TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 31, 2013

KODI YA SIMU KURUDI BUNGENI AGOSTI MWAKA HUU KWA AJILI YA KUJADILIWA UPYA


SAKATA la kodi ya simu ya Sh 1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayolipwa na watumiaji wa simu, litamalizwa bungeni kisheria. 

Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesema wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala wa kodi hiyo.

Alisema hayo alipozungumza jana na Habari leo, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 344, kutoka Benki ya Dunia, ili isaidie masuala mbalimbali katika sekta ya usafirishaji. 
 
Mgimwa alisema katika suala hilo, masuala ya kisheria yatafikishwa bungeni mwezi ujao, ili kumaliza utata wa kodi hiyo.


Alisema uamuzi wa kushughulikia suala hilo, ulifikiwa kutokana na agizo la Rais Kikwete la hivi karibuni, kutaka wizara hiyo na ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa na kampuni za simu kumaliza utata uliojitokeza kuhusu kodi hiyo.

Awali Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya mawasiliano.

Mbali na Moat, pia baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi, walipinga kodi hiyo kwa walichokieleza kuwa itaongeza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mtumiaji, hususan wa kipato cha chini.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alipozungumza na gazeti hili jana, alisema mara baada ya Rais kutoa agizo, wizara husika zilikutana kufanyia kazi agizo hilo.
"Rais akishaagiza kinachofuata ni utekelezaji na sisi kesho yake tulianza vikao na ninachoweza kukwambia tuko pazuri na tukikamilisha majadiliano yetu, tutatoa taarifa," alisema Makamba.

Alisema lengo ni kuangalia kama Serikali inaweza kupata Sh bilioni 178 kutoka vyanzo vingine, iwapo itaamua kufuta kodi inayotokana na tozo ya Sh 1,000 kutoka kwenye laini za simu.

Hivi karibuni, Rais Kikwete aliagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana kutafuta jinsi ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.

Alitoa maelekezo hayo baada ya kukutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel. 

Rais alisema lengo kuu la mkutano huo, liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh bilioni 178 ambazo zitapotea katika bajeti, iwapo kodi hiyo itafutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/14.

Aliwaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo litakalotokeza, huku tayari Bunge limezipangia matumizi.

“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la Sh bilioni 178, endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema Rais Kikwete.

Habari Leo

BODI YA MIKOPO YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA


Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni

mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.

RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14 

Tenga-wa-TFF1 90ab3RATIBA ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu.
Kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).
African Lyon (Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi B.
Timu za kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).
Tunapenda kukumbusha kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili ni Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
(HM)
 
WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.
Mtihani huo utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika mtihani huo. Chanzo: Boniface Wambura

UN: VIFO KUTOKANA NA HIV VYAPUNGUA AFRIKA

hiv 8da7b
UMOJA wa Mataifa umetangaza kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi Mashariki na Kusini mwa Afrika vimepungua kwa asili mia 40.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS umehusisha hatua za sasa na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi. (HM)
Umoja wa Mataifa umesema mataifa ya Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu wanaokufa kwa ukimwi kwa zaidi ya nusu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005. Chanzo: bbcswahili

