TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, May 31, 2013

MZUMBE SECONDARY YAFUNGWA...WANAFUNZI WAPEWA SIKU MBILI WAPOTEE KATIKA MAZINGIRA YA SHULE


Wananfunzi wakidato cha kwanza hadi cha sita katika shule ya sekondari Mzumbe Morogoro wamelazimika kuandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa huo wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu.

Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni pamoja na miundombinu, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.

Maandamano hayo yalizimwa mapema asubuhi baada ya jeshi la polisi kulazimika kufika katika eneo la
sangasanga barabara kuu ya Iringa Morogoro ambapo maandamano hayo yalikuwa yamefika kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Wananfunzi hawa wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro ya wenye vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.

Mkuu wa shule ya sekondari Mzumbe Dismas Njawa ameelezea namna alivyoweza kutatua baadhi ya matatizo lakini hayakukidhi haja za wanafunzi hao.

Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu alilazimika kwenda kuzungumza na wanafunzi hao akiahidi kuyafanyia kazi yale yatakayo wezekana.



Wanafunzi hawakuelewa, na ndipo Serikali ilipoamua kuifunga shule ya Sekondari ya vipaji maalumu, Mzumbe kwa muda usiofahamika na kuwapa wanafunzi siku mbili, kuanzia leo, kuondoka shuleni hapo
---
Monica Lyampawe,
TBC Morogoro.

NAIBU SPIKA AAPA KUTOMWADHIBU MBUNGE YEYOTE KWA MADAI KWAMBA AMECHOKA KUITWA ZEZETA


Naibu Spika wa Bunge,Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kuanzia sasa hatamwadhibu Mbunge yeyote anayeleta vurugu Bungeni kwakuwa amechoka lawama. 

 Akihojiwa na Redio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka leo asubuhi ,Ndugai amesema kuwa yeye amechoka kuitwa mzembe,zezeta na goigoi na vyombo vya habari.

Ndugai amesema kuwa hata kwa Wabunge waliosababisha tafrani Bungeni jana kiasi cha kuchana Nyaraka za Bunge,hawatachukuliwa hatua yoyote.

 "Kila Mbunge anayeadhibiwa na Kiti cha Spika anaonekana Shujaa. Sisi tunamuona mtovu wa nidhamu,wananchi wanamuona shujaa.Siko tayari tena kwa hilo".alisema Ndugai

Kuhusu uandalizi wa Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kama hupitiwa kabla ya kusomwa Bungeni,Ndugai amesema kuwa Bajeti hizo zinapaswa kujadili mafungu ya Bajeti husika ya Serikali na si vinginevyo. 


"Kwanza hawa wenzetu wanatoka na Bajeti zao nyumbani moja kwa moja na kuja kuzisoma pale.Hawapaswi kutunga za kwao.Wanatakiwa kujadili mafungu ya Bajeti ya Wizara husika tu. Wakati mwingine mtu mmoja anajiandikia tu Bajeti ya Upinzani wenzake hawawezi kumkana Bungeni" alisema kwa hasira Ndugai.

Alipoulizwa kuhusu kutenda haki kwa kuwaadhibu na Wabunge waCCM,Ndugai alikwepa na kuanza kufoka kuhusu Wabunge wa CHADEMA kuwa hawana nidhamu na hatowagusa tena. ‘Watanzania si ndivyo watakavyo….sawa,na sisi tutawaacha ili wasiwe mashujaa!’ alisisitiza Ndugai.

TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA


TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL – TANGA MEI 30, 2013
UTANGULIZI:Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.
Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam kwa maelezo kuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.
Mazingira ya kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda yalitia wasiwasi kuwa upo uwezekano, na dalili zilionyesha kwamba waliofanya kitendo hicho cha kinyama hawakuwa wezi wala majambazi kutokana na ukweli kwamba licha ya kuwa na fedha zipatazo shilingi milioni tatu taslimu ndani ya gari, laptop, simu tatu za gharama (ipad, iphone na Blackberry), watekaji hawa hawakuchukua chochote baada ya kukamilisha uhalifu wao.
Kibanda aliumizwa kwa kiwango kikubwa. Alitobolewa jicho la kushoto, akaumizwa vibaya kichwani kiasi cha kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa.

Aling’olewa meno mawili na kucha mbili, tena bila gazi. Watekaji hawa, katika unyama wa ajabu kabisa, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.Hali hiyo iliibua maswali mengi, watu wengi wakajiuliza na kutafuta sababu za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda kiasi hiki. 
Kutokana na kuwapo kwa maelezo mengi yanayotofautiana kuhusu tukio hilo, ikabidi Jukwaa la Wahariri Tanzania lifanye uamuzi.Katika kikao cha Machi 8, 2013 Jukwaa la Wahariri Tanzania liliunda TIMU ya watu watano na kuipa hadidu rejea za kufanya uchunguzi wa kihabari juu ya shambulio hilo kubaini limetokana na nini.

Timu hiyo iliundwa kufuatia uamuzi wa Jukwaa la Wahariri kufanya uchunguzi huo na baada ya kukubalika kwa ombi la ruzuku ya kufanya uchunguzi huo wa kihabari kutoka Mfuko wa Vyombo Vya Habari Tanzania (TMF). 
Ruzuku ya TMF ililenga kiujumla kutumia tukio la Kibanda kuwa chanzo cha kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi na wahariri na kwamba kiwango cha matukio ya kuteswa, kupigwa na kuuawa kwa waandishi yanapungua kila mwaka. Timu hii imefanya kazi usiku na mchana kwa kwa zaidi ya mwezi. Timu imezungumza na wadau 26.

