TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, April 29, 2014

Taarifa ya Kamanda Kova juu ya watoto waliofariki wakiwa wanaogelea ndani ya Swimming Pool.

sw
April 27  kulitokea vifo vya watoto 3 ambao walikua na birthday party nyumbani lakini baada ya kukamilika kwa taratibu za party ya nyumbani waliamua kuimalizia party hiyo hotel ya Landmark,walipofika walienda kuogelea kwenye swimming pool ya watoto lakini baadae watoto hao walitoka kwenye pool ile ya watoto wakaingia kwenye pool ya wakubwa na kwa bahati mbaya waliingia sehemu yenye kina kirefu.
Watoto wenzao walipoona wenzao wanazama walianza kuwavuta kuwatoa nje lakini hali zao tayari zilikua mbaya,mmoja wapo hali yake ilikua kidogo afadhari lakini kwa bahati mbaya nayeye alifia hospital wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Masana na kufanya Idadi ya watoto waliofariki kuwa 3 majina yao ni Janet Zacharia,Eva na Ndimbuni.
Kamanda Kova amesema>>’Kusema kweli sio mara ya kwanza kutokea,mara nyingi vifo vya watoto vinatokana na uangalifu au uzembe kutoka kwa wale wanaotakiwa kuwaangalia hao watoto wao,hizi hotel zote zenye swimming pool lile eneo la kuogelewa basi wasiruhusiwe watoto wadogo kuogelea au kuwe na mtu ambaye anajua kuogelea au kuokoa ambaye yupo pale’
‘Unajua watoto wana tabia ya kuigana mmoja akiingia akiogelea pengine anafahamu kidogo wengine wote wanafata mkumbo wanaona wanaweza,sisi kama jeshi la Polisi tumeamua hili kosa la uzembe kusababaisha kifo kisheria mtu anaweza kushtakiwa kwa kuzembea kwa kutochukua tahadhari mpaka watoto kama wale ambao hawana hatia uwezo wao mdogo wa kufikiri au kuijiokoa’
‘Tunafatilia kwa umakini lakini jukumu la kufatilia maisha ya watoto ni la wazazi mia kwa mia wasipofanya hivi wakiwa hawapo makini matokeo yake ni haya watoto 3 wamefariki,tunaendelea na uchunguzi na baadae tutatoa taarifa kamili’.

Cheki picha 11 za wanamichezo maarufu enzi zao wakiwa watoto

0
Wengi kati yao sura zao hazijabadirika sana tangu kipindi chao cha utotoni lakini picha hizi zitakuonyesha kwamba wanamichezo hawa wameanza kucheza michezo yao tangu wakiwa watoto.
Kwenye picha hizi kuna watu kama Cristiano Ronaldo,Lebron James,Lewis Hamilton,Tiger Woods,Michael Owen na wengine.
1 
Neymar
2 
David Beckham
3 
Michael Owen
4 
Lewis Hamilton
5 
Diego Maradona
6 
Messi
7 
Lebron James
8 
Tiger Woods
9 
Serena na Venus Williams
10 
Cristiano Ronaldo

Zaidi ya milioni 300 zimemtoka Peter wa P Square kununua gari hili jipya Bentley GT 2014

p spuare
Baada ya kumaliza matatizo yao kwenye familia na ndugu zake ambayo bado hayajajulikana kama yalikuwa ni kweli au ni stunt za biashara yao kwenye muziki, Peter amewaonyesha fans wake gari lake jipya lilimtoa zaidi ya milioni 300 kwenye pesa za kitanzania.
Peter na ndugu zake wawili ilisemakana kwamba hawakuwa kwenye maelewano mazuri kwa kipindi kifupi na baadae wote watatu wali-tweet maneno ambayo yaliashiria kwamba wamemaliza tofauti zao.
Cheki picha mbili za ndiga hiyo mpya ya pacha Peter Okoye.
p spuare2
p spuare3

Ukraine; Warusi zaidi wawekewa vikwazo 

140426122158_ukraine_512x288_ap_nocredit_6e081.jpg

Marekani imetoa taarifa kuhusu vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi na kuushutumu utawala wa Moscow kwa kushindwa kutimiza mkataba wa kimataifa uliolenga kusuluhisha mzozo wa Ukraine.
Vikwazo hivyo vimelenga washirika wa Karibu wa Rais wa Urusi Vladmir Putin na vimeongeza orodha ya vikwazo vilivyowekwa hapo awali kwa baadhi ya maafisa wa nchi hiyo baada ya Moscow kutwaa eneo la Crimea mwezi uliopita.
Miongoni mwa waliolengwa ni mmoja wa wanasiasa maarufu nchini Urusi Igor Sechinambaye wakati mmoja alikuwa afisa wa ujasusi na sasa ni afisa mkuu katika kampuni ya mafuta ya Rosneft ambayo kwa kiwango kikubwa inadhibitiwa na serikali.
Karibu asilimia sitini ya kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya uingeza BP na thamani ya hisa za kampuni hiyo ilishuka punde tu baada ya taarifa kuhusu vikwazo hivyo kutolewa.
Wengine waliolengwa ni Alexei Pushkov, ambaye huongoza kamati ya mambo ya nje katika bunge la Urusi,Naibu waziri mkuu na kampuni kumi na saba za Urusi.
Akizungumza hapo awali Rais Putin alisisitiza kuwa Ukraine haitaathirika kiuchumi kutokana na vikwazo hivyo.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema nia ya Marekani sio kumlenga moja kwa Rais Putin lakini ni katika juhudi za kuishawishi Urusi kufuata mwelekeo unaofaa.
Muungano wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vya usafiri na kuzuiliwa kwa mali dhidi ya watu 15 nchini Urusi lakini majina yao bado hayajatajwa.CHANZO BBC