ASHTON : MOHAMMED MORSI YUKO SALAMA 

050 71c67MWAKILISHI wa mambo ya nje katika Muungano wa Ulaya Catherine Ashton amekutana na Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi katika eneo lisilojulikana. Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi tangu kuondolewa madarakani mapema mwezi huu.
Ashton amewaambia waandishi wa habari mjini Cairo kwamba Bw. Morsi alikua salama na kwamba alikubaliwa kutazama habari kwenye runinga na kusoma gazeti.
Alisema walijadili haja ya Misri kuganga yajayo na kuweka amani.Baroness Ashton amesema mchakato wa utawala mpya sharti ushirikishe pande zote. (HM)
Msemaji wa Bi Catherene Ashton, alisema kuwa mkutano ulifanyika katika eneo lisilojulikana ambako Morsi anazuiliwa na kuwa ulidumu kwa masaa mawili.
Hakutoa maelezo kuhusu walichokijadili.
Hata hivyo tayari ameshakutana na maafisa kadhaa wa serikali akiwemo rais wa muda Adly Mansour, mkuu wa majeshi, Generali Abdel-Fattah al-Sisi na makamu wa rais wa maswala ya kigeni,Mohamed ElBaradei.
Alisema kuwa atatoa wito kwa pande zote mbili kushirikishwa katika serikali. Ziara ya Ashton ambayo ni ya pili nchini Misri inakuja baada ya wafuasi zaidi ya sabini wa Morsi kuuawa kwenye makabiliano na vikosi vya usalama nchini Misri.
Wafuasi wa kiongozi huyo wamesema kuwa wanapanga kufanya maandamano Jumanne huku serikali ya muda ikiwatahadharisha dhidi ya kuhusika na ghasia na kuwa watakaovunja sheria watachukuliwa hatua.
Maafisa wa usalama pia wametishia kuvunja maandamano ya wafuasi hao waliopiga kambi nje ya medani iliyo karibu na msikiti wa Rabaa al-Adawiya mjini Cairo. Chanzo: bbcswahili

FERNANDO GAGO ARUDI KWAO ARGENTINA

bwin 0a5b0
KIUNGO wa kiargentina Fernando Gago amekamilisha usajili wake wa kurudi kwenye klabu ya nyumbani kwao ya Boca Juniors akitokea Valencia baada ya kufaulu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitatu jumatatu.  (HM)

Gago tayari alishacheza kwa miezi Boca akitokea Valencia lakini Boca waliamua kumrudisha moja kwa moja kiungo huyo ambaye alianza kucheza soka la ushindani mnamo mwaka 2004 akiwa na klabu hiyo.
Gago alijiunga na Real Madrid mnamo mwaka 2007 na kusiadia klabu hiyo kushinda ubingwa wa La Liga mara mbili kabla ya kuhamia Valencia msimu uliopita akitokea AS Roma alipopelekwa kwa mkopo na Madrid baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.  Chanzo: shaffihdauda

KINDA LA BURKINA FASO lAMKUNA MOURINHO KWENYE PRE SEASON YA CHELSEA 

kinda 222e7
KINDA la Burkina Faso Bertrand Traore ni mmoja wa makinda waliomvutia sana kocha wa Chelsea Jose Mourinho katika mechi za maandalizi ya msimu mpya huko barani Asia. (HM)

Kwa sababu ya kanuni za usajili mchezaji huyo sio mchezaji rasmi wa The Blues mpaka atakapotimiza miaka 18 mnamo tarehe 6 September, hapo ndipo anaweza kusaini mkataba wa kuitumikia Chelsea.
Wiki hii katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya  Malaysia XI alifunga bao zuri sana na akaongeza bao jingine katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Indonesia All Stars.
"Ni kijana mdogo, lakini nina uhakika atakuja kuwa na umuhimu sana ndani ya kikosi cha Chelsea cha baadae," mchezaji mwenzie Gary Cahill alisema.
Traore alikuwa sehemu ya kikosi cha Burkina Faso kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 2012 zilizofanyika Equatorial Guinea na Gabon - alicheza katika mechi aliyotokea benchi dhidi ya Sudan katika mchezo wa makundi.

Cahill anasema Traore sio muoga na anajiamini sana akiwa mazoezini akicheza na wachezaji wakubwa wa kikosi cha kwanza. 

"Ameweza kuingia vizuri kwenye timu ya wakubwa. Amezoea. Ni mapema sana kusema yupo tayari kucheza kwenye level ya juu, itakuwa sio vizuri akijiamini kupita kiasi." - Cahil

Traore hakuitwa na kocha Paul Put kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mapema mwaka huu huko Afrika ya Kusini, ambapo timu yake ilienda na kushika nafasi ya pili nyuma ya Nigeria. Lakini amekuwemo katika kikosi cha sasa ambacho kipo katika nafasi nzuri ya kufuzu kuingia kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya kufuzu kombe la dunia. 

