TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, May 27, 2014

Labda umekua ukiusikia mwenge wa uhuru toka uko shule ya msingi ila hujawahi kujua gharama zake

Screen Shot 2014-05-27 at 11.27.07 AM
Bunge la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ( 104.4 CloudsFM ) ambapo leo May 27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya majibu yaliyotolewa ni kuhusu uwepo wa mbio za mwenge na gharama zake.
Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia amesema ‘serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka 2012 jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo milioni 450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua mwenyeji wa sherehe za kilele’
‘Kuhusu kiasi cha fedha kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba zinatofautiana kulingana na michango ya Wananchi katika wilaya husika kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012 Wananchi walichangia zaidi ya BILIONI 11 na milioni 500′
Screen Shot 2014-05-27 at 11.26.46 AM
Halmashauri za wilaya na manispaa zilichangia shilingi BILIONI 45, Wahisani na watu binafsi walichangia zaidi ya shilingi milioni 52 ambapo faida zinazopatikana kutokana na Mwenge wa Uhuru nchini ni pamoja na kuendelea kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa letu, kuhamasisha Wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na ubaguzi wa dini, rangi au ukabila’
‘Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao’
Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma Nkamia leo May 27 2014 bungeni, unalolote la kuchangia? mtazamo wako kwa ujumla niachie hapa chini kwenye comment mtu wangu.

Baada ya Adam Kuambiana, bongo movie imepata msiba mwingine wa huyu mwigizaji

Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.46 AM
Tukiwa na wiki moja toka tumzike muongozaji na muigizaji Adam Kuambiana leo asubuhi imetoka taarifa nyingine ya kifo cha miongoni mwa waigizaji wa kike toka Bongo Movie.
Aliefariki ni mwigizaji anaitwa Rachel Haule ambaye kacheza movie mbalimbali ikiwemo Vanesa in Dilema.
Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.59 AM
Chanzo cha kifo chake chake bado hakijafahamika ingawa taarifa za mwanzo zinasema alikua mjamzito na alikwenda Muhimbili kwa ajili ya kujifungua baadae alifanikiwa kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki nae hali ilibadilika akapelekwa ICU lakini baadae akafariki

Mafuriko sio Tanzania tu, hii imetokea China na kuua zaidi ya 20 ( picha5 )

Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.30 AM
Ni dhoruba kali iliyoleta majonzi Kaskazini mwa China ambako mpaka sasa tayari watu 26 wamefariki na wengine 10 hawajulikani walipo huku vyombo vya usalama na uokoaji vikizidi kutafuta njia ya kuepusha maafa zaidi kutokana na hali ya hewa.
Kwenye eneo la Guangdong ni watu 15 wamefariki toka Jumatano iliyopita na wengine watano hawajulikani walipo kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha.
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.41 AM
Picha zote hizi unazoziona zimepigwa May 25 2014 ambapo hii inaonyesha moja ya familia kwenye eneo hilo ikipata chakula juu ya maji yaliyojaa nyumbani kwao
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.22 AM
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.10 AM

 

Shindano la Big brother Africa linarudi… mabadiliko ya 2014 yako hapa

Screen Shot 2014-05-26 at 6.11.50 PM
Unaambiwa shindano hili ambalo limekua likifanyika na kuhusisha Watanzania toka lilipoanza ambapo ni Mtanzania mmoja tu (Richard) ndio alichukua ushindi katika miaka yote hiyo ya ushiriki.
Ilizoeleka shindano huwa linaanza mwezi May lakini la mwaka huu 2014 kutokana na kombe la dunia, litaanza September 7 ikiwa ni season 9 ambapo time hii idadi ya nchi zinazoshiriki ni ileile ya nchi 14 ila kuna nchi moja imeondolewa.
Angola wameondolewa na sasa Rwanda wameingizwa kwa mara ya kwanza huku nchi nyingine zitakazoshiriki zikitajwa kuwa niBotswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, Rwanda, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.
Screen Shot 2014-05-26 at 6.13.45 PM
Washiriki wote ni kuanzia walio na umri wa miaka 21 ambao ni lazima wawe ni Wananchi wa hizo nchi zenyewe na wawe na hati za kusaifiria kutoka nchi hizo.
Tarehe za kuwasaka washiriki wa mwaka huu zitatangazwa June ambapo kwa stori nyingine kuhusu BBA ya mwaka huu zitatoka mwezi ujao.
Kuhusu shindalo litakavyokuwa unaambiwa Biggie ndio atawasuprise watazamaji

Friday, May 23, 2014

Boko Haram ni magaidi wa kimataifa - UN 


Baraza la Usalama la UN
Baraza la usalama la umoja wa mataifa hatimaye limeidhinisha kuwekewa vikwazo kundi la Boko Haram baada ya utekaji nyara wa takriban wasichana 300 wa shule katika eneo la Chibok Nigeria.
Kundi hilo limeshutumiwa kuwaua maelfu ya watu nchini Nigeria katika miaka michache iliyopita.
Nigeria ni mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa nafasi hii imeweza kushinikiza baraza hilo kuimulikia tochi.(MM)
Vikwazo na adhabu
Hatua ya baraza hilo kuiorodhesha Boko Haram miongoni mwa magaidi wa kimataifa, wakipishana au hata kuhusishwa moja kwa moja na AL Qaeda, huenda isionekane kama hatua kubwa. Lakini hii ina maana kuwa sasa jamii ya kimataifa italichukulia kwa uzito mkubwa zaidi kundi hilo.
Baraza hilo limeidhinisha pia vikwazo kuwekewa kundi hilo, viongozi wake na yeyote anayehusishwa nalo. Hii ina maana kuwa hata mali zao zitazuiliwa na akaunti zao zote zinazojulikana kufungwa.
Jamii ya kimataifa
Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power amepongeza hatua hiyo akisema kuwa itaimarisha vita vya serikali ya Nigeria dhidi ya Kundi hilo, ambalo limetikisa jamii ya kimataifa mwezi uliopita kwa kuwateka zaidi ya wasichana mia mbili wa shule.
Kwa upande wake mjumbe wa Australia katika baraza hilo balozi Gary Quinlan amesema kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa Boko Haram wamepewa mafunzo na kundi la Al Qaeda hasa namna ya kujitengenezea mabomu, mtindo ambao umekuwa mbinu mpya zaidi ya ugaidi.
Abubakar Shekau wa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau amenukuliwa katika mtandao akitoa matamshi ya kuunga mkono AL Qaeda nchiuni Afghanistan, Yemen na Somalia.
Magaidi wanaojulikana
Kabla ya kujumuishwa Boko Haram katika orodha ya Al Qaeda, kulikuweko makundi 62 kote duniani waliowekewa vikwazo kuhusika na Ugaidi, na watu binafsi 162, ambao wamewekewa vikwazo vya usafiri na mali zao kutwaliwa.
Wamesababisha maafa
Shughuli za Boko Haram katika miaka 5 iliyopita zimesababisha vifo vya maelfu ya waislamu na wakristu wakiwemo watu 1500 waliouawa mwaka huu pekee.
Jina la Boko Haram lina maanisha masomo ya magharibi ni Haram na kundi hilo limetumia nembo hiyo kuendeleza mashambulio yao na chuki dhidi ya chochote kinachhusishwa na nchi za magharibi.
CHANZO:BBC