Mazungumzo ya amani Mashariki ya kati 

140113100156_wall_israeli_palestine_512x288_bbc_nocredit_a40b9.jpg

Muda wa mwisho uliowekwa na Marekani wa mpango wa mashariki ya kati umemalizika.
Mchakato huo unaonekana kugonga mwamba .
Israeli na Palestina wamekataa kuendelea na mazungumzo zaidi.
Mazungumzo yao yalivunjika pale Israeli ilipoukataa mpango wa amani baina ya makundi makuu mawili ya Wapalestina wa kuunda serikali ya Umoja na hasira ya wapalestina kutokana na ujenzi wa Israeli wa makazi mapya katika
maeneo ynayokaliwa .
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amekasirishwa na kitendo cha Israeli kuendelea kujenga maakazi ya Wayahudi na Palestina kupendelea kuunda serikali ya umoja na kundi la Hamas.
Hatahivyo haja kubali kushindwa anatumia maneno kama ''kusitishwa kwa muda kwa harakati za kutafuta amani''.
Kuna uwezekano kuwa huenda Marekani itafuatilia kwa karibu yanayoendelea huku ikishinikiza kurejelewa kwa mchakato wa kutafuta Amani.
Hatahivyo baadhi ya washirika wa Marekani katika mazungumzo hayo wanamasema kuwa muda wa kuleta Amani umekwisha.
Viongozi wa nchi za Ulaya na matiafa ya Kiarabu wameunga mkono juhudi za John Kerry katika kujaribu kulitafutia suluhu tatizo la Israil na Palestina na kushikilia msimamo kwamba Marekani ndio taifa pekee lenye uwezo mkubwa wa kufanikisha mchakato.CHANZO BBC

Monday, April 28, 2014

Hizi ndizo picha za Jeshi la Wananchi Tanzania zilizoleta stori mtaani.

8
Inawezekana raia wengi wa Tanzania tulikua hatujui nguvu ya jeshi letu la Wananchi,vifaa vyake pamoja na matumizi ya vifaa hivyo hasa inapotakiwa kuvitumia,April 26 Tanzania tulikua tukitimiza miaka 50 ya Muungano wetu kati ya Zanzibar na Tanganyika na kuzaliwa kwa Tanzania.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilivyovuta hisia za wengi ni namna vifaa vya Jeshi la Wananchi vilivyokuwa vikipita huku MC akitoa maelezo ya kila kimoja,hizi ni baadhi ya picha za vifaa hivyo vya JWTZ.
12
10
9
7
2
3
4
5
6
1

Ajari ya meli yasababisha waziri mkuu ajiuzulu cheo chake.

waziri
Baada ya ajali ya meli huko South Korea serikali ilikosolewa kwa jinsi ilivyodili na ajali hiyo. Meli hiyo ilivyozama sehemu kubwa ya abiria walikuwa ni wanafunzi na watu kama 100 hawakupatikana.
Kwenye hatua za ukoaji zilitumika meli 34 na helicopter 18 na njia nyingine lakini pia ukosoaji kwa serikali ulikuwepo. Kutokana na hilo waziri mkuu Chung Hong-won ametangaza kujiuzulu baada ya wananchi kutoridhishwa na utendaji wa serikali kwenye hili tatizo.
Chung Hong-won aliwahi kuzomewa na kurushiwa chupa za maji wakati alipotembelea waathirika wa ajali hiyo.
323

Hukumu ya Muslim Brotherhood kutolewa 


Mahakama moja katika mji wa Minya leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa mwezi uliopita kwa wafuasi 529 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo sasa limepigwa marufuku nchini humo.
Kesi hiyo ilizua shutuma kali kutoka jamii ya kimataifa.
Watu hao walipatikana na hatia ya kumuua afisa mmoja wa polisi katika rabsha zilizozuka mwezi Agosti mwaka uliopita.
Watu hao walihukumiwa kifo kwa mara ya kwanza mwezi Machi baada ya kesi kufanyika kwa takriban saa moja.
Mawakili wa utetezi walinyimwa fursa ya kujieleza na hata mashtaka hayakutangazwa.
Baadaye kesi hiyo iliwasilishwa mbele ya mmoja ya viongozi wakuu wa kidini ili kuamuliwa tena lakini maoni yake hayakuzingatiwa.
Miongoni mwa waliohukumiwa kunyongwa ni vijana wawili wenye umri wa miaka 17, mtu mmoja mlemavu na wakili aliyewakilisha baadhi ya
washukiwa hadi alipokamatwa.
Mawakili wa washtakiwa wamesema watakata rufaa iwapo mahakama itapitisha hukumu zilizotolewa.
Baadhi ya wataalam wa maswala ya sheria wametabiri kuwa huenda kesi dhidi ya waku hao ikasikizwa tena.
Mahakama pia inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ya pili dhidi ya watu 700 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood
baadhi wakikabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika machafuko.
CHANZO MWANANCHI

