye umri wa miaka 42, Rio de Janeiro

"wakati Brazil inapocheza mimi huenda zangu baharini, kucheza mchezo wa kuteleza kwa maji .
Nilienda baharini wakati wa mechi za kwanza zilizohusisha Brazil, kama nilivyofanya tu wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Wakati huo bahari huwa haina watu na wakati huo huwa ni mzuri sana kwangu.
Nchini Brazil, Kila kitu sasa kinahusu dimba la dunia, wakati michezo mingine haiungwi mkono. Kitu hicho kinanikasirisha sana.
Nilikasirika sana kuhusu hekaheka hizi zote za kombe la dunia.
Brazil inahitaji kuimarisha mambo mengi sana , sidhani kama soka ni moja ya mambo hayo.''

Elisa Nazarian, mwandishi, miaka 65 kutoka Sao Paulo

"napenda kuona wachezaji wakiingia uwanjani, wakishikana mikono na kuimba wimbo wa taifa wa nchi zao, hata wakati mwingine wakilia.
Hisia ambazo hutokana na michuano ya kombe la dunia hunigusa sana. Lakini punde baada ya mechi kuanza , mimi huzima televisheni. Sipendi soka sana.
Nakumbuka kusikiliza matangazo ya michuano ya kombe la dunia mwaka 1958 kupitia kwa redio. Hata nilitazama baadhi ya mechi, lakini mwaka 1970, hio ndio ilikuwa michuano ya mwisho kwangu kutazama.
Wachezaji wa siku hizi hawana msisimuko, hekaheka hizi zote za wachezaji ni kuhusu tu pesa.
Mimi nilitembeza Mbwa wangu wakati wa mchuano wa kwanza wa kombe hili la dunia. Sasa ndio wakati mzuri kwa sababu hakuna kelele kwani Mbwa huwa watulivu sana.
Mechi ilimalizika kwa sare tasa na hapakuw ana kelele hata kidogo.
CHANZO; BBC SWAHILI

MWANAMKE ALIYEASI DINI SUDANI AACHIWA HURU 

Meriam alihukumiwa akiwa mjamzito na kujifungulia gerezani
Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu
Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
CHANZO: BBC SWAHILI

GHANA YAKANA KUPANGA MECHI BRAZIL


Kocha wa Ghana Kwesi Nyantakyi amesema kuwa waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria
Na Mathias Canal
Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana , amekanusha madai kuwa shirikisho hilo lilikubali timu ya Taifa kucheza katika mechi ambazo timu nyingine zilikuwa zinajiandaa kupanga.
Shirikisho hilo, pia limewataka polisi kuchunguza madai hayo.
Madai yenyewe yalitolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na wandishi wa jarida la The Daily Telegraph.
"madai yaliyotolewa na gazeti hilo sio ya kweli,'' alisema Rais wa shirikisho la soka la Ghana GFA Kwesi Nyantakyi.
Shirikisho hilo limewataka maafisa wa polisi kuchunguza madai ya vyombo vya habari vya Uingereza kwamba mmoja wa maafisa wake alikubali timu ya nchi hiyo kucheza katika mechi zilizo fanyiwa ufisadi.
Mamlaka ya Soka nchini Ghana imekana madai ya jaribio lolote la kuuza mechi zake ama kuhusika kwa afisa yeyote katika ufisadi.
Madai hayo yametolewa kufuatia uchunguzi wa pamoja kati ya gazeti la Uingereza la Daily Telegraph na Runinga ya Channel Four.
Katika taarifa yake shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa hakuna ushahidi kwamba uadilifu wa michuano ya kombe la dunia umeathirika.
Shirikisho hilo limesema kuwa litamuwekea vikwazo vikali afisa yeyote atakayepatikana na makosa hayo.

Divock Origi Najivuania kuwa mkenya

Origi Ni bao la kujivunia kwa kenya familia yangu na Ubeljiji.
Na Mathias Canal
Mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa , Mkenya Divorc Origi ambaye ni raiya ya Ubelgiji aliyeifungia Ubeljiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika mechi yao ya pili ya kundi H amesema kuwa anajivunia kuwa mkenya licha ya kuwa anaiwakilisha Ubeljiji.
Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.
Origi ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku alifuma bao hilo la kipekee kunako dakika ya 88 ya kipindi cha pili ya mechi hiyo alipopokea pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard .

Origi, mwanawe Mike Okoth, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars atakua mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kuiwakilisha Ubeljiji, na yuko pamoja na wachezaji nyota kama vile Vincent Kompany wa Manchester City na Eden Hazard wa Chelsea.
Akizungumza na BBC Origi anasema:''aliamua kuichezea Ubeljiji baada ya kutilia maanani mambo mengi kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo, mizizi yake ya kandanda iliyoko huko, marafiki, ushauri wa babake pamoja na Ubelgiji kufuzu kwa kombe la dunia kwani haijulikani ni mwaka upi Kenya itafuzu kwa kombe la dunia.
Origi aliiambia BBC kuwa anafurahia mizizi yake na kuwa anajivunia bao hilo na familia yake iliyokuwa uwanjani kumshabikia .
Origi alisema kuwa hii ilikuwa ni tukuio spesheli kwake kwa Kenya na Ubeljiji.