Germain Katanga ahukumiwa jela miaka 12

Germain Katanga
Kiongozi wa zamani wa wapiganaji waasi DRC Germain Katanga
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu kiongozi wa zamanai wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita.
Bwana Katanga alipatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mamia ya wanavijiji katikaeneo la Ituri Katanga mwezi Machi mwaka 2003.
Jimbo la Katanga ni jimbo lenye utajiri wa madini ya dhahabu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo . Lakini kiongozi huyo wa waasi mwenye umri wa miaka thelathini na sita hakupatikana na hatia ya kuwatumikisha watoto vitani na makosa mengine ya ubakaji.(MM)
CHANZO:BBC

Waziri ajiua kwa kushindwa uchaguzi 

Kabla ya kujiua, aliacha ujumbe kwamba amechukua hatua hiyo baada ya kutokea migongano ya kisiasa.
Wakati Rais wa Malawi, Joyce Banda akizidi kuelemewa kwenye uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki hii, Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa, Godfrey Kamanya amejiua baada ya kubaini ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge.
Kamanya alijipiga risasi nyumbani kwake mjini Lilongwe saa 9:30 asubuhi baada ya kupewa taarifa hizo kwa ujumbe mfupi wa simu.
Kabla ya kujiua, aliacha ujumbe kwamba amechukua hatua hiyo baada ya kutokea migongano ya kisiasa.
Kamanya aligombea ubunge katika Jimbo la Nzonzi Kusini kupitia People's Party (PP) na mwili wake ulikutwa chumbani kwake na ulipelekewa kuhifadhiwa kwenye Hospitali Kuu ya Kamuzu.(P.T)
Taarifa nyingine zinaeleza kwamba waziri huyo alijiua kutokana na vitisho kutoka kwa mtu asiyefahamika.
Katika matokeo yasiyo rasmi kutoka kituo cha kuhesabia kura cha Lilongwe yaliyotolewa Jumatano asubuhi, mgombea huyo alikuwa ameshika nafasi ya tano kati ya wagombea saba waliowania ubunge kwenye jimbo hilo.
Katika matokeo hayo ya awali, Kamanya alipata kura 1,738 huku mgombea wa Malawi Congress Party (MCP), Higton Jiya akiongoza kwa kura 4,625.
Wakati tukio hilo likitokea, mke wa Kamanya alimpigia simu waziri wa zamani wa usafirishaji, Ulemu Chilapondwa ambaye alikuwa rafiki ya mumewe na kumweleza kuwa amesikia mlio chumbani wakati mlango umefungwa.
Kutokana na taarifa hiyo, Chilapondwa alipofika nyumbani kwa marehemu akiwa na watu wengine wawili walivunja mlango na kukuta mwanasiasa huyo ameshaaga dunia baada ya kujipiga risasi kifuani.
Tukio hilo limekuja wakati mgombea urais kupitia chama chake, Rais Joyce Banda akiwa katika nafasi ya pili akiwa na asilimia 22 ya kura akigongana na Lazarous Chakwera wa Malawi Congress Party (MCP). Anayeongoza ni mgombea urais kupitia Democratic Progressive (DPP), Peter Mutharika kwa zaidi ya asimilia 30.
Chanzo:Mwananchi

Kupima Virusi vya Ukimwi ni jambo la hiari 

taaaaaaaaaa_d82f0.jpg

Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar

Kupima Virusi vya Ukimwi linabaki kuwa  jambo la hiari  kwa muhusika na linaweza kuwa ni kitu cha lazima iwapo  Daktari au Mahakama wamefikia maamuzi ya  kufanya hivyo kwa  sababu maalum ya  kupatiwa ufafanuzi  wa  jambo. (FS)

Hayo yamesemwa jana huko Baraza la Wawakilishi  Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji wakati akijibu suali la Mwakilishi   Jaku Hashimu Ayoub alieitaka  Serikali kuwalazimisha  wananchi  kupima virusi vya ukimwi  kwa kuanzia viongozi wa Serikali na Wanasiasa.

Alisema  Zanzibar ni Sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeridhia mikataba ya Kimatafa na Kikanda  na kuheshimu haki za Binadamu, hivyo Zanzibar inawajibu wa kuzingatia na kutekeleza kwa vitendo maazimio ya Ulimwengu ambayo yanakataza kuwalazimisha watu kupima ukimwi.

 “Muongozo wa Shirika la Kazi Duniani juu ya masuala ya ukimwi ni sehemu za kazi  na linapinga kuwalazimisha watu kupima virusi vya ukimwi hasa  wanapotaka kuomba kazi au shurutisho kwa waajiriwa,”alisema Waziri Fatma.

Aidha Waziri huyo alisema kua kushurutisha upimaji wa virusi vya ukimwi ni njia mojawapo ya kuwanyanyapaa na kuwabagua watu waishio na  hivyo na hilo pia ni kinyume na sera za nchi na Mikataba ya Kimataafa dhidi ya ugaguzi.

Hata hivyo Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais alisema sera ya Taifa ya 2006 imeweka miongozo tosha ya upimaji virusi vya ukimwi kwa lazima pale ambapo Mahakama na Hospitali  zitalazimika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

“Hatua hii itafanyika iwapo  pametokea udhalilishaji wa kijinsia na ubakaji, naomba nisisitize kwamba suala la ajira, nafasi za uongozi wa kisiasa na Serikali halikuwekewa ulazima wa kuchunguza virusi vya ukimwi,” aliongeza Waziri.

