TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, November 16, 2013

WAHABESHI 22 WAKAMATWA DAR 

wahabeshi-300x169 77722
RAIA 22 wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Uhamiaji Mkoa, Grace Hokororo, alisema Wahabeshi hao walikamatwa juzi usiku katika maeneo ya Kinondoni wakiwa katika pagale ambamo walikuwa wamejificha.(HD)
Alisema baada ya wananchi kuwaona waliwatilia mashaka na ndipo walipotoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakamata.
"Hii hali ilikuwa imepoa lakini hivi sasa naona tena wameibuka kwa kweli kazi ipo na hawa tunategemea kuwasafirisha na kuwarudisha kwao wakiwemo Wanyarwanda tisa,'' alisema Hokororo.
Alisema wiki tatu zilizopota jumla ya wahamiaji 42 wakiwemo Wahabeshi, Wasomali na Wanyarwanda walisafirishwa na kurudishwa makwao.
Alisema pamoja na jitihada za idara hiyo kuwakamata raia hao, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi na magari, jambo alilosema limekuwa likikwamisha jitihada za idara hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
"Watumishi wengi wamechukuliwa na NIDA na hapa nimebakiwa na wachache na magari pia ni tatizo tunaiomba serikali iliangalie na ione umuhimu wa kutuongezea watumishi ili tuweze kufanya kazi vizuri," alisema.

HASSAN DILUNGA ATUA YANGA

dilunga a6713
SAA chache baada ya kufunguliwa kwa Dirisha Dogo la Usajili kwa msimu wa 2013/14, vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga jana walifanikiwa kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.(HD)
Kwa mujibu wa kanuni, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji, usajili uliofunguliwa jana Novemba 15 na kutarajiwa kufungwa Desemba 15.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema jana kwamba usajili wa kiungo huyo ni utekelezaji wa maagizo ya Kocha Mkuu, Ernie Brandts, aliyoyaacha na benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuboresha kikosi.
"Kocha aliacha mapendekezo ya usajili tuyafanyie kazi, la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunampata Kaseja ili kuongeza nguvu miongoni mwa makipa, ambao tuliukamilisha mwishoni mwa wiki na sasa tumelimaliza la kiungo Hassan Dilunga," alisema Bin Kleb na kuongeza.
Kikubwa kuhakikisha kuwa, tunatekeleza maagizo yote yaliyo katika ripoti ya benchi la ufundi na kuyafanyia kazi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Usajili wa Dilunga kiungo aliyeteuliwa kikosi cha timu ya taifa, 'Taifa Stars', inayojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars, ametua Jangwani siku chache baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu walipomsajili mlinda mlango wa zamani wa Simba na Stars, Juma Kaseja, aliyekuwa hana timu tangu kumaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.

NIDA:WATENDAJI WANAODAI FEDHA ZA VITAMBULISHO KUKIONA

NIDA1 a9f58
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaonya baadhi ya watendaji wa mitaa jijini Dar es Salaam wanaodaiwa kuwatoza fedha wananchi kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua za sheria.(HD)
Aidha, imesema zoezi la utaoji wa vitambulisho limefikia katika hatua ya kuchukua alama za vidole na picha kwa watu waliojaza fomu za kuviomba.
Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu, akizungumza katika mahojiano na Radio One, alisema zoezi la vitambulisho linagharamiwa na serikali kwa asilimia 100, hivyo hairuhusiwi mtendaji yeyote kumtoza fedha mwananchi.
Alisema zoezi linaendelea katika wilaya za Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar na kuwa wanaopuuza kupata vitambulisho vya taifa watapata athari ikiwamo kushindwa kupata huduma mbalimbali kama kufungua akaunti au kupata ajira.
Kuna madai kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa katika jijini Dar es Salaam wamekuwa wakiwatoza Sh. 2,000 watu wanaokwenda katika ofisi zao ili kugongewa mihuli.
CHANZO: NIPASHE

MAREKANI YAIWEKA PABAYA TANZANIA YAIITA KITOVU CHA ‘BIASHARA’ YA BINADAMU

UzaMtuClip 79203
Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.(HD)
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
"Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii," inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na majumbani nchini Tanzania.
"Baadhi ya raia kutoka nchi jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati," inaeleza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya baruapepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.
Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.
"Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma. Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa kutoka kwao," alisema.
Lawama kwa Serikali
Ripoti hiyo inaitupia lawama Tanzania kwa kutokuwa na sheria thabiti za kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu, huku ikitolea mfano namna ilivyoshindwa kuwasaidia raia wake waliokuwa wakinyanyaswa nje ya nchi.
"Kamati ya Serikali ya kupambana na usafirishaji binadamu, haijachukua hatua za kutosha katika kutekeleza mpango mkakati wa kupambana na vitendo hivyo," inaeleza na kuongeza:Serikali imeshindwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa usafirishaji wa binadamu kama ambavyo inaelekezwa kwenye sheria ya kudhibiti biashara hiyo ya 2008."
Taarifa hiyo inaitaka Tanzania kuongeza nguvu katika kutekeleza sheria ya kudhibiti biashara ya kusafirisha binadamu ya 2008 kwa kuwakamata na kuwashtaki wahusika wote, lakini ikaikosoa kwa kusema inatoa adhabu ndogo kwa mtu anayebainika kufanya makosa, ikiwa ni pamoja na kumhukumu kwenda jela miaka 10, kulipa faini au vyote viwili kwa pamoja.
"Sheria hiyo haifanani na nyingine kama za mtu anayepatikana na kosa la kubaka au kufanya kosa jingine la jinai. Mamlaka imesema ina kesi nne inazozichunguza, saba zipo mahakamani toka mwaka jana, zikiwepo mbili mpya," inasema ripoti.
Pia, Serikali ya Tanzania imelaumiwa kwa kushindwa kuripoti maendeleo ya uchunguzi wa maofisa wake waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu.
LHRC na TGNP
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema tatizo la usafirishaji wa binadamu pia linachangiwa na wasichana kuwa na tamaa ya maisha mazuri, hivyo kukubali ahadi ambazo hupewa kwamba wanapelekwa kusoma, wasifahamu wanarubuniwa.
"Wengi wanatamani kwenda 'majuu' wakidhani watapata elimu, lakini baadaye wanaingizwa kwenye vitendo vinavyowafedhehesha na kuwafanya wakate tamaa kabisa," alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana waliochukuliwa vijijini kwenda mijini kufanya kazi.
Alisema pamoja na tatizo hilo kuongezeka hapa nchini, hakuna tafiti za kutosha ambazo zimefanywa na wadau mbalimbali kuonyesha madhara yaliyopatikana hadi sasa.
"Katika siku za usoni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya kunyimwa chakula, kupigwa na kufukuzwa kazi huku wasichana wengine wakitumika kwenye biashara ya ngono," alisema na kuongeza:
"Ripoti hii isiishie kwenye makabrasha bali ifanyiwe kazi ili jamii yote ijue kuwa hili ni tatizo."
Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu 47,000 pekee ndio walioweza kuokolewa mwaka jana kutoka kwenye mazingira ya utumikishwaji kati ya milioni 27 waliopo katika hali hiyo duniani.Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 44 ambazo zinajaribu kupambana na biashara hiyo, lakini hali inazidi kuwa mbaya zaidi.:CHANZO MWANANCHI