Mapema January 2011, Traore alikaririwa akiongea na kipindi cha Fast Track cha BBC akisema; "Nataka kucheza kwenye kikosi cha kwanza Chelsea, nataka kucheza kwenye Champions league na timu zenye majina makubwa.

"Nataka kucheza kila mechi ya timu ya Chelsea na huko mbeleni ningependa kuja kuwa mchezaji bora kutoka Afrika kuichezea Chelsea." Chanzo: shaffihdauda

WAZAZI WA GARETH BALE WAINGILIA KATI SUALA LA USAJILI WA MTOTO WAO

bareth edd87
Wazazi wa mchezaji GARETH BALE wameingilia kati suala la uhamisho wa mtoto wao anayetakiwa na Real Madrid kwa udi na uvumba katika dirisha hili usajili. (HM)

Real Madrid inasemekana wametoa ofa ya kiasi cha £81m kwa Tottenham kwa ajili ya kumsaini winga huyo wa kimataifa wa Wales lakini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesisitiza mchezaji huyo hauzwi.

Lakini baada ya mchezaji husika kusemekana kwamba anataka kuondoka Spurs na kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa ulaya huku Spurs ikiweka ngumu, jana wazazi wa mchezaji wameingilia kati suala hili baada ya kuonekana wakiwa kwenye mkutano mzito na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy.
Kwa mujibu wa shuhuda wa gazeti la The Sun ni kwamba jana wazazi wa Bale walikutana na Levy kwenye ofisi za Spurs zilizopo kwenye viwanja vya mazoezi vya timu hiyo: “Sikuweza kuamini wakati Bale alipowasili kwenye uwanja wa mazoezi na wazazi wake, mungu anajua nini walienda kuongea na Mr Levy.
”Mwenyekiti huyo wa Spurs alikatisha muda wake wa mapumziko na familia yake na kwa haraka amerudi jijini London kwa ajili kushghulikia suala la Bale.
Lakini pia imeripotiwa kwamba Raisi wa Real Madrid Florentino Perez anatarajiwa kukutana na Levy jijini Miami mapema wiki ijayo ili kuzungumza kuhusu sakata hili la usajili wa Bale.
 

Perez tayari yupo nchini Marekani - mahala ilipo timu yake ikiwa inajiandaa na msimu mpya.Inaaminika kwamba baada ya Spurs kukataa ofa ya paundi millioni 82, Real wamerudi na ofa inayohusisha kiasi cha £51 pamoja na wachezaji wwili wa Madrid Angel Di Maria na Fabio Coentrao.
Lakini bado vilabu hivyo vinabishana kuhusu thamani halisi ya wachezaji hao wawili wanaowekwa kwenye dili la usajili wa Bale. Chanzo: shaffihdauda

MKOA WA RUKWA KUJENGA CHUO KIKUU

IMG 1295 c867c
Jennifer Chamila-Maelezo
MKOA wa Rukwa unatarajia kuanzisha chuo kikuu ambacho kitasaidia vijana wengi wanaokosa nafasi za kuendelea na elimu ya juu kwa kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.
Mkakati huo unaosimamiwa na Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa(JUMARU) ambao ni halali chini ya sheria za nchi ilioanzishwa mwaka 2009 na wakazi wa mkoa wa Rukwa(Wanarukwa) kwa lengo la kuunganisha nguvu za wanarukwa wote ili kuleta maendeleo katika mkoa huo na wakazi wake.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Sekretariati wa JUMARU Bw.Joachim Sikulumbwe amesema kuwa wameandaa kongamano la wanarukwa wote waishio jijini Dar es Salaam litakalo fanyika Septemba 01 mwaka huu,katika ukumbi wa Ubungo –Urafiki Social hall.
"Kongamano hilo litazungumzia maliasili na rasilimali za mkoa wa Rukwa na maendelao yake ,kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni nawaomba wanarukwa wajitokeze na kuhudhuria kwa wingi"alisema bw. Sikulumbwe,
Naye Makamo mwenyekiti kamati ya wahadhiri mchakato wa chuo kikuu cha Rukwa bw.Bernard Kasimila amesema sababu ya kuanzisha chuo hicho ni kuwezesha vijana wenye sifa za kuendelea na masomo kupata fursa ya kujiunga na chuo kikuu.
Mkoa wa Rukwa ni sehemu ya Tanzania iliyoko nyanda za juu kusini yenye wakazi zaidi yawakazi milioni moja kwa sense ya 2012 , una wilaya 3, halmashauri 4,tarafa 17,kata 64,na vijiji 202,unajishughuli zaidi na kilimo,uvuvi na utalii.
Mwisho

TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUBADILISH​ANA WAFUNGWA

photo 21543
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(kulia) pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Mhe. Sura Pong Tovichakehaikul(kushoto)wakisaini Mkataba wa kubadilishana Wafungwa kati ya Tanzania na Thailand(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

WAZIRI MKUU WA THAILAND AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA SIKU 3

Picha na 5 8a80a
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
Picha na 7 1345a
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
VIJANA WAASWA
PIX1 c2886Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
PIX3 dc37f
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam

Na Frank Shija - Maelezo
Vijana nchini wameaswa kujitambua na kuthubutu kwa malengo chanya pamoja ikiwa ni pamoja na kujituma kufanya kazi zikiwemo za kujitolea kwa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kujikwamua na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla..
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara alipokuwa akifungua kambi ya dunia ya vijana leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Fenella amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoe na kufuata mikomba ambapo ni hatari sana matokeo yake wamekuwa wakijikuta wakitenda tofauti na malengo yao.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa vijana kujitambua na kubadilisha fikra zao hili waweze kujiletea maendeleo wao wenyewe baadala ya kulalamika kama ambavyo wamekuwa wakifanya.
"Ni muhimu vijina mjitambue na mthubutu kwa malengo chanya, na muanze kwa kila mmoja wenu kujituma kufanya kazi na wakati mwingine jitoleeni kwa faida ya jamii zenu". Alisema Waziri Fenella
Aliongeza kuwa Mungu amewajali vijana Talanta na vipaji tofauti hivyo ni muhimu vikatumika kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla na kuongeza kuwa kujitambua kwa vijana kuendane na uthubutu ili kujikwamu kimaendeleo.
Kwa upande wake mwanzilishi wa IYF duniani Pastor Park Ock Soo amesema kuwa ni faraja kwake kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki kambi hiyo akiamini malengo ya kuanzishwa kwa taasisi yake yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.
Pastor Park ameongeza kuwa vijana wanapaswa kubadili fikra na mitazamo yao ili kuenenda na kasi ya kujiletea maendeleo badala ya kulalamika na kusubiri kufanyiwa kazi.
Kambi hii ya vijana ni inafanyika hapa nchini kwa mara ya tano na imeandaliwa na taasisi ya International Youth Fellowship (IYF) kutoka Korea kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "Badilisha Fikra ktuoka mtazomo hasi kuw chanya"

Tuesday, July 30, 2013

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.

Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.
WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA
CIMG8385 aa063
CIMG8390 44a58
Wizara ya Afya yapokea msaada wa magari mawili na pikipiki kumi zenye thamani ya sh.milion 124,202,800 kutoka shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani.