PAPA WAWILI WATANGAZWA WATAKATIFU  Norman Hinog Bantug "Most glorious God, we give you profound thanks for the holy lives of Pope John XXIII and Pope John Paul II. As the world more deeply embraced the darkness of this age, you sent these two courageous men to bear light to your people and renew the joy of the Gospel in their hearts. By the faithful example of these two shepherds and the power of your Holy Spirit, may we persevere in spreading the love of Christ to everyone we meet. We rejoice with all of heaven as your servants are now crowned with the glory of sainthood and we long for the day when we may see you, our God, face to face. All glory be to the Father, the Son and the Holy Spirit both now and forever. Amen.

RAIS KIKWETE AONANA NA RAIS MSTAAFU WA NAMIBIA MHE SAM NUJOMA

sam_3_5410f.jpg
nujoma_f24a2.jpg
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtembezea sehemu mbalimbali za Ikulu na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma aliyemtembelea  hivi karibuni. Mhe Nujoma alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru tarehe 26 Aprili, 2014. (FS)

Sunday, April 27, 2014

KAMATI YA MAADILI NA HAKI YAKWAMA KUMUHUKUMU WENJE

WENJE 7c351
Na Hudugu Ng'amilo
Hukumu dhidi ya mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ezekiah Wenje imekwama kutolewa jana baada ya mjumbe huyo kushindwa kupatikana ili kuwasilisha utetezi wake.
Wenje anadaiwa kuwatuhumu mawaziri wanne akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kutoa rushwa kwa wajumbe wa kundi la 201, ili wapitishe kura ya wazi na kuunga mkono serikali mbili.
Viongozi wengine waliohusishwa na tuhuma hizo ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta aliamua kulipeleka shauri kwenye kamati ya maadili na haki za Bunge, baada ya Wenje kukataa kufuta kauli yake na kuwaomba radhi wajumbe hao.
Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni jana kwa niaba ya mwenyekiti, Pandu Ameir Kificho, makamu mwenyekiti, Dk Susan Kolimba alisema jitihada za kumtafuta Wenje bado zinaendelea.
Hata hivyo Dk Kolimba alisema kamati yake imefanikiwa kuwahoji Dk Kawambwa na Kabaka pamoja na wajumbe wawili kutoka kundi la 201 waliolalamika, Esther Mlimba na Dk Eve Semakafu.
"Mwenyekiti alipomtaka kuomba radhi alisema anaweza kuomba radhi kwa msingi tu kwamba ukweli aliousema umewaudhi watu, hivyo anaomba radhi kwa ukweli aliousema," alisema Dk Kolimba.
Alisema baada ya Wenje kutopatikana, kamati hiyo iliona ni busara kuwasikiliza mawaziri waliotuhumiwa pamoja na wale waliolalamikia kauli hiyo ya Wenje ambao ni Semakafu na Mlimba.
"Jitihada za kumtafuta Maghembe zilishindikana...Tunatarajia baada ya Wenje kufika mbele ya kamati tutawasilisha mapendekezo yetu mbele ya Bunge hili,"alisema Dk Kolimba.
Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, Sitta alisema suala hilo litaamuliwa hapo baadaye baada ya kamati hiyo kukamilisha kazi yake ikiwamo kumhoji Wenje na wengine waliotuhumiwa.
:Chanzo Mwananchi.