KILI STARS YAPANGWA NA ZAMBIA, BURUNDI CHALLENGE 2013 

9_e471e.jpg
Kikosi cha Taifa Stars amacho kinaundwa na wachezaji wengi wa Bara
Na Prince Akbar, Dar es Salaam
TANZANIA Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imepangwa katika Kundi B kwenye michuano ya CECAFA Challenge pamoja na Zambia, Burundi na Somalia.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 27 mjini Nairobi, Kenya, wenyeji Harambee Stars wamepangwa na Ethiopia, Zanzibar na Sudan Kusini katika Kundi A.
Mabingwa watetezi, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea. Ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.
MAKUNDI CHALLENGE 2013:
KUNDI A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
KUNDI B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia
KUNDI C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.(P.T)

TANGAZO TANESCO 

aa_29e0f.jpg
Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Badra Masoud akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika ili kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.(P.T)
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
MPR/PR/12
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) linasikitika kuwajulisha wateja wake wote kwamba kutawepo na upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika.
Lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.
Kutokana na Matengozo hayo Mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifaa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme.
Imetolewa na: BADRA MASOUD
MENEJA UHUSIANO

TRA MBARONI KWA MENO YA TEMBO ZANZIBAR 


Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemhine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).(P.T)
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.
Kamishna Mussa amesema Watuhumiwa wengine wawili ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa Mizigo ya Island Sea Food Limited, Mohammed Suleiman Mussa(45) na Juma Ali Makame(34) wao walikamatwa siku ya tukio la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo kwenye Bandari ya Zanzibar.
Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa kwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi.Pamoja na mambo mengine, kusafirishwa kwa watuhumiwa hao kwenda Jijini Dar es Salaam, kunatokana na Zanzibar kutokuwa na Sheria maalumu inayohusu wanyamapori.
Maafisa wa Idara ya Wanyamapori nchini, leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na kulinganisha vipande 1,023 vya meno ya tembo vilivyokamatwa jana kwenye Bandari ya Zanzibar na kubaini idadi ya tembo waliouawa kuwa ni 305.
Meno hao yenye uzito wa kilo 2,915 yenye thamani ya Dolla 4,775,000 sawa na shilingi 7,480,125,000 za Tanzania (Bil.7.4), yalikamatwa juzi yakiwa yamehifadhiwa katika magunia 98 na kuwekwa kwenye konteina moja la futi 40 lenye namba PCIU 857619/0 lillilokuwa tayari kupakiwa kwenye meli ya MV Kota Henning kupelekwa nchini Ufilipino kwa magendo.
Hadi sasa bado Makachero wa Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini kwa kushirikiana na Makachero wa Polisi Zanzibar, idara ya wanyamapori makao makuu wanaendelea na upelelezi wa kuwabaini wale tote waliohusika na kashfa hiyo.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha kuwa upelelezi wa kina unafanyika ili kuwakamata wale wote wanaohusika na mtandao huo.
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado linamsaka tajiri aliyewezesha mipango ya kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili kusafirishwa nje ya nchi.

Friday, November 15, 2013

SMZ YAANDAA MASHINDANO YA MICHEZO YA 17 KUHADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

zanznoibar_bb026.jpg
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Ali Mbaruk akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu michezo mbalimbali itakayofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo adhimishwa Mwezi January 2014,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)(P.T)
Frank Mvungi - Maelezo
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeandaa mashindano ya michezo 17 kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi hayo itakayofikia kilele januari 12,2014 ambayo ni siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari , Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Mh. Said Ali mbaruk wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya michezo ya kuadhimisha mapinduzi hayo.
Mh. Said Ali Mbaruk amesema kuwa katika kuadhimisha mapinduzi hayo michezo mbalimbali itafanyika ikiwemo mpira wa miguu,riadha,volleyball,Table tenis na mazoezi ya viungo.
Akifafanua zaidi Alisema michezo hiyo pia itawahusisha watu wenye ulemavu ambapo kwa kushirikiana na Kamisheni ya utalii michezo mingine itakayofanyika ni karata,bao,squash na kuogelea .
Akieleza zaidi Mh. Said Ali Mbaruk aisema kuwa katika michezo hiyo kutakuwa na timu zaZanziba,Tanzania bara,Afrika Mashariki,ambapo mashindano hayo yanapata hadhi ya kimataifa.
Pia alizitaja timu zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni Azam FC,Simba, Yanga,Mbeya city kwa upande wa Tanzania bara, baadhi ya timu toka Zanzibar ni chuoni,Pemba combine na Unguja combine.
Katika maadhimisho hayo mechi zote zitatangazwa moja kwa moja kupitia ZBC TV,kwa kushirikiana na Azam TV.

LOWASSA:TULIOHUZUNIKA,TUTASHINDA PAMOJA

lowassapx a10b6
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema waliofurahi na kuhuzunika naye pia watashinda pamoja naye.
Bila kufafanua kauli yake jana, Lowassa aliwaambia wakazi wa Monduli mkoani Arusha kuwa: "Kumbukeni kaulimbiu yangu wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja".(HD)
Mbunge huyo wa Monduli alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi mbili za ghorofa za wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.
Katika hotuba yake fupi, pia alitamba kwamba atayashinda majaribu. Hata hivyo, hakufafanua majaribu hayo... "Kuna vita kubwa, lakini ambacho naweza kusema ni kuwa nayaweza yote kwa yeye anitiaye nguvu."
Kuhusu afya yake ambayo mara kadhaa imeelezwa kuwa siyo imara, kiongozi huyo alisema kwa sasa ni nzuri na imeimarika kupita kipindi kingine chochote.
Lowassa alisema kuanza ujenzi wa majengo hayo ambayo ni utekelezaji wa ahadi zake, ni moja ya ushindi na kuwataka wakazi wa Monduli, kumshukuru Mungu kwa yanayotokea.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole aliwataka wakazi wa Monduli, kumshukuru Mungu kwa kuwa na mbunge Lowassa ambaye anapendwa nchi nzima.
"Monduli Mungu awape nini, Lowassa anaitwa kila mahala kusaidia kutokana na moyo wake wa huruma na hapa ametekeleza ilani yote ya uchaguzi," alisema.
Kauli ya Lowassa imekuja siku chache tangu mtangulizi wake katika nafasi ya Waziri Mkuu, Frederick Sumaye alipomtuhumu hadharani kwamba amekuwa akimhujumu na kumwekea vikwazo vya kisiasa kwa kutumia mbinu chafu. Miongoni mwa mambo yaliyoonekana kumkera Sumaye ni habari iliyoandikwa na gazeti hili Septemba 16, mwaka huu inayohusu mradi wa maji Ziwa Victoria, ambayo Lowassa alinukuliwa akisema kuwa wakati akiwa Waziri wa Maji, aliungwa mkono na mawaziri watatu tu alipopendekeza mradi huo wa maji.
Sumaye alisema: "Najua mhusika ametumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua. Amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi nilikuwa Waziri Mkuu na mradi umetekelezwa chini ya uangalizi wangu," alisema na kuongeza:
"Kama waziri anaweza kubuni na kutekeleza mradi mkubwa hivyo peke yake, sasa akiwa Waziri Mkuu si maji yangefika Dodoma? Mbona hata bado kuna sehemu za Kanda ya Ziwa bado kuna shida ya maji?"
Tangu Sumaye atoe tuhuma hizo ambazo zinahusishwa na vita ya kuwania urais wa 2015, Lowassa hakuwahi kujibu chochote wala kusikika akizungumza hadharani, hadi jana.Lowassa alisema mafanikio yaliyopatikana katika jimbo lake na mengine nchini, yanatokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambao umefanywa na Rais Jakaya Kikwete.
"Hakuna kipindi ambacho ilani ya uchaguzi imetekelezwa kwa kiasi kikubwa kama kipindi cha Rais Kikwete naomba sote tumpongeze," alisema Lowassa.
Alisema hivi karibuni amekutana na Rais Kikwete ambaye ametoa Sh3 bilioni za ujenzi wa mabwawa 10 katika wilaya hiyo ili kukabiliana na tatizo la maji.
Wodi hizo za kisasa zinajengwa na Kampuni za Meelo Constraction na Bulem Constraction za Arusha kwa gharama ya Sh1.9 bilioni na zitakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 140 wakati mmoja.