MASTAA 10 WA KIKE KUTOKA HOLLYWOOD WALIOLIPWA MAMILION YA DOLA ZAIDI YA MASTAA WENGINE WOTE KWA MWAKA 2012-2013

hollywood-sign
Nani analipwa pesa nyingi kwa movie anazofanya?, swali hili limeleta utata mara kadhaa pale mastaa wengi wa bongomovie wanapoulizwa na vyombo vya habari na kushindwa kujua hadi leo msanii yupi analipwa pesa nyingi kwa movie anazocheza. Lakini ukija kwenye anga za Hollywood, sio siri hata kidogo kuhusiana na nani kavuna pesa nyingi mwaka huu kwenye kazi za uigizaji. Kitu hiki pia kinasaidia kuongeza thamani na hata uhitaji wa movie producer na directors wengi kutaka kupanga waigizaji hawa kwenye movie zao kwasababu ya image wanayoipata  kwa jamii baada ya kujulikana kuwa wanaolipwa pesa nyingi kwenye uchezaji wa movie zao. Bongomovie siku moja itakuwa nzuri ikiwa tukijua hata kwa mwaka mmoja uliopita nani kavuna pesa nyingi kwenye kazi za uigizaji.
Hii hapa ndiyo list ya waigizaji wa kike huko Hollywood walivuna pesa nyingi sana kuanzia June 2012 hadi June 2013.
World War Z - World Premiere - Red Carpet Arrivals
Angeline Jolie – $33 million
Mkali wa movie kama Mr and Mrs Smith,Tom Rider, Tourist na nyingine nyingi mara kadhaa amehusishwa kwenye mdahalo wa kwanini Angeline Jolie ni most powerful woman in Hollywood. Hii list inaendelea ku-prove ukweli juu ya sentensi hii, Angelina Jolie ambaye pia ameanza kujihusisha na maswala ku-direct movie ameingiza kiasi cha dola millioni 33 katika kipindi cha miezi 12. Angeline ana miaka 38 na watoto sita ikiwa wengine ni wa ku-adopt.
'Jimmy P. (Psychotherapy Of A Plains Indian)' Premiere - The 66th Annual Cannes Film Festival
Jennifer Lawrence- $26 million
Mshindi wa tuzo kubwa na zenye heshima kwenye movie industry huko Hollywood, hapa nazungumzia Oscar Awards ambazo mastaa wengi wanatamani kuzipata lakini yeye ameipata kama muigizaji bora wa kike akiwa na miaka 22 tu. Unaambiwa hadi jarida la Times walimuweka kwenye list ya 1oo most influential people duniani.Profile hii ni kubwa sana, kuna kipi cha kumzuia asiwe kati ya waigizaji wanaolipwa pesa nyingi huko Hollywood. Young,talented and still getting it kwenye bank account.
85th Annual Academy Awards - Arrivals
Kristen Stewart – $22 million
Watu wangu wa The Twilight mtakuwa mnamsoma huyu actress, kati ya mastaa wakubwa watatu wa movie za Twilight na yeye ndiyo msichana pekee. Mwaka jana alikuwa ndio actress anayelipwa ziadi kuliko wote huko Hollywood, mwaka huu amekuwa watatu kitu ambacho sio kibaya.
"Just Go With It" New York Premiere - Outside Arrivals
Jennifer Aniston – $20 million
Licha ya kupata mkwanja mwingine kupitia bidhaa zake kama mineral water na vipodozi vingine, Jennifer Aston bado anakamata nafasi ya pili katika hii list. Pia media zinampenda sana kama Wema huku Bongo, huwa haishiwi story  za kuandikwa. Mwaka 2012 vyombo vingi vya habari viliandika kuhusu kuvishwa kwake pete na actor Justin Theroux
Emma Stone Sighting In New York City - May 28, 2013
Emma Stone – $16 million
Kama ulishawahi kuangalia Amazing Spiderman, yule girlfriend wa spiderman ndiyo huyu Emma Stone. Amazing spiderman ni moja kati ya movie zenye bajeti kubwa alizowahi kufanya, so kwanini asilipwe pesa nyingi kama anafanya movie zenye bajeti kubwa kama Amazing Spiderman.
17th Annual Critics Choice Movie Awards - Arrivals
Charlize Theron – $15 million
Mwaka 2011 alifanya movie kama Young Adult,2012 alifanya movie maarufu ya Snow White and the Huntsman. Charlie Theron anakamata namba 6 kwa kuingiza dola millioni 15.
7
Sandra Bullock – $14 million
Mshindi mwingine wa Oscar,ameingiza dola za kimarekani millioni 14. Yupo namba saba kwenye list ya actress wanaolipwa zaidi huo Hollywood.
Natalie Portman
Natalie Portman – $14 million
Star Wars films, Thor zote hizi anahusika nazo. Kitu kingine ni kwamba Natalie ni mshindi wa tuzo za Oscar, hii ni sababu ya msingi sana ya kufanikiwa kupata kazi kubwa za kumuigizia pesa nyingi.
Oz: The Great And Powerful - UK Premiere - Red Carpet Arrivals
Mila Kunis – $11 million
Mwanamke ambaye pia anatajwa kati ya wanawake warembo huko Hollywood , mwaka huu ameingia kwenye hii list kutokana na movie kubwa kama TED najua hii  wengi mnaijua kutoka na kuwa maarufu sana. Pia movie kama Oz: The Great and Powerfulearned  ambazo kwa pamoja zimefanya vizuri na kuingiza dola za kimarekani zaidi ya billioni moja. Mila Kunis pia alifanya vizuri kwenye movie ya Friends with Benefit akiwa na Justin Timberlake ambayo pia ni moja kati ya movie zake maarufu miaka iliyopita.
Julia Roberts
Julia ROberts – $11 million
Julia ni actress ambaye anachagua sana movie za kufanya, lakini hiyo sio sababu ya kumfanya asiwe kwenye hii list. Licha ya kuchagua hizo movie, yeye ndiyo anatufungia list hii kwa kuwa na dola millioni 11.