Kati ya hawa yumo Kibanda mwenyewe, mke wake, ndugu zake, wasaidizi wake, waajiri wake wa zamani na wa sasa, viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola kutafuta ukweli wa jambo hili. 
Pia tumesoma matamko na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya kati ya Machi 5, 2012 na Aprili 5, 2012 kwa nia ya kufanya ulinganishi wa taarifa tulizozipata kutokana na uchunguzi na habari zilizochapishwa baada ya kutekwa kwake.
Vyombo vya dola akiwamo Waziri mwenye dhamana walikataa kuhojiwa wakisema kuna tume ya serikali inayofanya kazi hiyo na kwamba kuhojiwa kungeonyesha kutokuwa na imani na tume hiyo.

Leo tunawasilisha muhtasari wa ripoti hii. Ripoti kubwa pamoja na viambatanisho vyake, itachapishwa na kuwekwa katika kitabu kimoja. Utaratibu mwingine wa kuchapisha habari ambazo hazijachapishwa kuhusiana na tukio hili (untold stories) pia utaandaliwa kwa ushirikiano na Jukwaa la Wahariri kwa nia ya kuieleza jamii maajabu juu ya kadhia hii.Tulipewa Hadidu Rejea ziafuatazo:

HADIDU REJEA:
1. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.
2. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.
3. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006), Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.
4. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.
5. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika

YALIYOJIRI KATIKA UCHUNGUZI:
1.0. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.Timu ya uchunguzi ilitumia muda mwingi katika eneo hili, kubaini iwapo kulikuwapo viashiria, sababu au matukio ya wazi yenye mwelekeo wa kujitokeza kwa shambulio hili. 
Tuliangalia pia iwapo wapo watu au makundi yaliyokwishapata kuonyesha ishara kwa matendo au kwa kauli juu ya uwapo wa nia hii. 
Uchunguzi umebaini kuwa kuliwapo viashiria vingi, isipokuwa Kibanda au watu wake wa karibu hawakupata kufikiri kuwa huenda vingeweza kuleta madhara makubwa kiasi hiki kama ifuatayo:-

1.1. Wiki tatu kabla ya Kibanda kuvamiwa, kutekwa na kuumizwa, gari la polisi aina ya gofu Na PT 180 liliwafuatilia kwa muda mrefu Absalom Kibanda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe likiwa limeegeshwa nje ya ofisi zao Sinza Kijiweni na baadaye likawafuatilia hadi Sinza Makaburini, ambapo walisimamisha magari yao na kuzungumza na polisi hao waliosema walikuwa wanatilia shaka magari yao. Baada ya kuzungumza kwa muda polisi waliondoka.

1.2. Usiku wa Februari 25, mwaka huu majira ya saa 09:00 usiku, Kibanda walivamiwa na watu walioingia kwenye uzio wa nyumba yao wakavunja kioo cha gari analotumia, lakini kioo kilipovunjwa ‘alarm’ ilipiga kelele, Kibanda akatoka nje na watu hao wakakimbia.

1.3. Kutokana na uvamizi huo, Kibanda na wapangaji wengine katika nyumba zilizopo kwenye uzio mmoja, waliona hatari ya kuvamiwa hivyo wakaanza mazungumzo na kampuni ya Ulinzi ya Kiwango, iliyowataka kufunga kamera za usalama na kuweka walinzi watano. Hadi Kibanda anatekwa, walikuwa hawajahitimisha mazungumzo na kampuni hii ya Kiwango.

1.4. Kuna askari anayefanya kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) miezi minane kabla alipata kumpa Kibanda taarifa za kinteligensia, kuwa kulikuwapo mpango wa kumteka na kumuumiza. 
Taarifa kama hizo pia alipewa na wasamaria wanaofanya kazi katika Jeshi la Polisi. Kwa maneno yake Kibanda alisema:“Kuna rafiki yangu askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama miezi minane au tisa hivi aliwahi kuniambia ‘unaandika sana usidhani kama watu wanakupenda. Chukua tahadhari hasa unapofika getini nyumbani kwako’.
 Tangu wakati huo nimekuwa nikichukua tahadhari sana.“Wiki mbili kabla ya tukio, niliwahi kuhisi kitu kama hicho [cha kuvamiwa] nikiwa getini. Nilipiga honi wakachelewa kuja kunifungulia, niliogopa sana. 
Hata nilipoingia ndani nilikuwa nimekosa raha kabisa.“Pia kuna rafiki zangu polisi waliwahi kuniambia kwamba ninatafutwa na kwamba watu wananifuatilia na ikibidi wanitengenezee ajali au kunifanyia kama Ulimboka au Kubenea.”

1.5. Ndani ya miezi mitatu mbele ya mlango wa ofisi yake Kibanda (Free Media Limited) ilikuwa mara kwa mara muda wa asubuhi anapofika ofisini anakuta damu. Haikufahamika kama damu hiyo ilikuwa ni ya binadamu, kuku, ng’ombe, kunguru au mbuzi, bali waliipuuza wakidhani ni masuala ya ushirikina. Mhariri Mtendaji wa sasa, Ansbert Ngurumo, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
1.6. Mfanyakazi mwandamizi wa Kampuni ya New Habari anakofanya kazi sasa Kibanda ndani ya wiki mbili kabla ya kutekwa na kuumizwa kwake alipata kumwabia Kibanda maneno mazito mara tatu, na hapa tunamnukuhu Kibanda:“Aliniambia Danny Mwakiteleko [aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari] hakufa kwa ajali, bali alikufa kutokana na blood clotting (kuganda kwa damu). 
Hivyo ikitokea mtu ukapata ajali au ukapigwa na kuumizwa sana sehemu za kichwa hivi au tumbo, ni lazima madaktari wadhibiti sana blood clotting.“Na kweli, nilivyoletwa hapa Milpark hospitalini, madaktari walikuwa wananidunga sindano sita kila siku kwenye kitovu kuzuia blood clotting. …. (jina linahifadhiwa) aliniambia maneno haya mara tatu, katika mazingira yasiliyotarajiwa na kwa msisitizo ambao sikujua maana yake. Nasema …. (jina linahifadhiwa) naye achunguzwe kwa kina. 
Inawezekana kuna jambo analijua.”Ofisa huyu, alipishana dakika chache na Kibanda muda wa kutoka ofisini baada ya kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Real Madrid na Manchester united kumaliza nusu ya kwanza (half time). Dakika ishirini baadaye Kibanda alishambuliwa.