HAWA NDIO MABILIONEA WANNE VINARA TANZANIA

rostam 7da3e
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja Sh1.6 trilioni.(HD)
Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji 'Mo'. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.
Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).
Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.
Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni).
Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni).
Rostam, Mengi na Bakhresa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku Mo akisema kwamba asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa jana alikuwa katika mapumziko ya Sikukuu ya Ashura.
Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye anajenga Kiwanda cha Saruji huko Mtwara ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Afrika, akiwa na utajiri wa Dola20 bilioni (Sh31.7 trilioni), akifuatiwa na familia ya Johanny Rupert ya Afrika Kusini yenye utajiri wa Dola7 bilioni (Sh10.7 trilioni) na Nick Oppenheimer, pia wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 6.6 bilioni (Sh10.3 trilioni).
1)Rostam Aziz
Jarida la Forbes limeripoti kuwa utajiri wa Rostam unachangiwa zaidi na biashara ya mawasiliano ya simu za mkononi, ujenzi na uchimbaji wa madini.Pia anamiliki Kampuni ya Caspian, ambayo inafanya kazi za kuchimba madini katika migodi inayomilikiwa na Kampuni za BHP Billiton na Barrick Gold.
Pia ana hisa katika Kampuni ya Hutchison Wampoa inayofanya kazi za kupakua mizigo bandarini na anamiliki majumba nchini na katika nchi za Mashariki ya Kati.
2) Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP.
Utajiri wake unatokana na kumiliki vyombo vya habari, kiwanda cha vinywaji baridi na madini.
Mengi anamiliki magazeti kumi na moja, vituo vitatu vya televisheni na takriban vituo 10 vya redio.
Pia ana mgodi wa madini ya dhahabu na viwanda vya CocaCola.
Kwa mujibu jarida hilo, Mengi alizaliwa katika familia maskini na baadaye kusomea uhasibu huko Uingereza na kufanya kazi huko.
Alijiunga na Chama cha Wahasibu cha Uingereza kabla ya kurejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Ukaguzi ya Coopers & Lybrand Tanzania (sasa Price Water House Coopers) hadi mwaka 1989, alipoacha kazi na kujikita zaidi katika biashara.
3) Bakhresa
Said Salim Bakhresa ni mwasisi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa Group na ana utajiri wa Dola500 milioni (Sh783 bilioni).Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza biashara ya kuuza viazi mbatata. Baada ya hapo alifungua mgahawa na baadaye kuingia katika biashara ya kusaga nafaka.
4) Mo
Mafanikio yake yamechangiwa zaidi baada ya kuendeleza mali ya wazazi wake. Anafanya biashara ya nyumba, kuuza mazao na viwanda vya mafuta.
Mo alirejea Tanzania baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani na kuendeleza biashara ya maduka ambayo yalianzishwa na baba yake.
Alinufaika baada ya kununua viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali.
Alivifanya viwanda hivyo kutengeneza faida na kuinyanyua Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL) kuwa miongoni mwa kampuni zenye mafanikio makubwa Tanzania.
Mo pia anajihusisha na biashara ya usambazaji bidhaa, viwanda vya nguo na kilimo.
Jarida hilo lilipiga hesabu za utajiri wa wafanyabiashara hao kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazouzwa na kampuni zao, mikataba yao na hasa wale walio kwenye sekta ya mafuta na ukubwa wa kampuni zao.CHANZO MWANANCHI

WAPATANISHI WA PALESTINA WAJIUZULU

017221858_35400_013e7.jpg
Mpatanishi mkuu wa Palestina aliyejiuzulu, Saeb Erekat
Viongozi wa timu ya wapatanishi wa Palestina kwenye mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati, wamewasilisha barua za kujiuzulu katika kupinga ujenzi wa makaazi ya walowezi unaofanywa na Israel, Ukingo wa Magharibi.
Viongozi waliowasilisha barua za kujiuzulu ni pamoja na mpatanishi mkuu Saeb Erakat na Mohammed Shtayyeh, hatua walioichukua baada ya Waziri wa Makaazi na Ujenzi wa Israel, Uri Ariel kutangaza kuendeleza ujenzi wa nyumba zipatazo 24,000 kwenye Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.
Hata hivyo mpango huo mpya ulikosolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na alimuamuru Waziri Ariel kuusitisha akisema kuwa utasababisha mvutano usio wa lazima na jumuiya ya kimataifa.(P.T)
Afisa wa chama cha ukombozi wa Wapalestina-PLO, Xavier Abu Eid amesema Erakat na Shtayyeh waliwasilisha barua zao kwa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kabla ya Netanyahu hajasitisha ujenzi huo. Netanyahu amesema waziri wake alifanya maamuzi hayo peke yake bila kumshirikisha.
Abbas na Kerry wazungumza kwa simu
Jana Jumatano (13.11.2013) Abbas alizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry anayesimamia mazungumzo hayo kwa kiasi kikubwa, na akamuhakikishia nia yake ya kutaka kuendelea kwa mazungumzo hayo. Abbas amesema mazungumzo yataendelea hata kama ujumbe wa wapatanishi wa Palestina umejiondoa.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Misri cha CBC, Abbas amesema wanajaribu kuwashawishi wapatanishi hao kurejea kwenye mazungumzo hayo ya amani, ama watachagua wapatanishi wapya. Hata hivyo, bado haijafahamika wazi iwapo Abbas atakubali barua hizo za kujiuzulu, hadi hapo atakapokubali kusaini.
Afisa mwandamizi wa PLO, Hanan Ashrawi amesema iwapo hatua ya kujiuzulu wapatanishi hao itakuwa rasmi, itakuwa vigumu kwa Abbas kutafuta wapatanishi wengine, kwa sababu hakuna mtu ambaye anataka kujihusisha katika mchakato wa amani ambao mwelekeo wake haueleweki.
Israel ilitangaza mpango wa ujenzi wa makaazi mwezi uliopita
Mwezi uliopita Ariel alitangaza zabuni kwa mpango wa kujenga kiasi nyumba 20,000 katika Ukingo wa Magharibi na nyumba 4,000 Jerusalem Mashariki, bila kushauriana na Netanyahu.
Kutangazwa kwa zabuni hizo ni hatua za awali za mchakato wa ujenzi. Netanyahu amesema mvutano kuhusu ujenzi wa makaazi ya walowezi unatishia kudhoofisha kampeni dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran. Palestina inalichukulia eneo la Ukingo wa Magharibi kama taifa lake la baadaye.
Waziri wa Nishati wa Israel, Silvan Shalom jana ameweka bayana kwamba nchi hiyo itaendelea na ujenzi wa makaazi ya walowezi, huku ikiwa makini katika suala la kuutangaza mpango huo katika siku za usoni. Katika ziara yake ya Mashariki ya Kati hivi karibuni, Kerry aliitolea wito Israel kuweka mpaka katika kazi ya ujenzi wa makaazi ya walowezi, ili kusaidia juhudi za mchakato wa amani kuendelea.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/DPAE,RTRE
Mhariri: Yusuf, Saumu