WARIOBA ATUNUKIWA NISHANI ILIYOTUKUKA

unnamed19 1e6c5
Na Hudugu Ng'amilo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba juzi usiku alikuwa miongoni mwa viongozi na watu mashuhuri waliotunukiwa nishani na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika maelezo ya kutoa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la kwanza, ilielezwa kuwa Jaji Warioba, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuenzi na bado anauenzi Muungano huo.
"Katika kipindi chako, pamoja na nyadhifa nyingine, ulikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...katika kipindi hicho na hadi sasa umeendelea kuwa mwaminifu, umeutunza, umeulinda na umeuenzi Muungano," ilisema sehemu ya taarifa ya kutoa nishani.
Hivi karibuni, Jaji Warioba amekuwa akishambuliwa na baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba, pia baadhi ya wana CCM kutokana na Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza, kupendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu.
Hata hivyo, upande mwingine wajumbe wanaojitambulisha kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamekuwa wakiunga mkono mapendekezo ya rasimu hiyo.
Mbali na Jaji Warioba, wengine waliopewa nishani katika daraja hilo ni Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Aman Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk Salmin Amour Juma.
Wengine ni Omar Ali Juma na Idrissa Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.
Walioanza kupata tuzo na nishani hizo ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume(wote ni marehemu) na walioendeleza ambao ni Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
Wengine waliopewa tuzo ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama akiwemo Mkuu wa Jenshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa akiwemo, Jenerali Mirisho Sarakikya, Jenerali David Musuguri.
Katika nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne lilikuwa na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano.Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.
Wasifu
Mwenyewe Joseph Warioba aliingia serikalini mwaka 1966, akiwa mwanasheria wa mji wa Dar er Salaam, nafasi aliyoitumikia kwa muda wa miaka miwili, kisha kuhamia kuwa mwanasheria wa Baraza la Jiji mpaka mwaka 1970.
Kuanzia mwaka 1976 mpaka 1983 Warioba alitumikia taifa kwa wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Warioba pia aliwahi kuwa Waziri wa Sheria katika awamu ya kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere.
Mwaka 1984 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 1990.
Mwaka 1996 Rais Benjamin Mkapa alimteua kuongoza tume ya kupambana na rushwa.
Mwaka 2007 alioongoza jopo la waangalizi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola katika uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Nigeria.
Mwaka 2012 Rais wa awamu ya nne alimteua Warioba kuongoza Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
CHANZO MWANANCHI

Thursday, April 24, 2014

Uamsho: wamtaka Lukuvi athibitishe kauli yake

Khamis-Yusuf-Khamis-April25-2014 57014
Na Hudugu Ng'amilo.
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), maarufu kama Uamsho imemjia juu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ikimtaka athibitishe kauli yake ya kuwahusisha na Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na vitendo vya uhalifu visiwani humo.
Uhalifu ambao Lukuvi anadaiwa kuihusisha Uamsho ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kanisani, ni pamoja na kuuawa kwa padri, kuchoma makanisa na uharibifu wa miundombinu Zanzibar.
Kutokana na hali hiyo, Uamsho wamemwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kumtaka ambane Lukuvi athibitishe tuhuma hizo, vinginevyo watatumia sheria kumchukulia hatua.
Nakala ya barua hiyo, ambayo imeambatanishwa na nakala ya DVD inayoonyesha kauli zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi wa kidini uliofanywa na Lukuvi, imepelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete; Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein; Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Spika wa Baraza la Wawakilishi na wawakilishi wote.