CHADEMA HAINA UBAVU WA KUMKATAA TENDWA


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Chadema kinaitambua ofisi ya Msajili wa Vyama tu lakini hakimtambui Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

“Hatumpelekei hata barua huyu hatunzi sheria siyo mtu wa kulea vyama ni mlezi wa chama kimoja, hayuko serious na hatushirikiani naye mpaka aondoke madarakani.

“Tukiandika barua hatuweki jina lake lakini tunaitambua ofisi yake, hata yeye mwenyewe analijua hilo na akijibu barua zetu haweki jina lake,” alidai Dk. Slaa.

Akijibu hoja hizo, Naibu Msajili alisema Chadema hawana ubavu wa kutomtambua Tendwa kwa sababu amewekwa kisheria na ofisi yake ipo kisheria.

Alisisitiza Tendwa ataendelea kuwa mlezi wa vyama vyote na siyo chama kimoja kama inavyodaiwa na kuvitaka vyama vyote kuheshimu sheria iliyomuweka madarakani msajili huyo.


Mtanzania.

MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI


Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu


"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:

 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huy

MONACO YATHIBITISHA MAN U IMEWAPA OFA YA KUMSAJILI LUIS NANI

 nani1 1773621a d6f60

MATAJIRI wapya katika soko la usajili barani ulaya klabu ya AS Monaco imesema kwamba walipewa ofa ya kumnunua winga wa klabu ya Manchester United Nani. (HM)

 Winga huyo wa timu ya taifa ya Ureno amekuwa njia panda kujua hatma yake ndani ya Old Trafford kabla ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mpaka sasa chini ya manager mpya David Moyes. 

Billionea anayemiliki klabu ya Monaco - Vadim Vasilyev amekiri kwamba United walimpa ofa ya kumsajili  Nani.

Alisema: “Nani tulipewa ofa kumnunua. Ni mchezaji mzuri, lakini hakujawahi kuwa na mazungumo mpaka sasa.”


Monaco wamekuwa na vurugu sana kwenye soko la usajili hivi karibuni, wakiwasajili wachezaji kama Falcao, James Rodriguez  Joao Moutinho kwa bei mbaya sana. Chanzo: shaffihdauda

SABABU ZA YANGA KUPINGA MKATABA WA KAMATI LIGI /TFF NA ZAM TV

manji 768af
Viongozi wa Yanga SC, kutoka kulia Balozi Ammy Mpungwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini, Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji, Waziri George Mkuchika, Mwenyekiti Baraza la Wadhamini, Francis Kifukwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini na Clement Sanga, makamu mwenyekiti (HM)

Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu  kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari: 
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.

Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:

1. BODI YA TPL

1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.

1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.

1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA

2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani. 

2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie  urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.

2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania  watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.

2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa: 

2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi; 

2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama; 

2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.

3. MIGOGORO YA MASLAHI

3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na  kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.

3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira  wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.

3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.

4. KUTOKUWA NA UWAZI

4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari,  na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).

4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.

5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA 

5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia  kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."

5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji  wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo 
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA  Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)  walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.

Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.

Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
MAN UNITED YAUA 5-2
man u c976c
Mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United wamecheza mechi yao ya tano katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya  Kitchee ndani ya uwanja wa  Hong Kong  na kuibuka na ushindi wa mabao 5-2. (HM)
Mechi ya jana ilitakiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini Kocha wa United, David Moyes alilazimika kuahirisha mechi kwa madai kuwa uwanja wa Hong Kong ulikuwa mbovu kufuatia mvua kunyesha na uwanja kujaa matope, huku ukiwa umetumika mfululizo katika michuano ya kombe la  Barclays la Asia.
Hali ya uwanja siku ya jumamosi wakati wa fainali ya Sunderland na Manchester City ilikuwa mbaya sana, lakini viongozi walijitahidi kufanya jitihada za kurekebisha kabla ya mchezo wa jana.
Kikosi cha Kitchee: Comi, Rodriguez, Rehman, Kei, Alkande, Belencoso, Wai, Annan, Yang, To.
Wachezaji wa akiba: Jianqiao, Wen, To, Fung, Quankun, Hau, Fai, Paramo, Lam, Deshuai, Lung
Waliofunga Magoli yao: Lam (53), Alkande (69)
Kikosi cha Manchester United: Amos, Evra (Buttner HT), Anderson, Smalling, Carrick (Jones 72), Young (Januzaj HT), Welbeck (Lingard HT), Fabio (Rafael 72), Cleverley, Zaha, Keane.
Wachezaji wa Akiba: Lindegaard, Rafael, Jones, Ferdinand, Giggs, Van Persie, Buttner, Lingard, Januzaj.
Waliofunga mabao: Welbeck (16), Smalling (22), Fabio (26), Januzaj (47), Lingard (80). Chanzo: Baraka Mpenja

PEPE REINA:LIVERPOOL WAMENILAZIMISHA KUJIUNGA NA NAPOLI KWA MKOPOpepe 0ce14

PEPE Reina amechukizwa na kitendo cha uongozi wa klabu yake ya Liverpool kumlazimisha kujiunga na klabu ya Napoli bila ya kuongea naye kwanza. (HM)
Kipa huyo raia wa Hispania ameandika barua ya wazi kwa viongozi wa Liverpool na kuichapisha katika mtandao wake, huku akiwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuunga mkono wakati akiwa Anfield, lakini kwa sasa amejiunga na kocha wake wa zamani Rafa Benitez anayeifundiha miamba hiyo ya  Serie A.
Liverpool wamemsajili kipa mahiri wa Sunderland Simon Mignolet  na kukubaliana na kocha wa  Napoli  Rafa Benitez  kumchukua Reina kwa mkopo.