2.0. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.
2.1.Familia ya Kibanda na Kibanda Mwenyewe hawakuwa na wasiwasi wowote siku hiyo kwani hawakuwa na hisia wala wazo kuwa ungetokea uvamizi huo.

2.2. Kibanda alipopiga honi, mlinzi alisogea langoni kumfungulia. Ghafla akasikia kishindo kikubwa. Akasikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Kijana huyu Baraka Ibrahim mwenye umri wa miaka 27, aliogopa. 
Aliogopa kwa mana hakuwa na silaha yoyote mkononi. Hakuwa na panga, kisu, rungu, wala filimbi. Kwa maneno yake anasema:“Nilivyoona ningefungua geti hata mimi ningekufa, nilikimbia kuwaamsha majirani. Sikuwa hata na namba ya simu ya mtu yeyote kati ya mabosi wangu ninaowalinda. 
Nilikuwa mimi tu, imani yangu na Mungu wangu…. kutokana na maisha naifanya hivyo hivyo tu. Vinginevyo milele nisingefanya kazi hii ya ulinzi.”Mlinzi huyo alikimbilia kwa majirani katika nyumba aliyoamini yumo mwanaume, lakini akaanza kumwamsha House Girl, ili house girl amwamshe baba mwenyenyumba. 
Kitendo cha kuamshana na kuwapa taarifa kilichukua dakika tano hadi saba, na ndani ya muda huo, Mlinzi anasema watekaji wa Kibanda walifanyafanya unyama na uasi huo na kuondoka ndani ya muda mfupi kiasi hicho. “Watu hawa wana mafunzo maalumu,” anahitimisha.
2.3. Mke wake alikwenda kazini asubuhi na kurejea nyumbani jioni, lakini tofauti na utaratibu wake wa kawaida ambapo huwa anaangalia televisheni sebuleni hadi Kibanda anaporejea nyumbani, siku hiyo alikwenda kuangalia televisheni akiwa chumbani na usingizi ukampitia. 
Anasema hakusikia honi wala tukio la Kibanda kutekwa. “Hii inanitesa sana moyoni. Najiuliza kwa nini siku hiyo tu sikukaa sebuleni? Kwa nini siku hiyo tu nimelala mapema kabla Baba Joshua hajarudi (machozi yanamlengalenga). Najiuliza sipati jibu.”
2.4. Mmoja kati ya wasaidizi wawili wa nyumbani kwa Kibanda, alisikia kelele za Kibanda akiomba msaada. 
Alimwamsha mwenzake na kumwambia. “Nasikia Baba Joshua anapiga kelele kama amevamiwa hivi.” Mwenzake alimwambia “Unaota maana kuna kelele za mpira.” Siku hiyo kulikuwa na mechi kati ya Real Madrid na Manchester United.Ni kweli zilikuwapo pia kelele za wanaoshangilia mpira siku hiyo, hivyo Kibanda alipoomba msaada, hata waliosikia walidhani watu wanashangilia mpira. 
Binti aliwaamsha Angela na mwenzake, wakaenda sebuleni, wakakaa na kuchungulia dirishani, wakaona mwanga wa gari getini, lakini baada ya kutosikia kelele yoyote wakarejea kulala wakidhani siye. Lakini binti mmoja alibaki sebuleni. Baada ya muda jirani mmoja akampigia simu Angela kumweleza kuwa mumewe ameshambuliwa.2.5. Kibanda kwa upande wake, anasema alipofika getini, alipiga honi, ghafla akaona watu wawili wamesimama pembeni mwa gari lake na mtu wa tatu akiwa kwa mbali. Kisha akasikia kishindo kikubwa, akidhani wanataka kuiba gari, aliatokea mlango wa abiria na kuanza kukimbia huku akiita. “Mama Joshua nisaidieeeeee.”Katika kukimbia, aliteleza akaanguka. Huku watesaji wake wakisema mara tatu “Afande piga risasi.” Kibanda alijaribu kupambana, akashika rungu, akawahoji amewakosea nini hadi wampige kiasi hicho, lakini hawakumjibu lolote. Waliendelea kumpiga, hadi akapoteza fahamu. Hakujua jicho limetobolewa saa ngapi, meno yameng’olewaje na wala pingiri ya kidole chake imekatawaje. Ifuatayo ni sauti ya Kibanda mwenyewe. Inasikitisha ila tuwe wavumilivu na tuisikilize.

3.0. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.

3.1. Mazingira ya kazi ndani ya New Habari (2006) Limited na Freemedia Limited, yanaacha maswali kadhaa yenye kustahili majibu. Kama ilivyoelezwa kwenye Hadidu Rejea Na: 1, ndani ya kampuni ya New Habari imekuwapo misuguano isiyo na afya kwa kazi ya Kibanda kama mwandishi na tasnia ya habari kwa ujumla.