Pamoja na hayo Waziri Fatma alisema Baraza la Wawakilishi lilipitisha mswada wa sheria  desemba 2013 wa  kuweka masharti  ya kukinga na kusimamia masuala ya ukimwi  Zanzibar kulinda na kuheshimu haki za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi..

Waziri huyo alisema hivi sasa ziko baadhi ya Skuli zimeanzisha  somo la ukimwi zikiwa na lengo la kuwajengea wanafunzi  uelewa zaidi wa tatizo hilo ili kuweza kujikinga nalo

Kauli ya Wayne Rooney ikiwa Van Persie akiwa nahodha wa Man United

Screen Shot 2014-05-23 at 11.22.34 AM 
Tangu Nemanja Vidic alipotangaza rasmi kwamba msimu ujao hatokuwepo Old Trafford kulianza tetesi juu ya mchezaji gani atapewa nafasi ya kurithi mikoba ya unahodha ambapo Wayne Rooney mmoja wa wachezaji wakubwa ndani ya klabu ya Manchester United alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha mpya wa United wakati timu hiyo ikiwa chini ya David Moyes.
Baada ya kutimuliwa kwa kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Louis Van Gaal, mshambuliaji wa Uholanzi na nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie amekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Vidic, huku Van Gaal akisema kwamba yeye na RVP wana filosofia moja hivyo wanakuwa na urahisi wa kufanya kazi pamoja kama kocha na nahodha wake.
Hali hiyo imepelekea Wayne Rooney ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya unahodha msimu ujao kuzungumza akisema “navutiwa na suala la kuwa nahodha, nimeshawahi kuwa anahodha wa muda United kwa mara kadhaa na kupata jukumu hilo moja kwa moja litakuwa jambo zuri sana.”
Screen Shot 2014-05-23 at 11.30.39 AM
Akizungumzia suala la Van Persie kupewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha ajaye wa United, Rooney anakwambia ikiwa kocha wetu atamchagua mtu mwingine basi kiukweli kabisa sitokuwa na tatizo na hilo, nitaheshimu maamuzi yake… Robin ni nahodha wa nchi yake, ameshawahi kuwa nahodha wa Arsenal na ikiwa atapata nafasi hiyo United basi naamini atafanya kazi nzuri.”

Polisi wanamchunguza David Moyes, anadaiwa kumpiga huyu kijana kwenye hii baa

Screen Shot 2014-05-23 at 8.12.31 AM
Kocha David Moyes ambae alifukuzwa kuiongoza Manchester United mwezi uliopita alikwenda kwenye hii Baa yeye na rafiki zake ambapo kwenye mida ya saa nne usiku ishu ndio ikatokea.
Polisi wa Lancashire ndio wanachunguza kuhusiana na madai ya shambulio lililotokea Wine Bar baada ya kudaiwa yeye na wenzake kuhusika kumchambulia kijana wa miaka 23 kwenye baa hiyo huko Clitheroe usiku wa Jumatano.
Screen Shot 2014-05-23 at 8.10.02 AM
Hata hivyo kijana alieshambuliwa hakuhitaji matibabu yeyote hivyo hakwenda hospitali lakini hilo halijalishi manake
Polisi wanaendelea kupitia rekodi za video za camera za CCTV za eneo hilo ili kujua kila kilichotokea na aliehusika.
“Kulikua na mashambulizi nje ya bar hii lakini hakuna mfanyakazi aliyeumia, polisi wanashughulika na uchunguzi mpaka sasa”Alisema mzungumzaji wa Bar hiyo.
Screen Shot 2014-05-23 at 8.12.16 AM
Pamoja na kwamba Polisi hawajatoa ripoti, mmoja wa mashuhuda amesema huyu kijana alipigwa na Moyes baada ya kumtusi. kumchana kuhusu kufukuzwa kwake Man United na kumwita jina la kitu ambacho hakijawahi kufanikiwa au kupata ushindi.
Huu ugomvi ulitokea nje tu ya baa hiyo kwenye meza na viti ambapo kwenye purukushani glasi zilitupwa chini na kijana huyu kuumia kichwani na begani baada ya yeye na kundi lake kuanza kutoa vijembe walipomuona David Moyes.

Wednesday, May 21, 2014

"MADENI YA WALIMU KULIPWA KABLA YA JULAI" 

bunge-dom_467c7.png
SERIKALI imesisisitiza kuwa italipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya walimu kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha, 2013/14. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa, alieleza hayo bungeni juzi jioni wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Bunge lilipitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 ya Sh bilioni 799 zikiwamo Sh bilioni 344.2 za matumizi ya kawaida na Sh bilioni 454.8 kwa ajili ya maendeleo.(Martha Magessa)
Majaliwa alisema madeni ya walimu yalielezwa kufikia Sh bilioni 61 na kwamba kumekuwa kukifanyika uhakiki, na kwa baada ya uhakiki, Februari mwaka huu, walilipa Sh bilioni 19.
“Lakini pia Machi na Aprili tayari kuna fedha nyingine zimelipwa, kwa bahati mbaya sikuja na takwimu hapa, lakini Serikali itahakikisha kuwa madeni yote yanalipwa katika mwaka huu wa fedha kabla haujamalizika,” alisema Majaliwa.
Aidha, alisema fedha nyingine za malimbikizo yakiwamo ya likizo, matibabu, usafiri na masomo zinalipwa kwa kupitia katika halmashauri husika.
Kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu, alisema tayari nyumba 1,200 zinajengwa ambapo kati yake 268 zimekamilika na zimetengwa Sh bilioni 200.
Kuhusu fedha za chenji za rada, Naibu Waziri alisema hadi sasa zimeshanunulia madawati 93,988 ambayo yatagawanywa 600 kwa kila halmashauri katika awamu ya kwanza na awamu ya pili madawati 400.
Akizungumzia walimu kuwa na waajiri tofauti, alisema mwajiriwa wa walimu ni Katibu Mkuu Tamisemi, na katika ngazi ya mikoa wako chini ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) na katika Halmashauri, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED).
Akichangia hoja hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia alisema walimu wanaona unafuu zaidi tangu wawe chini ya Tamisemi, huku akiwataka wabunge kuacha kupotosha dhana ya kuchangia maendeleo.
Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, alitetea uamuzi wa kubadili madaraja ya ufaulu, akisema si kitu kigeni duniani. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, aliahidi kukutana na wadau ili kujadili kuundwa kwa chombo kimoja cha kushughulikia masuala ya walimu.
CHANZO:HABARILEO