Kaondoka zake: Pepe Reina amewashukia viongozi wa Liverpool kumlazimisha kuihama klabu yake

Katika barua aliyochapisha katika mtandao wake, Pepe Reina ameandika hivi: ‘ Najutia kitu kimoja tu, ni jinsi nilivyoondoka”.
“Ni hali ya kawaida kwa kila mtu, hata mimi nimekatishwa tamaa sana baada ya viongozi wa Liverpool kukubaliana na Napoli ili nikacheze kwa mkopo bila kunihusisha, nafikiri nilistahili heshima ingawa naelewa kuwa katika mchezo wa soka kuna wakati maamuzi magumu yanafanyika“ Chanzo: Baraka Mpenja
MKWASA : NIMEKISUKA KIKOSI CHANGU
mkwasas 3556f
Wakati siku zinazidi kuyoyoma kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote kushuka dimbani, hekaheka za maandalizi zinazidi kushika kasi huku makocha wakihaha kusuka vikosi vya ushindani zaidi. (HM)
Maafande wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani wamesema wamekibadili kikosi chao kwa kusajili wachezaji wapya ambao watasaidia kutwaa ubingwa au kushika nafasi tatu za juu.
Akizungumza na FULLSHANGWE, Kocha Mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Masta” amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi huku akijivunia wachezaji wapya waliowasajili wakiwemo Stephano Mwasyika kutoka Yanga, Elias Maguli kutoka Prisons na wengine wengi.
Mkwasa alisema lengo lao ni kufanya vizuri msimu ujao endapo tu  waamuzi wataacha kasumba ya kuzibeba baadhi ya timu.
“Msimu uliopita waamuzi walitukwamisha sana, walikuwa wanachezesha hovyo na kushindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka, endapo watabadilika na kuzingatia weledi wa taaluma yao, basi tutafika mbali”. Alisema Mkwasa.
Pia Mkwasa alibainisha kuwa msimu uliopita tatizo kubwa lilikuwa safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inakosa nafasi nyingi za kufunga, na ndio maana wamemsajili aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Tanzania Prisons, Elias Maguli.
“Kazi yangu kubwa kwa sasa ni kunoa vijana wangu wa safu ya ushambuliaji, kila wakati naongea nao kuhusu umuhimu wa kutumia nafasi adimu wanazopata wawapo uwanjani. Unajua tatizo la wachezaji wetu ni kukosa umakini, lakini tunapambana nao ili kuwarekebisha na kufika pale tulipokusudia”. Alisema  Mkwasa. Chanzo: Baraka Mpenja

Monday, July 29, 2013

MBONI AFUTURISHA
 
Rais Mstaafu wa Awamu wa Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza baada ya futari.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (CCM), Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) naye alikuwa miongoni mwa waalikwa.
Sauda Mwilima (kushoto), mchumba wa Diamond Penny Mungilwa (kati) na dada wa Diamond Hasna (kulia) wakifuturu.
Mwanamuziki  wa miondoko ya mduara Zuwema Mohamed 'Shilole' (wa pili kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa.
Baadhi ya wageni waalikwa.
Meya wa Ilala Jerry Slaa (kulia) na wageni wengine wakati wa futari hiyo.
Mkurugenzi  wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Asha Baraka (kushoto) naye alikuwepo.
Mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba akiongea jambo.
Shekhe Sharif (kushoto) naye alikuwepo kwenye futari hiyo.
Mboni akiwa na baba yake mzazi mzee Masimba.
Mboni akifanya mahojiano na Mzee Mwinyi.
Mboni akimkabidhi zawadi ya kikombe Mzee Mwinyi.
Mboni akimuelekeza Mzee Mwinyi sehemu ya kusaini.
Mzee Mwinyi, Mboni pamoja na Asha Rose Migiro wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima kutoka vituo mbalimbali.

Penny, Husna na Joan katika pozi.
Kutoka kulia: Shilole, Husna, Penny katika pozi na baadhi ya waalikwa.
MTANGAZAJI wa kipindi cha Mboni Show kinachorushwa kupitia televisheni ya East Afrika, Mboni Masimba jana alifuturisha wageni mbalimbali na viongozi akiwepo Rais Mstaafu  wa Awamu ya Pili, Mhe Ali Hassan Mwinyi na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (CCM) ambaye pia alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa, Dk. Asha - Rose Migiro, katika ukumbi wa Karimjee uliopo Posta jijni Dar es Salaam.