Nakala ya barua hiyo pia imepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Amiri wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Amiri wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar, Ofisi ya Mufti Zanzibar, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Jumaza), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Maimamu wote.
Pia imepelekwa kwa Waziri wa Mipango, Sera na Uratibu wa Bunge, Ofisi ya Spika wa Bunge, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Kamati ya Maridhiano Zanzibar, vyombo vya habari, Waislamu na wapenda amani wote Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa Uamsho, Sheikh Yusuph Hamis Yusuph, alitangaza tamko la jumuiya hiyo, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema wanapeleka nakala za DVD hiyo kwa Sitta ili awaonyeshe wajumbe wa Bunge hilo jinsi zinavyoonyesha uchochezi wa kidini uliofanywa na Lukuvi ndani ya kanisa na bungeni.
Pia jumuiya hiyo inadai kuwa Lukuvi amekuwa ikidai sera za Uamsho ni sera za chama cha CUF na pia wanapenda sana kufanya vurugu.
Alisema wamelazimika kufunga safari kutoka Zanzibari kwenda Dar es Salaam kuzungumza na waandishi wa habari kutokana na kuchoshwa na maneno, ambayo yamekuwa yakitolewa na Lukuvi katika Bunge hilo dhidi ya Uamsho.
"Lukuvi alitakiwa kuzungumzia jinsi katiba mpya itakavyopatikana na siyo kuzungumzia maneno ambayo hana ushahidi nayo juu ya Uamsho," alisema Sheikh Yusuph.
Alisema kutokana na kitendo cha Lukuvi kuuzungumza maneno machafu na ya uchochezi dhidi ya Uamsho bungeni, wanamuomba Sitta atumie nafasi aliyonayo amwamuru atoe ushahidi wowote anaoujua juu ya jumuiya hiyo.
Sheikh Yusuph alisema kama Lukuvi atashindwa kufanya hivyo, watawasiliana na wanasheria na hatua dhidi yake zitafuatwa.
Alisema pia wanataka kujua kauli ya serikali juu ya kauli ya Lukuvi aliyoitoa katika Kanisa la Methodist Jimbo la Dodoma kuwa iwapo serikali tatu zitakuwapo nchi itachukuliwa na wanajeshi, pia makanisa yote nchini yatafungwa na nchi itakosa amani.
Lukuvi alitoa kauli hiyo katika kanisa hilo wakati wa sherehe za kumtawaza Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu.
Sheikh Yusuph pia alisema Lukuvi hakuishia hapo, bali alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa wanaotaka nchi yao Wazanzibari hawawezi kujitegemea, bali wanataka serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa nchi ya Kiislamu na kwamba, Uamsho ni taasisi ya Waislamu wenye msimamo mkali.
"Sisi Jumuiya tuna amini hayo ni maoni ya serikali kwa vile yeye amekwenda kwa niaba ya waziri mkuu. Pia ni msemaji wa wizara na mpaka sasa serikali kwa nini imekaa kimya na hiyo inaonyesha kwamba, inaunga mkono ubaguzi wa dini aliouchochea Lukuvu," alisema.
Alisema mwaka 2004 Jumuiya hiyo ilituhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea Zanzibar, ikiwamo milipuko ya mabomu, kuchomwa makanisa, kuchomwa gari la polisi na kuharibiwa kwa miundombinu.
Sheikh Yusuph alisema kwa matukio hayo, ziliundwa tume mbili kwa ajili ya uchunguzi, lakini mpaka sasa ni miaka 10, matokeo ya uchunguzi huo bado hayajatolewa.
Alisema Uamsho inasikitishwa sana pale viongozi wa dini ya Kiislamu wanapozungumza masuala ya kijamii na kisiasa wanaonekana wametekeleza katiba na uhuru wao wa kujieleza.
Lakini akasema kwa bahati mbaya inapotokea kwa viongozi wa Kiislamu kutoa maoni yao juu ya mambo hayo, hutokea baadhi ya viongozi wa serikali kuwalaumu na kuwatuhumu juu ya uvunjifu wa amani, uchochezi, kuchanganya dini na siasa na kutaka kusababisha vurugu.
Alisema Watanzania wanatakiwa kujionea Lukuvi alivyokwenda kuchanganya dini na siasa kanisani.
Sheikh Yusuph alisema kibaya zaidi Lukuvi alileta uchochezi kati ya Waislamu na Wakristo na kutangaza wazi dhamira ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni uadui na kuukandamiza Uislamu na Waislamu.
Alisema Uamisho ni taasisi iliyosajiliwa kihalali na SMZ na kwamba, tangu ilipopata usajili, imekuwa ikifanya kazi zake kisheria na haijawahi kupatikana na hatia ya aina yoyote ya uvunjifu wa sheria.
Sheikh Yusuph alisema mbali na hayo, hata viongozi wa Uamsho hawajawahi kupatikana na hatia zaidi ya kufunguliwa kesi, ambazo hadi hazijathibitishwa.
CHANZO: NIPASHE