3.2.Mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ni utata. Uhusiano katika chumba cha habari si mzuri. Ndani ya kampuni hawaaminiani na imefikia hatua wanatuhumiana kuwa huenda baadhi ya viongozi ndani ya New Habari wamehusika kumteka na kumuumiza Kibanda. Haya yameandikwa ndani ya mitandao ya kijamii, ikidai kwamba kiongozi mmoja ndani ya kampuni hiyo alihusika na utekaji wa Kibanda.Mkurugenzi wa Uhariri, Prince Bagenda anasema waliohusika kusambaza taarifa chafu dhidi ya kiongozi huyo wa New Habari wanatoka ndani ya kampuni hiyo.

3.3. Timu ya uchunguzi ilibaini kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya New Habari (2006) Ltd kwa kuwapo kundi la ‘Habari Wazawa’ na ‘Habari wa Kuja’. Malalamiko mengi yanajikita katika msingi kuwa ajira hazitangazwi na watu wanaajiriwa bila kuzingatia sifa za kitaaluma.

3.4. Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:“Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo.”Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka. Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke.

4.0. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.

4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.

4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.

4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10. 4.4. Daniel Chongolo aliiambia timu kuwa alfajiri ya Machi 6, siku anayodai kutekwa Ludovick yeye alimuona eneo la Mabibo wakati anatoka Muhimbili. Chongolo alikwenda kituo cha polisi Mabibo na kupewa taarifa kuwa Ludovick alitoa taarifa polisi kuwa alikuwa ametekwa ila akarudishiwa mali zake zote. “Alipouliza amefuata nini polisi, akawambia kama raia mwema amefika kuandikisha kumbukumbu kwa nia ya kuonyesha kiwango cha uhalifu kinavyoongezeka nchini,” anasema Chongolo. Timu ya uchunguzi ilikataliwa kupitia leja ya polisi kama itakavyoelezwa hapa chini.

4.5. Pia taarifa za uchunguzi wa timu hii zinathibitisha kuwapo kwa utata juu ya madai ya kuibwa kwa simu za Joseph Ludovick, kwani simu yake ya tigo (inayodaiwa kuibwa) ilitumika saa 01:21 asubuhi siku ya Machi 6, 2013. Muda huu ofisi za Serikali na Kampuni ya Tigo zilikuwa hazijafunguliwa

5.0. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika.

5.1. Uchunguzi umebaini kuwa maisha ya wanahabari yapo hatarini. Hatari hii inatokana na makundi mengi yenye masilahi kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa masilahi yao haramu. Kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

5.2. Uchunguzi umebaini kuwa usiri umepungua katika vyombo vya habari. Tofauti na zamani ambapo habari nyeti ziliandikwa kwa kuhifadhi majina ya waandishi wakitumia jina la MWANDISHI WETU. Simu hizi hata habari za kutisha waandishi wanaweka majina yao na hata wasipoweka, ndani ya vyumba vya habari vingi waandishi wapo tayari kutaja nani ameandika habari fulani.

5.3. Usaliti miongoni mwa waandishi wenyewe ndani ya vyumba vya habari unazidi kuongezeka na usipodhibitiwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi. Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi anasema: “Hili ni jambo muhimu sana. Tuache usaliti vinginevyo wengi wataumia.”

5.4. Pia alishauri waandishi wa habari kurejea katika msingi wa taaluma, ambayo inawataka wao kuwa ndio wenye kuendesha vyombo vya habari badala ya kutegemea matakwa ya wamiliki au makundi yenye masilahi binafsi.

6.0. KILICHOBAINIKA:
6.1. Uchambuzi uliofanywa ni timu hii umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa kuhusiana na kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda. Hoja hizi ni:-(i) Kazi yake ya uandishi wa habari(ii) Uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali(iii)Uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi(iv) Vitendo vya rushwa.

6.2. Timu imejiridhisha kutokana na majibu ya wengi kuwa dhana ya mapenzi na rushwa, havina nafasi yoyote katika tukio hili. Wote waliohojiwa walieleza pasi na shaka kwamba suala hili la kushambuliwa na kuumizwa kwa kiwango kikubwa kwa Kibanda, halina uhusiano wowote na rushwa au mapenzi.

6.3. Kutokana na yaliyotajwa hapo juu kazi yake na siasa vikiunganishwa vimechangia kwa kiasi kikubwa kuvamiwa kwa Kibanda. Timu imebaini kuwa kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. Mchezo huu mchafu unaweza ukawa mwanzo wa kuumizwa kwa Kibanda na waandishin wengine.

6.4. Baadhi ya waliohojiwa walidai kuwa utekaji huu umefanywa na vyombo vya dola ukiwa sehemu ya mpango mkakati wa vyombo hivi kukihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vitendo vya ugaidi.6.5. Wanayataja matukio ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga, maandamano ya Morogoro na Mkanda anaodaiwa kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare kuwa vililenga kukifanya CHADEMA kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja kama chama cha kigaidi ambacho kinateka watu na kinawaumiza.

6.6. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anadai kwamba mpango kama huo vyombo vya dola viliutumia kwa NCCR Mageuzi vikakisambaratisha, Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa udini kikapoteza mwelekeo na sasa vyombo hivyo vililenga kukifanya CHADEMA kionekane cha kigaidi mbele ya macho ya jamii ndiyo maana imerekodiwa mikanda kwa nia ya kuitumia kujenga hoja hiyo.

6.7. Wakati Mbowe akisema hayo, baadhi ya watu waliohojiwa wanadai kuwa CHADEMA kimepewa mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya watu maarufu nchini wakiwamo waandishi na wanasiasa, basi wananchi wataamini kuwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza kazi ya kuua wanaowapinga.

6.8. Kwa njia hiyo, inaelezwa kuwa hesabu za Chadema ni kuwa wananchi wataichukia CCM na Serikali yake na kukipa nafasi ya kuingia madarakani. Hapa kauli ya Chadema kuwa NCHI HAITATAWALIKA itakuwa imetimia.