UGONJWA WA KISUKARI WAENDELEA KULETA MADHARA

AFYA_-_1_39429.jpg

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akitoa tamko la Serikali kuhusu Siku ya Ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Novemba 14. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Seif Rashid.
AFYA_-2_ef5f9.jpg
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando akitoa ufafanuzi wa namna ya kujikinga na ugonjwa wa kisukari leo jijini Dar es salaam wakati mkutano na waandishi wa habari.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.(P.T)
UGONJWA WA WAENDELEA KULETA MADHARA , WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA TABIA YA KUPIMA AFYA NA KUFANYA MAZOEZI.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
14/11/2013 – Dar es salaam.
Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara, kupima afya na kuepuka tabia hatarishi zinazochangia uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu Siku ya Ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Novemba 14.
Amesema Tanzania kama zilivyo nchi nyingine inaadhimisha siku hiyo kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa kisukari Tanzania kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhra mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huo.
Amesema maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2013 yataongozwa na kauli mbiu isemayo "Linda Maisha yajayo dhidi ya Ugonjwa kisukari" inayolenga kuhamasisha jamii juu ya matatizo mbalimbali yanayotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii.
Ameeleza kuwa athari za ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu na kuongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikua na wagonjwa milioni 246 duniani huku mwaka 2012 kukiwa na wagonjwa milioni 371 ambapo nusu ya idadi ya wagonjwa hao walikua hawajaanza kupata matibabu.
Kuhusu dalili za ugonjwa huo Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni rahisi kuzitambua na huambatana na mgonjwa kuwa na kiu isiyoisha, kukojoa mara kwa mara, kupungua uzito, kusikia njaa kila wakati na mwili kukosa nguvu na kuongeza kuwa athari za ugonjwa huo ni kubwa kutokana na ugonjwa huo kuharibu mishipa ya damu na fahamu, macho, figo, kusababisha upofu, moyo na figo kushindwa kufanya kazi na miguu kufa nganzi na kuwa na vidonda.
Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wote duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na kuongeza kuwa utafiti uliofanyika mwaka 2012 nchini Tanzania kwa kuzihusisha wilaya 50 unaonyesha kuwa asilimia 9.1 ya watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.
"Ni jambo lililo wazi kuwa lazima tubadili tabia hasa tabia hatarishi zinazochangia ugonjwa wa kisukari zikiwemo unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji usiofaa, ulaji usiofaa na tabia ya kupuuza kufanya mazoezi", sasa Tanzania katika nchi 10 za Afrika zinazoongoza kwa kisukari barani Afrika inashika nafasi ya 8" Amesema Dkt. Mwinyi.
Kuhusu sababu zinazochangia ugonjwa huo Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni pamoja na tabia ya ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi kwa wingi , mafuta na sukari, uzito uliozidi, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi , uvutaji wa sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku pamoja, kula vyakula vyenye mafuta mengi hasa yatokanayo na wanyama, sukari nyingi,kula chakula kupita kiasi, kukoboa nafaka, kutokula mbogamboga na matunda na unywaji wa pombe kupita kiasi.
Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuepuka mambo yanayochangia chakula kilicholiwa kutotumika vizuri ikiwemo tabia ya kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi huku akisisitiza kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi huharibu maini na kusababisha utapiamlo kwa wale wanaoishia kunywa pombe Zaidi bila kula chakula.
" Natoa ushauri hasa kwa watumishi kuepuka kuketi ofisini, darasani au kuangalia runinga kwa muda mrefu na hata kutumia lifti kwenda ghorofani badala ya ngazi na matumizi ya magari katika umbali mfupi unaoweza kufikika kwa kutembea tu"
Dkt. Mwinyi ameleza kuwa serikali imejipanga kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 unaendelea kwa kuhakikisha kuwa utoaji wa hudunma za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari unafanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Ameeleza kuwa serikali kwa kutambua gharama za kutibu ugonjwa wa kisukari kuanzia mwaka 1983 ilitoa msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wote wa kisukari kutochangia gharama za matibabu pia kuhakikisha kuwa dawa muhimu zinapatikana katika kliniki mbalimbali zilizopo nchini.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando amewataka vijana kote nchini ambao ni kundi kubwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kuepuka maisha ya anasa ambayo huwaweka katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Amesema mapambano ya ugonjwa wa kisukari yanahitaji ushiriki wa kila mwananchi hasa kuzingatia kanuni za Afya na kujenga mazoea ya kufanya mazoezi mara mara.
MWISHO.

MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI NCHINI TANZANIA YATOLEWA 

TAKWIMU-_1_4722e.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (katikati) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu matokeo ya utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Takwimu_-_2_2_4214b.jpg
Afisa Mwandamizi wa Benki ya Dunia Bw. Richard Martini (katikati) akitoa salaam za Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Phillipe Dongier, ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuzingatia vigezo vya tafiti vya kimataifa katika kutoa matokeo ya Mapato na Matumizi ya Kaya nchini.
TAKWIMU_-_3_57228.jpg
Sehemu ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.(P.T)
MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI NCHINI TANZANIA YATOLEWA, LICHA YA CHANGAMOTO ZA UMASKINI KAYA NYINGI ZAONYESHA MAFANIKIO.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
14/11/2013, Dar es salaam.
Uwezo wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi nchini kwa mwaka 2011/2012 unaonyesha kuongezeka kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika sekta ya elimu, afya, umiliki wa biashara, shughuli za kilimo, umiliki wa Vifaa na Rasilimali , makazi bora, ongezeko la shughuli za kiuchumi na ajira.
Akitoa taarifa ya Utafiti ulioendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuangalia tathmini ya kiwango cha umasikini wa kaya kwa kutumia kipato na masuala mengine yasiyo ya umasikini wa kipato leo jijini Dar es salaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa kukua kwa kiwango cha elimu, matumizi ya nishati ya umeme, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali ni miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa uwezo wa mapato na matumizi ya kaya.
Amesema kuwa utafiti huo ulifanyika kuanzia mwezi Oktoba 2011 hadi Oktoba 2012 ambapo jumla ya kaya 10,186 kati ya 10,400 zilizokuwa zimelengwa zilihojiwa katika maeneo ya Dar es salaam na maeneo mengine ya mijini na vijijini kwa Tanzania Bara.
Amesema uchumi wa Tanzania kwa sasa umekua kutokana na kuimarika kwa sekta za ujenzi, usafirishaji, Elimu, shughuli za mawasiliano, huduma za afya na huduma za kifedha.
" Serikali imefanya mambo makubwa na sasa uchumi wa Tanzania umekua kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa katika kuboresha miundombinu ,kuwekeza katika sekta ya elimu, usafirishaji, mawasiliano pamoja na ongezeko la huduma za kifedha" amesema.
Amesema kumekuwa na jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali zikiwemo kuongeza ujenzi wa shule Zaidi hasa zile za sekondari ambazo zimewezesha kupanda kwa kiwango cha wanafunzi wanaojiunga katika elimu ya sekondari kutoka 15% mwaka 2007 hadi asilimia 29% 2011/12.
Amefafanua kuwa idadi ya kaya zinazoishi katika nyumba zilizojengwa kwa vifaa vya ujenzi vya kisasa, paa za kisasa, vigae na matumizi ya zege na kuta imara tangu mwaka 2007 imeongezeka kwa 66%.
Ameongeza kuwa matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 4% ya kaya zinamiliki pikipiki, 55% zinamiliki radio na 57% ya kaya zote angalau mwanakaya mmoja anamiliki simu ya mkononi na kufafanua kuwa kiasi cha asilimia 78 ya kaya za maeneo ya mengine ya mjini na asilimi 88 ya kaya za Dar es salaam zinamiliki angalau simu moja ya mkononi.
Katika hatua nyingine Dkt. Servacius ameeleza wastani wa kiwango cha umasikini wa chakula kitaifa ni asilimia 9.7 na kuongeza kuwa kiwango hicho kinafikia asilimia 11.3 kwa maeneo ya vijijini huku Dar es salaam ikiwa na kiwango cha chini kabisa cha umasikini wa chakula kwa asilimia 1.0 na maeneo mengine ya mjini yakiwa na umasikini wa chakula kwa asilimia 8.7.
Amesema miji mikubwa ina kiwango cha chini cha umasikini wa chakula kwa asilimia 1.0 ambapo wananchi wanaoishi maeneo mengine ya mjini wana umasikini wa chakula wa asilimia 8.7.
Ameongeza kuwa umasikini wa mahitaji ya msingi kwa Tanzania bara ni asilimia 28.2 ikilinganishwa na asilimia 33.3 kwa maeneo ya vijini na asilimia 21.7 kwa maeneo mengine ya mjini na kubainisha kuwa Dar es salaam ina kiwango cha chini cha umasikini wa mahitaji ya msingi cha asilimia 4.1.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Benki ya Dunia Bw. Richard Martini akitoa salaam za Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Phillipe Dongier, ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuzingatia vigezo vya tafiti vya kimataifa katika kufuatilia hali ya umasikini na kipato nchini.
Amesema twakimu za utafiti huo zilizotolewa zinaonyesha hali halisi ya maisha wanayoishi wanachi na kuongeza kuwa zitaisaidia serikali, wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuelewa na kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo na kukabiliana na changamoto za umasikini zilizopo nchini.
MWISHO.