SIKU 67 ZA MIPASHO, MATUSI,BUNGE MAALUM LA KATIBA 

bunge 4c2f3
Na Hudugu Ng'amilo.
Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta "Mzee wa Kasi na Viwango" linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.
Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
"Mwenendo wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote za kuonyesha kungetokea matatizo ndani yake kutokana na mipasho ambayo ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha ambazo siyo za staha wakati wa kutengeneza kanuni," alisema Oluoch na kuongeza:
"Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha, mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni," alisema Olouch.
Hata hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha Bunge hilo kwa umakini mkubwa na kwamba kila anaposikia lugha chafu amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru kufuta kauli au kuomba radhi kwa matamshi. "Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo mojawapo ya mambo ambayo huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango inapotolewa na wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili, kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu," alisema Suluhu.
Alikiri kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi na kwamba masuala yao hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.
Matakwa ya Kanuni
Sehemu ya Tano ya Kanuni za Bunge Maalumu inatoa mwongozo wa mambo yanayokatazwa na yale yanayopaswa kufuatwa wakati wa mjadala.
Kanuni ya 46 imeorodhesha mambo yasiyoruhusiwa ambayo ni pamoja na kusema uongo, kutoa taarifa zisizokuwa za kweli, kuzungumza jambo lolote ambalo halipo kwenye mjadala na kutumia majina ya marais na waasisi wa Taifa kwa dhihaka.Pia inazuia matumizi ya lugha ya kuudhi, kubagua, kunyanyapaa au inayodhalilisha watu wengine, kuzomea, kupiga kelele za aina yoyote zinazoweza kuvuruga mjadala au mwenendo bora wa shughuli za Bunge hilo.
Licha ya makatazo hayo, wajumbe wamekuwa wakikiuka kanuni bila kuchukuliwa hatua na hali hiyo imekuwa chanzo cha mivutano, zomeazomea, kelele na mambo mengine hadi kundi la Ukawa kususia kikao wakieleza kutokuridhishwa na mwenendo wa Bunge.
Kuufyata na kuufyatua
Baadhi ya kauli tata zilizojitokeza ni pamoja na ile iliyotolewa na Asha Bakari Makame kwa mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kuwa anafanana na watu wenye mabusha nyuma ambao ndiyo huufyata.
Makame ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alikwenda mbali zaidi na kumwambia Jussa kuwa ana matatizo ya kiafya na si mwanamume kamili, kwani ameshindwa kuoa na hana watoto wakati ana umri mkubwa.
"Huyu Jussa anasema kwamba tumeufyata, hapa tuwekane sawa, maana ya kuufyata ni mtu kuwa na mabusha pale yanapokuwa nyuma ndiyo kuufyata kwa hiyo yeye ndiyo ameufyata, ana busha huyu," alisema Bakari.
Naye Profesa Ibrahim Lipumba alichafua hali ya hewa pale alipowafananisha wajumbe wa Bunge Maalumu na kundi la mauaji nchini Rwanda, Intarahamwe.
"Tumechoka kusikiliza matusi. "Tumechoka kudharau mawazo ya wananchi, tumechoka ubaguzi hatuwezi kuwa sehemu ya kundi la Intarahamwe linalohamasisha ubaguzi ndani ya Tanzania hili hatulikubali. Tunawaachia, watu wote tunaotaka Katiba ya wananchi tunawaachia Intarahamwe mwendelee na Bunge lenu."
Mjumbe mwingine ni Mwanakhamis Kassim Said aliyesema: "Mimi nilikuwa namwomba baba yangu mdogo Seif (Maalim Seif Sharif Hamad) awarejeshe watu wake humu (bungeni) kwa sababu mpira unachezwa huku ndani. Hatutakii mema humu, tena ana choyo na husuda. Namwomba baba mdogo atuache, alichokitaka amekipata, king'ora anazunguka saa 24 Dar es Salaam, Unguja. Mheshimiwa Mwenyekiti Baba mdogo kila mara yuko kwenye pipa (ndege) mara Uingereza, mara Canada mara wapi? Hicho ndicho anachokitaka amekipata."
Mjumbe mwingine, Mohamed Seif Khatibu alisema: "Nimejifunza kuwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani ni vinyonga. Lakini Maalim Seif ni kinyonga, wakipita kwenye mvua wanakuwa na rangi ya mvua, kwenye jua wanakuwa na rangi ya jua, baharini wanakuwa na rangi ya bahari."
Tuhuma za rushwa
Mjumbe Ezekiah Wenje alisema baadhi ya mawaziri wamewahonga wajumbe wa kundi la 201 ili waunge mkono msimamo wao, lakini alipotakiwa kufuta kauli hiyo alikataa na suala lake kufikishwa kwenye kamati ya kanuni.Kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku, wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha."
Kuingia msituni
Kapteni John Komba alitangaza kuingia msituni iwapo Bunge Maalumu la Katiba litapitisha muundo wa serikali tatu, huku akimshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na timu yake ni waasi kama Adamu na Eva waliomuasi Mungu kutokana na kile walichokifanya cha kupendekeza serikali tatu. Mwingine katika orodha ni Bernard Membe aliyesema, Tume ya Mzee Warioba itakuja kukumbukwa kwa kuratibu mauaji ya Muungano na Bunge nalo litakuja kulaaniwa kwa kubariki mauaji hayo.
Watoto wa shetani
Mjumbe Paul Makonda alisema: "Shetani alikuja duniani kuiharibu dunia, kuiangamiza na kuteketeza kila kilichostahili kuungana... watoto wake ni Mheshimiwa Jussa, watoto wake ni Mheshimiwa Mbowe, watoto wake ni Mheshimiwa Lipumba... Hawa ni watoto wa shetani".
Mwingine: Waride Bakari Jabu alisema: "Chiku Abwao mimi namshangaa sana anayesema bora Muungano uvunjike lakini Tanganyika iwepo. Tunafahamu asili yake mwenyewe ni Mkongo mumewe ndiye Mtanganyika, namwambia Muungano huu utakuwepo na utaendelea kuwapo."
Mjumbe Tundu Lissu alisema: "Tanganyika haikuuawa na makubaliano ya Muungano, bali iliuawa kwa amri za Nyerere.... Mwalimu Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote ya kikatiba ya kutunga amri na kuua Tanganyika."
Imeandikwa na Neville Meena, Daniel Mjema, Sharon Sauwa na Beatrice Moses
CHANZO MWANANCHI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Aprili 24, 2014

MKENYA OGWAYO KUCHEZESHA STARS, BURUNDI
Mwamuzi Anthony Ogwayo mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa keshokutwa (Aprili 26 mwaka huu)  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ogwayo katika mechi hiyo ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, atasaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya. Mwamuzi wa mezani atakuwa Israel Mujuni wa Tanzania.


Burundi inatarajia kuwasili nchini leo (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways na itafanya mazoezi kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza tangu kuanza kwa mpango wa maboresho wa timu hiyo.

Makocha wa timu zote mbili pamoja na manahodha wao kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mechi hiyo.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

KOCHA MPYA STARS KUTUA JUMAMOSI
Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.

Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


BONIFACE WAMBURA, OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) (FS)

WATU 4 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NAIROBI 

130923165553_sp_policial_quenia_304x171_afp_nocredit_2d623.jpg
Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi. Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."
Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.BBC SWAHILI

 

Full Time ya Real Madrid vs Bayern Munchen April 23 2014

Screen Shot 2014-04-23 at 10.11.40 PM
Full Time ya mechi hii ya UEFA Champions league leo imesomeka 1-0 ambapo Real ndio wamechukua ushindi wa hilo goli lililofungwa na Benzema kwenye dakika ya 19.
Hizi hapa chini ni baadhi ya rekodi ambazo zilitolewa na Sky sports kabla ya hii mechi ya leo.
Screen Shot 2014-04-23 at 11.30.35 PM
Screen Shot 2014-04-23 at 11.29.54 PM

Bomu jingine tena limelipuka Kenya na kuua

 Matukio ya kigaidi yamekua yakichukua vichwa vya habari mara nyingi nchini Kenya hasa baada ya nchi hiyo kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.