6.9. Dhana nyingine iliyojitokeza ni kuwa wapo wafanyabiashara ambao wana vita binafsi, hivyo wanaamua kuumiza watu wasiowaunga mkono katika mipango yao na hilo ndilo limemkumba Kibanda, baada ya kuwa ameepusha mauaji ya mwandishi mmoja na aliyekuwa ameandaa mpango wa kuua mwandishi huyo hakuridhika hivyo akaamua amshughulikie Kibanda.

7.0. MAPENDEKEZO:Baada ya Timu kupata taarifa hizi na nyingine nyingi, inapendekeza yafuatayo:-

7.1. Taarifa hii ichukuliwe kama chanzo cha uchunguzi zaidi wa vyombo husika.7.2.

Yanahitajika marekebisho makubwa na ya haraka katika mifumo ya uendeshaji wa vyumba vya habari kwa nia ya kurejesha misingi ya uandishi wa habari inayokubalika.

7.3. Usalama wa wanahabari unapaswa kupewa kipaumbele na wamiliki, wanahabari wenyewe na jamii kwa ujumla. Hapa Timu inapendekeza yawepo mafunzo ya kuwawezesha wanahabari kutambua viashiria vya hatari na kuchukua hatua mara moja.

7.4. Kwa kiwango alichoumizwa Kibanda iwapo mwajiri wake asingejitolea kugharamia matibabu, hatujui hatima yake ingekuwaje leo hii. Tunapendekeza taasisi na mifuko mbalimbali inayojihusisha na masuala ya wanahabari kama Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuanzisha mfuko wa pamoja utakaotumika kugharamia matibabu ya waandishi watakaoumia wakiwa kazini.

7.5. Tukio la kutekwa kwa Kibanda limeonyesha mwanga kuwa wahariri tumegawanyika mno. Habari zilizochapishwa katika magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii zimeonyesha haja ya kuwafanya wahariri kuwa kitu kimoja kwa kuondoa tofauti zao zisizo na masilahi kwa tasnia ya habari.

7.6. Kuna viashiria vingi kuwa kuelekea mwaka 2015 matukio ya waandishi kuumizwa au kutekwa yanaweza kuongezeka kutokana na wanasiasa na vyama kuwania madaraka huku wakitumia baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola. Kwa mantiki hiyo, vyombo vya habari na waandishi wa habari wachukue tahadhari kuanzia sasa.

7.7. Taasisi za habari zifanye juhudi za makusudi kukutana na vyama viwili vya siasa vya CCM na CHADEMA haraka iwezekanavyo, kuzungumzia viashiria hivi vya hatari vinavyoelekea kuvuruga amani ya Tanzania.

8.0. HITIMISHO:Ni dhahiri kuwa kupigwa na kuteswa kwa Kibanda kumejiegemeza katika siasa na kazi yake, hali inayofanya makundi muhimu kuchukua wajibu wa msingi. Kwa upande wa Serikali ni muhimu kufuatilia viashiria katika taarifa hii kwa nia ya kupata ukweli zaidi na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya wahusika.Na kwa upande wa vyombo vya habari na taasisi za kihabari zinapaswa kutambua viashiria vinavyohatarisha usalama wa waandishi wa habari na wahariri na kutengeneza mazingira yatayokuwa salama zaidi kwa waandishi kufanya kazi zao.

9.0. SHUKRANI:

9.1. Tunapenda kulishukuru Jukwaa la Wahariri Tanzania, kwa kufanya uamuzi sahihi wa kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi huu ulioanza kuonyesha mwanga wa nini kilitokea.

9.2. Tunapenda kulishukuru Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushiriki kikamilifu na kuiwezesha timu hii kwa Rasilimali Watu na Mali kufanikisha kazi hii.

9.3. Tunapenda kuwashukuru Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) kwa uwezeshaji wa ruzuku, uliofanikisha kufanya uchunguzi wa kihabari uliohusisha kwenda nchini Afrika Kusini kufanya mahojiano na Kibanda. Uwezeshaji huo pia unahusisha kutengeneza mwongozo kwa waandishi wenye lengo la kuwaepusha na hatari za kiusalama.

9.4. Tunawashukuru Kibanda, mkewe Angela, wanafamilia, ndugu na jamaa wa Kibanda na wanahabari wote waliohojiwa kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Timu hii.

9.5. Tunawashukuru wahariri wote kila mtu kwa nafasi yake, kutokana na ushauri wa mara kwa mara mliotupatia katika kufanikisha uchunguzi huu.

10.0. WAJUMBE WA TIMU:Timu hii iliundwa na wajumbe watano ambalo ni:1. Deodatus Balile – Mwenyekiti2. Pili Mtambalike – Mjumbe3. Jane Mihanji – Mjumbe4. Tumaini Mwailenge – Mjumbe5. Rashid Kejo – Katibu

HALI YA M TO THE P YAIMARIKA...... NGWAIR ATARAJIWA KUAGWA JUMAPILI


-Msanii M2 the P anaendelea vizuri, leo ameweza kuongea na ametolewa ICU kupelekwa wodini
  
-Mwili wa Albert Kenneth Mangwair unatarajiwa kuwasili jijini Dar Jumamosi Juni 1, 2013 na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.

 
-Ngwair anatarajiwa kuagwa siku ya Jumapili katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar.

 
-Msanii Bushoke alaani watu wanaotoa taarifa zisizo sahii kuhusu sababu za kifo cha Ngwair pamoja na kusambaza picha za mwili wa marehemu kwenye mitandao ya kijamii.
TAARIFA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.

Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu. 

Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. 
Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

 
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

KUPATA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012 >>BOFYA HAPA<<

P- FUNK AWACHANA TENA CLOUDS FM.... AELEZA JINSI MAREHEMU NGWEA ALIVYOGEUZWA NG'OMBE WA MAZIWA


Kwa mara nyingine  tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa. 

Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya.

 “Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.”  P funk
Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records  zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema:

“Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm. 
Sababu kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita  number one radio station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka. 

Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.” Mimi cha kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingie kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha pili mnaingiza hela sana ya wadhamini  lakini hamui-distribute kwa wanaohusika...
"Mfumo wa kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi . Hivyo nitakua wa kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.”

Thursday, May 30, 2013

AMMY NANDO WA TANZANIA NDANI YA BAFU MOJA NA MREMBO WA NAMIMBIA....


Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time).

 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.

Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uzuri wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania.  

Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. 

Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger.
 

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi ya  kukumbwa na Eviction

WATU 92 WAFIKISHWA MAHAKAMANI MTWARA KUHUSIANA NA VURUGU ZA GESI


Watu 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mtwara na kusomewa mashitaka mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo, kuvunja nyumba, kuiba, kujeruhi na kuhujumu uchumi katika vurugu zilizotekea mjini Mtwara, Mei 22, mwaka huu.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mussa Esanju.
Waendesha Mashitaka wa Serikali, Justine Sanga, na Renatus Mkude, walidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo katika tarehe hiyo. 

Watuhumiwa kwa pamoja walikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande.
Uamuzi huo unatokana na wengi wa washtakiwa kukabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi, kosa ambalo mahakama hiyo haina uwezo wa kuwaachia kwa dhamana.
Hakimu Esanju aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.

HABARI  IMEANDIKWA  KWA  KIREFU KATIKA  GAZETI LA NIPASHE
RAIS WA TFF KUZINDUA KOZI YA MAKOCHA JUMATATU DAR ES SALAAM
Tenga-wa-TFF a0606
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumatatu (Juni 3, 2013) kwenye Ukumbi wa Hobours Club, uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo itakayohusisha amakocha 26.
Alisema kozi hiyo itakayomalizika Juni 28 itakuwa imewezesha kupatikana makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.

Aliwataja makocha wa kozi hiyo kuwa ni Shadrack Nsajigwa, Benard Mwalala, Steven Nyenge, Jemedari Said Kazumari, Zubeiri Katwila, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, David William Ngaga, Idd Abushir Mwinchumu, Rajab Mohamed Nakuchema, Lubigisa Madata, Bakari Mahad, Greyson Swai, Chiwanga  A. Chiwanga, Sizza Mapunda na  Muhibu Kanu.

Wengine ni Omari Mbarouk, Omari Mohamed, Samuel Galafawo, Abdallah Mbogolo, Hassan Msonzo, Akida Said, Emanuel Gabriel, Barton Msengi, Edgar Method Katembo, Elly Kaiza na Renatus Benard.  
 Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas Kassongo.

Wengine walioingia madarakani katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden ni Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.
YANGA YAZAWADIWA SH.25 M NA TBL KWA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU
yanga2 028c8
Meneja wa kampuni ya bia ya TBL George Kavishe akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 25 kwa katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako

yanga 72fc9

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na mabingwa watetezi wa kombe la Kagame, klabu ya Yanga ya Dar es salaam wamepewa zawadi ya sh. Milioni 25 kutoka kwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wameizawadia klabu hiyo Sh. Milioni 25 kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara uliomalizika mei 18 mwaka huu.
 TBL, wanaoidhamini Yanga na Simba kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milion 25 leo kwa Yanga katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Safari Pub, uliopo makao makuu ya TBL, Ilala, Dar es Salaam. 
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe wakati akikabidhi mfano wa hundi hiyo alisema Kilimanjaro Premium Lager imefurahishwa sana na ubingwa wa Yanga na kusema imejizatiti kikamilifu kuisaidia timu ambayo imeibuka bingwa katika ligi yenye ushindani mkubwa kutokana na kuibuka kwa timu mpya zenye nguvu.
“Yanga imekuwa akionesha soka safi kwa kipindi chote, ligi ni ngumu sana lakini wamecheza soka maridadi, hivyo kuibuka mabingwa sio ajabau kabisa. Napenda kuwapongeza wachezaji wa Yanga, kocha na Uongozi mzima wa Yanga kwa  matokeo mazuri ya kushinda Ligi kuu kwa mara ya 24 sasa.” Alisema Kavishe.
Kavishe aliongeza kuwa zawadi hiyo ni sehemu ya sh bilioni 1.5 ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga   na imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa ushindi zaidi na kusaidia klabu katika maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ambayo tayari Yanga ina sifa za kushiriki kutokana na ubingwa waliojipatia.
Akipokea hundi hiyo, Katibu mkuu wa Yanga , Bwana Lawrence Mwalusako alisema Yanga inaishukuru sana Kilimanjaro Premium Lager kwa mchango wao. Aliongeza kuwa Yanga ni timu nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi imara pamoja na udhamini mkubwa kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.   
‘‘Mafanikio yetu ya uwanjani ni kielelezo cha mafanikio ya kampuni na pia (TBL) na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa ujumla ambayo imekuwa ikitusaidia sana.’’ alisema Mwalusako.
Mwalusako aliongeza kuwa kwa sasa Yanga ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa la soka kutokana na mafanikio hayo na kuahidi kujipanga zaidi kufanbya makubwa zaidi.
Yanga itawakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Kagame. Chanzo: Baraka Mpenja
MALUMBANO YA CUF NA CHADEMA BUNGENI YASABABISHA KIKAO KIAHIRISHWE KABLA YA WAKATI
chadema-logo-i2 11f96CUF-LOGO 11e99