Wednesday, November 13, 2013

KASHFA NZITO YA TUME YA UCHAGUZI nec d795e

na Abdallah Khamis
TUME ya Uchaguzi nchini (NEC) inadaiwa kuingia katika mchakato wa mwisho wa kuzipa zabuni ya kuandaa vifaa vya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution zinazodaiwa kuwa na rekodi mbaya ya utendaji.(HD)
Tanzania Daima limedokezwa kuwa mkakati huo unahusishwa na njama za kutaka kukibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo kwa kuchakachua matokeo ya kukibakiza madarakani.
Kampuni hizo ambazo katika zabuni ya Tume ya Uchaguzi zimetajwa kushirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya M/S SCI Tanzania Limited, mbali ya kutojulikana zinapotoka, pia ndizo zimekuwa na gharama kubwa kuliko kampuni nyingine zilizoomba kazi hiyo.
Kiwango ambacho kampuni hizo zilitaja na kukubaliwa na NEC kwa ajili ya kuandaa vifaa vya kielektroniki vya kusajili wapiga kura (Biometric Voters Registration) ni zaidi ya euro milioni 60, sawa na sh bilioni 126.3, wakati kampuni zinazofuata zikihitaji kuanzia euro milioni 40.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ni mmoja wa viongozi waliofichua mkakati huo, akidai unafanywa na serikali ya CCM ili kuhakikisha wanajiandaa kudhibiti kila eneo ili waweze kubaki madarakani.
Alisema lengo ni kuhakikisha mchakato wa vitambulisho vya kupigia kura vya kielektroniki vina kuwa na faida kwa CCM na kukiingizia fedha chama hicho za kutumia kwenye uchaguzi huo kupitia mfumo huo dhaifu wa vitambulisho hivyo.
Zitto alisema kutokana na hali hiyo, amemwandikia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) barua ya kutaka ukaguzi wa zabuni hiyo ufanyike kwa kushirikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kujiridhisha.
"Wenzetu CCM wanafanya mikakati ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuhakikisha wanapata fedha za kutosha na hata mazingira mabaya ya vifaa vitakavyotumika katika upigaji kura na sasa wameshaingia hata katika Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kutengeneza mazingira," alisema Zitto.
Aliongeza kuwa kiasi kilichotolewa ni kodi ya Watanzania na kwamba ni vema taifa likajiridhisha kuwa matatizo yaliyotokea Kenya na Ghana hayatajirudia Tanzania, hasa wakati wa upigaji kura.
Gazeti hili limeona barua hiyo ya Zitto kwenda kwa CAG, ya Novemba 7, 2013, yenye kichwa cha habari; 'Zabuni ya Biometric Voters Registration (BRV KITS) No. IE/018/2012-13/HQ/G/19 yenye thamani ya sh bilioni 126.3.'
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini anasema kuwa NEC imekuwa katika mchakato wa zabuni tajwa hapo juu.
"Zabuni hiyo sasa imeanza kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kutokana na kinachosemekana kuwa kampuni iliyopewa zabuni hiyo haina uwezo kiteknolojia, pia bei zao ni kubwa.
"Katika mafunzo ya hivi karibuni ya SADCOPAC jijini Nairobi tuliazimia kuwa ni vema kwenye zabuni nyeti kama za namna hii, SAIs wawe na uwezo wa kufanya ukaguzi kabla ya zabuni kutolewa na kuanza kutekelezwa," alisema.
Kwa mujibu wa nyaraka za NEC ambazo Tanzania Daima linazo, kampuni zilizopewa tenda ya pamoja yenye kugharimu kiasi cha dola 78, 987,636.00, sawa na sh 126,291,375,455 ni M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution ambazo hazijulikani nchi zinapotoka zikiwa zinashirikiana na M/S SCI Tanzania Limited.
Katika nyaraka hizo kampuni zilizokosa tenda na ambazo zimelalamika kwa Mkurugenzi wa NEC namna mchakato wa kutoa zabuni hiyo ulivyoendeshwa zimeainishwa kuwa ni M/S Zetes SA ya nchini Ubalgiji, M/S IRIS Corporation Technology ya Malaysia, M/S Lithotech Exports ya Afrika Kusini, M/S Safran Morpho ya Ufaransa na M/S Avante International Technology, Inc ya Marerkani.
Kampuni hizo zinahoji njia na sababu zilizowafanya wakose tenda hiyo licha ya kuwa na uzoefu, vifaa bora pamoja na kuwa na kiwango kidogo cha gharama tofauti na kampuni iliyopewa kazi.
Katika moja ya malalamiko yao, Kampuni ya M/S Morpho, inalalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo licha ya kuwa na sifa za kimataifa za kufanya kazi huku ikiwa imetoa bei nafuu kuliko kampuni iliyopata kazi.
"Tulikuwa miongoni mwa washindani muhimu kwa kuwa kiwango chetu kilikuwa ni sh bilioni 97.8 ambazo ni sawa na euro 44,939,912 + sh 3,843,736,140.
"Ujuzi, vigezo na uzoefu wetu havilingani, duniani kote tumefanya kazi katika maeneo mengine kwa ufanisi na tunashindwa kuelewa kivipi walishinda hao ambao wamepata kazi kwa kiwango cha zaidi ya sh bilioni 27.8 ikilinganishwa na yetu," ilisomeka sehemu ya barua.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema hawezi kuliongelea suala hilo katika simu na kuomba mwandishi awasiliane na Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Dk. Sist Cariah, ambaye alisema mchakato wa kupata kampuni ulifuatwa kisheria.
Dk. Cariah alisema si kweli kwamba kampuni iliyopewa kazi haina uwezo bali malalamiko yanatoka kwa watu walioshindwa kupata kazi hiyo.
Alipoulizwa juu ya uzoefu wa kampuni hiyo na wapi ilifanya kazi, Dk. Cariah alisema kwa maelezo waliyonayo ni kwamba kampuni hiyo ina uzoefu wa miaka 35 wa kufanya kazi, huku akishindwa kuainisha sehemu ilizowahi kufanya kazi.
Kuhusu wapi zimetoka kampuni hizo, Dk. Cariah alisema suala la kutoainishwa kimaandishi ni makosa ya kawaida, huku akitaja kuwa zinatoka katika nchi ya India na Australia.
Kuhusu gharama, Dk. Cariah alisema licha ya makampuni mengine kutaja gharama za chini, zingeweza kuwa na gharama kubwa zaidi wakati wa kukamilisha kazi hiyo kutokana na kuwa na gharama zilizojificha.(CHANZO TANZANIA DAIMA)

BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU LAPATA WAJUMBE WAPYA

017193165_35400_b9b99.jpg
Mataifa manne yanayoshutumiwa kuwa na rekodi mbaya ya haki za binaadamu, yameshinda viti katika Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, kwa miaka mitatu.
Wajumbe wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa wakiwa mkutanoni
Uchaguzi huo umefanyika licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu na vikwazo juu ya uhuru kwenye nchi hizo.
Mataifa hayo China, Cuba, Urusi na Saudi Arabia, ni miongoni mwa mengine 14 yaliyojishindia viti hivyo katika uchaguzi wa mwaka, baada ya kupata theluthi moja ya kura za wajumbe wa baraza hilo lenye makao yake mjini Geneva.(P.T)
Nchi nyingine zilizojipatia viti katika baraza hilo lenye wanachama 47, ni pamoja na Algeria, Uingereza, Ufaransa, Mexico, Maldives, Morocco, Namibia, Afrika Kusini, Vietnam na Macedonia.
Nchi hizo zimechaguliwa juzi Jumanne (12.11.2013) na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193, huku balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power akielezea wasiwasi wake kuhusu uteuzi wa baadhi ya nchi.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamepinga uteuzi wa mataifa hayo.
Baraza hilo lakabiliwa na changamoto
Mkurugenzi Mtetezi wa kimataifa wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch, Peggy Hicks, amesema kuwa wanachama hao wanne wapya pamoja na Algeria, walikataa kuwaruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuzuru kwenye nchi hizo kuchunguza madai ya kuwepo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki.
Hicks amesema wanachama wa baraza hilo itabidi wafanye juhudi zaidi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto kadhaa.
Kwa mujibu wa shirika la utetezi la Umoja wa Mataifa, linaloufuatilia umoja huo, ni nchi nne tu kati ya wagombea 16 waliokuwa wanawania viti hivyo 14, ndizo zilizokuwa na sifa ya kuwa wanachama wa baraza hilo la haki za binaadamu.
Nchi hizo ni Uingereza, Ufaransa, Macedonia na Mexico.
Mataifa mapya yaliyochaguliwa, yataanza kazi rasmi kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Iran na Syria zilikuwa zinapanga kuwania nafasi hiyo, lakini zilijiondoa baada ya kukosolewa kutokana na rekodi yao ya haki za binaadamu.
Jordan yajiondoa kuipa nafasi Saudi Arabia
Hadi wiki iliyopita, Jordan ilikuwa inagombea kiti hicho, lakini ikajiondoa ili kuiruhusu Saudi Arabia igombee bila ya kuwa na mpinzani.
Jordan inataka kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi iliyoachwa na Saudi Arabia, ambayo ilikataa kiti hicho kuanzia mwaka 2014 hadi 2015, mwezi uliopita.
Tangu kuundwa kwake, Baraza la Haki za Binadaamu la Umoja wa Mataifa limekuwa likikabiliwa na changamoto kadhaa, huku kazi ya kuzifuatilia nchi wanachama ikiwa ni jukumu gumu.
Aidha, Bibi Power amesema uchaguzi huo unakumbusha kwamba kazi muhimu ya baraza hilo bado haijakamilika.
Nchi zilizoangushwa katika uchaguzi huo ni Uruguay, iliyoshindwa na Cuba na Mexico katika viti vya Amerika ya Kusini na kundi la Caribbean, pamoja na Sudan Kusini ambayo ilishindwa kupata kura za kutosha ili kushinda kiti kimoja kati ya vinne vya Afrika.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/RTRE,APE
Mhariri: Daniel Gakuba

TANZANIA YAZIDI KUKAMATA MENO YA TEMBO 

 meno_ya_tembo_cfb5e.jpg

Kwa mara nyingine katika kipindi kisichozidi wiki mbili, polisi nchini Tanzania wamenasa shehena kubwa ya meno ya tembo yakiwa yamefichwa katika kontena, bandarini Zanzibar.
Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na meno hayo.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, meno hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika kontena la futi arobaini yakiwa yamechanganywa katika mifuko iliyohifadhi makombe ya konokono wa baharini, tayari kwa kusafirishwa nje.
Kamishna Mussa amesema, kwa sasa kiasi hicho cha meno ya tembo bado hakijafahamika kutokana na kuendelea kwa kazi ya kupakua kutoka kontena hilo.(P.T)
Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na meno 706 ya tembo, sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.
Kukamatwa kwa meno haya ya tembo, kumekuja wakati tayari serikali imetangaza kusitisha Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ililenga kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka kutokana na kuuawa katika hifadhi za taifa nchini Tanzania. Wanyama wanaolengwa zaidi na majangili kutokana na meno yao na pembe ni tembo na faru.
Matukio ya kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Afrika Mashariki yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Oktoba, 20, 2012, tani nne za meno ya tembo yenye thamani ya dola milioni 3.4 za Kimarekani yalikamatwa Hong Kong, yakidaiwa kusafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Pia Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 sawa na dola zaidi ya elfu 11, yakisafirishwa kwenda nje.