Saa tatu na nusu usiku wa April 23 2014 millardayo.com imepokea taarifa kutoka kwa ripota wake nchini humo Julius Kipkoitch kwamba bomu jingine limelipuka ndani ya gari karibu na kituo cha Polisi Nairobi.
Waziri wa mambo ya ndani amethibitisha kwa kusema Polisi wawili wamepoteza maisha kati ya watu wanne ambao wameuwawa huku hao wengine wawili wakihofiwa kuwa ni Mahabusu waliokuwemo kwenye gari hilo na Polisi.
Ripota Julius wa TZA anaendelea kufatilia zaidi kwa ajili ya kukufahamisha hapahapa kupitia

Hiki ndio kiasi cha fedha alicholipwa David Moyes baada ya kutimuliwa

article-2609490-1D411CD200000578-628_634x505
Siku moja baada ya kutimuliwa kutoka kwenye kibarua cha kuifundisha klabu ya Manchester United imefahamika kwamba kocha David Moyes atalipwa fidia kutokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wa miaka sita walioingia mwaka jana mwezi wa tano.
David Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na Manchester United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake na klabu hiyo.
Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele kinachoeleza ikiwa Manchester United ingefeli kufuzu kucheza Champions League msimu huu basi ikatokea United wakaamua kusitisha mkataba wake basi fidia isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.

Tuesday, April 22, 2014

Wakulima wa nyanya Iringa watakiwa kuunda vikundi 

nyanya_95bbb.jpg
Iringa. Wakulima wa nyanya mkoani Iringa, wameshauriwa kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na misaada mbalimbali pamoja na mikopo kutoka katika taasisi za fedha ikiwamo benki na vicoba ili kuinua thamani ya mazao wanayozalisha.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gelard Guninita wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Nyanya iliyofanyika katika Kijiji cha Nzih Tarafa ya Kalenga mkoani hapa.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Muunganisho wa Ujasilimali Vijijini (Muvi) kwa ushirikiano na wadau wa kilimo kutoka sekta binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa za taasisi hiyo, zao la nyanya katika mkoa huo limeongezeka kutoka tani 100,009 mwaka 2010 na kufikia tani 100,400 kwa kipindi cha mwaka 2013 katika maeneo ambayo taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Guninita, ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alisema ikiwa wakulima hao wataunda vikundi na kusajili, watakuwa wametambuliwa na kuwa na sifa za kupata mikopo katika taasisi za fedha jambo linaloweza kuwasaidia kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli zao. "Ninaomba mjiunge katika vikundi na sisi serikalini tunasaidia pale itakapoonekana kuna ulazima," alisema.(E.L)

Usalama wadhibitiwa Boston Marathon 

Maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushiriki mbio za Boston Marathon baadaye hii leo huku kukiwa na usalama wa hali ya juu.
Mbio hizo za kila mwaka zinafanyika baada ya mlipuko wa bomu kuwaua watu watatu na kuwajeruhi mamia wengine wakati wa mbio hizo mwaka jana.
Makundi ya Polisi kutoka majimbo mengi pamoja na wale waliovaa sare za raia wamepelekwa katika mkondo wa mbio hizo kuimarisha usalama.
Mashabiki nao pia watakaguliwa na wataruhusiwa kubeba tu mifuko ya plastiki inayoonyesha vitu walivyobeba.
Wanariadha elfu 36 watashiriki katika mbio hizo zaidi ya idadi ya kawaida iliyotarajiwa.
Wanariadha watakaa kimya kwa sekunde kadhaa katika mwanzo wa mbio hizo ili kuwakumbuka waathiriwa wa mkasa wa bomu.(P.T)

PUTIN ATAHADHARI KUHUSU UKRAINE

Rais wa Russia, Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin, amesema kuwa anatumai sana sana kwamba hatalazimika kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.
Katika kipindi chake cha kila wiki, Putin amekanusha madai kuwa Urusi ilihusika katika maandamano ambayo yanakumba Ukraine lakini akakiri kwamba kwa mara ya kwanza wanajeshi wa Urusi walioenekana katika jimbo la Crimea.
Mjini Geneva mashauriano yameanza kwa mara ya kwanza kati ya Marekani, Muungano wa Ulaya, Urusi na Ukraine katika juhudi za kupunguza uhasama Mashariki mwa Ukraine.
Mkutano huo, ambao ni wa kwanza kuhudhuriwa na makundi hayo manne kujadiliana hali ya Ukraine, unafanywa baada ya usiku wa mapigano makali.
Wizara ya mambo ya nje nchini Ukraine imesema watu watatu wanaounga mkono Urusi waliuawa walipojaribu kushambulia kambi moja ya jeshi katika mji wa Marioupol.
Wajumbe wanne wanaokutana Geneva wameafikiana kwa swala moja muhimu kwamba hali katika Ukraine Mashariki ni mbaya sana na lazima itulizwe.
Ili kutuliza hali hiyo, Marekani na Jumuiya ya Ulaya wametoa wito Urusi iwaondoe wanajeshi wake kutoka mipaka na Ukraine. Hadi kufikia sasa wameandaa vikwazo watakavyowekea Urusi iwapo haifanyi hivyo.
Kwa upande wake Urusi inasema watu wachache wanaoongea Kirusi Mashariki mwa Ukraine wanapaswa wanahitaji kupewa ulinzi. Huenda Urusi inachunguza ishara iwapo Ukraine iko tayari kutoa Uhuru kwa maeneo yaliyo Mashariki mwa taifa hilo.
Wakati huohuo Ukraine inataka hakikisho kuwa Crimea bado ni sehemu moja ya Ukraine. Mabalozi walio Geneva wana mengi ya kujadiliana ingawa mashauriano hayo ni ya masaa machache tu huku uhasama unaoendelea nchini Ukraine ukizidi kutokota.
BBC/SWAHILI