MAPINDUZI MAKUBWA YA VIWANDA 


WIZARA ya Viwanda na Biashara imewasilisha bungeni bajeti yake inayoonesha mapinduzi makubwa katika viwanda, ikiwamo kuanza kwa miradi ya chuma ya Liganga na Mchuchuma na kiwanda cha kuua viluwiluwi vya mbu waenezao malaria.
Pia kiwanda cha matairi cha General Tyre kinatarajiwa kuanza tena uzalishaji katika mwaka ujao wa fedha. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliwasilisha bajeti yake hiyo bungeni jana.(Martha Magessa)
Dk Kigoda alisema ukuaji wa sekta ya viwanda ni mzuri kwani umeongezeka kutoka asilimia 5.5 mwaka 1998 hadi asilimia 7.7 mwaka 2013, ingawa ukuaji huo uko chini kidogo ukilinganisha na mwaka 2012.
“Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani, hususani viwanda vya vinywaji, saruji, bidhaa za chuma, na usindikaji wa mazao ya kilimo,” alisema Dk Kigoda.
Kuhusu Liganga na Mchuchuma, alisema katika mwaka 2013/14, utafiti uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) umethibitisha kuwapo kwa mashapo ya makaa ya mawe ya tani milioni 370 katika eeno la kilometa za mraba 30.
Alisema utafiti huo, pia umethibitisha kuwapo kwa mashapo ya madini ya chuma ya tani milioni 219 katika eneo la kilometa za mraba 10.
“Mpango wa awali ni kuzalisha tani milioni moja za chuma na megawati 600 za umeme. Kiasi hicho cha uzalishaji wa chuma kitaifanya Tanzania kuwa ya tatu barani Afrika katika uzalishaji chuma.
“Aidha, kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha ajira zipatazo 32,000 na mapato ya takriban Sh trilioni 2.8,” alisema Dk Kigoda.
Alieleza kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba tayari dola za Marekani bilioni tatu (Sh trilioni tano) zimepatikana na wabia wa miradi hiyo, NDC na Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL) na kuwezesha ujenzi wa viwanda vya chuma kuanza mwaka 2014/15.
Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu waenezao malaria mjini Kibaha, kwa kutumia teknolojia kutoka Cuba, alisema ujenzi wa majengo umekamilika kwa asilimia 90.
“Mitambo imekwishanunuliwa na kufikishwa katika eneo la ujenzi na hivi sasa inawekwa tayari kwa uzalishaji mwanzoni mwa mwaka 2014/205 yaani mwezi Julai 2014,” alisema Waziri.
Alisema kukamilika kwa mradi huo ni ukombozi mkubwa kwa Taifa katika kupambana na malaria kwa kuwa viuadudu vitakavyozalishwa, kazi yake ni kuua mbu kuzaliana na hivyo kupunguza wagonjwa wa malaria, gharama za kununua vyandarua na dawa za kuulia mbu.
Akizungumzia kiwanda cha General Tyre Ltd (GTEA), alisema NDC imekamilisha kukarabati majengo na ukarabati wa mfumo wa umeme unaendelea na kisha utafuatiwa na kujaribu mitambo.Kuhusu uzalishaji wa magadi soda Ziwa Natron na Engaruka, alisema utafiti umekamilika kuhusu wingi na ubora wa rasilimali za magadi.
Alisema kiasi cha meta za ujazo bilioni 4.68 za magadi ambazo huongezeka kwa kiasi cha mita za ujazo milioni 1,8675 zimegundulika katika Bonde la Engaruka. Kwa sasa, anatafutwa mtaalamu mshauri na makadirio ya ujenzi wa yatajulikana baada ya usanifu wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza uzalishaji mwaka 2016/17.
Utaingiza dola za Marekani milioni 320 kwa mwaka na utatoa fursa za ajira 3,900. Dk Kigoda akizungumzia saruji alisema kumeanzishwa viwanda katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani, na miradi hiyo itakapokamilika pamoja na viwanda vilivyopo, vitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni sita kwa mwaka na kutoa ajira zaidi ya 5,000.
“Kiasi hicho cha saruji kitakuwa mara mbili ya mahitaji ya saruji nchini, na hivyo kuwezesha kujitosheleza kabisa,” alisema waziri.
Kuhusu fidia katika maeneo yaliyochukuliwa kwa ajili ya uwekezaji, Dk Kigoda alisema kimsingi Serikali inawajibika kuwalipa fidia wananchi katika maeneo hayo, itajaribu kukamilisha fidia hiyo mwaka 2014/15.
Aliyataja maeneo yenye kuhitaji fidia kuwa ni Kurasini Dar es Salaam, Bagamoyo, Ruvuma, Mtwara na Tanga.
Aliyataja baadhi ya malengo ya mwaka 2014/15 ni kukamilisha Sheria ya Kusimamia Biashara ya Chuma Chakavu na kuandaa kanuni zake, kuandaa Sera ya Taifa ya Kumlinda mlaji na kuendeleza utekelezaji wa utaratibu wa kupima ubora wa bidhaa zote mahali zinapotoka kabla ya kuingia nchini.
Katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara ya Viwanda na Biashara imeomba kutengewa jumla ya Sh 112,497,801,000.
 CHANZO:HABARILEO

UKAWA WAMPONZA ASKOFU KAKOBE 

UkawaWalivyosusa_5f2a2.png
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.
Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.
"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.
Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.
Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.
"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake,” alisema.
Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.(Martha Magessa)
Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.
Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.
Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.
CHANZO:HABARILEO