Nukuu kutoka JF:
JF:Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cCUF kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita CHADEMA ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha CUF.
Mbunge huyo wa CUF ameomba Spika achukue hatua za dhidi ya CHADEMA asipofanya hivyo CUF watachukua hatua dhidi ya CHADEMA na Bunge.
Kumetokea vurugu bungeni ambapo Spika ameliahirisha Bunge hadi jioni.
Quote:
By Tumaini Makene
Kipengele kinachowasumbua katika hotuba ya Wenje ni hiki hapa...ambacho kimejaa facts na ukweli. Wakanushe hizi facts. Wajibu hoja si kumshambulia mtoa hoja. That is what argumentation is all about, let alone critical thinking....
Kitu gani si cha kweli hapa?
3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa 'United Nations University'(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania 'Donor Assistance and Political Reform in Tanzania', inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.
Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada hiyo.
Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.
Mheshimiwa Spika, CCM wao 'wanajiita' kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni 'Socialist International' kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na "kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga". Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: "tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji". Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .
AFUNGWA MWAKA MMOJA KWA KUMTUMIA SMS MBAYA WAZIRI 
Mwema41 533aeMkazi Wa Mburahati Jogoo jijini Dar es salaam, Nassor Issa Mohamed (25) amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni tatu kwa kosa la kuwatumia ujumbe wenye nia mbaya wa simu ya mkononi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi na Inspekta General wa Polisi Said Mwema.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Helen Riwa wa mahakama Kisutu aliiambia mahakama kuwa Mohamed alisajili kadi zake za simu kwa majina tofauti na kwa mitandao tofauti kwa nia ya kutumia kadi hizo kutuma ujumbe wa simu wenye nia mbaya kwa viongozi hao.
Alisema mshtakiwa alikutwa akiwa na kadi ya simu yenye namba 0759 799956 ya Vodacom iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issah, nyingine ya Airtel 0687 521948 iliyosajiliwa kwa jina la Godfrey Joseph na kadi yenye namba 0687521947 ya Airtel iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issa.
Hakimu Riwa aliitaka jamii kutumia kwa uangalifu mitandao kwa kuwa ni teknolojia mpya ambapo makosa yake yanakuwa ni mapya na sheria ni mpya. Alisema ametoa adhabu hiyo kwa kutumia Sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 kifungu cha 132 ili iwe fundisho kwa wote wenye nia ya kufanya makosa kama hayo.
Awali Mwendesha Mashitaka Ladislaus Komanya aliiambia mahakama kuwa mnamo Mei 20 mwaka huu taarifa za kiinteligensia zilifikishwa kwa Maafisa wa juu wa jeshi la Polisi kuwa kuna mtu aliyesajili simu zake kwa mitandao tofauti anatumia simu hizo kuwatumia ujumbe mbaya wa simu ya mkononi Waziri Nchimbi na IGP na baada ya upelelezi ilipobainika kuwa namba hizo zilikuwa zimesajiliwa kwa majina tofauti.
Alisema iligundulika kuwa namba hizo zilikuwa zinamilikiwa na mtu huyo ambaye jina lake halisi ni Nassor Issah Mohamed
Alisema Mohamed alikamatwa Mei 25mwaka huu na baada ya mahojiano alikiri kumiliki kadi ya simu na kwamba ndiyo yeye aliyesajili namba hizo kwa mitandao tofauti akitumia majina tofauti ili kuficha utambulisho wake akiwa na lengo lakufanya uhalifu. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka huu na kukiri mashitaka.
BALOZI BISWARO AWAPA CHANGAMOTO TAIFA STARS
Wambura 658dc
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Ametoa changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

"Watanzania tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga Morocco mabao 3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga. Tunataka kuwaona Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi mtanikuta kule," amesema Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi kuichezea timu ya Yanga.
Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa Addis Ababa.
Balozi Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri.
Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga nacho Juni 3 mwaka huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu.
Wachezaji walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Addis Ababa
+251 919910240

"SIELEWI MSINGI WA KAULI YA SITTA "JOHN MAGUFULI
d1 e3e51

Kauli ya Magufuli
Akizungumza na gazeti hili nje ya ukumbi wa Bunge jana, Dk Magufuli alisema haelewi msingi wa kauli ya waziri mwenzake huyo, kwani hajui chochote katika mtandao wa urais alioutaja.
Magufuli alisisitiza kusema hana kundi, hakuwahi kuzungumza wala kuhudhuria vikao vya kundi lolote, na kwamba kundi lake ni CCM na Mwenyekiti wake ni Jakaya Kikwete.
“Sina kundi. Sijawahi kuwa na kundi na sitarajii kuwa na kundi lolote. Ninachojua kundi langu ni CCM na kiongozi wake ni mwenyekiti wake, Rais Kikwete,” alisema Dk Magufuli.
Hata hivyo, Dk Magufuli pia alipuuza taarifa kuwa alichangia harambee hiyo akisema, “Si kweli, Mwanza sijatoa hata senti na hata siku ilipofanyika hafla hiyo, nilikuwa Dar es Salaam katika mkutano na makandarasi.” Licha ya kutajwa kuwa miongoni mwa vinara wa urais 2015, Magufuli alieleza kuwa hakuwahi kuzungumza na Sitta suala hilo linalohusu makundi ya urais mwaka 2015.
Sitta azungumza
Akizungumza na gazeti hili baadaye jana, Sitta alikiri kuwa hawakuwahi kuzungumzia suala la kuwania urais isipokuwa ni hisia zinazojengwa na kuwa majina yanatajwa kuwa wanautaka urais.
“Nilishasema kuwa umoja wetu tuliouunda ni wenye sauti sawa ni kupigania hali za wananchi wanyonge, na hata kwenye mikutano yetu ya ndani tunasema sisi ni dhidi ya watu wanaokwenda kinyume na maisha ya wanyonge.
“Na ni kweli nilitamka kuwa katika umoja wetu, ikiwa itaonekana mmoja wetu anafaa na watu wakataka awanie urais, basi itakuwa hivyo.” CHANZO: MWANANCHI