WAKENYA TUPO KATIKA MAJUTO

uhuru_bab35.jpg
Dalili ya mvua ni mawingu. Mawingu yanayofunika anga la Kenya wakati huu yanaashiria kwamba mvua itakayonyesha itasababisha mafuriko katika nyanja za kisiasa na kiuchumi.
Ni kwa sababu hii wote wanaojali hatima ya nchi hawana budi kujitokeza kimasomaso ili kuona athari za vitendo vya Serikali ya Jubilee kwa nchi na kutafuta jinsi ya kuepukana nazo.
Jukumu hili liko juu ya mabega ya vyama vya upinzani haswa Muungano wa CORD unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na wengine.
Ni wakati wa CORD kuonyesha kuwa haiwezi kusita kueleza na kuihakiki Serikali ya Uhuru Kenyatta pia ni dhabiti na kwamba viongozi wake watakuwa wanazungumza kwa sauti moja wanapoikosoa Serikali.(P.T)
Wengi walitarajia kwamba viongozi wa Cord wangetengana baada ya uchaguzi mkuu, lakini Raila, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula bado ni wanachama wa CORD.
Historia ya vyama vya kisiasa nchini inaonyesha kwamba, viongozi huunda vyama kwa lengo la kushinda uchaguzi lakini baada ya miezi michache vyama hivyo husambaratika.
Kwa mfano, kiongozi wa United Democratic From (UDF), Musalia Mudavadi anajitayarisha kujiunga na Serikali ya Uhuru kama waziri. Gazeti moja la kila siku limenukuliwa likiripoti kwamba, Mudavadi hivi karibuni ataingizwa kwenye serikali.
Tatizo nini?
Upinzani umegundua kwamba Serikali ya Jubilee imeanza kuonyesha kucha zake miezi michache baada ya kujifanya kwamba inafuata sheria na kulinda Katiba. Ilifanya hivyo kwa kuteua Baraza la Mawaziri inavyotakiwa kisheria, lakini sasa mambo yamebadilika.
Uhuru na Makamu wake,William Ruto, wameonyesha kuwa hawajali lolote zuri linaloiweka Kenya kwenye jukwaa la mataifa yanayowalinda wananchi wake. Kwa wiki moja iliyopita, Upande wa Serikali bungeni umepitisha miswada miwili inayorudisha nyuma hatua nzuri zilizokuwa zimepigwa.
Kumekuwa na kilio kikuu kutoka kwa Wakenya kuhusu hatua ya Serikali kutaka kuzima uhuru wa wanahabari na pia kukata msaada kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka kwa mashirika ya maendeleo ya nchi za Ulaya na Magharibi.
Si jukumu la upinzani kuisifu Serikali na kuchochea maendeleo. Huu si wakati wa kupakana mafuta kwenye mgongo wa chupa kwani mshuka ngazi na mpanda ngazi kamwe hawawezi kushikana mikono.
Jukumu lake ni kuhakikisha Serikali inafuata mkondo unaofaa inapoendesha shughuli zake. Ni jukumu la kusukuma Serikali ili izingatie ahadi zake zote ilizotoa kwa Wakenya wakati wa kampeni na uchaguzi na hatimaye wakati wa kuapishwa kwake Uhuru na Ruto Aprili 9, 2013.
Kuna orodha ndefu ya mambo yasiyofurahisha wengi nchini, na chimbuko la haya yote ni Serikali ya Jubilee. Wakenya bado wanajiuliza maswali kuhusu jinsi mkuu wa majeshi alivyokuwa amekana kwamba kikosi chake hakikupora mali wakati wa mashambulizi ya Westgate.
Maji yalipozidi unga, Serikali ilikiri kwamba kweli, wanajeshi walikuwa wamepora. Kwanini Wakenya wachukuliwe kana kwamba ni majuha? Mbona Serikali haikukiri mara moja kwamba makosa yalifanyika badala ya kujaribu kuficha ukweli?
Muswada wa ushuru wa chakula na bidhaa nyingine muhimu ulipelekea kupanda kwa gharama ilhali mapato ya wananchi ni yale yale. Baada ya kilio kutoka kwa raia, Serikali ilitoa sababu kwamba haikuwa inalenga bidhaa muhimu kama vile maziwa na mikate walipoupitisha muswada huu.
Sote twafahamu ni kina nani wanaoshikilia sekta ya maziwa na wangefaidi kutokana na kuongezeka kwa bei ya maziwa na bidhaa nyingine.
Isitoshe, kuna maswali mengi kuhusu jinsi pesa za umma zinavyotumiwa. Tangu vikao vya kesi zinazomkabili Ruto ianze The Hague zaidi ya mwezi mmoja uliopita, wabunge na wafanyakazi wa umma wamekuwa wakimtembelea kiongozi huyu kila wiki ili kumpa moyo kortini.
Je, wabunge na wafanya kazi wa umma wanaosafiri kila mara kumtembelea Makamu wa Rais wanafanya hivyo kwa kujigharamia au fedha za umma ndizo zinatumiwa?
Pia, Waziri wa Masuala ya Nchi za Nje, Amina Mohammed amekuwa kiguu na njia tangu ateuliwe. Kazi ya kutumikia wananchi imewekwa kando badala yake kesi ya Uhuru imepewa kipaumbele.
Mohammed ametembelea nchi nyingi kutafuta uungwaji mkono kwa kesi hizi. Uhuru na Ruto walikuwa wamewahakikishia wananchi wakati wa kampeni na hata walipokuwa wakifanya kampeni kwamba, kesi zao ni za kibinafsi. Lakini sasa zimekuwa za kitaifa na hata kimataifa. Wakenya wangetaka kujua pesa hizo zote za nauli na kadhalika zinalipiwa na nani.
Shirika moja lisilo la kiserikali, Mars Group linaunga mkono juhudi za Upinzani za kutaka kujua jinsi safari hizi za kila mara zinavyogharamiwa. Mkurugenzi Mkuu wa Mars Group Kenya, Mwalimu Mati anataka Uhuru aeleze ikiwa matumizi ya pesa kwenye shughuli za kibinafsi kama hizi zilijadiliwa kama muswada katika Bunge la kitaifa na kupitishwa.
Upinzani ungetaka kujua mfuko wa fedha unaotumiwa na Uhuru na Ruto kuzuru nchi mbalimbali za Afrika kukutana na viongozi wa kisiasa barani ili wawaunge mkono kuhusiana na kesi za Hague.
Rais mwenyewe alizuru Botswana Jumatano wiki jana na kukutana na Rais Ian Khama kujadili kile maofisa wao wametaja kama masuala ya uhusiano ya nchi hizi mbili, barani na kimataifa.
Itakumbukwa hata hivyo kwamba, Botswana inapinga vikali jaribio la Rais Uhuru kutaka kesi dhidi yake kuahirishwa ama kufutiliwa mbali. Zaidi ya hayo, Botswana ilikuwa imetishia kumnasa Uhuru na kumkabidhi mikononi mwa Mahakama ya Kitaifa ya Uhalifu (ICC) ikiwa atatembelea nchi hiyo.
Ilibidi Uhuru amtembelee Khama kumshawishi amuunge mkono ili kesi yake iahirishwe. Haijulikani kama kiongozi huyo alikubali ama la.
Wiki jana Rais aliwatuma mawaziri Mohammed, Najib Balala na Fred Matiang'I kutafuta uungwaji mkono katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kesi zinazomkabili Uhuru.
Uhuru pia amewapigia simu si haba Rais Barack Obama wa Amerika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.
Matokeo ya juhudi hizo yamebakia kuwa siri kubwa ya Ikulu
Hata hivyo, viongozi wa upinzani sasa wanamtaka Uhuru aubebe msalaba wake mwenyewe kwa kuhudhuria vikao vya ICC kuanzia Februari 5, mwaka ujao.
Viongozi hao hawataki kumpaka Uhuru mafuta kwa mgongo wa chupa jinsi wanasiasa wa chama chake cha Jubilee wanavyofanya.
Upinzani umesimama kidete na kuiambia ICC isisite kumtupa kizimbani Uhuru ajibu kesi zinazomkabili. Ameambiwa wazi afikirie vizuri athari za yeye kususia kesi hizo. Je, Kenya itaendelea namna gani ikiwa yeye atakosa kufika kizimbani?
Mohamed Dida ambaye pia aligombea naye urais, hakutaka kuachwa nyuma. Anasema Uhuru na Ruto wana shida nyingi sana na hata hawana wakati wa kuwatumikia Wakenya. Anasema, tulionywa na Amerika kabla ya uchaguzi kwamba tukichagua Uhuru na Ruto tungejuta na sasa tumejuta.
Dida anashangaa kwamba licha ya onyo hilo Wakenya 6,000,000 walimchagua Uhuru. Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
Dida anasema Uhuru amefanya vibaya katika kuendeleza nchi na yaweza kupata alama nne kwa kumi.
Mwezi jana Martha Karua ambaye pia alipigania urais alisema kwamba hajuti kamwe kwa kusaidia ICC kupata ushahidi dhidi ya viongozi hao wawili kuhusu jinsi walivyochangia katika mapigano ya 2007/2008.
Chanzo:Mwananchi