Mabalozi 12 EU wamlima Pinda barua kuhusu albino 


Dar es Salaam. Mabalozi 12 wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini wamemtumia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda barua ya wazi wakimtaka kuchukua hatua stahiki kwa watu waliofanya mauaji ya albino wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.
“Tumesikitishwa na mauaji ya kikatili ya albino Munghu Lugata yaliyotokea Mei 12, 2014 wilayani Bariadi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na mabalozi 12 wa nchi wanachama wa EU Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo nchini, Filiberto Sebregondi. (J M)
Mabalozi wengine waliosaini barua hiyo ni Dianna Melrose wa Uingereza, Koenraad Adam wa Ubeligiji, Johnny Flento wa Denmark, Sinikka Antila wa Finland, Marcel Escure wa Ufaransa, Fionnuala Gilsenan wa Ireland, Luigi Scotto wa Italia, Jaap Frederiks wa Uholanzi, Luis Manuel Cuesta Civis wa Uhispania, Lennarth Hjelmaker wa Sweden na Kaimu Balozi wa Ujerumani, Hans Koeppel.
Katika tukio hilo linalohusishwa na ushirikina, watu wasiofahamika walimuua Lugata na mwili wake ulikutwa nje ya nyumba yake ukiwa umejeruhiwa vibaya.
Barua hiyo ilisema kuwa Pinda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo hivyo, bila shaka atahamasisha mamlaka za chini yake kuchukua hatua za kisheria.
“Tunakuomba kwa mara nyingine kuhamasisha mamlaka zako kutokomeza vitendo hivi vya kikatili kwa kuhakikisha havijirudii tena na kufanya uchunguzi makini na kuwafungulia mashtaka wale wote waliohusika,” ilisema.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Lugata ni albino wa 73 kuuawa nchini tangu mwaka 2000 na wa kwanza kwa mwaka 2014.
Katika barua hiyo ambayo pia ilithibitishwa na Mkuu wa Idara ya Siasa, Habari na Mawasiliano ya EU, Tom Vens, mabalozi hao 12 wanafahamu fika kuwa waganga wawili wa jadi wanahusika katika mauaji hayo.
Wakati huohuo; Ubalozi wa Uingereza nchini umezungumzia suala la uchunguzi wa uchotaji wa zaidi ya Sh200 bilioni katika Akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ukisisitiza kuwa suala hilo lishughulikiwe ipasavyo na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pia ubalozi huo umekanusha madai ya balozi wake nchini kuhusika katika mkakati wa kujaribu kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Taarifa ya ubalozi huo iliyotolewa jana, ilieleza kwamba unafuatilia kwa karibu kuhusu taarifa za ubadhirifu uliofanywa kupitia Kampuni ya IPTL, ikihusisha Akaunti ya Escrow na BoT, lakini hauna sababu ya kuingilia kukwamisha bajeti ya Wizara ya Madini kama ilivyotajwa na baadhi ya vyombo vya habari. Chanzo mwananchi

Baada ya Kikombe cha Babu, dhahabu yaibuka Samunge


Arusha. Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika  katika eneo hilo. (J M)
Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.
Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.
“Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka, hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba,” alisema Sandea.
Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.
“Kuna wengine wanapata hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi,” alisema.
Ulinzi waimarishwa
Diwani huyo alisema ulinzi umeanza kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo, kunaweza kutokea vurugu kubwa na hata mauaji.
“Sisi kama viongozi, tumeweka utaratibu mzuri wa kuchimba madini kiusalama na hata wale ambao wameanza kuuza mashamba yao, tunawawekea utaratibu mzuri,” alisema.
Maofisa madini kutua Samunge
Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu katika eneo la Samunge, maofisa wake wanajiandaa kwenda kijijini hapo.
Alisema taarifa za kitaalamu kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo Samunge itatolewa baada ya maofisa hao kufika katika eneo hilo na kufanya utafiti. CHANZO MWANANCHI

MELI YA KIKWETE KUKAMILIKA 2016

Mwanza. Siku kama ya leo mwaka 1996, ilikuwa ni vilio kila kona ya nchi, lakini Kanda ya Ziwa iliathirika zaidi na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na kuteketeza mamia ya wananchi. (J M)
Kuzama kwa Mv Bukoba inaelezwa ni kutokana na kuwa ubovu. Tukio hilo ambalo haliwezi kufutika vichwani mwa wakazi wa Kanda ya Ziwa, lakini kilio chao cha kupatiwa meli mpya licha ya Rais Jakaya Kikwete kuahidi Serikali kununua mwaka 2010, haijanunuliwa hadi sasa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ujenzi wa meli hiyo mpya iliyoahidiwa na Rais Kikwete kwa Ziwa Victoria unatarajia kukamilika mwaka 2016.
Akizungumza ofisini kwake wiki hii, Ofisa Masoko wa Huduma za Meli Mwanza Obedi Nkongoki alisema mjenzi wa meli hiyo Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (Danida) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
“Ujenzi huu unahusisha meli nne ingawa Rais aliahidi tatu; Ziwa Victoria moja, mbili Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Nyasa ambazo zinatarajiwa kukamilika 2018, huku ya Ziwa Victoria ikitarajiwa kukamilika 2016,” alisema Nkongoki.
Alisema meli mpya itakuwa na kasi kwa kutumia saa tano kwenda Bukoba na kurudi Mwanza, itakuwa ikifanya kazi mchana badala ya usiku pekee, ikibeba wastani wa abiria ni 500 na tani 56 za mizigo. Gharama hazitakuwa kubwa zaidi na haitakuwa tofauti na mabasi ila zitazingatia soko na bei ya mafuta,” alisema Nkongoki na kuongeza:
“2016 itapatikana meli mpya, hapo tutaanza ukarabati wa meli za Serengeti na Victoria, baadaye tutaifanyia ukarabati meli ya Umoja, ambao utaziweka katika hali nzuri na zitakazokwenda na wakati. Tunalenga kujiimarisha kiuchumi kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo, Uganda, Zambia, Rwanda na Malawi.”
Alisema meli zinazohudumu zilitengenzwa mwaka 1938 na kwamba, ambayo inaonekana mpya ni ya mwaka 1988, hivyo wamekuwa na uzoefu wa mabadiliko ya meli kulingana na hali ya hewa.
“Hivyo tuna uhakika wa kuepuka ajali, kwani tunajitahidi kufanya ukaguzi mara kwa mara. Pia, tunaajiri wataalamu wenye taaluma ili kuimarisha usalama wa abiria na mali zao,” alisema.
Victoria hivi sasa inabeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo, huku Serengeti ikibeba abiria 593 na tani 350 za mizigo. Hivyo ujio wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizopo unatazamiwa kuwa ni mkombozi kwa usafiri Ziwa Victoria. Chanzo Mwananchi