HOFU ILICHANGIA VIFO NDANI YA FERRY YA KOREA KUSINI 

Habari zilizotangazwa juu ya mawasiliano ya mwisho kati ya wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea Kusini na maafisa wa kudumisha usalama baharini zinaonyesha kuwa kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya mkasa huo, ambayo huenda ilichangia pakubwa vifo vya abiria wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya imetolewa jana alasiri wakati ambapo imethibitishwa kuwa maiti 62
zimepatikana kwenye mabaki ya feri hiyo, na kufanya idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufikia 58. Zaidi ya watu 240 hawajulikani waliko hivi sasa.
Jamii za watu ambao hawakuwa wamepatikana walifanya maombi ya Pasaka Jumapili katika chumba cha kufanyia mazoezi katika eneo la Jindo, ambako mamia ya watu wamekusanyika tangu feri hiyo kupinduka wakisubiri habari kuwahusu wapendwa wao.
Mama mmoja alisema kuwa watoto waliofariki walikuwa wakitunzwa vizuri.
"Naamini watoto hao wako mbinguni na Mwenyezi Mungu aliyefufuka. Naamini Naamini mimi," mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea kuzisaidia familia za walioathirika, alisema kuwa jamaa za watu wasiojulikana waliko wanapaswa kusikia kilichotokea kwa njia moja au nyingine.
"ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata miili yao haraka iwezekanavyo. Na iwapo kutatokea muujiza basi turejeshewe watoto hao upesi pia, alisema mfanyakazi huyo wa kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo walikuwa wanafunzi wa shule ya upili waliokuwa wakienda kwenye mojawapo wa kisiwa kubarizi. Hadi kufikia sasa kumekuwa kungali kuna ubishi mkubwa iwapo nahodha mwenyewe alikuwa ameshikilia sukani.
CHANZO: BBC/SWAHILI

Saturday, April 19, 2014

Mjumbe wa Iran azuiwa kungia Marekani 


140212215034_sp_barack_obama_signs_order_304x171_getty_2b1e4.jpg

Rais Obama ametia sahihi mswada unaomzuia balozi mteule wa Iran katika umoja wa mataifa kuchukua wadhfa wake mjini New York.
Ikulu ya whiteshouse tayari ilikuwa imetangaza kuwa mwanadiplomasia huyo mwenye uzoefu mkubwa Hamid Abutalebi,hatapewa Viza.
Bwana Abutalebi anashirikishwa na utekaji wa ubalozi wa Marekani nchini Iran mnamo mwaka 1979,ijapokuwa amesisitiza kuwa alikuwa mkalimani wa watekaji hao.
Iran imesema kuwa Marekani haiwezi kumzuia mjumbe wa umoja wa mataifa kutekeleza wajibu wake.
Bunge la Congress lilipitisha mswada huo ili kumzuia mtu yeyote anayashukiwa kujihusisha na upelelezi ama ugaidi dhidi ya Marekani ama mtu ambaye ni tishio kwa usalama wa taifa hilo.(BBC).

Wasichana 14 zaidi watoroka Boko Haram 

 140307165520_nigeria_military_640x360_bbc_nocredit_7c518.jpg

Kamishna wa elimu katika jimbo la Borno nchini Nigeria amesema kuwa wasichana 14 zaidi wamefanikiwa kutoroka katika mikono ya wanamgambo wa kiislamu waliowatekanyara Jumatatu usiku.
Musa Inuwo Kubo, amesema wasichana 44 sasa wamewatoroka watekaji hao na kwamba wasichana wengine 85 hawajulikani walipo
Vikosi vya Usalama,makundi ya vijana wa kuweka usalama mitaani pamoja na familia za wasichana hao wanaendelea kuwatafuta.
Wasichana hao wanaaminika kutekwanyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa wasichana wamekuwa wakitekwanyara na kundi hilo lakini sio katika kiwango kama cha sasa.
Amesema kuwa wapiganaji hao wanapinga kuwepo kwa elimu ya kidunia na kwamba wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu.BBC(A.I)