MWILI WA WA DKT. SENGONDO MVUNGI KUWASILI IJUMAA , NOVEMBE 15, 2013 

Mvungi-3 1650f
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.(HD)

THAT IS MY PRODUCT IN THE MARKET SO IF YOU NEED IT YOU CAN GET IT , YOUR WELL COME , MY PHONE NUMBER IS 0656 5071 30 OR email adress habarikamili@gmail.com


Hizo zilizo oneshwa hapo ni baadhi ya sample tu na ukiitaka waweza kuipata mzigo upo wa kutosha karibuni sana

Tuesday, November 12, 2013

Dr. SENGONDO MVUNGI AMEFARIKI DUNIA HOSPITALINI SOUTH AFRIKA

Sengondo Mvungi 1
Ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi uliofanywa dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Taarifa iliyotumwa millardayo.com inasema Dr Mvungi amefariki dunia akiwa mahututi hospitalini nchini Afrika Kusini muda mfupi uliopita na taarifa kutumwa nyumbani Tanzania ambapo wafanyakazi wenzake ofisi ya tume ya mabadiliko ya katiba wameambiwa wakae karibu na simu zao ili kikitokea chochote kingine wafahamishwe.
Tayari viongozi mbalimbali kama Mh. Warioba, Katibu wa tume, naibu na watumishi wengine wachache wamekwenda nyumbani kwa marehemu.

UMOJA WA MATAIFA KUONGEZA MAJESHI YA AMISOM 

AU 9fd76
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza nyongeza ya wanajeshi elfu nne zaidi kusaidia kikosi cha Umoja wa Afrika kinachopambana na wanamgambo wa Somalia. (HM)

Baraza hilo pia liliidhinisha Umoja wa Mataifa kutoa msaada wa chakula , maji na vifaa vingine kwa jeshi la kitaifa la Somalia,wakati linapofanya operesheni za pamoja na kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo kinachojulikana kama AMISOM.
Uingereza ilidhamini azmio hilo kupitia balozi wake katika Umoja wa Mataifa Mark Lyall Grant. Balozi huyo alisema kikosi cha AMISOM kimefanya juhudi kubwa kudhoofisha nguvu za kundi la wanamgambo wa al- Shabab. Chanzo: Voaswahili

WENGER ATAKA KUMTIA PINGU YA MIAKA MINNE MERTESACKER 

arsernal 887f4
KLABU ya Arsenal inajiamini beki wake tegemeo, Per Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa muda mrefu. (HM)

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani juu ya vipengele vya Mkataba na inafahamika mazungumzo yanaendelea vizuri.
Mertesacker amedhihirisha yeye ni mwamba wa safu ya ulinzi ya The Gunners akitengeneza ukuta mgumu wa mabeki wanne akicheza sambamba na Laurent Koscielny.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza miezi 18 katika Mkataba wake wa sasa, ambao unamfanya alipwe mshahara wa Pauni 65,000 kwa wiki na kocha Arsene Wenger anataka mustakabali wake ukamilishwe haraka iwezekanavyo.
Na ikiwa mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa, Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa miaka minne, ambao utahusisha kupanda kwa maslahi yake kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Baada ya kuwa mwanzo na mgumu Uwanja wa Emirates, hatimaye beki huyo wa nguvu wa kati amefanikiwa kuteka hisia za mashabiki wa klabu hiyo ya London Kaskazini- akifanya kazi nzuri mwanzoni mwa msimu huu. Chanzo: binzubeiry

MTOTO WA BECKHAM AITEMA MAN UNITED NA KUTUA FULHAM

 beckham2 000ef

KINDA Brooklyn Beckham amepiga hatua nyingine katika harakati za kufuata nyayo za baba yake, kwa kufanya mazoezi na Fulham. (HM)

Beckham mkubwa amestaafu rasmi soka Mei mwaka huu, lakini sasa mtoto wa kiume wa David mwenye umri wa miaka 14 anaweza kuendeleza jina la baba yake katika soka.
Kinda huyo aliongozana na mama yake, Victoria kwenda kucheza mechi katika Uwanja ambao milango ilifungwa akiichezea timu ya vijana ya Fulham chini ya umri wa miaka 15 dhidi ya Southend jana.
Beckham ataendelea kufanya mazozei Motspur Park HQ, Uwanja wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ulio karibu na nyumbani kwao.
Kijana huyo ameonyesha nia ya dhati ya kufuata nyayo za baba yake kwa kufanya mazoezi na klabu nyingine kadhaa England, ikiwemo timu ya zamani ya baba yake, Manchester United mwezi uliopita ambako aliwavutia makocha wa akademi.
Beckham mdogo pia amefanya mazoezi na Chelsea na Queens Park Rangers mwaka huu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO PLC, JIJINI DAR LEO 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Afisa Utawala wa Benki ya Maendeleo, Rose Mushi, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Wa pili (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene (kulia) ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene. (P.T)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa kadi ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account katika benki hiyo, Elianasa Marco Njiu,mkazi wa jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Nov 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa kwanza kupata mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa bemki hiyo,leo.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.

TANAPA YAJIKITA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI 

Tanapa_4_1d54a.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema hii leo juu ya mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya uwekezaji, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Tanapa_5_69f4f.jpg
Baadhi ya waandish wa Habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakati akielezea mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya uwekezaji.
Picha na Eliphace Marwa, MAELEZO (P.T)
Tanapa_2_40f46.jpg
Hifadhi ya Serengeti ni moja kati ya maajabu Saba Barani Afrika.
Tanapa_3_ad8b9.jpg
Hifadhi ya Mikumi inapatikana Mkoa wa Morogoro
Tanapa_1_5f558.jpg
Hifadhi za milima Udzungwa inapatikana katika mkoa wa Morogoro ni moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetenga maeneo 34 kwa ajili ya uwekezaji katika huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi mwa nchi kwa ajili ya utalii.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mkuu wa TANAPA bw. Allan Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya shirika hilo kupanua Sekta ya utalii hapa nchini hasa kwa kupanua huduma za malazikatikahifadhizaKilimanjaro,Katavi,Mikumi,Mkomazi,Ruaha,Saadani,tarangire,Rubondo na Kitulo.
Akifafanua zaidi bw. Kijazi alisema lengo la Tanapa ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyotengwa yanapata wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kutafanyika kongamano maalum mwezi Februari 2014.
Bw. Kijazi alisema kuwa kongamano hilo litawaleta pamoja wakezaji wakubwa na wadogo ambao watapata fursa ya kuyafahamu maeneo hayo na namna gani uwekezaji wao utakavyoleta faida kwa sekta ya utalii na uchumi nchini.
Aidha Bw. Kijazi alisema kwamba vitanda katika maeneo ya hifadhi kwa sasa kuna vitanda 6,681 ambapo kwa miaka mitano ijayo idadi hii itafikia vitanda 8,421.
Aliweka bayana kuwa uamuzi wa TANAPA kutenga maeneo mapya ya uwekezaji umezingatia ukuaji wa sekta ya utalii nchini ambapo karibu asilimia 75 ya wageni wanaofika nchini ni watalii.
Baadhi ya vivutio vinavyoifanya Tanzania kuongoza katika Afrika na Dunia katika Sekta ya utalii ni pamoja na Hifadhi za Taifa Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire.
Vivutio vingine ni Ziwa manyara, Arusha,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na pori la Akiba la Selous.
Mwisho