WENYE VYETI FEKI WAKAANGWA BUNGENI


Dodoma. Wabunge juzi jioni walichachamaa wakitaka mawaziri na wabunge wanaohusishwa na vyeti feki kulithibitishia Bunge juu ya uhalali wa vyeti vyao. (J M)
Suala hilo lilijitokeza wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2014/15.
Wabunge hao walikuwa wakijadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Ole, Rajabu Mohamed Mbarouk (Cuf) aliyeitaka Serikali kueleza ni kwa nini Baraza la Mitihani ya Taifa (Necta) linashindwa kudhibiti vyeti feki. Alisema kuna mchezo mchafu unaoathiri mfumo wa elimu nchini na uchumi wa Taifa.
Alisema kuzagaa kwa vyeti hivyo kunaifanya hadhi ya Necta kushuka na kukosa imani hata katika jumuiya za kimataifa.
“Suala la vyeti feki ambalo Baraza la Mitihani la Taifa ndilo lenye dhamana na jukumu la kuhakikisha halitokei katika taifa limeonekana kama suala la kawaida,” alisema na kuongeza; “Vyeti feki ni vingi kiasi kwamba linasababisha kuajiriwa kwa watendaji ambao ni feki na mawaziri mizigo.”
Alisema kuzagaa kwa vyeti hivyo kunasababisha kupata makatibu wakuu na watendaji feki.
Mbarouk alisema hivi karibuni katika Chuo cha Polisi cha Moshi walirejeshwa wadahiliwa 122 kwa sababu ya kukutwa na vyeti feki.
Alihoji ni kwa nini Necta inashindwa kudhibiti vyeti hivyo.
Akitoa ufafanuzi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema Necta baada ya kugundua udanganyifu wa vyeti ilibadilisha namna ya kuchapa vyeti hivyo.
“Hivi sasa vyeti vinavyotolewa vina Serial number, jina la mhitimu katika cheti cha kuzaliwa na picha na kwamba siyo rahisi kughushi vyeti hivyo,” alisema.
Hata hivyo, Mbarouk alikataa ufafanuzi huo na kusema asilimia sita ya wanaoomba kazi nchini wana vyeti feki.
Alitaka kufahamu hatua zilizochukuliwa ikiwamo za kinidhamu katika kukabiliana na suala hilo. CHANZO MWANANCHI

Dengue kuwakumbusha usafi wa Mazingira


Mwanza. Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Stephen amewataka viongozi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanasimamia utunzaji mazingira ili kukabilina na ugonjwa wa Dengue ambao umeshika kasi Dar es Salaam. (J M)
Pia, Dk Kebwe amewagiza viongozi wa mkoa huo kukutana na viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Kanda ya Ziwa, kuanza mara moja kupulizia dawa kwenye mabasi yanayoingia na kutoka mkoani hapa.
Akifungua mpango wa uzazi kwa kutumia nyota ya kijani mkoani hapa jana, Dk Kabwe alisema kutokana ugonjwa wa Dengue kusambaa kwa kasi Dar es Salaam, Serikali imedhamiria kuhakikisha ugonjwa huo hauinei mikoa mingine. Alisema wameanza kutoa elimu na kuwagiza viongozi wa Serikali za mikoa kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kwenye mikoa yao.
“Nimekuja Mwanza kwa lengo la kuhakikisha tunapambana na ugonjwa wa Dengue, Dar es Salaam tumeanza kwa kupulizia dawa kwenye magari ya abiria na mitaa mbalimbali, naomba vingozi wa hapa mkutane na Sumatra na kwamba mara moja utaratibu huo uanze,”alisema Dk Kebwe na kuongeza:
“Kesho (leo) mkutane na kuanza kuweka mkikakti hiyo, naomba agizo hili lizingatiwe kuhakikisha ugonjwa huu hausambai Kanda ya Ziwa,”alisema.
Dk Kebwe alisema ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya Aedes mosquito, ambao hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus.
“Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo, naomba wananchi mjikinge kwa kuvaa nguo ndefu, kufukia mashiomo ya majitaka na utunzaji mazingira, Serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa huo hausambia maeneo mengine ya nchi,”alisema.
Dk Kebwe aliwataka wakazi wa Mkoa wa Mwanza kutumia njia za uzazi wa mpango, kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na kutozingatia uzazi wa mpango.
Dk Kebwe alisema wametenga Sh3 bilioni kwa ajili ya kuboresha masuala ya uzazi wa mpango, lengo likiwa ni kuhakikisha wanapunguza vifo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga alisema takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kati vizazi hai 100,000, wanaofariki kwa matatizo ya uzazi ni 454. CHANZO MWANANCHI

BOSI WA UDA KUJIELEZA BUNGENI

udapress f5f67
Mgogoro wa uwekezaji katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salama (Uda) umechukua sura mpya baada ya Bunge kuamua Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika hilo, Robert Kisena ahojiwe na Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kutokana na kuingilia kati madaraka hayo.
Agizo hilo lilitolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alitaka tuhuma zilizotolewa na Kisena dhidi ya Bunge na wabunge zijadiliwe kwa sababu ameingilia uhuru na kinga za Bunge kwa kuzungumza nje ya Bunge masuala ambayo yametolewa maelezo na Serikali bungeni.
Hoja ya Mnyika ilitokana na taarifa za baadhi ya magazeti yaliyotolewa Mei 19, mwaka huu yakimnukuu Kisena akisema kuwa wabunge wa Dar es Salaam wamehongwa na mfanyabiashara mmoja na kwamba kampuni yake inamiliki hisa nyingi tofauti na majibu ya Serikali bungeni.
Akinukuu majibu ya Serikali katika swali lililoulizwa na Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, Mnyika alisema kuwa Serikali ililieleza Bunge kuwa mgawanyo halali wa hisa za Uda upo kama ulivyosajiliwa kwa msajili wa mashirika ya umma, kwamba shirika hilo linamilikiwa na Serikali na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika kujenga hoja yake Mnyika alisema majibu hayo yalionyesha kuwa Uda ni Shirika la Umma, jambo ambalo lilipingwa na Kisena kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, akisema Uda inamilikiwa na kampuni yake kwa asilimia 76.
Alisema kuwa mwekezaji huyo ameingilia haki, kinga na madaraka ya Bunge kinyume na utaratibu na kuanza kuwatuhumu wabunge ambao walisema ukweli ndani ya Bunge.
Mnyika alisema uhuru wa Bunge wa mawazo umehojiwa nje ya Bunge kinyume cha kanuni, kinga na haki za Bunge jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Bunge.
"Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja na wabunge wenzangu naomba waniunge mkono ili jambo hili liweze kujadiliwa ili Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge imuite na ahojiwe kikamilifu," alisema Mnyika.
Baada ya hoja hiyo, wabunge wengi walisimama kwa pande zote bila ya kujali itikadi zao za vyama wakiongozwa na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hata hivyo, Spika Makinda alisimama na kuwataka waketi, ndipo akatangaza kuwa suala hilo haliwezi kujadiliwa bungeni, bali kamati husika itamuita Kisena na kumhoji.
Kisena hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na hata alipopigiwa, simu yake iliita bila ya kupokewa na alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakujibu
CHANZO MWANANCHI.