Wednesday, May 29, 2013

PICHA ZA WASANII KAITKA KIKAO CHA MIPANGO YA MAZISHI YA NGWEA 
Geez Mabovu Na Q Chief
Flavian Matata, Sajjo Na Mwana FA
G Nako, Bab Tale, Said Fella, Maneke Na Quick Rocka
Dj Choka Na Duke
Snura
Shilole
Wajumbe Wa Kamati Ya Mazishi
Msemaji Wa Kamati Adam Juma Akizungumza Na Vyombo Vya Habari.

MOYES ATAKA KUMSAJILI FABREGAS MAN UNITED
fab2 dbe7e

Fabregas
 fab dd9b4
KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes anataka mchezaji wake wa kwanza kumsajili, awe kiungo wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas.
Kocha huyo mpya wa Mashetani Wekundu anataka mchezeshaji huyo atue Old Trafford kumaliza tatizo la safu ya kiungo la Manchester United na klabu yake ya sasa, Barcelona iko tayari kumuuza nyota huyo wa Hispania.
Huku Paul Scholes akistaafuna Anderson kushindwa kumaliza tatizo la safu hiyo, Fabregas anaweza kuwa suluhisho kwa mabingwa hao. Arsenal walipewa kipaumbele cha kumsajili tena Fabregas wakati atakapoondoka Barcelona, lakini Manchester United wanajiamini wataizidi nguvu Gunners kwa ushawishi wa kifedha.
BENITEZ AWEKA NGUMU CAVANA KUONDOKA NAPOLI
napoli 2f7b2
Cavan kulia
KOCHA mpya wa Napoli, Rafa Benitez anataka kumzuia kuondoka katika klabu hiyo mshambuliaji, Edinson Cavani na atafanya naye mazungumzo mshambuliaji wake nyota huyo kumshawishi abaki kwa mmoja zaidi.

Cavani, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwaniwa kwa muda mrefu na Manchester City na ameingia kwenye orodha ya washambuliaji tishio Ulaya kwa kuweza kufunga mabao 29 katika mechi 34 za ligi akiwa na Napoli.
Chelsea pia inamtaka mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 50 na anayetaka mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki. Wiki iliyopita, Napoli iliikata maini City katika mpango wa kumtaka Cavani, kwa kuwapa ofa ya Pauni Milioni 60 kwa ajili ya Edin Dzeko.

Rais wa klabu hiyo ya Italia, Aurelio De Laurentiis, ambaye alikuwa hataki kuizungumzia City awali, alisafiri hadi London Jumatatu kufanya mazungumzo Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo ya Ligi Kuu England, Riccardo Bigon.
City iko tayari kukubali Pauni Milioni 50 – kati ya hizo, Pauni Milioni 30 ni thamani ya Dzeko na kuongeza Pauni Milioni 20– lakini Napoli inataka Milioni 60 na De Laurentiis anasema ni wakati wa kumalizana aLaurentiis anasema ni wakati wa kumalizana au kuacha.
Benitez alitangazwa kuwa kocha mpya Napoli Jumatatu akipewa mkataba wa miaka miwili. Mspanyola huyo anachukua nafasi ya Walter Mazzarri ambaye anahamia Inter Milan, klabu ya zamani wa Benitez. Chanzo: Binzubeiry
SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI
IMG 0169 2be6f
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

IMG 0224 20ee9
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja viongozi wa dini.
MISS SINZA WATAKIWA KULINDA HESHIMA
untitled2 3cca1
Na Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania 2012 ambaye pia ni Redds Miss Sinza, Brigitte Alfred amewataka warembo wanaowania taji la mwaka huu la kituo cha Sinza kutomuangusha kwa kufauata nyayo zake katika shindano lililopangwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Meeda Club.

Brigitte alisema hayo juzi alipotembelea warembo wanaowania taji la mwaka huu katika kinyang'anyiro hicho kilichodhaminiwa na bia ya Redds Origional, Dodoma Wine, Clouds Media Group, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5.com na Sufiani Mafoto blog.
Alisema kuwa warembo wa kituo hicho wanakazi kubwa ya kushinda taji hilo na baadaye Miss Kinondoni na Miss Tanzania kama yeye alivyofanya.
Alifafanua kuwa siri kubwa ya mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani hata yeye alifundishwa na matroni wa sasa, Mwajabu Juma na waandaaji ni wale wale.
"Sioni sababu ya kushindwa kufanya vyema katika mashindano haya, Redds Miss Sinza ndiyo inatetea taji la Miss Kinondoni na Miss Tanzania pia, hivyo macho ya wadau wote wa urembo yatakuwa kwenu na ndicho kitongoji kinachofunga mashindano ya ngazi ya chini, mnatakiwa kujituma na kuwafanya majaji kuwa na kazi ya ziada kumpata mshindi," alisema Brigitte.
Alisema kuwa wadau wa masuala ya urembo wanaangalia Sinza mwaka huu itafanya nini baada ya mafanikio makubwa ya mwaka jana. "Sisi tumejenga msingi mkubwa na kuleta heshima kwa wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla, nanyi mna jukumu hilo," alisema.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na kiingilio ni sh 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 20,000 kwa viti vya VIP. Alisema kuwa wanakamilisha maandalizi ya burudani ya siku hiyo ambayo itakuwa ya aina yake.
Mwisho...
untitled 4252b