 

JE SARATANI YA TEZI-KIBOFU 'MARADHI YA ZINAA?

140411154927 prostate cancer 512x288 spl nocredit 9f382
                                                                                    Celi za Saratani ya Tezi Kibofu
Na Hudugu Ng'amilo
Huenda Saratani ya Tezi-Kibofu ni ugonjwa wa Zinaa unaosababishwa na ugonjwa wa zinaa ambao dalili zake sio wazi sana.
Hii ni kwa mujibu wa wanasanyansi nchini Marekani. Wanasema kwamba Saratani hiyo husababishwa na maradhi fulani ambayo huenezwa wakati wa kitendo cha ngono.
Lakini wataalamu wanasema kuwa ushahidi bado haupo kama kweli Saratani hiyo ni moja ya magonjwa ya zinaa na inasababishwa na magonjwa ya zinaa.
Ingawa baadhi ya Saratani husababishwa na maradhi fulani fulani, kitengo cha utafiti wa Saratani nchini Uingereza kinasema kuwa ni mapema mno kuongeza Saratani ya tezi kibofu kwa Saratani hizo.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo walichunguza celi za tezi kifobu cha binadamu katika maabara.
Waligundua kuwa maradhi ya zinaa yaitwayo, 'Trichomoniasis' yalichochea ongezeko la Saratani hiyo.

Hata hivyo mfumo wa maisha pia unachangia ongezezeko la visa vya magonjwa ya Saratani.
Ugonjwa wa 'Trichomoniasis' unaaminika kuwaathiri watu milioni 275 duniani na moja ya maradhi maarufu ya Zinaa ambayo hayasababishwi na Virusi
'Dalili za Trichomoniasis'
130316102845 prostate cancer damages sex life 304x171 bbc nocredit f0700
                                                  Seli zilizoambukizwa Saratani
Kawaida, mtu hatapata dalili za ugonjwa huo na inawezekana asijue kama anaugua ugonjwa huo.
Wanaume huhisi kujikuna sana ndani ya uume wao , kupata hisia za jotokali la mkojo wakati wanapokwenda haja ndogo au kuvuja majimaji meupe kutoka kwa uume wao.
Wanawake pia wana hisia tu sawa na hizo katika sehemu zao za isiri pamoja na kuwa na harufu mbaya.
Utafiti huu wa hivi karibuni sio wa kwanza kuhusisha ugonjwa wa 'Trichomoniasis' na Saratani ya Tezi kibofu.
Utafiti uliofanywa mwaka 2009 ulipata kuwa robo ya wanaume walio na Saratani hio walikuwa na dalili za ugonjwa wa Trichomoniasis na wanaume hawa pia walikuwa na uvimbe ambao ulikuwa umekomaa mno.
'Hoja ya Uchunguzi zaidi'
Uchunguzi huo pia unaonyesha njia ambazo ugonjwa huo wa zinaa unawaweka wanaume katika hatari ya kupata Saratani ya tezi kibofu.
Profesa Patricia Johnson na watafiti wenzake, waligundua kuwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa 'Trichomonas vaginalis' - huvuja proteni ambayo husababisha Saratani ya Tezi Kibofu kuzuka.
Mtaalamu wa afya, Nicola Smith,anasema uchunguzi huu unaonyesha tu njia ambazo ugonjwa wa zinaa wa Trichomonas vaginalis unazidisha uwezo wa mtu kuugua Saratani ya Tezi Kibofu na kuchochea seli kukuwa kwa kasi.
"Lakini uchunguzi huu ulifanywa tu katika maabara na matokeo ya awali kwa wagonjwa yalikosa kuonyesha uhusiano kati ya ugonjwa huo na Saratani ya Tezi Kibofu,'' alisema Bi Nicola
Kwa kauli hii wanasema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika ili kuabini hasa kinacho sababisha Saratani ya Tezi kibofu kwani ugonjwa wa Trichomoniasis husababisha tu mazinigira kwa ugonjwa huo kukomaa ila sio chanzo cha ugonjwa wenyewe.
CHANZO BBC

RAIS MASKINI ZAIDI DUNIANI.UNAMFAHAMU? 

140520140730 rais na papa 512x288 bbc nocredit 1470b
                             Rais Jose Mujica akiwa na Papa Francis.
Na Hudugu Ng'amilo
Sifa kwa wanasiasa kokote duniani ni nadra, hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu wamemmiminia sifa Rais wa Uruguay baadhi wakitamani kama marais wao wangekuwa kama Rais Jose Mujica wa Uruguay.
Kwenye Twitter kuna zaidi ya ujumbe laki moja wa watu nchini Uhispania wakitamani kama waziri mkuu wao angekuwa kama Rais Maskini zaidi duniani Jose Mujica wa Uruguay.

Rais huyo anasifika kwa kuendesha gari kuu kuu , kuishi maisha ya watu wa kawaida na sehemu kubwa ya mshahara wake yeye hupatia mashirika ya misaaada ya kibinadamu...kiasi kwamba anajulikana kama Rais masikini zaidi duniani.
140520140624 uruguay president 512x288 bbc nocredit b7033
      Rais Mujica (Kushoto) na waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy (Kulia)
Na ndio maana waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy huenda asifurahie sana kufananishwa na Rais wa Uruguay.
Lakini swali ni watu wangapi duniani wanaweza kufananisha Rais Uruguay na marais wao? Ni Marais wangapi duniani wanatoa mishahara yao kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu, kuishi maisha ya kawaida na kuendesha gari lililochoka?
Baadhi ya wananchi wanahoji kwa nini nchi kama Uruguay ambayo haina uchumi mkubwa ina huduma bora zaidi kwa jamii kuliko Hispania ambayo imekomaa kiuchumi wakati rais wake hana uchu wa madaraka na tamaa ya pesa?
Mitandao ya kijamii hutumiwa sana kwa mijadala kama hii. Swali ni je nani ana jambo zuri la kusema kumhusu Rais wake hasa katika hizi nchi zetu za Afrika? Unadhani kiongozi yupi barani Afrika anaweza kufananishwa na huyu Rais wa Uruguay? Je kuna Rais asiyeishi maisha ya kifahari enzi hizi?
CHANZO BBC

 

Monday, May 19, 2014

SHERIA YA KIJESHI YATANGAZWA THAILAND 

1_d2b40.jpg
Jeshi la Thailand limetangaza kuweka sheria za kijeshi katika juhudi za kurejesha utulivu wakati nchi hiyo imekumbwa na mzozo wa kisiasa kwa muda.
Jeshi hilo pia limejitwika nguvu nyingi zaidi ili kuweza kutekeleza sheria hiyo.
Hata hivyo Jeshi hilo, ambalo lilinyakua mamlaka mnamo mwaka wa 2006 limesema kuwa hatua yake sio mapinduzi bali ni hatua ya kudhibiti usalama wa taifa.
Sheria hiyo ya kijeshi imekuja kufuatia mvutano wa muda mrefu wa kisiasa kati ya serikali na upinzani.
Bado tuko uongozini
Mshauri mkuu wa masuala ya usalama kwa kaimu waziri mkuu, amesema kuwa hawakushauriwa juu ya hatua hiyo.
Bwana Paradorn Pattanatabut amesisitiza kuwa kila kitu kinaendelea kama kawaida isipokuwa tu jeshi limedhibiti masuala yote ya usalama nchini humo.
Wanajeshi wameshika doria katika sehemu muhimu za nchi ikiwemo eneo ambapo wafuasi wa serikali wamekuwa wakiandamana nje kidogo ya mji mkuu Bangkok.
Tunataka demokrasia
Wafuasi hao wa serikali wamesema kuwa wataendelea na maandamano yao hadi utawala wa kidemokrasia utakaporejeshwa. Misuko suko imemzonga waziri mkuu huyo wa Thailand kwa muda huku akiamrishwa na mahakama ajiuzulu.
Upinzani pia umekuwa ukisisitiza kuwa unataka uongozi wa nchi ukabidhiwe kwa bodi ya usimamizi ambayo haikuchaguliwa kidemokrasia, ambayo kwa sasa inasimamia masuala ya marekebisho ya katiba.(P.T)

VAN GAAL MENEJA MPYA WA MAN UNITED

270px-Louis-van-gaal2 38e0f
Na Hudugu Ng'amilo
Situation actuelle
Équipe Pays-Bas
Biographie
Nom Aloysius Paulus Maria van Gaal
Nationalité Pays-Bas
Naissance 8 août 1951 (62 ans)
Lieu Amsterdam (Pays-Bas)
Poste milieu de terrain, entraîneur
Parcours professionnel 1
Saisons Club M. (B.)
1971-1973 Ajax Amsterdam 10 (9)
1973-1977 Royal Antwerp FC 43 (7)
1977-1978 Stormvogels Telstar 25 (1)
1978-1986 Sparta Rotterdam 248 (28)
1986-1987 AZ Alkmaar 17 (0)
Équipes entraînées
Années Équipe Stats
1986-1988 AZ Alkmaar (adjoint)
1988-1991 Ajax Amsterdam (adjoint)
1991-1997 Ajax Amsterdam
1997-2000 FC Barcelone
2000-2002 Pays-Bas (sélectionneur) 8v 2n 2d
2002-2003 FC Barcelone
2003-2004 Ajax Amsterdam (directeur technique)
2005-2009 AZ Alkmaar
2009-2011 Bayern Munich 56v 19n 16d
2012-2014 Pays-Bas 11v 7n 2d
2014- Manchester United....

WANAWAKE WATAKA MAPADRE WARUHUSIWE KUOA

 140427093717 francis pope 304x171 gettyimages nocredit 23e21

Na Hudugu Ng'amilo
Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.
Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa ujane,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.

CHANZO BBC

Sunday, May 18, 2014

Mafuriko sio Dar tu, yamewakuta na ndugu zetu wa Serbia, Bosnia na Austria.

Screen Shot 2014-05-19 at 5.12.50 AM
Bado Dar es salaam na mikoa jirani haijasahau kilichotokea wiki chache zilizopita baada ya mvua iliyopitiliza kunyesha mfululizo kwa siku kadhaa na kusababisha vifo, majeruhi na wengine kukosa makazi kwa muda.
Hizi ni picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Euro News za kilichowakuta ndugu zetu wa Serbia, Bosnia na Austria ambapo kwenye sehemu kama Bosnia imebidi zitumike Helikopta kuokoa watu waliokua wamesimama juu ya nyumba zao baada ya maji kuzidi.
Wanasema katika eneo hilo maafuriko haya ni ya kipekee kuwahi kutokea ndani ya kipindi cha miaka mia moja na ishirini ambapo yamesababisha zaidi ya nyumba laki tatu kukosa umeme huku vifo vikizidi kuongezeka na kufikia 37 huko Serbia kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Screen Shot 2014-05-19 at 5.06.01 AM
Kwa sasa kazi inafanywa na Wanajeshi, Polisi na vikosi vingine vya uokoaji kwenye sehemu ambayo imeathirika na bado watu wamo.
Screen Shot 2014-05-19 at 5.41.55 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.05.50 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.06.28 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.07.58 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.09.46 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.10.16 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.11.38 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.11.57 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.12.50 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 5.13.15 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 4.31.07 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 4.31.20 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 4.31.40 AM
Unaweza kutazama hii video hapa chini ili kuona zaidi.